Prof. Muhongo, TANESCO, REA na EWURA Mnaumiza wananchi

Bontowar

JF-Expert Member
Feb 21, 2009
520
53
Prof. Muhongo tokea umeingia umekagua mashine zoote za kutumia maji nakuongele suala la bei ya umeme kwamba Tanesco wanazalisha umeme kwa bei ndogo Sanaa lakini tunaona halifanyiwi kazi .Pia tunaona Tanesco walituma punguzo la service charge EWURA mpaka leo hakuna Majibu sasa mnaonyesha slogan ya HAPA KAZI TU inapuuziwa.

Pia tunaon hawa REA, EWURA wanawekwa kwa nini kwenye malipo hapa? kwa kazi gani wanayofanya wakati VAT ipo hapo. Huu ni unyonyaji na kutia ugumu wa maisha.

Rais Magufuli siku ya kuweka Jiwe la msingi kwa ajili ya kinyerezi 2 alisema GAS ipo Mabwawa yote yamejaaa sasa sijui kwa nini mnatuumiza

CHARGES ZA TANESCO

  1. Sercive Charge (TSh.5520)
  2. VAT (18%) ambayo bado ni kubwa saanaaaaa
  3. EWURA (1%)Huyu tunamlipa kwanini wakati VAT tunalipa? Tunaomba kitolewe kama wizara haiwezi kufuatilia watumbuliwe
  4. REA (1%) Huyu ndio hatumuelewi kabisaaaa anafanya nini hapa na analipwa kwa sababu gani ? Tunaomba kitolewe kama wizara haiwezi kufuatilia watumbuliwe

Au ndani ya REA, EWURA tunawalipa IPTL?

Umeme we elfu 20000 ati unapewa unit 36

Rais Magufuli uliahidi kufuta kodi za hovyo zinazo kandamiza watu tunaomba hizi zitolewe
 
Siyo EWURA, REA ,SUMATRA au sijui nini na nini! Huu utitiri wa hayo mawakala wa serikali ni kumwongezea mlaji ama mpata huduma gharama za bure. Sasa watu hawalali wakifikiri jinsi ya kubuni wakala wa serrikali ili wale. Tusishangae kusikia wakala wa serikali wa kipindupindu, Ukimwi, mwenge, nyama, udongo, taarabu, mapenzi na hata siasa nk. Tusubiri
 
Mkuu, hao Mawakala wapo, sio wa kusubiri, labda wewe hawafahamu au hujakuatana nao katika majukumu yako. Ni hawa hapa: Wakala wa Serikali wa kipindupindu - Idara ya Maafa; Ukimwi - TACAIDS; mwenge - Idara ya Vijana; nyama - Wakala wa Vipimo; udongo - SUA; taarabu - BASATA; mapenzi - RITA; siasa - Msajili wa vyama vya Siasa.
 
Prof. Muhongo tokea umeingia umekagua mashine zoote za kutumia maji nakuongele suala la bei ya umeme kwamba Tanesco wanazalisha umeme kwa bei ndogo Sanaa lakini tunaona halifanyiwi kazi .Pia tunaona Tanesco walituma punguzo la service charge EWURA mpaka leo hakuna Majibu sasa mnaonyesha slogan ya HAPA KAZI TU inapuuziwa.

Pia tunaon hawa REA, EWURA wanawekwa kwa nini kwenye malipo hapa? kwa kazi gani wanayofanya wakati VAT ipo hapo. Huu ni unyonyaji na kutia ugumu wa maisha.

Rais Magufuli siku ya kuweka Jiwe la msingi kwa ajili ya kinyerezi 2 alisema GAS ipo Mabwawa yote yamejaaa sasa sijui kwa nini mnatuumiza

CHARGES ZA TANESCO

  1. Sercive Charge (TSh.5520)
  2. VAT (18%) ambayo bado ni kubwa saanaaaaa
  3. EWURA (1%)Huyu tunamlipa kwanini wakati VAT tunalipa? Tunaomba kitolewe kama wizara haiwezi kufuatilia watumbuliwe
  4. REA (1%) Huyu ndio hatumuelewi kabisaaaa anafanya nini hapa na analipwa kwa sababu gani ? Tunaomba kitolewe kama wizara haiwezi kufuatilia watumbuliwe

Au ndani ya REA, EWURA tunawalipa IPTL?

Umeme we elfu 20000 ati unapewa unit 36

Rais Magufuli uliahidi kufuta kodi za hovyo zinazo kandamiza watu tunaomba hizi zitolewe
Msing'ang'anie service charge tu kuna hii kitu wanaita tariff ni tatizo kubwa Wateja wote tunastahili kuwekwa tariff 4.haiingi akilini mtu ukinunua umeme mwingi unauziwa kwa gharama kubwa nawashauri Tanesco igeni tabia ya kampuni za mafuta au simu kujua umeme kadri utumiavyo na si bei hovyohovyo.
 
Mkuu suala tariff ni mdudu mkubwa sanaaaaaaaaaaaa wananchi hatujui wakati kila siku ukinunua wanakupiga faini sasa sisi tuta juaje

na utaona waandishi wa habari hawatalitoa kwenye magazeti kabisaaaaaa
 
Kitu service charge kinaniumiza sana hapa home mwez uliopita nanunua umeme wa elf 15 napewa unit 11 nizaid ya maajabu.
 
EWURA sio msaada kwa wananchi, ni muendelezo wa vitengo vya kuwapa ajira washkaji zao na kupigia ufisadi, kiuhalisia haina tija na kina yakhe.
 
JPM kama kuna suala angelipa maamuzi ya haraka ni bei ya umeme kwa mtumiaji.
Umeme unatugharimu sana kuna wizi wa waziwazi halafu tunakamuliwa wanachi fedha wanalipwa iptl na aggreko hii Haiingii akilini mishahara yenyewe midogo bado umeme una gharama kubwa.
 
Rais Magufuli tunaona swala hili lichukulie uharaka na mpaka leo haujatumbua JIPU la TANESCO

inamaana hakuna JIPU sidhani wanatuumiza sanaaa
 
Yaani hapa nina machungu hataree.... mara ya mwisho nimenunua umeme Januari, sasa jana umeisha.... kwa jinsi bajeti ilivyobana basi kila nikinunua wanagoma eti hela haitoshi, nilianza na elfu 10 ikagoma, leo nimekopa kwa jirani elfu 5 iwe 15 imegoma kisa eti nadaiwa service charge na ungese kibao... kwa nini wasinipe ila waendelee kunidai? maana matumizi ya umeme hayaepukiki. mbona Airtel wanatukopesha hadi laki? yaani Tanesco ni jipu.
 
Mnanipa machungu tu mkisema TANESCO ngoja nitulie mana sikuiz nimeamua kuiba umeme wao sio kisa napenda bali wamenilazimisha nanunua wa bk 20 ukiisha na connect wa wizi mpaka mwezi uishe mana kwa mwezi mimi natumia umeme wa elfu 20 tu ikizidi hapo na connect full stop, najua kunikamata ni ngum mana mi mwenyewe mtahalamu
 
Kweli Kabisa Mkuu, Kati Ya Vitu Ambavyo Ni Kero Kubwa Mno Ni Hivi Vitu Na Bei Kubwa Ya Umeme (Units)!
 
Back
Top Bottom