Prof. Muhongo, TANESCO, REA na EWURA Mnaumiza wananchi

Prof. Muhongo, TANESCO, REA na EWURA Mnaumiza wananchi

Naomba kuuliza, ni vigezo gani huwa TANESCO wanaangalia ili mteja aweze kuunganishwa na Tariff?
 
Ni mwendo wa kuwaibia tu hakuna namna! Eti nilipe 50000 kila mwezi kwa umeme tu? Thubutuu
Wakati simu yako unatumia 25000/-mkeo 20000/-housegirl 5000/- asilimia 80% ya maongezi mnaongea na michepuko.umeme umekupa mwanga,kupasi nguo,kucharge simu,kuangalia habari n.k Ndiyo maana Lowassa alisema Watanzania wamekosa elimu.
 
Jamani kuilaumu Tanesco ni kuionea Ila kiukweli shirika linajitaidi kumaliza kero zote za umeme na mwisho wa siku kila kitu kitakuwa sawa na maisha yatendelea. Lakini kwa upande mwingine sisi wananchi ndo tunarudisha maendeleo nyuma kwa kuaribu miundo mbinu mwisho wa siku Umeme ukikatika lawama nyingi kumbe chanzo ni sisi wenyewe
wew ndo kilaza kweli hivi ukimwekea mtumia bei rafiki kwa matumizi ni lini huyo mwananchi ataanza kufikiria hilo la kuharibu miundo mbinu , tatizo hizi bei sio rafiki ndo maana kila siku watu wanachokonoa mita ili wapate unafuu
 
Uandishi wako tu unaonyesha ulivyo na uwezo mdogo wa kufikiri eti na wewe unajiita great thinker!
1.Uanzishwaji wa EWURA na REA upo kwa majibu wa sheria zilizotungwa na bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala sio maamuzi ya wafanyakazi wa EWURA na REA
2.Tozo za EWURA na REA zipo kwa mujibu wa sheria zilizounda taasisi hizo
3.Hakuna mabwawa ya gesi
4.Mchakato wa kupunguza au kuongeza tariff una taratibu zake ambazo zinaanzia TANESCO kupeleka maombi EWURA,EWURA kufanya analysis kulingana na maombi yalivyotumwa na kupitia evidences,Kuitisha kikao cha wadau wote na kukusanya maoni yao,kuyapitia maoni ya wadau kama yako valid na kuyaingiza kwenye analysis,kukaa exit meeting kati ya TANESCO,EWURA,EWURA CCC, Government Consultative Council, CTI n.k then mamlaka inasubmit kwa wizara husika kwa ajili ya kuidhinisha.hiyo process inapaswa iwe ndani ya siku 60.
5.Kama huzijui kazi za EWURA na REA kapitie website ufanye homework vizuri.

Watu kama nyie so full of yourselves and officialdom and pompousnes..!!
Hivi unayemfundisha hayo ni nani? wote tunayajua..... tunachosema ni kuwa tumechoka kunyonywa na serikali yetu kwa kupitia hizi agencies za ki wizi!
Kwa hiyo sikianzishwa kisheria sisi tukenuwe meno na kuchekelea!! Hivi wewe unaishi mtaa gani hasa!! Don't get me started on this....

Usidhani wewe peke yako ndo unajuwa kazi za hizo agencies.... na zilivyoanzishwa... hapa tunaongelea jinsi zinavyosababisha maisha ya tunaolalamika (you excluded) kuzidi kuwa magumu.
 
Kuanzia mwezi ujao, nadhani makato ya service charge yatasitishwa. Still gharama za umeme zipo juu sana.
 
Angalia bosi wao kazi kunenepesha mashavu tu,uongo mwingi na msururu wa miradi ya kusadikika.
 
Hivi tulipo danganywa kuwa upatikanaji wa umeme sasa utakuwa stable ni karibu mwaka sasa na hali inayo tokea sasa jijini isiyo tolewa taarifa ndio tusemeje kama ni kukamua majipu basi ni kwa kuchagua watu sio wote.
 
tumeambiwa mda mrefu kuwa tanesco wamepeleka maombi yakushusha bei ya umeme kwa EWURA hadi saa ivi hatujasikia badiliko lolote, service charges za kila mwezi ni wizi tu wanazidi kutukamua wananchi wao hawalipii gharama za umeme, ewura 1%, rea 1% zoooote za nini mnatuumiza kwa kweli wananchi kwani hakuna vyanzo vingine vya mapato? mnatulenga sisi wananchi huu sio uungwana wajameni, sijui ni ujamaa wa chura? kilio chake kinaenda na maji

Binafsi nadhani tatizo kubwa lipo kwny service charge ambayo hata computation yake haieleweki. Kuhusu 3% ya REA wakuwalaumu ni wabunge wetu ndio waliopitisha kiwango hicho. Kuilaumu Tanesco moja kwa moja katika hili ni kuionea. Hakuna charge yoyote inayokuwa initiated na Tanesco, badala yake serikali hupeleka miswada hiyo bungeni na wabunge ndio wanaopitisha.

Tukumbuke jinsi wabunge wa upinzani walivyopiga kelele juu ya kupandisha bei ya mafuta ya taa kwa hoja kuwa itasaidia kuthibiti uchakachuaji. Pia, mapato yatakayopatikana kama kodi yataelekezwa kusambaza umeme vijijini ili ku-replace matumizi ya mafuta ya taa. So, taasisi hizi zisilaumiwe moja kwa moja bali kunauzembe wa mihimili mingine kuto wajali wananchi/consumers.
 
Tuliahidiwa gesi ikianza kutumika umeme utashuka sana bei kumbe bei yenyewe asilimia moja kumbafff tumechoka kutapeliwa jinsi unavombana mlaji ujue ndio anavozidi kubuni namna ya kuiba zaidi

Mkuu umeongea vizuri sana.
 
Uandishi wako tu unaonyesha ulivyo na uwezo mdogo wa kufikiri eti na wewe unajiita great thinker!
1.Uanzishwaji wa EWURA na REA upo kwa majibu wa sheria zilizotungwa na bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala sio maamuzi ya wafanyakazi wa EWURA na REA
2.Tozo za EWURA na REA zipo kwa mujibu wa sheria zilizounda taasisi hizo
3.Hakuna mabwawa ya gesi
4.Mchakato wa kupunguza au kuongeza tariff una taratibu zake ambazo zinaanzia TANESCO kupeleka maombi EWURA,EWURA kufanya analysis kulingana na maombi yalivyotumwa na kupitia evidences,Kuitisha kikao cha wadau wote na kukusanya maoni yao,kuyapitia maoni ya wadau kama yako valid na kuyaingiza kwenye analysis,kukaa exit meeting kati ya TANESCO,EWURA,EWURA CCC, Government Consultative Council, CTI n.k then mamlaka inasubmit kwa wizara husika kwa ajili ya kuidhinisha.hiyo process inapaswa iwe ndani ya siku 60.
5.Kama huzijui kazi za EWURA na REA kapitie website ufanye homework vizuri.
Wakuu huyu Engeez ndo mtu gani. Watu tunalia na maisha huyu anatuambia habari ya sheria. Very stupid , kwani kitu kusomeka kwenye sheria ndo wananchi kuridhika??? Sheria hii ni kandamizi afu wananchi hawakuhusishwa watunga sheria ndo kina prof Maji marefu na Airo . It seems huyu jamaa ni mnufaika na ewura and the like. Bora unyamaze kuliko kuwapuuza watu na machungu yao and wacha nile ban. WE'RE NI MSALITI NA MS..ENZI SANA
 
Tunataka Kuona hawa waandishi wa habari na wanaotakia mema wananchi wao kama tutaisikia habari hii
TANESCO, REA na EWURA hawa ndio wana fanya maisha yanakuwa magumu

Kwa anaejua Uogngozi wa Juu EA na EWURA atutajie majina yao vyeo na kama mishahara inajulikana

ili watumbuliwe hawa

Itumbueni serikali na Bunge wana
wewe umetumwa nini wanaitahidi nini wakati hao ndio waliokuwa wanaleta mikataba ya hovyo na mpaka sasa wananchi ndio tunaumia unafikiria umeme ukiwa bei cheee nani ataiba na kuwa na sheria ngumu na zinafuatiliwa

weweeeeeeeeeeeee


Sidhani kama Tanesco on their own walikuwa na uwezo wa kuingia mkataba wowote bila maelekezo ya viongozi wa kisiasa. Haya mambo yamejadiliwa sana na vielelezo vimetolewa sana juu ya kuingiliwa na wanasiasa katika maamuzi ya mashirika mengi ya umma ikiwemo Tanesco. Sio sahihi sana kuilaumu Tanesco moja kwa moja kwa kuwa imeshindwa ku-exercise autonomy katika mipango yake. Lakini pia serikali kwa ujumla ilijisahau kuwekeza katika vyanzo vingine vya umeme licha ya dalili za muda mrefu za mabadiliko ya hali ya hewa. Kama serikali ingekuwa proactive katika kuwekeza then tusingeingia kwenye mtego wa kukodisha mitambo, ambayo kwa hali yoyote ile ni ya ghali sana duniani kote.

Kuhusu tozo za REA (3%) + EWURA (1%) = 4% ambapo katika kila shilingi 100 ukitoa REA na EWURA unabakia na sh. 96 binafsi sioni kama ni mzigo sana. Tatizo lipo kwenye service charges ambazo kiwango chake na calculation yake haipo clear. Lakini pia naona tunaziandama sana taasisi kama REA na Ewura wakati makato makubwa ni VAT ambayo ni 18%
Just imagine kama VAT na sercice charge zingeondolewa hususani kwa wateja wa kipato cha chini, tusinge-feel huo mzigo wa kununua umeme kwa bei juu.
 
Ccm haiwezi kumaliza wizi na ufisadi maana ni mfumo ni sio ishu ya mtu mmojammoja..
 
Huu umeme hapa mjini dsm tu hautoshi huko vijijini utatosha kweli. Tuache masihara kwenye suala la msingi umeme uko juu ndio maana watu wanachakachua
 
Uandishi wako tu unaonyesha ulivyo na uwezo mdogo wa kufikiri eti na wewe unajiita great thinker!
1.Uanzishwaji wa EWURA na REA upo kwa majibu wa sheria zilizotungwa na bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala sio maamuzi ya wafanyakazi wa EWURA na REA
2.Tozo za EWURA na REA zipo kwa mujibu wa sheria zilizounda taasisi hizo
3.Hakuna mabwawa ya gesi
4.Mchakato wa kupunguza au kuongeza tariff una taratibu zake ambazo zinaanzia TANESCO kupeleka maombi EWURA,EWURA kufanya analysis kulingana na maombi yalivyotumwa na kupitia evidences,Kuitisha kikao cha wadau wote na kukusanya maoni yao,kuyapitia maoni ya wadau kama yako valid na kuyaingiza kwenye analysis,kukaa exit meeting kati ya TANESCO,EWURA,EWURA CCC, Government Consultative Council, CTI n.k then mamlaka inasubmit kwa wizara husika kwa ajili ya kuidhinisha.hiyo process inapaswa iwe ndani ya siku 60.
5.Kama huzijui kazi za EWURA na REA kapitie website ufanye homework vizuri.


wewe inaonekana umetumwa kuna mtu humu anatakujua EWURA na REA inafanya kazi gani? hakuna alikuomba jipu weweeeee

Kwani hao wabunge si majipu ukiwa na weweeeeeeee jipu kubwa

watu humu wanaongelea maisha maisha yalivyokuwa magumu kwa ajili ya Majupu na mafisadi wenzako
 
Wakuu huyu Engeez ndo mtu gani. Watu tunalia na maisha huyu anatuambia habari ya sheria. Very stupid , kwani kitu kusomeka kwenye sheria ndo wananchi kuridhika??? Sheria hii ni kandamizi afu wananchi hawakuhusishwa watunga sheria ndo kina prof Maji marefu na Airo . It seems huyu jamaa ni mnufaika na ewura and the like. Bora unyamaze kuliko kuwapuuza watu na machungu yao and wacha nile ban. WE'RE NI MSALITI NA MS..ENZI SANA
Tengeneza hoja, punguza jazba, Kwani Prof.Majimarefu na Airo wamechaguliwa na nani?si ni wananchi nyie wenye maisha magumu ndio mmewachagua?Ili ubadilishe hizo formalities ambazo zinasababisha EWURA na REA wapewe 4% inabidi uanzie kwenye sheria ya Umeme ya mwaka 2008, Sheria ya EWURA na Sheria ya REA. na pia tariff review ina regulation zake huwezi kuiharakisha bila kufanya adequate analysis ndo maana imepewa siku 60. Watu wataendelea kupuuzika na kudharaulika endapo wataendelea kuchagua wabunge wasioweza kuweka manufaa ya nchi mbele bila kujua wao ndo waathirika wakuu wa mifumo inayotokana na wabunge vilaza.
 
wewe inaonekana umetumwa kuna mtu humu anatakujua EWURA na REA inafanya kazi gani? hakuna alikuomba jipu weweeeee

Kwani hao wabunge si majipu ukiwa na weweeeeeeee jipu kubwa

watu humu wanaongelea maisha maisha yalivyokuwa magumu kwa ajili ya Majupu na mafisadi wenzako
Wewe ni kishoka au kilaza si bure! kwenye post yako umesema hao EWURA na REA wanafanya kazi gani hadi wapate hizo percent ukaweka alama ya kuuza?Ukasema kwenye hotuba ya rais alisema "mabwawa yamejaa gas", pia ukasema TANESCO imeomba kupunguza bei EWURA haijibu chochote, kwa hiyo nilikuwa nakusaidia ili usiwe 'TAJIRI KICHWA SANA"
 
Back
Top Bottom