Prof. Mussa Assad atoa maoni yake kuhusu Ripoti ya CAG, asikitishwa na yanayoendelea

Profesa Mussa Assad ameonyesha masikitiko yake kuhusiana na wezi wa mali ya umma wanaochekewa.

Mussa Assad aliyewahi kuhudumu kwenye nafasi ya CAG kwa mafanikio , na baadaye kuondolewa kinyume cha Katiba na John Magufuli aliyekasirishwa na kufichuliwa ubadhirifu wa kutisha wa Serikali yake, ni miongoni mwa Watanzania wachache makini sana.

Akihojiwa na Azam TV, hasa kwenye hatua za kuchukua ili kudhibiti wizi kwenye Taasisi za serikali, amesema kwamba, ziko njia mbili za haraka ambazo zaweza kuchukuliwa, mosi ametaja ni ya kuwajibisha mtu binafsi, kwamba mkurugenzi wa shirika akatwe mshahara kwa kiasi fulani kila mwezi na iwe kwa kuongezeka kila mwezi ili baada ya miezi kadhaa awe hana mshahara kabisa, anadai kwa adhabu ya namna hii viongozi wa mashirika watawajibika ili kulinda mishahara yao.

Jambo la pili alilolitaja ni kwa serikali kuwajibisha moja kwa moja wajumbe wa bodi za mashirika kwa njia itakayooneka inafaa ili wasizembee kwenye usimamizi.

Prof. Assad amesema mengi sana mazuri ambayo si rahisi kuyaweka yote hapa.

Chanzo: Azam TV

FtEFokbaAAEf1nw.jpeg


Screenshot_20230408-192357.jpg
 
Back
Top Bottom