Prof Mbele: Usomi haukamiliki bila kejeli na dhihaka?

Professa Mbele ana points na hoja ya maana lakini hajazipangilia hoja zake vizuri kwasababu kuna lots of contradictions,anasema suluhisho la kutokukaa vijiweni nk ni kusoma,je waliosoma si ndio mafisadi waliotufikisha hapa.

Ni kweli utamaduni wa mtanzania ndio huo wa kukaa vijiweni na kupiga soga,sasa viongozi wanahamasisha ama wao ni kusema sisi ni masikini kila kukicha?Kama viongozi wanasema ili tuendelee inabidi tuwe omba omba unategemea wananchi wawe kitu gani?

Kwanini huyu professa anatumia upuuzi kiasi hiki kusapoti status quo bila constructive points?

Anazungumzia kuhusu ujuzi na maarifa ie knowledge economy,sasa nani kamwambia professa kuwa ni lazima kila mwananchi awe na ujuzi na maarifa ili Taifa liendelee?.

Ni wazi kuwa matatizo tuliyonayo yanachangiwa sana na utamaduni,je viongozi wameshachukua hatua gani ili kujiwekea misingi ya kuachana na tamaduni mbovu zenye kuturudisha nyuma?

Professa huyu inaonyesha wazi kuwa anawarundikia wananchi lawama zote kutokana na mwenendo wa Taifa letu,mbona hajaweka short comings zozote kutoka kwa viongozi?je ana maana wao ni malaika?wasababu mara zote Professa huyu amekuwa akisema "hakuna haja ya kuwalaumu viongozi"je haya ni kweli?

Hata kama kuna ukweli kuhusu kuwaangushia wananchi lawama,sio kweli kwamba wananchi peke yao ndio vilaza kama anavyoelekea kuimply professa huyu, hatuwezi kupata maendeleo bila ya kuwashirikisha viongozi ambao ndio watatoa dira na mwelekeo.

Kwa viongozi kuspend kama Taifa tajiri na huku wakiendelea kuomba omba na pia kuwaambia wananchi sisi ni masikini,je hiyo ndiyo namna ya kuwaambia wananchi ondokeni vijiweni na muache uvivu?Nani anayesababisha "ganzi" hapo?

Eti "mkimshambulia rais,jishambulieni na ninyi" Huyu professa nina wasi wasi naye sana....Kama anajipendekeza kwa status quo,basi huo ni upuuzi wake asituletee wengine.

Sina muda wa kutosha la sivyo ningeijibu makala ya professa huyo hoja kwa hoja,ila pointi chache zinamtosha na hopefully atatafakari,ama atajiunga hapa JF ili apate changamoto...Viongozi are to blame kwasababu hawajaonyesha kulitambua tatizo kabla hata ya kujaribu kulitatua tatizo lenyewe,na kama maprofessa wa kumshauri ndio hawa,basi msimamo wangu uko pale pale kuwa REVOLUTION IS A MUST.

Mkuu hii nimeipenda sana! nimeshaandika hawa maprofesa sasa wanatumika kama masekretari wazuri kwa ccm.
Hivi huyu profesa gani asiyeelewa kuwa kiongozi anapochaguliwa kuiongoza nchi anategemewa aitoe jamii mahali alipoanzia kuipeleka mbele zaidi kwa kuibadilisha hata kimawazo licha ya kiuchumi? Kama wao viongozi walijua udhaifu wa wananchi wao kwanini hawakulifanyia kazi hilo? Huku ndiko kule kusoma bila kuelimika halafu ukawa profesa! Forget these theoreticians! Mwambie agombee ubunge watampa uwaziri sasa hivi..... while we count "Another ccm decorating secretary is born"!!

Jmushi and MpendaTz

Nimesoma post zenu naenda kuangalia movie!

why?

Because I am happy!
 
"Ufinyu wa mawazo unajitokeza hapo watu wanapodhani kuwa kazi ya kujenga nchi ni ya rais"

I guess prof has never watched Fox news!!!!!!!!!! tehe tehe!!!!!!!!!! tehe!!
 
All in all, kama ni kweli prof. ndiye aliyeandika hii habari basi tuna matatizo yanayohitaji immediate attention:

1. Prof ametoa hoja zake kwa mtindo ule ule anaoupinga......... "kijiweni style"

2. Hoja zake zimekaa kimipasho zaidi na si za kiuanazuoni. Is like anajibu barua au hotuba ya mtu fulani in "an open letter style"

3. Prof nadhani ana mentality ya kizamani ya kudhani ukiwa prof tena Marekani basi you can say whateva u want bila kupingwa.
 
Kuhusu swala la Kikwete na CCM, huyu Joseph (Mbele) angefuga mdomo aendelee kufundisha English hapo St Olaf College kuliko kuanza kujiingiza kwenye propaganda za kisiasa ambazo hana uzoefu nazo. Kama anataka kutumia elimu yake kusaidia jamii ya kitanzania kisiasa, ni afadhali angekuwa anatoa makala zake za uchambuzi kwa kiwango cha juu cha kitaaluma kama afanyavyo mwazake Isa (Shivji) kuliko kuandika kama mwanasiasa wa kitengo cha propaganda.

Tabia ya wasomi kugeuka kuwa wapiga debe wakuu wa CCM wakati wa uchaguzi imekuwa kama njia ya yao kututukana na kuua demokrasi nchini kwa vile inakuwa inachangia sana kujenga jamii ambayo haikueleimika (uninformed electorate), na imesababisha hata wananchi wa kawaida wasione maana ya elimu ya juu kwa vile CCM inayopigiwa debe na hao wasomi inajulikana kabisa kushindwa kuongoza nchi. Vile vile tabia ya namna hii inaweza kuwa inachanguia kukua kwa wanasiasa wanaojipachika udaktari wa kununua kwa sababau hawaoni tofauti yoyote baina yao na hao madaktari waliobobea kama huyu Mbele.
 
Niliwahi kukataa hoja ya reverend kwamba watanzania wengi ni wababaishaji na wala rushwa! in the same line nakataa hoja za Prof. Mbelle si kweli kwamba watanzania wengi ni wavivu na wapige sogo! hivyo nilikataa hoja ya JK kwamba kwamba wa Tanzania no wadokozi alipokuwa anaongea na mmiliki moja wa hoteli kule bagamoyo

Sababu za kutokukuabliana na JK, Mbelle na Rev. Kishoka nilizitaja napenda nirudie hapa
a) Watanzania 80-90% tunafanya kazi rural au informal sector huko watu wanahangaika, wanabuni, wanateseka usiku na mchana kusurvive hakuna uvivu..ukilala unakufa na njaa..wakati huo huo waliopewa dhamana kutuangalia kwenye mambo ya msingi kama miundo mbinu hawana habari wala hawaboreshi chochote japo kodi tunalipa????

b) JK, Mbelle na Rev. Kishoka ubabaishaji, udokozi na ufisadi wanazungumzia tabaka la wananchi wasomi na walioko mjini wanaiba serikalini, wanategea kazi ofisini, sio wabunifu nk wakiwemo wanasiasa kwenye kundi hili ambalo ni chini ya 10% ya watu mili 40!!

Hizi streotape hadi kwa Rais kwa wananchi wake eti kwakuwa amemuuliza mmiliki wa hoteli moja kwanini ameajiri mkenya akasema eti watanzania ni wadokozi..what type of sample is this? ku make judgement kwa watanzania wote? anafikiri watanzania ni malaika?

Uchambuzi huu ni feki unasathili kulaaniwa na kupigwa vita..akitaka aende mitaani na mashambani aone watu wanavyojishughulisha kipindi hiki cha kilimo?
 
Ntawajibu wote kwa mpigo!

Ni miaka karibu 50 sasa tangu tupate Uhuru wetu, kutoka makucha ya Wakoloni na Ubepari, lakini kama jamii inayojitawala, bado hatujaweza kuzinduka kutoka kwenye Usingizi wa Pono na Cherekochereko za kuelewa kwa nini tumepata Uhuru.

Tumelewa nderemo na vifijo, lakini kujituma na kujitutumua kujitumikia na kujiboresha ina kuwa ni vigumu kwetu bila kusukumwasukumwa na hivyo masikio na mategemeo yetu yote ni kuwa tutakuwa na Kiongozi fulani atakayetuletea neema kama Mana kutoka mbinguni.

Watanzania tunatabia mbaya sna ya Utegemezi na kusubiri tufanyiwe kazi au tuletewe matunda tuyafurahie. Ama ni asili yetu kutokana na Vizazi vya Mababu wa Mababu zetu waliishi maisha ya kuridhika kwa kujipatia kile cha kutosha na bila kufikiria kile cha kesho au ni dhahiri kuwa sisi ni jadi yetu kuwa Wavivu na tuna mategemeo makubwa na mengi kuliko uwezo wetu.

Suala la kusoma au kujielimisha si la mtu kwenda Chuo Kikuu, kuwa mtaaluma au mtaalamu au umahiri fulani wa kunyumbulisha au kukokotoa mambo, bali ni hata vitu vidogovidogo na dhahiri ambavyo havihitaji mtu awe na Udaktari!

Fikiria jukumu dogo sana la Uraia la mtu kuwa na uwezo wa kupima mbunge au mwakilishi wake. Je ni elimu ya daraja gani inahitajika kubaini kuwa mbunge huyu ambaye kawakilisha jimbo tangu mwaka 1965 ni mbabaishaji mwenye kauli bila vitendo, lakini kila wakati wa kupiga kura tunaruhusu udhaifu na kumpa dhamana ya kuendelea kuwa kiongozi?

Nikimsoma Mwalimu Mbele, naona nasoma fasihi ambayo ni tata na si lazima ipokelewe kuwa anaifagilia CCM au kumfagilia Kikwete. Waweza niita Ngwini, lakini mimi nimepokea anachosema Mwalimu Mbele kwa kujipima nafasi yangu kwanza kabla ya kunyooshea Serikali na Kiongozi Mkuu kidole.

Ni kweli tuna udhaifu wa hali ya juu katika safu ya Uongozi na mfumo wa Kisiasa Tanzania na inajionyesha mapokeo yake hata kwa jamii tunavyofanya mambo yetu.

Tulianza safari yetu baada ya kupata Uhuru vizuri sana kwa kuwa na mshikamano na msisimko wa kujitawala na kujiongoza. Lakini katika safari hii, hatukuwa na nidhamu au uwezo wa kuhimili safari na ugumu wa safari yenyewe kwa kuwa tulidhania kuwa kwa kujitawala na kuwa huru, basi kama Mgogo mambo ni Mswano na kama Mnyiramba tutasema ni wakati wa kujiogoga.

Mara nyingine inakuwa kana kwamba tumekwama kwenye tope au tumepotea jangwani bila kujua tunakoelekea wala kujua ni mbinu gani zinahitajika tujikwamue kutoka kwenye tope.

Tumeridhika sana na udhaifu na umasikini na kama mkimwangalia Kikwete anavyolalama kila siku kuwa hajui ni kwa nini Taifa letu ni masikini au kutokuelewa kwake yeye Kikwete kuwa vitu havipatikani kwa urahisi bali vinahitaji si mikakati tuu, bali pia ufuatiliaji, utaona taswira karibu ya kila Mtanzania inafanana na Rais wetu.

Sasa kama safu ya viongozi wetu tumeshaizoea kuwa ni ya watu kama Kikwete au kama sisi ambao hatujitumi au kujitutumua, kwa nini tuogope kumpa dhamana mtu mpya tusiyemjua ili naye tujifunze kwake? Au lile la Zimwi likujualo lina pande mbili la sisi kama Raia na Wananchi kuridhika na mfumo butu na mfumo wetu kuridhika na sisi Raia na Wananchi BUTU?

Unapokubali kuonewa na kuburuzwa kila siku bila kusimama kidete na kutunisha misuli kulinda utu wako na haki yako, daima utaendelea kuwa mnyonge na kuamini kuwa ni haki yako kuwa mnyonge. Ni mpaka pale utakapo amka na kujitutumua na kupukuta mavumbi na kuanza kutetea na kujivunia utu wako na kuweza kusimama na kuitetea nafsi yako bila woga kwa ujasiri, ndipo utakapoanza heshimika na yule aliyemnyanyasaji ama atalegeza kamba au kufungasha virago na kuondoka.

Tulipigania Uhuru kwa nguvu sana, je ili kuwa ni kwa sababu gani? Je ni ile chuki yetu ya kufanyishwa kazi na Mkoloni katika nchi yetu? mbona tabia hiyo bado tunaendelea nayo popote pale ambapo tupo nje ya kujitawala wenyewe?

Angalia Watanzania walioko Diaspora, wengi ni mahiri na wanajituma kwa bidii katika kila nyanja hata kama ni Udereva Teksi. Watanzania walioko nje ya nchi wanafanya kazi kwa kujituma, juhudi ,maarifa na kwa nidhamu za hali ya juu, inakuwaje nyumbani tunashindwa kuwa na nidhamu na mvuto ule ule wa kuwa wachapakazi hodari wenye kutumia juhudi na maarifa?

Je tutalaumu mishahara na ufinyu wa vipato? mpaka lini tuendelee kulialia kuwa tunapunjwa? Je tumeshasimama na kumhoji yule tuliyempa dhamana ya kutuongoza na kufanya mipango ya maendeleo nchini mwetu na kutaka kujua ni lini tutaona maendeleo chanya au msukumo chanya?

Wakati wa Nyerere, tulikuwa na mategemeo mengi, tuliposhindwa kupata tulichotaka (ambacho ukweli mpaka leo hatukijui), tukasema hafai na katuletea umasikini. Ndio maana kuna wengine wanaamini kwa dhati kuwa Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ndio chimbuko la Umasikini wa Mtanzania.

Akaja Mwinyi ambaye tukamshangilia kwa utawala wake unaofanana na Babu au Mjomba poa, maduka yakajaa, tukaanza kuchekelea neema ya fahari ya macho na kuimba ruksa kama vile basi tumefika ile nchi tulioahidiwa. Tukachukua bilauri na kata na kuanza kujipongeja kwa maduka na bidhaa kuongezeka, lakini sisi wenyewe kufanya kazi kujizalishia ikawa ni shida.

Mkapa akatuambia sisi ni wavivu na wenye wivu, tukakasirika na kuzira, akahamasisha mipango ya sisi kujihujumu wenyewe na kuwa Taifa linalotegemea uagizaji na si uzalishaji wa ndani kama vile Mwinyi alivyofanya, tukanyamaa kwa miaka 10 akishirikiana na wenzake ambao walishaamini kuwa sisi ni Zimwi liliwalo, haliwezi kwisha kulika kutokana na UBUTU wetu, na kama zawadi ya kazi nzuri aliyofanya ambayo imelihujumu Taifa, akahakikisha tunapewa mtu dhaifu kama kiongozi na tukampokea Kikwete kwa vifijo na nderemo!

Sasa Kikwete kafanya lile tulilojua mapema na kwa hiari tukampa dhamana, leo tunahamaki?

Msishangae kwa Mchungaji kuunganisha nafsi yake katika kujisuta pamoja na kuwa wengi wenu mnamshangilia anavyomchambua Kikwete na uongozi wa CCM. Siwezi kujitoa kutoka lawama kisa nimeandika s c r ew Muungwana au Ajizi ya Kibuge.

Ninachofanya ni kukubali wazi kuwa sisi kama jamii, tutaendelea kutaabika mpaka pale tutakapoanza kubadilisha mienendo kwa kujipima wenyewe kwanza, kujihakiki na kujiwekea nidhamu na malengo katika ubinafsi na nafsi zetu kama mtu mmoja mmoja, ndipo tutakapoweza kwenda kwa umoja kama Taifa.

Lakini, nimewahi kuuliza mara kadhaa hapo awali, je tafsiri ya Mtanzania ya maendeleo na utajiri ni nini? sijapata jibu la uhakika na hata kama leo tutasoma majedwali ya kimataifa yanayoonyesha viwango vya umasikini na utajiri, je tunavielewaje kwa nafsi zetu na mazingira yetu?

Mmeuliza kwa nini nilihoji watu kukaa vijiweni Dar, nitawaambia hili, pale Dar na hata mikoani ambako niliona watu wakiamka asubuhi kwenda kulibwia tembo na si kufanya kazi, kuna nafasi nyingi sana za Watanzania kuweza kujiendeleza kiuzalishaji mali na si lazima iwe kwa kupitia kuajiriwa.

Ndio maana nikakaa chini na kuhoji kama tulilipokea Azimio la Arusha kwa makosa na hivyo sera za Ujamaa na baadhi ya vipendele tulivyoviimba kwa nguvu kuwa hatutaki Ubepari au watu binafsi kuwa wazalishaji huru ni sehemu moja na nyeti inayohusiana kwa kiwango kikubwa na Umasikini, Unyonge na Udhaifu wa Mtanzania (na hili la UUU ni kwa mtazamo wangu, mtu mwingine anaweza kusema karidhika na alichonacho na hana tatizo!).

Hivyo, binafsi, Mwalimu Mbele, JMushi, Tumain, Mwanakijiji na Michuzi tunajukumu la kujihoji nafsi na kujichambua na kujipima je tunajipimaje kama wananchi na ni halali kwetu kuelekeza vidole vyote vya lawama kwa mtu mmoja au Serikali bila kuhoji nafasi yetu katika matatizo yanayotukabili?

Uchanga wa Tanzania na Watanzania na ufinyu wa upeo, si jambo la kupuuziwa, na ndio maana Mzee Mwanakijiji ana kampeni ya kuleta mabadiliko mwaka huu. Lakini mabadiliko si kumuondoa Kikwete na kutuletea Mwakyembe kisa eti tunapiga vita Ufisadi. Je tukimwondoa Kikwete na kumleta Mwakyembe, Sitta, Lipumba au Sitta basi ndipo tutabadilika fikra?

Nakumbuka wakati Mzee Mwinyi na Azimio la Zanzibar lilipokuja, nakumbuka suala la cost sharing lilipokuja, sisi tulidumaa na kupoteza nafasi muhimu kuhoji madhumuni na mbinu zitakazotumika katika mfumo huo mpya. Kama bendera inayofuata upepo, tukaridhika kimya kimya na kukubali kuburuzwa bila kuelezwa kinagaubaga kuwa mabadiliko haya yana maana gani na kwa manufaa ya nani?

Imekuwa ni kawaida yetu, kutafuta mchawi wa kumtupia lawama. Kikwete ana gunia elfu za lawama kutupiwa, CCM ina magunia laki ya lawama kubebeshwa, lakini mimi, wewe na yule na wote katika nafsi yetu ya binafsi kama mtu mmoja mmoja na kwa umoja kama Taifa, tujitwishe magunia yetu Milioni kadhaa ya lawama!
 
Rev, nadhani umerudi palapale unampiga mbwa aliyekufa

Sijaelewa ulichoandika hapa ni kwa nani hasa , maana naona kuna uwezekano mkubwa tukawa tunaongelea group dogo la watu.

Kumbuka article yako imelenga hasa kwa watu waliosoma , wenye upeo na uwezo wa kufanya mambo lakini hawafanyi. kule vijijini ukisema ulichosema hapa unawaonea sana.

well, nakubaliana na wewe swala la kutokuwa makini katika kuchagua viongozi ambao ni ugonjwa wa waliosoma na wasiosoma, waliosoma wengi huchagua viongozi wakilenga matakwa yao, na wasiosoma wanachagua viongozi as a civil duty! na hii ndio unaitumia kama fimbo ya kuwachapa watanzania wengi. Ni kama vile unasema mtoto akililia wembe mpe, au asiyesikia la mkuu huvunjika guu! au sikio la kufa halisikii dawa! yaani unachokisema viongozi wanajua na wanatumia mwanya huo huo kuwalalia watanzania! what a shame!,(Msekwa alisema zaidi ya miaka 20 ijayo CCM watakuwa kwenye power)! hali hakijua wao mafisadi! ni sawa na mzee wa miaka 40 analala na mtoto wa miaka 15 halafu anajitetea alikubali mwenyewe! what a shame!

These some people need to be educated, believe me watanzania wako receptive. Ndiyo hao hao walikuwa nyuma ya Mkwawa wakati anawaponda wajerumani, ndio waliokuwa nyuma ya Rumanyika, Kimweri, Mirambo, Mputa, ndio hao walikuwa nyuma ya akina Mangi sina na mandara! Hawa watu hawajalala fofofo; wana akili , kuna sababu hatutaki kuisema hapa!

1995 Mrema aliweza kuleta moto na ukawaingia watanzania wengi, ilikuwa miaka 3 tu baada ya mfumo mpya kuingizwa! Today tukimpata kiongozi mmoja tu 'kichaa' awaamshe watanzania wataamka! Lakini ndio hivyo, matapeli ndio wanajiita wapinzani!, ukienda makanisani na misikitini CCM wako huko. Mtanzania hana sehemu ya kukimbilia-tukiwaza vita nani atatupokea??! watu wanatumia asili, tabia na culture kumnyonya mtanzania. Kwa nini haukubali kuwa waliosoma hapo zamani ndio wanatudanganya, na ndio waliotakiwa kuwaamsha watanzania? Just

Imagine Nyerere angekuwa na msimamo kama wako mwaka 1961!!! au unafikiri msimamo wa Nyerere wa kusomesha watu leo is obsolete??

Ona watoto wanavyohangaika kupata mkopo tu! wakati akina Dr. Rashid na akina Chenge wanafanya deal la radar , gavana anawaza kujenga paradiso! kesho ukiingia mtaani uandamane FFU hao!

Nimefurahi umezungumzia kujisomea! hii pia ni utamaduni mkuu, Rev. umeshawahi kwenda kijijini kwenu kuhimiza watu wajisomee? serikali imeshawahi kuhamasiha hili swala, Yaani form no where mtu ataanza kujisome tu wakati hajui manufaa ya kujisomea?? umeshawahi kuona familia ya wasomi yenye watoto wasiosoma??

Umasikini, Unyonge na Udhaifu ulivyosema vyote vina vyanzo vyake!
Meseji zenu zimelenga kwa watu fulani, hazijalenga taifa kwa ujumla,

Nimekuwa nikiandika post, kuwa watanzania na Tanzania hatuna shida saaana ya kuwafanya watu waamke! tutaamka siku mali asili zikiondoka, neema ikiisha, ukame, shida ya maji, njaa. Siku ambayo asilimia 80 ya watanzania watakosa mahitaji muhimu ndiyo tutaamka! This is absolute true! but we dont need to wait till that day! leaders , I repeat Leaders should see this , sould deal with these behaviour and change it!

Viongozi wanalinda maslahi yao, hakuna atakayesema hawa jamaa tuwaamshe, hii ni mbaya sana!

Asante umesema ile article ya Mbele umejiangalia na kujipima! unafikiri mtanzania aliyeko Bukoba, kahororo, kijiji cha Kabare atajipima kwenye kioo gani! nadhani watu tu kujiunga vyama vya upinzani ni dalili nzuri kabisa kuwa wanataka mabadiliko! what failed them is strategy and real leaders!

wapinzania ndio hawa tulionao-wamelala. Imefika wakati jamii hii imekata tamaa, guess what, jamii ikikata tamaa , violence zitaongezeka, ole wao kwa watawala maana wao watakuwa wa kwanza kutafutwa!

Unless kama unasuggest indirectly kuwa kwa Tanzania vita ndio suluhisho!

Hiyo article yako inanifaa mimi na JF members wengine wote. Lakini hamfai kijana wa kijijini asiyejua what is real going on in this planet!

Nimeandika hapo awali,baadhi ya hawa watu hawajui jinsi ya kuchagua viongozi, hawajui kuwa ni wavivu, hawajui kuwa hawana elimu, hawajui kuwa wamelala, yaani kwa kifupi hawajui whats up in this world, ndio hao hao unataka wajiamshe
 
Ntawajibu wote kwa mpigo!

Ni miaka karibu 50 sasa tangu tupate Uhuru wetu, kutoka makucha ya Wakoloni na Ubepari, lakini kama jamii inayojitawala, bado hatujaweza kuzinduka kutoka kwenye Usingizi wa Pono na Cherekochereko za kuelewa kwa nini tumepata Uhuru.

Tumelewa nderemo na vifijo, lakini kujituma na kujitutumua kujitumikia na kujiboresha ina kuwa ni vigumu kwetu bila kusukumwasukumwa na hivyo masikio na mategemeo yetu yote ni kuwa tutakuwa na Kiongozi fulani atakayetuletea neema kama Mana kutoka mbinguni.

Watanzania tunatabia mbaya sna ya Utegemezi na kusubiri tufanyiwe kazi au tuletewe matunda tuyafurahie. Ama ni asili yetu kutokana na Vizazi vya Mababu wa Mababu zetu waliishi maisha ya kuridhika kwa kujipatia kile cha kutosha na bila kufikiria kile cha kesho au ni dhahiri kuwa sisi ni jadi yetu kuwa Wavivu na tuna mategemeo makubwa na mengi kuliko uwezo wetu.

Suala la kusoma au kujielimisha si la mtu kwenda Chuo Kikuu, kuwa mtaaluma au mtaalamu au umahiri fulani wa kunyumbulisha au kukokotoa mambo, bali ni hata vitu vidogovidogo na dhahiri ambavyo havihitaji mtu awe na Udaktari!

Fikiria jukumu dogo sana la Uraia la mtu kuwa na uwezo wa kupima mbunge au mwakilishi wake. Je ni elimu ya daraja gani inahitajika kubaini kuwa mbunge huyu ambaye kawakilisha jimbo tangu mwaka 1965 ni mbabaishaji mwenye kauli bila vitendo, lakini kila wakati wa kupiga kura tunaruhusu udhaifu na kumpa dhamana ya kuendelea kuwa kiongozi?

Nikimsoma Mwalimu Mbele, naona nasoma fasihi ambayo ni tata na si lazima ipokelewe kuwa anaifagilia CCM au kumfagilia Kikwete. Waweza niita Ngwini, lakini mimi nimepokea anachosema Mwalimu Mbele kwa kujipima nafasi yangu kwanza kabla ya kunyooshea Serikali na Kiongozi Mkuu kidole.

Ni kweli tuna udhaifu wa hali ya juu katika safu ya Uongozi na mfumo wa Kisiasa Tanzania na inajionyesha mapokeo yake hata kwa jamii tunavyofanya mambo yetu.

Tulianza safari yetu baada ya kupata Uhuru vizuri sana kwa kuwa na mshikamano na msisimko wa kujitawala na kujiongoza. Lakini katika safari hii, hatukuwa na nidhamu au uwezo wa kuhimili safari na ugumu wa safari yenyewe kwa kuwa tulidhania kuwa kwa kujitawala na kuwa huru, basi kama Mgogo mambo ni Mswano na kama Mnyiramba tutasema ni wakati wa kujiogoga.

Mara nyingine inakuwa kana kwamba tumekwama kwenye tope au tumepotea jangwani bila kujua tunakoelekea wala kujua ni mbinu gani zinahitajika tujikwamue kutoka kwenye tope.

Tumeridhika sana na udhaifu na umasikini na kama mkimwangalia Kikwete anavyolalama kila siku kuwa hajui ni kwa nini Taifa letu ni masikini au kutokuelewa kwake yeye Kikwete kuwa vitu havipatikani kwa urahisi bali vinahitaji si mikakati tuu, bali pia ufuatiliaji, utaona taswira karibu ya kila Mtanzania inafanana na Rais wetu.

Sasa kama safu ya viongozi wetu tumeshaizoea kuwa ni ya watu kama Kikwete au kama sisi ambao hatujitumi au kujitutumua, kwa nini tuogope kumpa dhamana mtu mpya tusiyemjua ili naye tujifunze kwake? Au lile la Zimwi likujualo lina pande mbili la sisi kama Raia na Wananchi kuridhika na mfumo butu na mfumo wetu kuridhika na sisi Raia na Wananchi BUTU?

Unapokubali kuonewa na kuburuzwa kila siku bila kusimama kidete na kutunisha misuli kulinda utu wako na haki yako, daima utaendelea kuwa mnyonge na kuamini kuwa ni haki yako kuwa mnyonge. Ni mpaka pale utakapo amka na kujitutumua na kupukuta mavumbi na kuanza kutetea na kujivunia utu wako na kuweza kusimama na kuitetea nafsi yako bila woga kwa ujasiri, ndipo utakapoanza heshimika na yule aliyemnyanyasaji ama atalegeza kamba au kufungasha virago na kuondoka.

Tulipigania Uhuru kwa nguvu sana, je ili kuwa ni kwa sababu gani? Je ni ile chuki yetu ya kufanyishwa kazi na Mkoloni katika nchi yetu? mbona tabia hiyo bado tunaendelea nayo popote pale ambapo tupo nje ya kujitawala wenyewe?

Angalia Watanzania walioko Diaspora, wengi ni mahiri na wanajituma kwa bidii katika kila nyanja hata kama ni Udereva Teksi. Watanzania walioko nje ya nchi wanafanya kazi kwa kujituma, juhudi ,maarifa na kwa nidhamu za hali ya juu, inakuwaje nyumbani tunashindwa kuwa na nidhamu na mvuto ule ule wa kuwa wachapakazi hodari wenye kutumia juhudi na maarifa?

Je tutalaumu mishahara na ufinyu wa vipato? mpaka lini tuendelee kulialia kuwa tunapunjwa? Je tumeshasimama na kumhoji yule tuliyempa dhamana ya kutuongoza na kufanya mipango ya maendeleo nchini mwetu na kutaka kujua ni lini tutaona maendeleo chanya au msukumo chanya?

Wakati wa Nyerere, tulikuwa na mategemeo mengi, tuliposhindwa kupata tulichotaka (ambacho ukweli mpaka leo hatukijui), tukasema hafai na katuletea umasikini. Ndio maana kuna wengine wanaamini kwa dhati kuwa Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ndio chimbuko la Umasikini wa Mtanzania.

Akaja Mwinyi ambaye tukamshangilia kwa utawala wake unaofanana na Babu au Mjomba poa, maduka yakajaa, tukaanza kuchekelea neema ya fahari ya macho na kuimba ruksa kama vile basi tumefika ile nchi tulioahidiwa. Tukachukua bilauri na kata na kuanza kujipongeja kwa maduka na bidhaa kuongezeka, lakini sisi wenyewe kufanya kazi kujizalishia ikawa ni shida.

Mkapa akatuambia sisi ni wavivu na wenye wivu, tukakasirika na kuzira, akahamasisha mipango ya sisi kujihujumu wenyewe na kuwa Taifa linalotegemea uagizaji na si uzalishaji wa ndani kama vile Mwinyi alivyofanya, tukanyamaa kwa miaka 10 akishirikiana na wenzake ambao walishaamini kuwa sisi ni Zimwi liliwalo, haliwezi kwisha kulika kutokana na UBUTU wetu, na kama zawadi ya kazi nzuri aliyofanya ambayo imelihujumu Taifa, akahakikisha tunapewa mtu dhaifu kama kiongozi na tukampokea Kikwete kwa vifijo na nderemo!

Sasa Kikwete kafanya lile tulilojua mapema na kwa hiari tukampa dhamana, leo tunahamaki?

Msishangae kwa Mchungaji kuunganisha nafsi yake katika kujisuta pamoja na kuwa wengi wenu mnamshangilia anavyomchambua Kikwete na uongozi wa CCM. Siwezi kujitoa kutoka lawama kisa nimeandika s c r ew Muungwana au Ajizi ya Kibuge.

Ninachofanya ni kukubali wazi kuwa sisi kama jamii, tutaendelea kutaabika mpaka pale tutakapoanza kubadilisha mienendo kwa kujipima wenyewe kwanza, kujihakiki na kujiwekea nidhamu na malengo katika ubinafsi na nafsi zetu kama mtu mmoja mmoja, ndipo tutakapoweza kwenda kwa umoja kama Taifa.

Lakini, nimewahi kuuliza mara kadhaa hapo awali, je tafsiri ya Mtanzania ya maendeleo na utajiri ni nini? sijapata jibu la uhakika na hata kama leo tutasoma majedwali ya kimataifa yanayoonyesha viwango vya umasikini na utajiri, je tunavielewaje kwa nafsi zetu na mazingira yetu?

Mmeuliza kwa nini nilihoji watu kukaa vijiweni Dar, nitawaambia hili, pale Dar na hata mikoani ambako niliona watu wakiamka asubuhi kwenda kulibwia tembo na si kufanya kazi, kuna nafasi nyingi sana za Watanzania kuweza kujiendeleza kiuzalishaji mali na si lazima iwe kwa kupitia kuajiriwa.

Ndio maana nikakaa chini na kuhoji kama tulilipokea Azimio la Arusha kwa makosa na hivyo sera za Ujamaa na baadhi ya vipendele tulivyoviimba kwa nguvu kuwa hatutaki Ubepari au watu binafsi kuwa wazalishaji huru ni sehemu moja na nyeti inayohusiana kwa kiwango kikubwa na Umasikini, Unyonge na Udhaifu wa Mtanzania (na hili la UUU ni kwa mtazamo wangu, mtu mwingine anaweza kusema karidhika na alichonacho na hana tatizo!).

Hivyo, binafsi, Mwalimu Mbele, JMushi, Tumain, Mwanakijiji na Michuzi tunajukumu la kujihoji nafsi na kujichambua na kujipima je tunajipimaje kama wananchi na ni halali kwetu kuelekeza vidole vyote vya lawama kwa mtu mmoja au Serikali bila kuhoji nafasi yetu katika matatizo yanayotukabili?

Uchanga wa Tanzania na Watanzania na ufinyu wa upeo, si jambo la kupuuziwa, na ndio maana Mzee Mwanakijiji ana kampeni ya kuleta mabadiliko mwaka huu. Lakini mabadiliko si kumuondoa Kikwete na kutuletea Mwakyembe kisa eti tunapiga vita Ufisadi. Je tukimwondoa Kikwete na kumleta Mwakyembe, Sitta, Lipumba au Sitta basi ndipo tutabadilika fikra?

Nakumbuka wakati Mzee Mwinyi na Azimio la Zanzibar lilipokuja, nakumbuka suala la cost sharing lilipokuja, sisi tulidumaa na kupoteza nafasi muhimu kuhoji madhumuni na mbinu zitakazotumika katika mfumo huo mpya. Kama bendera inayofuata upepo, tukaridhika kimya kimya na kukubali kuburuzwa bila kuelezwa kinagaubaga kuwa mabadiliko haya yana maana gani na kwa manufaa ya nani?

Imekuwa ni kawaida yetu, kutafuta mchawi wa kumtupia lawama. Kikwete ana gunia elfu za lawama kutupiwa, CCM ina magunia laki ya lawama kubebeshwa, lakini mimi, wewe na yule na wote katika nafsi yetu ya binafsi kama mtu mmoja mmoja na kwa umoja kama Taifa, tujitwishe magunia yetu Milioni kadhaa ya lawama!

Reverend,naomba nami nikujibu kwa ujumla.

Tulipopata uhuru tulikuwa na matumaini makubwa kwamba wakati umefika wa kusimamia maendeleo yetu wenyewe kwa faida yetu (japo mie nilikuwa sijazaliwa wakati huo).Lakini tusiilinganishe nchi na ndoa,kwamba kama umeoa na kisha kugundua mke/mume ni bomu basi jitihada zitafanyika chap chap ili atalikiwe.Uhuru uliambatana na kuundwa kwa taasisi za utawala na uongozi.Waliojaribu mapema kupambana na kile walichokiona "mwelekeo mbaya wa vioungozi/watawala wetu" waliishia kuwekwa vizuizini.Hapa nazungumzia harakati za kuiondoa serikali madarakani zilizopelekea kesi za uhaini.Whether walikuwa na nia ya dhati ya kubadilisha mambo kwa niaba ya umma au walifanya hivyo kama vibaraka,mie siko katika nafasi nzuri ya kutoa hitimisho.Ninaloweza kusema ni kwamba some tried/dared to try....na matokeo yake tunayafahamu.

Ni rahisi kuwalaumu Watanzania iwapo anayelaumu ana-neglect mfumo wa siasa uliotawala nchi yetu tangu kipindi cha uhuru hadi mwanzoni mwa miaka ya 90 watawala wetu walipolazimika kwa shingo upande kukubali kubadili mfumo wa kisiasa,uchumi na maeneo mengineyo.Hata hivyo,takriban miongo miwili baadaye,Tanzania bado kwa kiasi kikubwa imeendelea kukumbatia mfumo wa kidikteta usioruhusu mawazo mbadala hata kama mawazo hayo ni kwa manufaa ya wananchi walio wengi.Reverend,unatarajia nini kwa mwananchi wa kawaida wakati watawala wetu wanamwaga mamilioni ya fedha za walipa kodi kuhakikisha nafasi zao zinaendelea kuwa salama?Hapa nazungumzia matumizi mabaya ya vyombo vyetu vya dola na usalama ambavyo vimeendelea kuwa sehemu muhimu ya hegemony ya CCM.

Kwa anayesoma juu juu mtazamo wa Reverend,anaweza kuamini kuwa Watanzania ni sado-masochists wanaopata raha kutoka kwenye mateso na uonevu wanaokumbana nao kila kukicha.Ukweli ni tofauti sana.Laiti siku itapokuja tukabaini, kwa mfano, ni namna gani CCM imekuwa ikivutumia vyombo vya dola kudumisha utawala wake,ni dhahiri kuna wenzetu watakaolazimika kuwaomba radhi Watanzania wenzao waliokuwa wakiwatuhumu kwa uzembe wa kutofanya jitihada za kuleta mabadiliko.

Sie hatuna tofauti sana na Wapalestina.Hawafurahii mateso wanayoshushiwa na Waisraeli lakini hawana uwezo wa hapo kwa hapo kukomesha mateso hayo.Na kwa namna hiyohiyo,mateso yanayoendelezwa na tawala kama za Korea ya Kaskazini,Iran,China,Cuba na kwingineko-kama ilivyokuwa kwenye tawala za kikomunisti-sio kitu kinachowapendeza "wateswa" lakini kuendelea kwa mateso hayo ni matokeo ya watawala husika kujenga mazingira ya kuhakikisha kila aina ya upinzani unakuwa crushed na kudhibitiwa kabla haujaathiri "ulaji" wao.Comparative analysis ni muhimu katika kubaini namna mfumo wa kikandamizaji unavyodhibiti kila avenue ya wanyanyaswaji kujikomboa.

Tunapowalaumu Watanzania kwa "kuridhia kila baya" tunapaswa pia kutafiti kwanini "wanaridhia mateso hayo".Na ni muhimu pia kutambua kuwa umasikini wetu unawanufaisha sana watawala.Ikumbukwe kuwa kwa mwenye njaa,pishi ya mchele na sukari inaweza kabisa kumfanya asahau haki yake.Tumbo lenye jaa haliwezi kuelewa habari za "kutumia kura yako vizuri".Watawala wetu wanalitambua hilo na,I hypothise,umaskini wa Watanzania ulio wengi unatumika kama mtaji wa kisiasa kwa watawala wetu kwa vile unawasaidia kuepuka maswali muhimu kama "unatuomba kura sasa wakati miaka mitano iliyopita hukutufanyia lolote kati ya uliyoahidi".Busara zinatueleza kwamba "mpe mtu umaskini na atakuwa mtumwa wako kwa muda mrefu sana".Iliwezekana kwenye slavery na feudalism, na sasa pia inawezekana pia.

Naomba nifafanue kidogo kuhusu mtizamo wako unaposema "Angalia Watanzania walioko Diaspora, wengi ni mahiri na wanajituma kwa bidii katika kila nyanja hata kama ni Udereva Teksi. Watanzania walioko nje ya nchi wanafanya kazi kwa kujituma, juhudi ,maarifa na kwa nidhamu za hali ya juu, inakuwaje nyumbani tunashindwa kuwa na nidhamu na mvuto ule ule wa kuwa wachapakazi hodari wenye kutumia juhudi na maarifa?
.Hivi umeshajiuliza kwanini wengi wanajituma?Lakini hata pasipo kujiuliza,kwa hapa UK kuna ushahidi wa kutosha wa baadhi ya wenzetu waliobwetekwa baada ya kupewa "makaratasi yao" na wameridhika na social benefits kutoka Idara ya Kazi na Pensheni (DWP).Hawataki kuajiriwa au kuajiriwa kwa vile tu wanajua kila baada ya wiki mbili kuna fedha zinazoingia kwenye akaunti zao.Ukitaka kufanya utafiti,nakushauri uanzie Milton Keynes,Coventry,Birmingham,Reading,Leicester na hata London.However,I noticed you said BAADHI,nami nasema ni section ndogo tu ya wenzetu.

Jibu langu fupi kuhusu ufanisi wa baadhi ya wabongo wanaojituma huku ughaibuni ni kwamba kwa kiasi kikubwa waajiri wa huku wanathamini service ya mwajiriwa.Kama unalipwa kinachotosheleza kumudu maisha yako-na pengine hatimaye kumudu kufanya "vurugu za hapa na pale mtaani"-kwanini usimnyenyekee mwajiri wa aina hiyo?Ni banadamu gani mwenye akili timamu ataipenda kazi inayokulipa mshahara kiduchu kana kwamba mwezi una siku 5?Morali na ufanisi wa watumishi unachangiwa sana na malipo mazuri yanayoendana na mazingira mazuri ya kazi.Lakini pia sheria zinazozuia ubabaishaji pia zinasaidia kuhakikisha kuwa hakuna fursa za wazi kwa "wababaishaji".

Hiyo ni kinyume na ajira za upendeleo zinazotolewa kwa kuangalia majina ambapo si ajabu bosi wako akawa hana hata robo ya sifa za kitaaluma au ujuzi ulionao.Add to that,mshahara kiduchu usio na hakika ya kutoka in time,na mazingira mabaya ya kazi (kwa mfano walimu wanaofundisha watoto wanaokaa chini).Mwajiriwa mwenye utashi hapaswi kufikiri mshahara tu bali pia kile kinachompatia mshahara.

Lakini pia tusiwasahau wakulima walioajirajiri wenyewe mashambani.As I mentioned earlier,hawa ni chaguo rahisi la kuonewa na watawala.Wanashinda mshambani,wanahangaika kupata mazao bora huku mifuko ya pembejeo na mbolea ikirutubisha nyumba ndogo za watawala,lakini wanapopata mavuno wanashurutika kuyapeleka vyama vya ushirika,ambapo mazao hayo yanageuka mtaji wa bure wa viongozi wa vyama vya ushirika...wanakopa na kukopa na baadaye "kuua" vyama huku mkulima akiendela na dua zake kutarajia miujiza ya kulipwa deni lake.

Wamachinga nao.Wanajitahidi kununua bidhaa waziuze kama mobile shops.Badala ya kutengenezewa mfumo mzuri wa ku-encourage kujiajiri,wanageuka maadui nambari wani wa mgambo wa jiji (ambao nao wana uchu wa bidhaa za wamachinga kwa kisingizio cha 'kutekeleza sheria za jiji/manispaa).Akina mama ntilie nao wamegeuzwa migahawa ya bure kwa mgambo hao.Ma"baa meidi" nao wanalipwa mshahara mdogo kuliko idadi ya bia wanazohudumia kwa siku,hali inayowalazimisha kutegemea fadhila za wateja wao huku wakiomba dua wasivunje glasi au chupa za bia-suala linaloweza kuwageuza permanent sex slaves wa bar managers."Mahauzigeli" na "mahauziboi" wameendelea kuwa watumwa waliohalalishwa hasa kwa vile watawala wetu ni miongoni mwa waajiri wao wakuu.Taasisi zisizo za kiserikali zinazoanzishwa kuwatetea zimegeuka miradi muhimu ya kuongezea nyumba ndogo.Badala ya kuletewa mipango ya kujiajiri,watu wale wale wenye majukumu ya kusaidia ajira wanakuja na "dili" za kuwapeleka vijana "shamba" kuleta "unga" utakaozidi kuhujumu uwezo wa nguvukazi ya taifa.Na miongoni mwa "wabuni miradi" hao ni wale wenye jukumu la kupambana na mihadarati!

Na mtizamo wako kuhusu Azimio la ARUSHA ni kana kwamba ilipigwa kura ya maoni ku-seek opinions za wananchi.Tulishurutishwa kulifuata,kuliamini na kulitekeleza.Actually,baadhi ya wachambuzi wanadai kwamba moja ya sababu ya kutofanikiwa kwa Azimio hilo ni namna lilivyowasilishwa kwa umma i.e. kuwalazimisha wananchi walitekeleze pasipo kutaka ridhaa yao.Na hatukulazimishwa kulipokea na kulitekeleza tu bali pia tulishurutishwa kulitukuza kwa nyimbo,mashairi na chereko chereko nyinginezo.Naamini Reverend ulipitia mfumo wa elimu wa enzi hizo,na utakumbuka "ulazima" wa kukupenda chama,kuamini itikadi zake,kukubali usahihi wa viongozi wake na upuuzi mwingine kama huo.Je tulifanya hayo kwa hiari?Nah!Ni katika namna hiyohiyo tawala dhalimu kama za enzi za Taleban,au huko Korea ya Kaskazini zinavyolazimisha matakwa yao kwa watawaliwa.

Naafikiana nawe kwamba ni muhimu kwa Watanzania kujiangalia wenyewe,na ikibidi kujilaumu kwa mapungufu yao (hakuna kiumbe hai aliye absolutely perfect,mie and you included) lakini lawama hizo pia ziendane na hali halisi ya namna wangeweza,wanaweza na wataweza kujikwamua na mfumo dhalimu.Kuna usemi maarufu wa kisiasa kwamba "kwa Afrika chama tawala hakipaswi kushindwa uchaguzi bali 'kinajishindishwa' chenyewe".Suala sio chaguzi zinazoweza kupelekea kuangushwa kwa vyama tawala bali hofu ya watawala kuwa "kikija chama kingine basi tumekwisha".Tuna wakuu wa vyombo vya dola wanao-abuse madaraka yao kwa vile wanafahamu kuwa watawala hawakuwateua kuutumikia umma bali wao (watawala).Wanafahamu fika kuwa "zikija sura mpya zisizo na ubia nao" patakuwa hapakaliki.Na kwa vile wao ni sehemu ya mfumo,kama ilivyo kwa watwala,wanafanya kila wawezalo kuhakikisha mfumo huo dhalimu unadumu as long as it takes.

Labda ufumbuzi ni kizazi cha kujitoa mhanga kama suicide bombers (hapa simaanishi watu wajilipue bali nashauri wajitolee kwa ajili ya manufaa ya wengi).Unless watu wataacha lawama na kuonyesha nini wanachoweza ku-sacrifice kurekebisha madhila yaliyodumu kwa takriban miaka 40,tusitarajie mabadiliko yoyote.Unahitajika ujasusi,hujuma,na kila aina ya mbinu kupambana na mfumo huu dhalimu.Si CCJ wala chama mbadala kinachoweza kuleta mabadiliko ya haraka kwa vile wanausalama wameshapenyezwa huko zamani ili kuharibu mambo pindi utapojiri wakati mwafaka.Adui yetu yuko well-equipped na yuko tayari kwa lolote kuhakikisha anaendelea kutukandamiza.

Bahati nzuri kwake ni kwamba ana nia,sababu,nguvu na nyenzo za kufanya hivyo.

Tuna safari ndefu.
 
Waberoya na Mlalahoi,

Naomba nitumie mfano mdogo sana kuonyesha kwa nini nasema Watanzania wameridhika na shida na ni kwa nini ni sisi wa kwanza kujiangalia na si Rais au Mfumo wa kisiasa.

Tuchukue mkoa wa Dar Es Salaam ambao ndio uti wa mgongo wa Taifa letu.

Kwa nini mpaka leo hii, anzia ngazi za mitaa mpaka Wabunge, hakuna Wapinzani wa kutosha? Je pamoja na kero zote za kukosekana maji, kukosa ajira, umeme wa shida, msongamano wa magari, ughali wa chakula na huduma za jamii, kuzorota kwa uadilifu, kutopatikana maendeleo ya kweli na Serikali kufanya kazi kwa manufaa ya Watu na Taifa, iweje Dar ambao wako kwenye kite cha mbele kabisa kwenye maonyesho, wanafumbia macho wanachokiona ambacho kwangu mimi nakiona si sahihi?

Labda nipunguze wigo na kulenga majimbo ya Kawe na Ubungo ambako kuna Wasomi wengi, je kwa nini kuna kuridhika na hali halisi na hakna fukuto kama lile la wakati wa kumpiga vita mkoloni na unyonyaji?

Iweje turidhike kunyanyaswa na Watawala ambao ni wenzetu lakini tumpige vita mkoloni bila kuhofia kupoteza maisha?

Sasa kama jamii yenye upeo na ufahamu mkubwa kama watu wa Dar Es Salaam, wao wako mstari wa mbele kuridhika, tutategemeaje wale walioko vijijini kuwa tofauti na si wao kuunga tela?

Hivyo basi, pamoja na matatizo ambayo kweli na dhahiri yanahitaji kufanyiwa kazi kwa dhati na kwa udharura, kamwe hatutawezakupata utatuzi kama hatutaanza kuleta mageuzi kwa kugeuka nafsi na hasa sisi ambao tumepata upeo.

Tunapopima mambo, tujiulize ni vipi na vitendea kazi gani vinavyotusukuma hapa tulipo?

Binafsi pamoja na kuwa ni mwamini wa Ujamaa, nimeachana na mazoea ya kuogopa kuhoji baadhi ya maandiko na matendo ya ujamaa na kupima kama kweli yalikuwa na manufaa kwetu au tuliyapokea vibaya (rejea thread yangu ya Udhaifu wa Azimio la Arusha).

Mzee Mwanakijiji kalonga majuzi akihoji watu kuogopa kuuliza maswali magumu, mimi nasema si kuuliza wengine tuu, bali ni kujiuliza wenyewe maswali magumu.

Nilipokuwa nyumbani, nilipata fursa ya kujifunza mengi na kwa upya. Nilipokwenda kijijini kwetu, nimekuta watu asubuhi wanaamka kwenda kukata masimbi, kisa tunasubiri mvua. Nikauliza kwani ni lazima tutegemee mazao yanayosubiri mvua? je ufugaji na shughuli nyingine za uzalishaji mali haziwezi kufanyika? nikaambiwa tuletee pesa!

Kijijini kwetu, hakuna maji ya bomba mpaka leo hii, watu wanatembea maili moja na nusu kwenda kwenye mto ulionyauka kuchima kisima. Lakini pale kijijini, water table iko juu sana kwamba ukichimba futi nne kwenda chini, kuna maji.

Wanakijiji wanakataa kujichimbia kisima wanasema wawekewee kisima na mashine. Wanataka mashirika na serikali ijenge kisima. Sasa nikawauliza, je mshachimba kisima ili Serikali au hizo taasisi zije kuleta matufali na pampu za maji kwa ajili ya kisima, jibu lake ni kuwa kwa nini Serikali au Taasisi zisibebee mzigo wote na kwa nini Taasisi na watu binafsi hawapeleki fedha?

Sasa hapo ndipo unajiuliza, je ni kweli ndugu zangu hawa, umasikini umewashika kwa kuwa Serikali haijafika na kuleta maendeleo kijijini au hata wao wenyewe kujituma kwa vitu vingine ambavyo wala havihitaji Serikali bali ni utashi binafsi wa kutaka kuwa na maisha bora jamaa zangu hawana mwamko na wameridhika na uduni wa maisha yao?

Nikajiuliza misaada isiyohesabika ambayo imeshapelekwa nami na wengine je imeishia kuwajenga na kuwapa nuru wawe na hamu ya kujipatia "maisha bora" au misaada hiyo ilionekana kuwa ni kitu cha matumizi lakini hakuna mwenye nia ya kujitegemea na kujijengea misingi mizuri ya kuwa na maisha bora?

Ndio maana kampeni yangu pamoja na kumpiga madongo Kikwete, najirudi na kujihoji mimi na jirani zangu tunafanya nini kubadilisha mtaamo wetu kifira kama hao ndugu zangu wa kijijini ambao ni dhahiri wameamua kuwa hawatafanya harambee yoyote ile iwe ni kujenga kisima, kutengeneza barabara au hata kuwa na madawati katika shule za watoto wao?

Je kila kitu ni lazima tufanyiwe au tusubiri fulani atufanyie au tumtupie mtu shutuma? Iangalieni Dar Es Salaam!
 
Wajbu wa mwamko na kuhamasisha jamii ni wetu sote, sisi hapa JF tunaelimishana na kwa mgongano wetu wa mawazo na fikra ndipo tunapata fursa mpya ambayo Wazazi wetu na Mababu zetu walishindwa kuitumia kujijenga kama jamii yenye afya iliyo na uwiano wa kifikra!
 
Daaah kulaleki walahi...watu mnaandika maandiko marefu hadi yanachosha kusoma.
 
Waberoya na Mlalahoi,

Naomba nitumie mfano mdogo sana kuonyesha kwa nini nasema Watanzania wameridhika na shida na ni kwa nini ni sisi wa kwanza kujiangalia na si Rais au Mfumo wa kisiasa.

Tuchukue mkoa wa Dar Es Salaam ambao ndio uti wa mgongo wa Taifa letu.

Kwa nini mpaka leo hii, anzia ngazi za mitaa mpaka Wabunge, hakuna Wapinzani wa kutosha? Je pamoja na kero zote za kukosekana maji, kukosa ajira, umeme wa shida, msongamano wa magari, ughali wa chakula na huduma za jamii, kuzorota kwa uadilifu, kutopatikana maendeleo ya kweli na Serikali kufanya kazi kwa manufaa ya Watu na Taifa, iweje Dar ambao wako kwenye kite cha mbele kabisa kwenye maonyesho, wanafumbia macho wanachokiona ambacho kwangu mimi nakiona si sahihi?

Labda nipunguze wigo na kulenga majimbo ya Kawe na Ubungo ambako kuna Wasomi wengi, je kwa nini kuna kuridhika na hali halisi na hakna fukuto kama lile la wakati wa kumpiga vita mkoloni na unyonyaji?

Iweje turidhike kunyanyaswa na Watawala ambao ni wenzetu lakini tumpige vita mkoloni bila kuhofia kupoteza maisha?

!

Hii post yako nzuri kaka, nashukuru kuwa unarudi palepale kuwa wa kulaumiwa ni wale walio na upeo wa kuona mambo(mimi na wewe). Mtu yeyote anayejiona ameelimika au msomi kweli kabisa ndiyo wa kulaumiwa na sio wa huko vijijini. Ila bado naona kama unataka kuwalaumu watu wa huko, ''watu wanakuambia wanasubiri mvua unataka kuwalazimisha lazima wamwagilie''! pengine walikuwa hajui kabisa issue za irrigation mpaka ulivyosema , ndiyo tunachotaka hicho. tunazalisha wataaalmu kibao wa kilimo SUA wanaishia customer care vodacom

Lazima nikiri kuwa na nilisema tangu mwanzoni tatizo letu ni kuridhika! nashukuru kwa maneno yako umeenda kinyume kabisa na kutofautiana na professor Mbele! pokea heshima kwa hilo! kumbe watanzania hawa si wavivu, wala wana kilema fulani ila wamejisahahu kwenye dimbwi la raha na kuwa shida ni sehemu yao ya maisha waliyoyakubali!

na kwa nini tunaridhika?? , well, lina maelezo marefu , ila naona ni ubinafsi(watu hawawazi vizazi vijavyo) kwa madai ya wao wamefight kivyao vyao! sababu nyingine ni kuwa hakuna kizazi cha Tanzania kilichoteseka ili kuleta maendeleo, so hakuna ile value ya utaifa na kulilinda taifa! wazee hawana hadithi za kusimulia watoto wao taifa limejengwa vipi, ila watakuambia sukari ilikuwa haipatikani miaka ya 80! wenzetu ngau waliopigana kidogo watasema jinsi walivyopambana na hali fulani, vita, majanga ili vijana waliopo wauenzi utaifa. niliongelea swala la baraka na neema zinazotuzunguka zimepofusha macho ya watu.

on contrary, Rev. mtoto wako hatutarajii afanye mgomo ili umpe mahitaji yake, ni wajibu wako wewe kujua wanataka nini. Unless kama serikali haitakiwi kufanya hivyo! so viongozi na kapu lao la lawama hawachomoki katika huu mjadala.

wapinzani?? please dont go there never even mention them! wapinzani hamna nchi hii, ninawajua CUF tu Zanzibar basi, wengine wote , ni wale wale wa kuwaza kula wao na watoto zao miaka iende iwe mwaka wa pili wa tatu na waseme kila kitu kizuri!

I dont believe in the current opposition parties, wao ndio wasaliti wakubwa wa nchi hii kuliko wengine wowote, I can tell this in one paragraph, that can be described in a book!

Nilisikia unaanzisha chama , sijajua umefikia wapi na una mipango gani. Please isiwe hii ya bla bla zinazoendelea!

Asante pia kusema indirectly kuwa viongozi wa sasa wanapeta kwa sababu wanajua matatizo yetu na udhaifu wetu, is still not ethical au sio?

However, our origin, culture and condition are three strong fold to be broken!
 
Nimeandika hapo awali,baadhi ya hawa watu hawajui jinsi ya kuchagua viongozi, hawajui kuwa ni wavivu, hawajui kuwa hawana elimu, hawajui kuwa wamelala, yaani kwa kifupi hawajui whats up in this world, ndio hao hao unataka wajiamshe

Thats the challenge and how do we resolve this? anyone
 
Kuna facts ambazo Mbele anatoa katika article yake hiyo lakini facts hizo hazitoshi kujengea conclusion ya kisomi kwa mtu wa caliber yake kama alivyofanya. Wakati ni kweli kuna watanzania wengi hawatumii muda wao effectively, ameshindwa kuangalia jinsi gani governance system inavyowa-encourage watu hao kutotumia muda wao effectively. Mbele angefanya jambo la maana kwa kuainisha mambo yanayosababisha watanzania wasitumie muda wao effectively badala ya ku-stereotyope kuwa wote ni wazembe. Angejitahidi akaangalia athari za serikali kushindwa kusimamia sheria zake kama sheria dhidi ya rushwa, sheria za uhamiaji, sheria za kazi na ajira, sheria za matumizi ya pesa za serikali, n.k. Nina imani anajua kuwa matokeo ya serikali kushindwa kusimamia sheria za namna hiyo kunachangia sana kuwafanya wananchi wengi kushindwa kutotumia muda wao effectively. Yote hayo ni serikali ndiyo itakayolaumiwa siyo wananchi. Badala yake yeye amesikikika akiipongeza serikali ya Kikwete na kupendekeza kuwa Kikwete huyu aendelee kutuongoza huku akisema akitutukana kuwa ni wajinga, wazembe, hatuna elimu na matusi mengine ya namna hiyo.
 
Back
Top Bottom