Prof Shivji aiponda Kauli Mbiu ya Rais Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof Shivji aiponda Kauli Mbiu ya Rais Kikwete

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Regia Mtema, Jun 26, 2010.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Jun 26, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Muda mfupi uliopita nimetoka kushiriki kwenye mdahalo wa kuandaa Agenda za Vijana za Tanzania tunayoitaka leo na baada ya uchaguzi kwa kifupi Ilani ya Vijana.

  Mjadala huu uliandaliwa na Asasi ya Vijana ya TYVA na umefanyika katika Hotel ya Peacock Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.Mgeni rasmi katika mdahalo huo alikuwa ni Professa Issa Shivji Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere.

  Katika ufunguzi wake kiongozi huyu machachari na mwenye uchungu wa dhati na nchi hii alisema mambo mengi lakini nitaleza machache yaliyonigusa sana.

  Prof alisema kuwa Azimio la Arusha limesahaulika kabisa na alishangazwa sana mwaka 2007 amabpo azimio hili lilikuwa linatimiza miaka 40 lakini Serikali na watu wengine hawakuthubutu kulikumbuka lakini Serikali iliazimisha miaka 30 ya Chama Cha Mapinduzi.

  Prof aliturudisha nyuma na kueleza kuwa Kauli Mbiu ya Azimio la Arusha ya Binadamu Wote ni Sawa na Afrika ni moja ni Kauli mbiu muhimu sana na yenye ku-inspire sana.

  Akaponda kauli mbiu ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania kuwa hainspire wala haina mvuto badala yake inasababisha kila mmoja kuhangaika kivyake iwe kwa kula rushwa au kwa njia yeyote ile ilmradi tu afikie hayo maisha bora. Akasema Slogan hii ni ya kibaguzi inaleta matabaka.

  Habari ndio hiyo.
   
 2. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 231
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  GS,

  Vijana mnafanyia mikutano yenu hotelini? Enzi za ujana wenu hilo lisingeliwezekana, tungelienda Jangwani.
   
 3. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hawa ni vijana waliozaliwa kwa matunda ya kifisadi ni lazima watakuwa na kila dalili kuwa watafuata nyayo za baba zao na ishara ndio hizo za kufanyia mikutano kwemye hoteli kubwa wakati kiwanja cha jangwani au kidongo chekundu viko wazi!!
   
 4. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  KWey kwey hivi kijana wa kawaida kabisa wa kitanzania ataruhusiwa kuingia kwa hotel zao za kina Mboni? :jaw:
   
 5. m

  magee Senior Member

  #5
  Jun 26, 2010
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Big up gender sensitive......wasikukatishe tamaa hawa,kwanza inapendeza kuona vijana wanashiriki kwenye makongamano kama haya na asante kutuhabarisha wengine namshauri N-HANDSOME,BULESI NA MUHEZA waandae kongamano lao pia pale jangwani na tutajitokeza kwa wingi tu badala ya kulaumu.....lamsingi hapa wapendwa ni mada iliyojadiliwa kwenye hilo kongamano....mm niko njiani kuzindua kitabu changu cha 'ANGUKO LA CCM NA DAWA YA KUIFUFUA' uzinduzi wa kitabu utakuwa KEMPISK cjui ndugu zangu mtaniita kafisadi kadogo??ukweli ni kwamba mabalozi wengi mno watahudhuria na haitakuwa busara kuwapeleka jangwani.................
   
 6. M

  Malunde JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 311
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Asasi hii ipanue wigo, kwa kuendesha midahalo nje ya dar es salaam ilikupata mawazo kwa vijana wanotoka kwenye mazingira tofauti. Kufanyia mdahalo mmoja Peacock kunaweza chukua gharama ya mikutano mingi ile tuliyokuwa tunaifanya nchini ya miembe enzi hizo
   
 7. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Slogans these days are just that "slogans".
   
 8. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kitabu chako kina tittle safi sana.....Ila naomba isomeke hivi "ANGUKO LA CCM" unatoa dawa ya kuifufua ili iweje??? wameshakula na inatosha.
  acha kianguke na kipotee.....dont tell them watakifufua vp.....wameanguka na basi.....ila samahani....hivi CCM imekufa??? kama sio why unaifufua??? Otherwise kitabu chako kiitwe "ANGUKO LA CCM na dawa ya KUIINUA"
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Jun 27, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mimi nadhani hii ngozi nyeusi ina manatizo sanaa. Leo hii hapa kwetu kuna maandamano makubwa sana ya kupinga malengo ya mikutano ya hawa vigogo wa G8 na G20 wanavyotutenda nchi maskini..Maajab ya Musssa hakuna ngozi nyeusi kabisaaa yaani kama wapo basi wanachungulia madirishani.

  Imefika mimi kujiuliza, hivi ndivyo tunategemea mabadiliko yanaweza kuja kwetu ikiwa sisi wenyewe tunajificha majumbani mwetu tukisubiri wazungu waandamane on our behalf?...kisha kesho utasikia tukilalama kwa matusi yote..

  Ni ushauri wangu tu Prof. Shivji kama unaweza kuyaona makosa kama haya kwa nini usiwe msitari wa mbele kuhamasisha wananchi ktk Upinzani badala yake ni kukosoa tu makosa mabyo tayari yamekwisha fanyika!. Uchaguzi mwezi wa 10 wewe umejjiandaa vipi kuwasaidia wananchi kukiondoa chama kinachowanyima haki zao za msingi!..
   
 10. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Did you personally join them?
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Jun 27, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hell noo!....Hawa walikuwa wanaandaa agenda na siyo kuendesha mkutano, nadhani hapo ndipo panapokupa presha!../Kuandaa agenda huwezi kukaa kwenye nyasi na kuandikia magotini, what for, wakati agenda ndiyo cream ya mkutano?...Tusijibane kupita kiasi hadi kuonekana vichaa bana!..Mi naona sahihi tu...GS, KEEP IT UP, na nampongeza Prof Shivji kwa kuweka hadharani jambo hilo!
   
 12. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #12
  Jun 27, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,457
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  ITV na TBC Sidhani kama watirusha hii hewani
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Jun 27, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  If not, how would I know what I know..
   
 14. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #14
  Jun 27, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  PJ.Asante sana kwa kunuisaidia kujibu hili baada ya kusoma post ya Muheza na Bulesi jibu langu lilkuwa ndo hilo..Naona hawaelewi maana ya kuandaa ilani wanafikiri ni kwenda Jangwani na kubwabwaja,Jangwani ni sehemu ya kubwabwaja na sio ya kutafakari kwa kina na kuandaa agenda..Big Up once again PJ kwa jibu lako.
   
 15. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #15
  Jun 27, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mkandara usikwepe hoja.Jibu swali....
   
 16. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #16
  Jun 27, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Huyu Prof Issa G. Shivji anajifanya anatetea sana sera za Mwalimu, huku akiwa mpinzani mkubwa sana wa Muungano ambao Nyerere aliupigania hadi mauti yake!

  Juzi hapa amekuwa champion wa ku-inspire Wazenj wamruhusu Karume kuendelea na uongozi baada ya muda wake kwisha bila hata kujali Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasemaje! Amekuwa pia mtetezi wa Uzanzibari dhidi ya Bara au kwa kifupi, ubaguzi!

  Soma vitabu vyake utaelewa ninasema nini! Amejifunika mwavuli eti kwamba anatetea mambo ya Azimio la Arusha, kumbe ni unafiki mtupu!
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Jun 27, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Gender Sensitive,
  Nikwepe vipi na nimejibu swali?..Yes, I was among marchers on Saturday...
  Mkuu mimi sina sababu la kulaumu pasipo kuona ilivyokuwa. Na ajabu ssijui mnataka kuonyesha kitu gani zaidi ya kuchukua Ujumbe wenyewe.

  Waafrika tuko nyuma sana ktk maswala ya kulilia haki zetu, sisi ni Watumwa wa akili hata ktk maswala mazito yanayotuathiri kila siku..
  Haya badala ya kujiuliza tukajipanga tunaanza kuulizana kama nilikuwepo..Hii akili kweli jamani?..
  Nina hakika sasa kwamba CCM itatawala mielele..
   
 18. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu Buchanan unauhakika na hilo nililowekea wino mwekundu? Naomba kama una nukuhu yake kwenye hilo u paste au uweke link/clip hapa mkuu
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Buchanan,
  Mkuu mimi sioni kosa la Prof.Shivji kutetea Wazanzibar panapo haki yao. yeye anachokizungumzia ni haki na freedom ya wahusika hata hao CCM wanamwona mnafiki anapokuwa upande wetu hali yeye ni mmoja wao (my guess).
  Na kuhusu swala la rais wa Zaibar hilo halituhusu Bara kabisa na sidhani kama linahusiana na Katiba kwani kisheria inatakiwa wao wamchague rais wao na sii bara kuingilia..Tunaingilia mara kwa mara maswala hata yasiyokuwa ya Muungano..

  Prof Shivji ni kichwa tukubali tusikubali isipokuwa nachoweza kusema ni kuwaomba watu kammna hawa wawe mstari wa mbele kama wameamua kijitoa mhanga kuzungumzia maswala ya siasa na utekelezaji wake. Inashangaza sana kuona watu kama Warioba, Butiku, Salim, Bilal, Prof.Shivji na vichwa vingine woote wenye mtazamo tofauti kiitikadi na chama hiki cha CCM bado ni members....Yaani inanishinda kabisa kuelewa, inabidi tu nichekee maliwatoni!
   
 20. Obuntu

  Obuntu JF-Expert Member

  #20
  Jun 28, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mkuu,

  Hapo kwenu, mbona na wewe ulikuwa unachungulia kwenye TV?

  Sijakuona hapa chini japo barabarani!
   
Loading...