Prof. Mbele: Tundu Lissu haichafui nchi, kumsema Spika wa Bunge na Serikali sio kuichafua nchi. Hata Nyerere alisema CCM ni kansa

Well said.

Hivi kina Kabudi akili za hivi waliziflashia kwenda septic tank ipi?
"Kutofautiana mawazo ndo uhai wa taaluma" amesema Prof. Mbele kwenye hilo andiko lake . Sasa ulitaka Prof. Kabudi mawazo yake yafanane na Prof. Mbele? kwasabbu tu yeye ameamua kuwa upande lissu? Huo siyo utamaduni wa wanataaluma. Wanataaluma wanapingana kwa hoja. Prof. Kabudi akiamua kujibu haya, unaweza ukahisi Prof.mbele alikurupuka usingizini akaandika bila kufikiri.

Sitoshangaa pia siku Prof. Mbele akitoa mawazo tofauti na mnayoyataka nyinyi, mtamgeuka kama mlivyomgeuka Kakobe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umelishwa ujinga umeushiba, sasa ni wakati wa kuja kuonyesha shibe ya huo ujinga hapa jukwaani. Ni mzungu gani amtegemee kiongozi aliye nje ya madaraka kulinda maslahi yake? Aliyekulisha huu ujinga ndiye aliyesema tunawadai Barrick 400t+. Tumekaa na hao Barrick miezi zaidi ya miwili tumeshindwa kudhibitisha hayo madai. Hao waliokulisha ujinga ndio walisema Acacia hawajasajiliwa hapa nchini, je hao Acacia wameondoka hapa nchini?

Lissu amejiingiza kutetea watu na kujiingiza kwenye siasa toka miaka ya mwisho ya 90. Hakuna siku yoyote aliyowahi kuondoka hapa nchini akakaa huko Ulaya/ Us nje ya haya matibabu kujadiliana na mzungu yoyote kuhusu maslahi yao kwani alikuwa mwiba mchungu kwa hao wazungu kwenye maslahi yao. Sishangai kwani uwezo wako wa kuelewa mambo upo ndani ya utashi wa kauli za watawala, chochote unachosikia toka kwao ndipo akili yako inapogota. Hao watawala lazima wamuite Lissu msaliti ili kuficha tuhuma za kushambuliwa risasi na hao watawala.
Bora kulishwa kauli za watawala kuliko kuwa msaliti. Kuishi humu nchini miaka yote hakuuondoi usaliti wa mtu kutoka nafsini mwake. Yapo mambo hayawezi kuandikwa humu kutokana na nature yake.
 
Bora kulishwa kauli za watawala kuliko kuwa msaliti. Kuishi humu nchini miaka yote hakuuondoi usaliti wa mtu kutoka nafsini mwake. Yapo mambo hayawezi kuandikwa humu kutokana na nature yake.

Hakuna mzungu mjinga anayemtegemea mbunge mmoja wa upinzani kulinda maslahi yake, wakati hakuna kiongozi yoyote wa kiafrika anayeweza kuzuia maslahi yao. Tumia akili yao usilishwe ujinga wa siasa za mihemko na ulimbukeni wa madaraka. Hao waliompiga Lissu risasi walitegemea angekufa uchumi ungekuwa bora zaidi ya huu uliopo? Shambulizi lile lilifanyika kwa mihemko na kutokuweza siasa za ushindani, anayesema usaliti anatumia utetezi huo kujisafisha kwani hana Utetezi ulio nje ya huo.
 
Mkuu tindo na wewe unalishwa matango pori. Ukiambiwa kwamba njama yote ya kumpiga risasi jamaa wa Singida ilitengenezwa na viongozi wake wa chama unaweza ukaamini?. Kuna mambo hayaandikiki humu ndani mkuu.
 
Narudia tena, shambulio la Lissu na anachoongea dhidi ya watawala, ingekuwa chama chake ndio wahusika kila kitu leo hii lingekuwa wazi na hata serikali ingekubali waangalizi wa kimataifa ili kujisafisha zaidi. Unapoona kigugumizi jua huyo anayetajwa na Lissu ndio muhusika na huu mwenendo wa uchunguzi kusitasita basi ujue wahusika ndio hao hao fullstop. Iwapo Mbowe yuko ndani mwezi wa tatu huu kwa kesi ya kubambikizia, ingekuwa yuko nyuma ya hilo shambulizi pangetosha?
 
Mbowe na Matiku wapo kizuizini miezi kadhaa sasa! Kuna jehanam nyingine zaidi tena?
Mahubusu walioko huko Ni Mbowe na Matiku tu hakuna wengine.....ukikosa dhamana utapelekwa mahabusu ya gerezani kwa yoyote yule haijalishi cheo chako kwa mujibu wa sheria
 
Anaandika Profesa Joseph Mbele

Mimi ninaufahamu vizuri utamaduni wa vyuo vikuu vya Marekani, kwa sababu nilisomea kule na ninafundisha kule. Nimeshatoa mihadhara katika vyuo vingi, sio Marekani tu bali sehemu mbali mbali za dunia.

Ninavyosikiliza mahojiano na hotuba za Tundu Lissu ninafahamu fika kwamba ataamsha fikra za wasikilizaje wake kwa kiwango cha juu. Ninafahamu pia kwamba katika vyuo vya Marekani, hawamwaliki mtu kwa ajili ya kumsikiliza tu, bali pia kwa ajili ya kumpiga masuali. Mtu anatoa hotuba halafu anakalishwa kitimoto.

Tundu Lissu ni hodari kwa yote hayo. Wanaombeza hapa Tanzania wanajisumbua. Kwa kusema hivyo, simaanishi kwamba mawazo yangu ni sawa na ya Tundu Lissu. Kuna ambayo ninatofautiana naye.

Lakini kutofautiana mitazamo ndio utamaduni wa watu wanaofikiri. Ndio utamaduni wa watu walioelimika. Vyuo vikuu ni mahali ambapo tunatofautiana na kulumbana muda wote. Ni uhai wa vyuo vikuu. Ni uhai wa taaluma. Tunawajibika sisi waalimu kujenga tabia hiyo miongoni mwa wale tunaowafundisha.

Kuna haya madai kwamba Tundu Lissu anaichafua nchi. Binafsi, sijawawahi kuona popote au siku yoyote ambapo Tundu Lissu ameichafua nchi. Anazilalamikia mamlaka za nchi, kama vile serikali na Bunge. Lakini serikali si nchi. Bunge si nchi. Anapomshutumu Spika, haichafui Tanzania. Spika si Tanzania.

Ingekuwa vinginevyo, basi kwa jinsi Mwalimu Nyerere alivyoandika kitabu cha "Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania" tungesema kwamba ameichafua nchi. Mwalimu anaiponda CCM na serikali yake, hadi kutamka kwamba kuna kansa katika CCM. Hadi akasema kwamba alitamani kitokee chama cha upinzani kilicho bora kuliko CCM ili kishike nchi badala ya CCM. Lakini itakuwa ni upuuzi kusema kuwa Mwalimu Nyerere aliichafua nchi.

Binafsi, siku nitakapoona Tundu Lissu anaichafua nchi, sitamlazia damu. Lakini sijaona. Badala yake, nimemsikia akitangaza kwamba yuko tayari kuitumikia nchi katika nafasi ya uongozi, iwapo atapata ridhaa. Ameelezea kuwa akishika uongozi, ataweka utawala wa sheria, haki za binadamu, na demokrasia. Kila mwenye kuwania uongozi wa nchi ana haki na wajibu wa kutueleza ana malengo gani. Kwa hayo malengo yake, sioni mantiki yoyote ya kusema kuwa Tundu Lissu anaichafua nchi.
Professor, mwalimu alilisemea hili ughaibuni?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna mtu analazimisha akili zetu watanzania wote tuziflash kwenye kipara chake. awaze yeye sisi tuitikie tu kama mang'ombe.
 
Wengi humu tulimsikia na kumfuatilia ndg Tundu kwa yote aliyoyanena huko ng'ambo.Wengi pia ama walimuunga mkono vilevile wengi pia hawakukubaliana naye.

Swali ni je kwa sheria zetu hapa Tz anayo kesi ya kujibu ama la?
 
Nawashauri CCM timizeni ahadi zenu kwa Watanzania ishu ya Lissu inazidi kuwachafua, kila mnaloandika mnazidi kujitia hatiani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengi humu tulimsikia na kumfuatilia ndg Tundu kwa yote aliyoyanena huko ng'ambo.Wengi pia ama walimuunga mkono vilevile wengi pia hawakukubaliana naye.

Swali ni je kwa sheria zetu hapa Tz anayo kesi ya kujibu ama la?
Mkosaji anahukumiwa kwa sheria ya nchi alikotendea kosa. Kama alichofanya ni kosa kwa mujibu za nchi aliyofanyia basi wale waliojeruhiwa Na kosa hilo wapeleke malalamiko kwenye mamlaka za sheria ya nchi husika.
Kama akirudi Tanzania mkamchokoza nae akaingia kwenye mtego kwa kurudia hayo atashitakiwa na kuhukumiwa chini ya sheria za Tanzania. Ili akamatwe na kushitakiwa lazima awepo mlalamikaji
 
Nyie serikali ya viwanda mmekosa cha kufanya ,nyie mnawaza kesi tu ,mmegeuka serikali ya vipalata ak.a.serikali ya vitambulisho vya machinga .
 
View attachment 1014113
Profesa Mbele akiongea na "Beberu" aliyefika kwenye meza yake wakati wa Tamasha la vitabu kwenye nchi Kuu ya Mabeberu Marekani. Kumbuka wengine huogopa kwenda kwenye nchi za mabeberu kwa kuwa hawajui kwa ufasaha Lugha na maisha ya watu kwenye nchi za Mabeberu.
Mkuu umenimaliza Mbavu Napiga Picha Hugo Beberu anavyosikiliza Kwa Makini.
 
Ahsante Profesa Mbele.Umetoa elimu ya bure kwa wale wasomi wenzio wanaofikiri kwa kutumia tumbo na mdomo na sio akili.Wamekumbwa na mihemuko ya kimaslahi na siasa majitaka na kuishia kutukana na kupayuka badala ya kutoa hoja au kujibu hoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom