Prof. Palamagamba Kabudi Aleta wawekezaji nchini

Prof. Palamagamba Kabudi Aleta wawekezaji nchini

mimi namuamini kabudi anajua kuchagua wawekezaji wazuri wa kichina,sio kama awamu zilizopita,,awamu hii tunaleta wawekezaji wazuri na kama ni bandari,tutaleta wawekezaji wa maana zaidi wajenge bandari nzuri pale ziwa victoria
Wazuri kama wale aliowasainisha mkataba wa korosho?
 
Nashauri yafuatayo;

Wawekewe kiwango cha ulipaji wa mishahara na iwe ni lazima kuajiri idadi flani ya watanzania. Hii itasaidia kutoa ajira na kuongeza mzunguko wetu wa fedha.

Kipaumbele kiwekwe kwenye uwekezaji ambao malighafi inapatikana hapa kwetu na si kutoka nje. Wachina wengi wanakuja kwetu kuwekeza kwenye biashara ambazo malighafi zinatoka kwao. Yaani ni kama vile wanakuja kutafuta masoko ya bidhaa za viwanda vyao na hivyo wanakuwa hawisaidii nchi kupata fedha za kigeni.
Mchina ni binaadam tu kama binaadam wengine. Ukiwa huna uelewa na unachotaka na hukidai, kama binaadam mwingine yeyote, atakichukua.

Tanzania tuna udhaifu mkubwa sana wa kutambua na kujua tunataka nini hasa tunapoingia kwenye mazungumzo ya mikataba ya kibiashara. Mi nadhani ni mhimu sana pawepo na uimarishaji wa watu wetu wanaotuwakilisha katika maswala haya ya makubaliano na mikataba. Tuwe na watu wanaotambua kwa wazi kabisa maslahi ya nchi yetu na kuyasimamia ipasavyo.

Sawa, hata katika 'ushauri' ulioutoa hapo, mimi ningekazia sana sana katika ujuzi wa watu wetu. "Skills, knowledge and technology Transfar" viwe ni vipaumbele namba moja kwa watu wetu.
Ni wakati mwafaka kabisa wa kulitilia nguvu jambo hili sasa. Tunataka nasi tuwe na uwezo wa kutengeneza vitu, hata kama ni vya ku'copy'. Siku hizi huwezi kutafuta mashine ya aina yoyote China ukashindwa kuipata. Jambo walilofanya kwa ufanisi mkubwa ni ku-'copy'. Hata kama zitakuwa ni mbovumbovu, lakini ndio hivyo, jamaa wamekwishapiga hatua moja mbele na hatua ya pili ni kuzifanya hizo mbovu ziwe imara zaidi.

Nitoe mfano: Sasa hivi tunajiandaa kuwa wauzaji maarufu wa 'Graphite' duniani. Madini haya tunayo mengi ya kutosha hapa nchini, China nao wanayo, lakini sasa wanayabania na badala yake wananunua yanayopatikana duniani, ikiwa ni pamoja na ya kwetu yatakapoingia sokoni.
Sisi hatuna mpango wowote na madini haya mbali ya mwekezaji kuyaqchimba, kuyauza nje na sisi kukatiwa hicho kiasi tutakachokuwa tumekubaliana na mwekezaji kama haki yetu. Mbali ya hapo, huko serikalini wana mawazo gani.

Haya ni madini, sio kama Almasi au Dhahabu, ambavyo ni vito, kwa jumla. Graphite ni madini ya kutengenezea vitu, hadi 'Peseli'. Ni nani asiyejua penseli! Nchi hii huagizwa penseli ngapi kwa mwaka? Ukisema tunaigia 'Digitali' na hatuhitaji penseli tena nitakukatalia kama nitakavyokata karatasi kutokuwepo tena.
Hata penseli nchi hakuna anyeweza kuzitengeneza hadi tuagize nje? Na sasa kwa vile haya madini yapo hapa hapa kwetu, inakuwaje hata tusiweze angalau kutumia masalia (reject) mtu akatengeneza penseli?
Graphite ina matumizi mengine ya mhimu zaidi kuliko hizo pensele, ndio sababu yanatafutwa kwa bei nzuri duniani, hasa ile ya kutengeneza betri n.k.; lakini pia tuna chuma hapa, kule Liganga, mchanganyiko wa chuma na graphite kunatoka mali nzuri ya kutengeneza vitu mbalimbali.

Nisiwachoshe. Mimi nashauri, hawa wawekezaji wanaokuja kuwekeza hapa hasa katika madini wasiwe wa kuchimba tu na kuuza nje.
Tuwakaribishe kwa wingi wanaoweza kuja hapa kuwekeza katika kuongeza thamani ya madini yetu hapahapa. Chuma chetu na 'alloys' mbalimbali na nickel na hiyo graphite, hata majirani zetu wanaounganisha magari, kama Kenya, tutawatengenezea baadhi ya vipuri na vifaa hapa hapa tukiwa na soko la bwerere!
Ndio maana nakazia tuwe na watu wetu watakaokuwa na uwezo wa kuvitengeneza vitu hivi, wakishapata ujuzi huo toka kwa waajiri wao wawekezaji.

Tuache woga, lakini tuwe makini katika kupigania tunachokitaka na ambacho ni stahiki yetu.
 
Kama balozi wa US alivyosema siku walivyo kutana maneno mengi tunataka tuone vitendo mpaka sasa hatujaona uwekezaji ni maneno tu.
Linalosikitisha ndio hilo, maneno mengi, lakini vitendo vikiwa tofauti.
Mfano mzuri ni hii miswada ya sheria inayopelekwa Bungeni kwa Hati ya Dharura. Tulilazimishwa kurekebisha ile ya Takwimu na wakubwa; lakini sijui kama marekebisho yanayofanyika yatakidhi mahitaji.
Hawa wawekezaji na hao World Bankna IMF, na wengineo huwezi kuwadanganya kama unavyoweza kuwapigia propaganda waTanzania hapa na kuwaburuza upendavyo.
Kama unaahidi kubadilisha mienendo yako, huna budi ubadilike kikwelikweli, vinginevyo utaendelea kuwa sehemu isiyovutia wawekezaji.
 
Ama kweli Tanzania haiishi vioja!! Hawa wachina si ndiyo juzi juzi mmesema wana mikataba ya kinyonyaji, watu waliotaka kuwajengea viwanda na bandari ya Bagamoyo? Leo mnaenda tena kwao wanyonyaji hawa hawa na maombi ya kujengewa viwanda? Huyu mtu wa jalalani, kwa nini hakurekebisha mkataba na ukafanana na utashi wa nchi? [emoji16][emoji16][emoji16], ama kweli uskistaajabu ya Musa utaona ua Kala Magamba Kabundi
Hivi ni akili hamna au ni pumba tu za kisiasa? Mkataba ndio ulikuwa wa kinyonyaji huwezi kusema taifa zima la China lilikaa kuunda huo mkataba.

Mna reason capacity ya kuku.
 
Waziri wa Mambo ya Nje Prof Palamagamba Kabudi amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Uwekezaji wa China-Africa Development Fund Ndugu Wang Yong leo Beijing. Mfuko huo umeelezea nia ya kuwekeza katika ujenzi wa maeneo ya viwanda pamoja na mradi wa bomba la mafuta.

Image

View attachment 1136398
Hawa watu ni wajinga sana, mahitaji ya wawekezaji hawa yatakuwa tofauti na ya wenzao waliotaka kuwekeza Bandari ya Bagamoyo? Serikali ya awamu ya 5 ya CCM ni ya kijinga sana wallah dah😅
 
Hivi ni akili hamna au ni pumba tu za kisiasa? Mkataba ndio ulikuwa wa kinyonyaji huwezi kusema taifa zima la China lilikaa kuunda huo mkataba.

Mna reason capacity ya kuku.
Ni kweli hapa ndipo tulipofikishwa, reasoning ya viongozi wetu ndiyo inatuongoza,.kama mkataba ulikuwa na kasoro si mnakaa na ku negotiate na kukubaliana? Kwama ulikuwa wa kinyonyaji,.mngeufanya wa kijamaa, na maisha yakaenda. Mimi nafikiria tu, na wewe umo katika kutokufikiria.
 
Waziri wa Mambo ya Nje Prof Palamagamba Kabudi amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Uwekezaji wa China-Africa Development Fund Ndugu Wang Yong leo Beijing. Mfuko huo umeelezea nia ya kuwekeza katika ujenzi wa maeneo ya viwanda pamoja na mradi wa bomba la mafuta.

Image

View attachment 1136398
Ni wachina hawa hawa?au wachina wengine?
 
Sielewi unapata wapi Taarifa au umaridadi wako wa kulifuatilia jambo kwa kina na kujiridhisha kabla ya commenting, kwamba walikaa na kufanya mazungumzo ya kipi kibaki kipi kiondoke sio hoja sababu mkataba umekua ukijadiliwa toka 2015 mpaka juzi ndio mazungumzo yalifika tamati

Kwa hiyo mazungumzo yalifika tamati ya kukubaliana kutokukubaliana ujenzi wa bandari hiyo baada ya maslahi ya Taifa kuminywa na kama unafuatilia hili suala utajua awamu iliyopita ilishampa mchina na muarabu wa Oman go ahead na jiwe la msingi lilishawekwa na fidia kulipwa.

Magufuli kaingia kaanza mazungumzo upya na hitimisho ndio hilo kila mtu anajua labda kama wewe una uwezo wa kuwashawishi wafanye kijamaa uende China utawakuta.
Ni kweli hapa ndipo tulipofikishwa, reasoning ya viongozi wetu ndiyo inatuongoza,.kama mkataba ulikuwa na kasoro si mnakaa na ku negotiate na kukubaliana? Kwama ulikuwa wa kinyonyaji,.mngeufanya wa kijamaa, na maisha yakaenda. Mimi nafikiria tu, na wewe umo katika kutokufikiria.
 
Waziri wa Mambo ya Nje Prof Palamagamba Kabudi amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Uwekezaji wa China-Africa Development Fund Ndugu Wang Yong leo Beijing. Mfuko huo umeelezea nia ya kuwekeza katika ujenzi wa maeneo ya viwanda pamoja na mradi wa bomba la mafuta.

Image

View attachment 1136398
China siyo MWEKEZAJI China ni MCHOTAJI. Hakuna wawekezaji wazuri zaidi ya nchi za magharibi. Wachina ni wezi wa kutaka kujitwalia Africa
 
Kabudi bado hana uzoefu wa biashara wala wa foreign affairs inambidi atembee polepole,hulu akielekezwa na watu waliobobea,ili kupunguza makosa yanayoweza kuigharimu nchi yetu.
 
Ngoja Wachina waje ,kuna fremu nyingi sana za Biashara Kariakoo
 
Waziri wa Mambo ya Nje Prof Palamagamba Kabudi amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Uwekezaji wa China-Africa Development Fund Ndugu Wang Yong leo Beijing. Mfuko huo umeelezea nia ya kuwekeza katika ujenzi wa maeneo ya viwanda pamoja na mradi wa bomba la mafuta.

Image

View attachment 1136398
Huyo kama Bashite. Hakuna kinachofaniwa.
 
Back
Top Bottom