Prof Mbele: Usomi haukamiliki bila kejeli na dhihaka? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof Mbele: Usomi haukamiliki bila kejeli na dhihaka?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlalahoi, Feb 7, 2010.

 1. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,067
  Likes Received: 402
  Trophy Points: 180
  Nimekutana nayo hii huko KwanzaJamii.Mwandishi ni Profesa Joseph Mbele

   
 2. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,480
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Ni wapi Mwalimu Mbele kadhihaki? Sikawaida yet Watanzania kuwa walalamishi, lakini kufanya kazi au kupiga bongo kufikiri hatupendi?

  Je ulisahau nilichoandika nilipokuwa Tanzania Ocroba ya 2009 nilippokuwa jiji la Dar zaidi ya asilimia 30 ni watu wabangaizaji? Je nilipoandika kuhusu Liwalo liwe na tabia ya Watanzania kuridhika na matatizo nalo lilikuwa kejeli na dhihaka au kwa kuwa Mchungaji kasema basi likaonekana bora?

  Hakuna alilosema Mwalimu Mbele ambalo halina tofauti na nililolisema tatizo ni sisi tuanze kubadilika kwanza ndipo viongozi watafuata!
   
 3. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2010
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 640
  Trophy Points: 280
  Huyu elitist professa(?) wa kwanza mmatengo kaishiwa ...
   
 4. tgeofrey

  tgeofrey JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 531
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  wanajilegeza wanangojea kusema wamezalilishwa
   
 5. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,355
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  Professa Mbele ana points na hoja ya maana lakini hajazipangilia hoja zake vizuri kwasababu kuna lots of contradictions,anasema suluhisho la kutokukaa vijiweni nk ni kusoma,je waliosoma si ndio mafisadi waliotufikisha hapa.

  Ni kweli utamaduni wa mtanzania ndio huo wa kukaa vijiweni na kupiga soga,sasa viongozi wanahamasisha ama wao ni kusema sisi ni masikini kila kukicha?Kama viongozi wanasema ili tuendelee inabidi tuwe omba omba unategemea wananchi wawe kitu gani?

  Kwanini huyu professa anatumia upuuzi kiasi hiki kusapoti status quo bila constructive points?

  Anazungumzia kuhusu ujuzi na maarifa ie knowledge economy,sasa nani kamwambia professa kuwa ni lazima kila mwananchi awe na ujuzi na maarifa ili Taifa liendelee?.

  Ni wazi kuwa matatizo tuliyonayo yanachangiwa sana na utamaduni,je viongozi wameshachukua hatua gani ili kujiwekea misingi ya kuachana na tamaduni mbovu zenye kuturudisha nyuma?

  Professa huyu inaonyesha wazi kuwa anawarundikia wananchi lawama zote kutokana na mwenendo wa Taifa letu,mbona hajaweka short comings zozote kutoka kwa viongozi?je ana maana wao ni malaika?wasababu mara zote Professa huyu amekuwa akisema "hakuna haja ya kuwalaumu viongozi"je haya ni kweli?

  Hata kama kuna ukweli kuhusu kuwaangushia wananchi lawama,sio kweli kwamba wananchi peke yao ndio vilaza kama anavyoelekea kuimply professa huyu, hatuwezi kupata maendeleo bila ya kuwashirikisha viongozi ambao ndio watatoa dira na mwelekeo.

  Kwa viongozi kuspend kama Taifa tajiri na huku wakiendelea kuomba omba na pia kuwaambia wananchi sisi ni masikini,je hiyo ndiyo namna ya kuwaambia wananchi ondokeni vijiweni na muache uvivu?Nani anayesababisha "ganzi" hapo?

  Eti "mkimshambulia rais,jishambulieni na ninyi" Huyu professa nina wasi wasi naye sana....Kama anajipendekeza kwa status quo,basi huo ni upuuzi wake asituletee wengine.

  Sina muda wa kutosha la sivyo ningeijibu makala ya professa huyo hoja kwa hoja,ila pointi chache zinamtosha na hopefully atatafakari,ama atajiunga hapa JF ili apate changamoto...Viongozi are to blame kwasababu hawajaonyesha kulitambua tatizo kabla hata ya kujaribu kulitatua tatizo lenyewe,na kama maprofessa wa kumshauri ndio hawa,basi msimamo wangu uko pale pale kuwa REVOLUTION IS A MUST.
   
 6. A

  AHAKU Member

  #6
  Feb 7, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naukaribisha uraia wa nchi mbili na uwe hata wa nchi ishirini labda ndugu zetu Wapemba na kipawa walichojaaliwa cha biashara na fedha walizo nazo watarudi kule mitaa ya Chokocho, Konde nk kuimarisha kisiwa
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Feb 7, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 78,282
  Likes Received: 40,525
  Trophy Points: 280
  Nadhani angeweza kutumia lugha ambayo iko polite kuliko hiyo kama hapo juu nilivyoinukuu. Na inavyoelekea yeye kajitoa kwenye hilo kundi wa watu wenye akili finyu na wasiojiamini. Anawesema Watanzania wengine ingawa na yeye ni Mtanzania vilevile kama hajabadili uraia wake. Sasa sijui yeye ni mwenye akili nyingi na mwenye kujiamini kwa vile anafundisha Marekani? Hilo sijui. Wengine mtaamua hilo.

  Ndio maana ninachompendea Julius Ngabu ni kwamba yeye asemapo "Miafrika Ndivyo Tulivyo" anahakikisha anatumia neno linalomjumuisha na yeye pia. Lakini hii ya kuwasema wengine wakati na wewe ni mmoja wa hao hao unaowasema vibaya ni ujinga na uwezo mdogo wa kuchanganua mambo!!
   
 8. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,067
  Likes Received: 402
  Trophy Points: 180
  Reverend,

  Navyofahamu mie,mwanataaluma anapaswa kuwa makini sana anapohitimisha jambo kwa mjumuisho pasipo sapoti ya takwimu.Mara kwa mara Profesa Mbele amekuwa akilaumu Watanzania kwa kupenda kupiga soga,kukaa vijiweni na ufinyu wa mawazo.Lakini sijawahi kuona hoja hiyo ikiwa supported na data za aina yoyote.Angalau Reverend umejaribu kudai "zaidi ya asilimia 30 ya watu ni wabangaizaji".Lakini swali la muhimu kwako ni hili: ulitafiti kufahamu kwanini wanabangaiza?Kwenye mambo ya kiroho ndiko tunapata majibu pasipo vyanzo au sababu lakini kitaaluma tunatarajiwa kutolea maelezo kila phenomenon tunayodiriki kuiweka hadharani.

  Binafsi,kama mzaliwa wa kijijini,naona ni matusi kulaumu "Watanzania kwa kupenda soga,ubangaizaji",na 'kashfa' kama hizo.Wakati Dar inaweza kutumika kama eneo la kutafiti tabia husika,ni muhimu kutambua kuwa kama ilivyo sehemu nyingine duniani,kuna division kubwa ya hali halisi kati ya rural na urban areas. Ni rahisi kuwalaumu Wamachinga "wanaobangaiza mijini" pasipo kuangalia political economy ya uzalishaji mali maeneo ya kusini.Kwa kukusaidia Reverend,nakushauri usome kitabu kiitwacho The Making of A Periphery: Economic Development and Cultural Encounters in Southern Tanzania kilichohaririwa na Pekka Seppala na Bertha Koda.Sura (chapter) mwafaka zaidi inaweza kuwa yenye kichwa The South-East Economic Backwater and the Urban Floating Wamachinga iliyoandikwa na E.P. Mihayo na N.N. Luanda.

  Ifahamike kwamba kupiga soga si kosa.Ikumbukwe pia kuwa hao wapiga soga hawaishi kwenye welfare state ambapo "hata wakipiga soga watalishwa na state".Kule kijijini kwetu,ni kawaida kwa watu kujumuika pamoja jioni baada ya siku nzima iliyoanza kwa kudamkia shambani kuhangaikia mazao ambayo yatapokuwa tayari yanaweza kuishia kwenye vyama vya ushirika vinavyojua kukopa lakini sio kulipa.Kuwaita watu wa aina hii "wabaingaizaji" ni kuwatukana .Wanajituma ili waweze kumudu maisha yao japo wanakwazwa na mpingo mibovu ya serikali yao sambamba na ufisadi.

  Tunawalaumu "wabangaizaji" pasipo kujiuliza ajira milioni 2 zilizoahidiwa na Kikwete mwaka 2005 zimeishia wapi.Au la msingi zaidi,ni kusahau kujiuliza ufumbuzi wa reserve army of labour linalozalishwa kila kukicha kutokana na ubinafsishaji unaoangalia zaidi wageni kuliko wazawa.Mtikisiko wa uchumi hapa Uingereza,na pengine kwingineko,umepelekea taifa hili kujikuta likiwa na watu waliopoteza ajira na kugeuka "wabangaizaji".Tofauti na huko nyumbani,serikali inafanya kila iwezalo kwa kushirikiana na social enterpises kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo,na taratibu "wabangaizaji" wanaanza kurejea makazini na wengine kuwezeshwa kujiajiri wenyewe.

  Tunasahau pia kuwa JK alipotangaza stimulus package, walengwa walikuwa taasisi za fedha kana kwamba uchumi wa Tanzania unategemea taasisi hizo badala ya kilimo.Na ukisikia ngonjera za kilimo kwanza utabaini kuwa hakuna seriousness katika upande wa viongozi wetu kukinusuru kilimo tunachofahamu kuwa ndio uti wa mgongo wa taifa letu.

  Vijana wanaojaribu kujiajiri migodini wanakumbwa na upinzani mkubwa kutoka kwa wawekezaji wenye uchu wa kusafisha raslimali zetu.Watoto wa walalahoi wanaojitahidi kupigana kiume kupata mafanikio ya kielimu wanaishia kukumbana na vikwazo kwa ajira zinazoangalia jina badala ya academic qualifications au experience.Nenda BOT au TRA kaangalie surnames za waajiriwa "wapya",utaishia kudhani taasisi hizo ni za familia za watawala wetu.Lakini vijana hao wanaokosa ajira sio kwa vile wanapenda kukaa vijiweni lakini kwa sababu tu hawatoki familia "zenye majina" wanaishia kuitwa "wabangaizaji".

  Ugonjwa unaowasumbua baadhi ya wachambuzi wetu ni wepesi wao wa kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu.Ni kweli kwamba serikali haiwezi kumsaidia kila mmoja wetu kupata ajira lakini ina wajibu usiokwepeka kutoa leadership,na ndio maana kila baada ya miaka mitano wanasiasa wetu wanatubembeleza tuwachague watuongoze.

  Tafiti za kuangalia kwa macho badala ya kutumia njia zinazokubalika kitaaluma ndio zinazopelekea mahitimisho yasiyojali sababu za msingi za vyanzo halisi vya matatizo.Ni kama kuhitimisha kuwa "bongo tambarare" kwa vile kuna vogue kibao barabarani,vikwangua unga vinavyoshamiri kama uyoga kila kukicha na kumbi za starehe zinazotapika wateja.Je pasipo kutafiti profile za wamiliki wa vogue na vikwangua anga tunawezajr kuhitimisha hicho kiitwacho "utambarare wa bongo"?Na pasipo kutafiti backgrounds za "wabangaizaji" wanaofurika vijiweni tunawezaje kuwatofautisha waliokosa ajira kwa vile si watoto wa vigogo na wauza unga wanaosubiri wateja wao?Au tunapoangalia baa zilizojaa wateja tutatofautisheje mafisadi wanaotumia fedha zao za wizi na wazalendo halisi wanaopunguza mawazo kwa moja moto moja baridi (baada ya kupewa mshahara usiokidhi mahitaji ya angalau wiki moja)?

  Ufinyu wa mawazo anaozungumzia Profesa Mbele ni sawa kabisa na ufinyu wa kitaaluma unaowakabili baadhi ya wasomi wetu wasiojihangaisha kutafiti vyanzo japo ni wepesi wa kufyatua findings zilizopatikana kwa "tafiti za macho".Busara ndogo tu inaweza kutueleza kuwa hata WEUPE na mtu unaweza kuwa na sababu tofauti: mkorogo au asili yake.

  Na hata tungekubaliana kuwa uzembe/uvivu wa kufikiri,ubangaizaji na kupiga soga ni tabia ya Watanzania wengi,bado swali la msingi lingekuwa WHY?Is it inherent or induced?Kwanini iwe hivyo kwa Watanzania wengi lakini sio kwa Rev Kishoka au Profesa Mbele.Je wenzetu wana vinasaba tofauti?

  Na kichekesho ni kwamba wachambuzi wetu WANALAUMU "tabia ya Watanzania walio wengi KUPENDA KULAUMU/KULALAMIKA" ilhali wachambuzi hao nao wanafanya hichohicho wanachokilaumu.Yaani wanalaumu wanaolaumu!Na bora basi wangelaumu na kutupa mapendekezo ya nini kifanyike.Mie siwalaumu as such kwa vile nafahamu ni rahisi kulaumu kuliko kutoa ushauri.

  Mwisho,ikumbukwe kila mtu anapenda kuwa na maisha bora,ya usalama na yenye furaha.Hiyo ni silika ya kila mwanadamu.Japo maisha hayo bora hayawezi kushuka kama mana ya Agano la Kale,ni dhahiri kuwa jitihada za mtu mmoja mmoja na jumuiya kwa ujumla zitapata shida kufanikiwa tukiwa na viongozi wanaokwamisha jitihada za kujiletea maendeleo.Mfanyabiashara wa bidhaa za ndani anayejaribu kufuata sheria za nchi ili ajiendeleze yeye na familia yake na kumudu maisha hawezi kuchuana na mafisadi wanaoingiza vitu kutoka nje pasipo kulipia kodi na kuviuza pasipo kuvuweka dukani kwa vile alishapewa tenda kabla hata hajapata leseni ya biashara.

  Na katika hali hiyo hiyo,mwajiriwa aliyeajiriwa on merit kutokana na taaluma na ujuzi wake,na ambaye anajitahidi kuzingatia maadili kwa kutojihusisha na rushwa au ubadhirifu hawezi kuchuana na yule aliyeajiriwa kwa vile tu ni mtoto wa flani,na ambaye anachukulia ofisi anayofanya kazi kama mahala pa kuvutia muda/kusubiria dili lililochongwa na mzee.

  Kulaumu "wabangaizaji" pasipo kujishughulisha kufahamu kilichopelekea ubangaizaji huo ni sawa kabisa na kuuchukia ugonjwa pasipo kufanya jitihada za kujua chanzo chake/sababu za kusambaa kwake.
   
 9. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #9
  Feb 7, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Duu Makala yake ina mvuto!
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Feb 7, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,355
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  Mbali na lugha bado sikubaliani na uchambuzi wa Professa huyu,binafsi kwasababu hayuko hapa JF,basi niko tayari kwenda hoja kwa hoja dhidi ya wale wanaoona ana make sense.
   
 11. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,355
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  Nini kilichokuvutia?Toa maelezo acha generalisation,la sivyo utaangukia kwenye kundi la "Uvivu wa kufikiri"
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Feb 7, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 78,282
  Likes Received: 40,525
  Trophy Points: 280
  Lakini Mangi, ina maana hukubali kuwa kuna angalau chembe ya ukweli katika akisemacho?
   
 13. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #13
  Feb 7, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,355
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  Hana hoja,ni nani kasema kuwa uraia wa nchi mbili nidio nguzo ya maendeleo ya Taifa?,ni misingi ipi hiyo aliyoitumia ku conclude kwamba kuna wanaosema kwamba "Ukosekanaji wa Uraia wa nchi mbili" ndio uliopelekea Taifa letu kuwa nyuma kimaendeleo?
  Uraia wa nchi mbili sio basis za kutupatia maendeleo,hilo liko wazi,ama ana bifu na watanzania wanaoishi nje ya nchi?
   
 14. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #14
  Feb 7, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,355
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  Kuna hoja za msingi lakini hazina mpangilio,sio kweli kuna wanaosema eti uchumi wetu uko nyuma kwasababu hatujapewa uraia wa nchi mbili.
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Feb 7, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 78,282
  Likes Received: 40,525
  Trophy Points: 280
  Hilo la uraia wa nchi mbili na uhusiano wake na maendeleo ya nchi hata mimi siafikiani nalo. Ila sitashangaa kuwepo kwa watu wafikiriao hivyo. Kwa hiyo na wewe kukataa kwako kuwepo kwa hao watu sio sawa vilevile.
   
 16. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #16
  Feb 7, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,078
  Likes Received: 4,451
  Trophy Points: 280

  Mmh,this is good start indeed, nadhani hapa professor amekosea, sijajua kina nani wasiojitambulisha. Kuwaambia watu wana akili finyu is a relative term, engineer anaweza kusema lawyer ana akili finyu, lawayer anaweza kusema the like so it depends grounds zipi mkuu huyu anazitumia, otherwise the feeling could be mutual.


  Mamilioni? Professor ameondoka lini DSM? wanakulaje hawa watu? kwa harakaharaka DSM kama hauna sehemu ya kupata fedha unakufa huku unajiona, professor alitakiwa atoe data.

  Kweli kuna 'wanaotega' wanajua watapata wapi hela, ili group we can say they are 'complacement' but not lazy, kuna watu wameshajenga nyumba zao miaka hiyo, au walinunua viwanja manzese kwa shilingi 100! leo wanakula fedha zao taratibu . Hili ni tatizo kubwa , kuridhika haraka na kutokutaka zaidi ila sio wavivu!! wanakaa vijiweni. Sijajua unless tuko kwenye age stone kuwa kila kitu unachuma shambani lakini kwa DSM kama huna hela unakufa, so professor alitakiwa alione hili ninachoona ni kuridhika kwa watu hilo ni tatizo kubwa.

  Hapa nitaeleza kwa mtazamo mwingine;

  Mkapa alijua tatizo la watanzania(the quality of leadership) alijua nini afanye ili watu wafanye kazi, tofauti na kipindi cha Mwinyi. alipunguza hela kwenye mzunguko wa fedha, ubinafishaji , na professionalism. watu walianza kupiga kazi.

  Leo hii professor kama anataka kumkomboa mtanzania wa kawaida basi huwezi ukamkwepesha kiongozi na hali hii

  Kiongozi anatakiwa awajue watu wake, matatizo ya watu wake, jinsi ya kuyakabili, ndiyo maana ya uongozi. Kiongozi anatakiwa atoke nje ya box awaze mbali na kwa upeo wa juu kuliko raia wa kawaida.

  Badili system, let say wafanyakazi wa serikali kuanzia leo waanze kulipwa kwa masaa, waje muda watakao lakini wafikie lengo. Whe I was working with vodacom hakuna mtu aliyewahi kuniuliza mbona umechelewa kazini, ikifika muda na saa watu wanataka report (udeliver) kuwa ulikuwa unaumwa jipu shauri zako! hatujaweka sheria na technique za kuwabana watu ili wafanye kazi kwa ubora, haraka na kwa muda mfupi

  Believe me, kuna watu wako serikalini ambao kwa siku anaweza akafanya kazi ya massa 2 kwa masaa 8, the same guy ukimpeleka private sector ataifanya the same kazi kwa masaa mawili.

  Kumkomboa huyu mtanzania haihitaji article ndeefu, viable and practicable solutions, nikimwona mtu kipofu sitaanza kumlaumu mbona wewe kipofu! nitafanya juu chini aishi maisha ya kawaida, matatizo ya watanzania sio upofu, yanatibika, yanaisha hapa tatizo ni viongozi tu, Kikwete akiwamo!

  So, viongozi hawajui wafanye nini ili kumponya mtanzania wa kawaida na kumbadilisha afikie standard ya akina Mbele wanayoitaka

  Uvivu wa watanzania umetokana na nini??

  1. Siasa ya ujamaa , is the same case we see in russia now, kuna watu wengi maskini na wa hali ya chini kwa sababu siasa hii real haikuzaa watu competent

  2. Kutawaliwa, athari za ukoloni bado zipo Mbele hajagusia ili, elimu ya kikoloni ililenga kuwasaidia wao. As a result wakati tunakua tuliambiwa na wazazi wetu elimu ni kukaa ofisini! we have society that people are not creative, innovative, initiative, productive etc, simply ni kwa sababu ya elimu!

  we have professors here that they can not create jobs! wanawaza kuendesha warsha kama professor Mbele!!(funny) we dont need lecture we need you to open company or anything else that you will employ Tanzanian!!

  3. Geographical position,

  Tanzanian is not disinguishable from other countries that are situated in equatorial regions, where we can experience all four season of the year! smoothly without any problem this alone is a big factor that people are relaxing because we have not any natural calamities/disaster problems with weather etc. wazungu kuwa na akili ni shida zao, kuishi kwenye mabarafu, etc! People are relaxing just go to our village now! why?? the food is there! hata kama wakipiga soga hawana matatizo hawa! nimekukatalia kuhusu mjini, mjini is another case kama nilivyosema hapo juu!
  Another issue, professor hajasema kwa nini watu hawajiamini this is a cultural problem! kwa mfano hivi sasa jimbo la Ontario-Canada wanaendesha seminar/short course kwa graduates ili wawe confident inaonekana wakanada na wamarekani, wakanada confident yao ipo chini! sasa angalau wenzetu wana hela wameona tatizo na wanalishughulikia! professor wetu yeye ataishia kusema hawana confident!and you know what..

  ''Kuna kipindi jamii ya wakanada hii ilipita kwenye tabia ya kusema ''dont talk to strangers'' wanaona imewaathiri sana! nani sisi ambaye hata anayefanya research kwa nini watanzania sio confident???

  Prof huyu hajasema matatizo ya lugha yanatokana na msukumo, walimu wabovu na kuwa hakuna kiongozi serikali ambaye ana muda wa kuwaza mtoto wa kapera ajue lugha!

  Professor Mbele yeye ni shahidi; wakati anaanza darasa la kwanza hakujua umuhimu wa elimu! hakujua kuwa kujua kiingereza ni lazima! naona ni kama vile professor analazimisha watu wawe na elimu kama yake au watazame kama yeye.

  1.Kuna wasijua umuhimu wa elimu, mathalan waliotoka kwenye familia ambazo hakuna aliyesoma. NA NDIYO sababu ya Nyerere kuweka shule bure kuvutia watu wasome! kuna relation kubwa kati ya mzazi na mtoto kwenye mambo ya elimu, wengi wetu tumechipuka tu kibahati!

  2. Kuna watu wanajua umuhimu wa elimu ila hawawezi kusoma, hawana uwezo wa kujisomesha

  3. Kuna wanaojua umuhimu wa elimu, wabinafsi na hawataki wengine kuwa kama wao!, ni viongozi waliofunguka macho, yet they are doing nothing to improve our education system

  4. Nadhani unajua kuna shule za english medium na kiswahili medium! na viongozi wanawapeleka watoto wao shule za nje kwa sababu hata wao wenyewe wanajua shule za ndani si nzuri, na wanaotakiwa kuzifanya nzuri ni wao!!


  Nani atahudhuria hii warsha? graduates, vijana walioishia darasa la saba, form four, au watu wooote! nataka kujua maana hii warsha yako ukishaaanza kuwabagua watu, kesho unawaita wavivu wanapiga soga, sipati logic behind

  Kujiamini ni swala la utamaduni na halianzii siku moja!  hitimisho

  Nimejaribu kuangalia kwa haraka sababu na solution za matatizo aliyoyasema Prof. Mbele is so sad kuwa Mbele anaonekana kugombana na watu wa kwenye internet waliojibu post zake za nyuma, ambao hawa wengi kwenye internet ni wasomi, wana kazi zao wengine ni professors, lecturer etc

  Ukiendelea kumsifia Kikwete hakuna shida ila nakueleza competent leader anatakiwa ajue matatizo ya watu wake.ndiyo maana huwa nashtuka nikisikia mtu anataka kuwa kiongozi.

  Unachokisema wewe ni matatizo ya watanzania, ukiwalaumu watanzania, hujajiweka nafasi kama ni kiongozi utatatua vipi haya matatizo. Maana yana reasons, nimekueleza political system iliyokuwepo, geographical position, kutawaliwa n.k

  hii article yake ikikataliwa ni sawa kabisa maana ameanza na matusi na hii ni dalili ya kujihami!

  ndimi professor mtarajiwa
   
 17. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #17
  Feb 7, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,355
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  Kama ulivyoelezea,umegundua kuwa nime acknowledge hilo from the previous posting(s),however siyo na haiwezi kuwa basis za hoja anayotaka kuijenga....Inaonekana kama ndiyo thesis.
   
 18. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #18
  Feb 7, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,078
  Likes Received: 4,451
  Trophy Points: 280
  Who is sisi?

  wasomi, raia wote, viongozi, wazee , vijana n.k who is excatly are yu referring from


  Najua unalisema group la watu ambao wana upeo, hawataki kutimiza wajibu wao kwenye maeneo ya kazi na maisha ya kila siku.

  My worry ni ile jamii ambayo, kwanza hawajui hawajasoma, hawajui ni wavivu, hawajui kuwa hawajui, hawajui dunia ikoje! hawa ndio tatizo langu mimi, nani wa kuwaokoa?? wenyewe?? how?

  Rev. tell me you are ability to analyse and see things imechangiwa sana na kwenda nje, at leas umeona tofauti ya maisha, cultural etc

  Ndiyo maana unasema ulipokuja bongo october uliona so and so, ungekuwa unaishi humo ungeona the same thing??wengi tunajua dunia inaenda vipi kwa sababu ya interactions,mawasiliano, internets, na kusoma. nje ya hapo ni ngumu kujua unatakiwa ufanye nini.

  Ni sawa na mtoto aliyezaliwa na mama kichaa jalalani, anakulia jalalani na anajua maisha ndiyo yalivyo, au mtoto wa bata kulelewa na kuku!

  These Tanzanians I have proved they are smart, good people, intelligent, hard worker, genius etc they need spark of light to fire them up

  Please when blaming Tanzanian we have to be careful in our history, culture na aina ya viongozi tunaowapata ambao walitakiwa wawakomboe hawa watu kifikra na mtazamo!sadly they are not doing that

  Nyerere alikuwa mjinga alivyowapa watu elimu ya bure mpaka tunapewa madaftari na kula chakula cha mchana day????? nimekula wali mchana Tambaza secondary mwaka 1993! pamoja na hayo kuna watu walikuwa hawataki shule na wanakimbia!

  au Nyerere angesema mbadilike wenyewe? au kazi aliyoianza Nyerere ilifika tamati? when? how? I am pretty sure labda useme kivingine huwezi ukamkwepesha Nyerere na elimu zenu akin Reverend! mmesahau Nyerere alivyowadekeza na mlivyata elimu na ufahamu, leo hii mnataka wengine waende kivyaovyao!!

  ndiyo hao unasema wabadilike au kina nani hasa??
   
 19. m

  madule Senior Member

  #19
  Feb 7, 2010
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli!
   
 20. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #20
  Feb 7, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,632
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Mkuu hii nimeipenda sana! nimeshaandika hawa maprofesa sasa wanatumika kama masekretari wazuri kwa ccm.
  Hivi huyu profesa gani asiyeelewa kuwa kiongozi anapochaguliwa kuiongoza nchi anategemewa aitoe jamii mahali alipoanzia kuipeleka mbele zaidi kwa kuibadilisha hata kimawazo licha ya kiuchumi? Kama wao viongozi walijua udhaifu wa wananchi wao kwanini hawakulifanyia kazi hilo? Huku ndiko kule kusoma bila kuelimika halafu ukawa profesa! Forget these theoreticians! Mwambie agombee ubunge watampa uwaziri sasa hivi..... while we count "Another ccm decorating secretary is born"!!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...