chakutaka
Senior Member
- Feb 6, 2015
- 150
- 14
Gazeti hili katika Toleo lake la tarehe 20, Aprili, 2017 limeandika kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Msomi, Prof. Sospeter Muhongo alishiriki kikao cha tarehe 28. Septemba, mwaka jana ambacho kilijadili mpango kazi wa TANESCO ambapo gazeti hilo linadai kuwa katika kikao hicho ilikubaliwa kuwa Shirika hilo lipeleke maombi ya kuongeza bei ya umeme kwa EWURA kabla ya Septemba 30.
Mawio limeandika kuwa kikao kilishirikisha wadau kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Benki ya Dunia na TANESCO.
mimi kama Great Thinker katika pitapita zangu nimekutana na Taarifa kutoka Wizara ya Nishati na Madini iliyofafanua suala hilo, iliyotoka tarehe 13/1/2017 ikifafanua madai hayo ya kumsakama Waziri Muhongo.
sehemu ya Taarifa hiyo inaeleza kuwa ,, Tarehe 2
8/9/2016
Wizara ilifanya kikao na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia ikiwa ni
mwendelezo wa vikao vya majadiliano kuhusu upatikanaji wa mkopo wa Dola za
Marekani Milioni 200 kwa ajili ya kuboresha uendeshaji (TANESCO). Kikao hicho pia kilihudhuriwa na taasisi nyingine zikiwemo Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA).
Katika kikao hicho masuala yaliyojadiliwa yalikuwa ni;
Upatikanaji wa umeme wa kutosha, uhakika na bei nafuu kwa ajili ya kuchochea shughuli za maendeleo ya kukuza uchumi wa nchi ikiwemo viwanda, biashara, kilimo na huduma za jamii, Kuongeza ufanisi wa utendaji wa Shirika la Umeme , Kupunguza deni la TANESCO.
Hivyo, katika kikao hicho, hakukuwa na makubaliano ya kupandisha bei ya Umeme kama ilivyoripotiwa na gazeti hilo.
kwa tunaofuatilia kauli za Muhongo ni kuwa ameshatamka mara kadhaa kwamba HAAMINI KUWA MATATIZO YA TANESCO YATATATULIWA KWA KUBEBESHA MZIGO WA WANANCHI KWA KUWAPANDISHIA BEI YA UMEME NA HATA WATENDAJI WA TANESCO WANAELEWA MSIMAMO HUO WA MUHONGO.
NI VIZURI MAWIO LIKASAKA TAARIFA SAHIHI KWA WATOA HABARI WAKE KWANI GAZETI HILI LINAJIPOTEZEA HESHIMA KWA KUANDIKA HABARI ZA KUPIKA ZISIZO NA USHAHIDI WA KIMAANDISHI, SAUTI AU VIDEO.