Prof Shivji ashauri walimu walipwe zaidi ya mawaziri

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Profesa Shivji ashauri walimu walipwe zaidi ya mawaziri

Mwanazuoni maarufu nchini, Profesa Issa Shivji, ameishauri serikali iwalipe walimu mishahara mizuri zaidi ya mawaziri kwa kuwa kazi wanayofanya ni ngumu.

Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati wa Jukwaa la Wazi la Uchumi wa Afrika lililofanyika katika viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).

Jukwaa hilo liliandaliwa kwa pamoja na mashirika ya ActionAid Tanzania, Oxfam, Forum CC, FemAct, Yuna na Kepa.

Profesa Shivji alisema elimu inazidi kuporomoka kwa kuwa hakuna jitihada zinazochukuliwa na serikali kuondoa hali hiyo.

Alisema serikali inaangalia zaidi ongezeko la majengo na idadi ya wanafunzi mashuleni jambo ambalo alisema haliwezi kuinua kiwango cha elimu.

“Mwalimu akiwa bora na akiwa katika mazingira mazuri ya kufundisha hata akifundishia chini ya mti, wanafunzi watafanya vizuri sana, lakini ukiwa na majengo mazuri mwalimu akawa mbovu ina maana elimu itakayopatikana hapo ni ya kiwango cha chini," alisema.

Alisema walimu wengi kutokana na hali ngumu wameamua kuachana na hali hiyo na sasa wanafanya shughuli zao za kuwaingizia vipato.

"Mimi sioni sababu kwanini mwalimu ambaye ni muhimu zaidi ya waziri kwenye jamii, alipwe mshahara kidogo na waziri alipwe mshahara mnono na marupurupu mengi kumzidi mwalimu," alisema.

Vile vile, Profesa Shivji alisema ingawa Tanzania ni ya pili kwa kuwa na mifugo mingi Afrika, wafugaji wamekuwa hawanufaiki na mifugo yao.

Alisema wafugaji wamekuwa wakihangaishwa kama vile si raia wa Tanzania kwa maeneo yao kuchukuliwa kiholela akitolea mfano wa Ngorongoro.

Awali, akifungua mkutano wa jukwaa hilo, Mkurugenzi wa ActionAid Tanzania, Aida Kiangi, alisema inaonekana mkazo mkubwa wa ustawi na ukuaji wa uchumi katika jukwaa hilo la kiuchumi umeelekezwa zaidi kulenga maslahi ya makampuni makubwa dhidi ya Waafrika walio wengi hususani wanawake, wakulima wadogo na wafupaji pamoja na maskini wanaozidi kuongezeka hasa maeneo ya mijini.

Kiangi alisema kumekuwa na ukuaji wa uchumi kwa nchi za Afrika lakini wanaonufaika na ukuaji wa uchumi huo ni wachache.

“Tunaweza kujiuliza ni nani anayenufaika zaidi na ukuaji wa uchumi huu," alihoji.


CHANZO: NIPASHE
 
Nakubaliana na wewe kabisa! Wasomi wengi ni matunda ya waalimu,Waziri naye ni matunda ya mwalimu sasa iweje mwl awe ni wa kiwango cha chini?
 
Matokeo ya mwaka huu yanaonyesha ni jinsi gani maslahi ya walimu yanahitaji kuboreshwa.
 
katika watu wote ninaowafahamu waliomaliza udsm fani ya education hakuna hata mmoja aliyekwenda kufundisha. . .nadhani hapo inabidi watafakari.
 
Nakubaliana na prof.hatuwezi kujenga juu ikiwa msingi ni mbovu,waziri hayupo bila mwalimu kwa nini wasiboreshewe maslah
 
Kazi ya walimu ni ngumu sana kuliko ya Waziri, hatuwezi kudanganyana.
Dhamana ya mwalimu iko kwa kuimbe/ taifa/ baba/mama/raisi/daktari wa kesho. Ni dhamana kubwa sana. Inabidi tujipange upya kufikiria.
Watoto/wanafunzi wana kaa muda mrefu sana na walimu au wazazi, kwa hio hawa ndio wanaoshape huyu mtua atakuwaje, je awe mvivu kufikiria, awe wa visingizio, awe mwongo, awe mchawi, awe mtoro, au awe mweli, jasiri, focused, hounorable, awe wa kuaminika maneno yake, awe mcha mungu, awe anasimamia ukweli, awe kiongozi bora yote haya yatatokana na waalimu wa shule aliosoma mtoto.

Tunachezea taifa la kesho,
Tusiwaachie hawa watu waendelee kutuchezea watoto wetu kwa hela yetu. Walimu wathaminiwe zaidi ya wakurugenzi wa idara na mabosi wao hazi ngazi ya waziri mkuu na rais
 
Back
Top Bottom