Prof. Muhongo atizamwe kwa jicho la tatu tusije tukapoteza jembe?

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Licha ya kuandamwa na kashfa za madini na escrow kuna umuhimu huyu mtaalamu akaangaliwa kwa jicho la tatu Kwa sababu bado nina amini huyu mzee ni jembe na mchapakazi......

Huyu mzee Nakumbuka ndio aliolinuaa shirika la tenesco na pamoja utaratibu wa umeme vijijini
Na hadi leo karibia asilimia 80 vijijini kuna umeme kwa sababu yake pamoja na kuinua shirika la tanesco hii muhimu sana ?

Ikumbukwe ya kwamba hata wiliam ngeleja alivyoondoka hii wizara huyu mzee ndio mtu pekee alipigana kulinua hili shirika....

Hivyo ushauli wangu huyu mtalaamu aangaliwe kwa macho mawili tena tusije tukampoteza badae tukaanza kulaumiana ?
 
Pamoja na yote hayo lakini ni hasara kiasi gani ambayo amelisababishia taifa?.
 
achana na muhongo muda huu atakuwa ndani ya Fly Emirates anaenda zake duniani kushughulikia issue za miamba, usichezee mtu aliyesoma mpaka mwisho.
ndio maana nikasema huyu mzee tusije tukampoteza bure
 
Kwani magu si alimsifia sana huyu jamaa na akwatukana wapinzani ma kiwaambia wajinyonge muhongo ni jembe imekuwaje leo
 
Kw jinsi alivotunyanyasa watu wa Lindi na Mtwara ususani kwenye sakata la Gas aisee Muhongo bora apotelee mbali na dharau zake....haiwezekan atandike mabomba ya Gas Kutoka huku kuelekea Dar alhali sisi tuko gizani.
 
Licha ya kuandamwa na kashfa za madini na escrow kuna umuhimu huyu mtaalamu akaangaliwa kwa jicho la tatu Kwa sababu bado nina amini huyu mzee ni jembe na mchapakazi......

Huyu mzee Nakumbuka ndio aliolinuaa shirika la tenesco na pamoja utaratibu wa umeme vijijini
Na hadi leo karibia asilimia 80 vijijini kuna umeme kwa sababu yake pamoja na kuinua shirika la tanesco hii muhimu sana ?

Ikumbukwe ya kwamba hata wiliam ngeleja alivyoondoka hii wizara huyu mzee ndio mtu pekee alipigana kulinua hili shirika....

Hivyo ushauli wangu huyu mtalaamu aangaliwe kwa macho mawili tena tusije tukampoteza badae tukaanza kulaumiana ?
Asilimia 80?!!ya vijiji vina umeme sio kweli!! Sasa aangaliwe vipi wakati kila balaa linamkuta iwe amehusika au ni kwenye wizara yake?! Ninacho weza mshauri ajiuzuru tu na ubunge akafanye kazi yake huko ulaya kwani matatizo ya Tz ni mfumo na wala sio mtu mmoja mmoja!! Sekta zote zilioza hakuna kwenye unafuu, leo ukienda maliasili nako ni balaaa!!
 
Back
Top Bottom