Prof. Mbarawa ni Presidential material! Tuwaspot na kuwagroom Presidential materials au tumwache tu yeyote awe?

Paskali tatizo la Professor Mbaruki hachaguliki kwao,kajaribu mara mbili hakuwavutia wazanzibari kwa lolote.

Presidential materials kama akina JF Kennedy, Julius Nyerere, Ronald Reagan,Baraka Obama wana sifa mbili kuu mvuto na speech eloquence.
Huku kwetu mara nyingi tunalazimisha impossibles ,wachache wanaamlia wengi.

Huwo mvuto haupatikani shuleni ni natural.
Wadau,
Dr. Shein sio great orator kama Obama, JFK au Regan; yet alipenya.

Huenda "bahati kama hiyo" akaipata Prof. Mbarawa.

Maana siasa hapa duniani, pamoja na umahiri wa kujieleza, bahati nayo huwa ipo.
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali,
Naanza kwa swali la msingi, Jee Tanzania, Tuanze Utamaduni wa Kuwaspoti Watanzania Wenye Uwezo wa Uraisi, Yaani Presidential Materials, na KuwaGroom ili Tupate Rais Bora, Au Tuendelee Kuwaacha Tuu Mtanzania Yoyote
Mwenye Sifa na Vigezo, Anayeutaka Urais, Awe Tuu Rais Wetu Hata Kama Sio Presidential Material, Hivyo Kuwa na Hatari ya Uwezekano wa Kumpata Bora Rais Badala ya Raisi Bora?.

Sifa za Urais wa Tanzania.
Nafasi ya urais wa JMT, inashikwa na raia yoyote wa JMT mwenye sifa na vigezo. Tangu JMT imezaliwa mwaka 1964, hadi leo Zaidi ya miaka 53, ni Mtanzania mmoja tuu kutoka Zanzibar, aliyekidhi sifa na vigezo hadi kuweza kuwa rais wa JMT, Wazanzibari wengine wote wenye sifa waliojaribu, hawakuweza kupata kutokana na kuzidiwa sifa na vigezo na wagombea kutoka bara, matokeo yake hadi leo sisi bara ni 4 kwa 1 Zanzibar. Hali hii ilipelekea nikashauri
Je, kunahitajika affirmative action ili Mzanzibari aweze tena kuwa Rais wa JMT?

Lakini leo, baada ya kumsikiliza Mtanzania huyu ambaye ni Mzanzibari, Prof. Makame Mbarawa, kiukweli kabisa, nimemkubali sana kuwa ana kidhi sifa na vigezo hadi sifa za ziada za nationalism ya Utanzania kwanza, na ni mzalendo wa kweli, kwa sababu kwa kauli na matendo, amethibitisha pasi shaka kuwa yeye kwanza ni Mtanzania, kisha ni Mzanzibari, wakati kiukweli kabisa, kwa Wanzanzibari walio wengi, wao kwanza ni Wazanzibari kwanza, kisha ndio Watanzania.

Hebu msikilize Prof. Mbarawa.


Tuwachagize Presidential Materials Wagombee?.
Kuna Watanzania wengi wenye sifa za kutuletaa rais bora kabisa, lakini wengine hawana vyama, wengine wala hawauwazi urais, hivyo wanapotokea watu wenye sifa kama Prof. Mbarawa, unaweza kukuta ndio wale type ya watu hawauwazii hata huo urais, lazima wachagizwe, hata katika hao wagombea Zaidi ya 40 wa CCM ile 2015, sio wote waliutaka urais, kuna baadhi walifuatwa na kuchagizwa kwenda kuchukua fomu na kugombea, hivyo mnaonaje wale wote wenye presidential personalities, or presidential materials, tuwachagize waanze kufikiria kugombea.

Hitimisho, Tusisubiri Marais Wajitokee Tuu, Tuanze Kutengeneza Marais.
Kuna kauli isemayo, leaders are born and not made, Mimi ni muumini wa good leaders are made, besides kuwa born, hivyo lets start making our leaders by grooming them to be good leaders. Kwa upande wangu kwa 2020, nimeishamspoti mmoja kutoka upinzani,
Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? ...Ameonyesha ...

Na kwa 2025, niliishamspoti mmoja.
Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa ... - jamiiforums.com
huyu Prof. Mbarawa ni wapili, tuendelee kuwaibua presidential materials ili kufikia 2025, tupate viongozi bora, japo mimi binafsi niko kwenye lile kundi tunaotaka 2025 katiba ibadilishwe Magufuli aendelee kama nilivyouliza hapa.
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa ...

Namalizia kwa lile lile swali la msingi, Jee Tanzania, Tuanze Utamaduni wa Kuwaspoti Watanzania Wenye Uwezo wa Uraisi, Yaani Presidential Materials, na KuwaGroom ili Tupate Rais Bora, Au Tuendelee Kuwaacha Tuu Mtanzania Yoyote
Mwenye Sifa na Vigezo, Anayeutaka Urais, Awe Tuu Rais Wetu Hata Kama Sio Presidential Material, Hivyo Kuwa na Hatari ya Uwezekano wa Kumpata Bora Rais Badala ya Raisi Bora?.
Mfano mzuri ni huyu Prof. Mbarawa, achagizwe akampokee Dr. Shein pale Zanzibar, 2020, ili 2025, aje kumpokea Magufuli huku bara.
Jumamosi Njema,

Paskali
Inahitaji kuwa na jicho lililopevuka kuyaona haya uliyoyasema. Makame Mbarawa ndio BACKUP ya Dr. Hussein MWINYI kwa mtazamo wangu binafsi.
Endapo litatokea tusililoliomba kwa MWINYI basi huyu ndiye mbadala wake. Au endapo MWINYI atashindwa kuhimili vishindo huyu ndio plan B.
Kuna Jambo watu hawalioni , Mara ya mwisho kuwaona Hawa watu wawili wakihutubia watu hadharani au kwenye mikusanyiko ya kiserikali bila wizara zao kuhusika moja moja kwa moja ulikuwa lini na wapi. Au lini umewaona wamewekwa pamoja kwenye mkutano mmoja wa hadhara ,uzinduzi au sherehe Ni lini na wapi?
Huenda Mimi sio mwandishi wa habari ndio maana siwaoni pamoja. Labda wewe Paskali kwa ukongwe wako wa habari umekutana nao Sana, hebu tujuze.

Kama nadharia hizo nilizoziona Ni kweli na hawajawahi kukutanishwa basi hiyo sio bahati mbaya. Huenda They are our DESIGNATED PRESIDENTS to be.

Why? This
1. Yumkini wanalindwa wasichafuliwe na skendo za kisiasa.

2.Yumkini wanapikwa kukidhi mahitaji ya cheo Cha Urais siku zijazo.

3.Wanajaribiwa kwenye sehemu maeneo nyeti kwa manufaa ya baadaye.

Kwa Sasa wacha nikuunge mkono kwa kukwambia Wanaotuchaguliaga viongozi wameshamaliza zoezi la 2025 - 2035. Anayebisha asubiri nyakati na Majaliwa ya uhai. Hawa watu wawili wataongoza JMT na ZNZ.

Kilio Cha Rais kutoka Zanzibar watamaliza Hawa na kero ya Zanzibar kujiona wameminywa watamaliza Hawa, bara tupo Sana labda tujipange kwa 2035 -2045.
Ahsante.
 

asante sana Mama.
P
Mkuu wewe utateuliwa lini , hadi walioiba mitihani Galanos wanakushinda ?
 

asante sana Mama.
P
Pascal Mayalla hivi mama hakuoni kweli au anakupotezea :rolleyes:
 
Back
Top Bottom