Prof. Mbarawa ni Presidential material! Tuwaspot na kuwagroom Presidential materials au tumwache tu yeyote awe?

Pamoja na mengine, Sifa kubwa anayotakiwa kuwa nayo Rais wa Tanzania ni uwezo wa kupambana na ufisadi

Akiwa na uwezo wa kudhibiti ufisadi itakuwa msafi tu automatically yeye binafsi maana huwezi kuwa unaona na kula peke yako, si rahisi

Sasa tupe historia ya profesa mbarawa katika suala hili.
He is very clean na mchapa kazi asiye na makuu. Nilipata kusafiri naye ndege moja bila kujua kama ni Waziri kwa jinsi anavyojishusha. New comer kwenye CCM hana makundi. Ni Presidential material. Ni mojawapo wa mawaziri wachapa kazi na wanaofata nyayo za Rais Magufuli kwa kuchukia UFISADI
 
kitu kimoja ni chama cha mapinduzi kina watu wengi wazuri wanaofikiriwa kugombea urais ni wakati wa vyama vya upinzani kutengeneza watu wao badala ya kusubiri wagombea walioshindwa kwenye mchujo wa ccm
Ni vigumu Mbalawa kupata nafasi kwani wazanzibar wana laana pale walipomkataa Salim kwa vigezo vya kibaguzi kumbuka wao ndio waliongoza kumchafua kama salim angekuwa rais uwezo ambao angeonyesha sidhani kama tungekuwa tunawahofu kuja kututawala ila ulimbukeni wao ukiongozwa na aliyekuwa rais wao Amani abeid Karumewasubiri sana kutoa rais wa muungano
 
Pascal Mayalla umesahahu misingi yetu? Je amelelewa katika misingi ya ukatoliki?
maana Tanzania bila kuwa mkatoliki unajidanganya,
mpaka tukiachana na ule mkataba wa vatican waliotuwekea bond kupata uhuru mwaka 1951 ikaja kuwa 1961,

inabidi uwe mkatoliki tena anayejua kusoma Kodi za siri yaan KAMELELE MARIA AIJWILE ENEEMA, kama hujui hiyo basi uwe muislamu zuga ambaye umekulia katika misingi ya katoliki, anafaa mwinyi au majaliwa, mark my words
 
kitu kimoja ni chama cha mapinduzi kina watu wengi wazuri wanaofikiriwa kugombea urais ni wakati wa vyama vya upinzani kutengeneza watu wao badala ya kusubiri wagombea walioshindwa kwenye mchujo wa ccm
Ni vigumu Mbalawa kupata nafasi kwani wazanzibar wana laana pale walipomkataa Salim kwa vigezo vya kibaguzi kumbuka wao ndio waliongoza kumchafua kama salim angekuwa rais uwezo ambao angeonyesha sidhani kama tungekuwa tunawahofu kuja kututawala ila ulimbukeni wao ukiongozwa na aliyekuwa rais wao Amani abeid Karumewasubiri sana kutoa rais wa muungano
Rais Magufuli man of decision hawezi kuleta mabadiliko yote halafu akiondoka mafisadi warudi tena. Atahakikisha ataacha nchi kwenye mikono salama inshaalah Mungu akipenda
 
miaka kumi katiba ya wapi ?
wacheni ulevi wa kuifanya katiba ya ZANUPF akaMACCM kuwa katiba ya nchi.
Pole, naona hukunisoma vizuri, Nilimaanisha miaka 5 iliyopo inatosha, kama aliyepo akiamua kugombeana akishinda, inakuwa mara ya mwisho. Miaka 5 inatosha. Rais wa miaka muda mrefu hawezi kuleta jipya. Wanajisahau na kuanza kufikiri ni wao tu ndio wanaoweza kuongoza. Hata Marehemu baba wa Taifa alisema, inatosha, akasems hata mkinipa miaka mingine, sitakuwa na jipya.
 
watu wa bara wameitawala zanzibar mfululizo,mkapa,kikwete,magu

natarajia mpambano mkali na mtoto wa mwinyi ambaye ni waziri wa ulinzi

pia mbarawa ajiepushe na kundi la kipara,maana linapingwa sana

pia nashauri apewe muda awe waziri wa mambo ya nje akapate uzoefu,tunaona wa sasa anavyoyumba katika siasa za kimataifa
Maiga hayumbi. Anayumbishwa. Mwanadiplomasia number moja nchi yoyote ni Rais. Ours is a disaster!
 
Nimekusoma Mkuu Paskal!Hongera kwa uchambuzi japo kuna baadhi ya Maneno ni mishale ya moto kwa walengwa.Kuna watu ukiangalia haiba zao,kauli zao,misimamo yao,historia yao kimsingi wanafaa kuwa marais kwa sasa Makame Mbarawa ni best choice yangu!Mama Samia na Hussein Mwinyi wako vizuri pia!Lkn CCM wakiacha kutengeneza mfumo wa kuandaa viongozi hasa urais tutarajie watu wanajitengeneza ambao wakifanikiwa kuwa marais tutashuhudia kauli na vitendo vyenye harufu ya chuki,uhasama na visasi.
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali,
Naanza kwa swali la msingi, Jee Tanzania, Tuanze Utamaduni wa Kuwaspoti Watanzania Presidential Materials, na KuwaGroom ili Tupate Rais Bora, Au Tuendelee Kuwaacha Tuu Yoyote Anayeutaka Urais, Awe Hata Kama Sio Presidential Material?.

Sifa za Urais wa Tanzania.
Nafasi ya urais wa JMT, inashikwa na raia yoyote wa JMT mwenye sifa na vigezo. Tangu JMT imezaliwa mwaka 1964, hadi leo Zaidi ya miaka 53, ni Mtanzania mmoja tuu kutoka Zanzibar, aliyekidhi sifa na vigezo hadi kuweza kuwa rais wa JMT, Wazanzibari wengine wote wenye sifa waliojaribu, hawakuweza kupata kutokana na kuzidiwa sifa na vigezo na wagombea kutoka bara, matokeo yake hadi leo sisi bara ni 4 kwa 1 Zanzibar. Hali hii ilipelekea nikashauri
Je, kunahitajika affirmative action ili Mzanzibari aweze tena kuwa Rais wa JMT?

Lakini leo, baada ya kumsikiliza Mtanzania huyu ambaye ni Mzanzibari, kiukweli kabisa, nimemkubali sana kuwa ana kidhi sifa na vigezo hadi sifa za ziada za nationalism ya Utanzania kwanza, na ni mzalendo wa kweli, kwa sababu kwa kauli na matendo, amethibitisha pasi shaka kuwa yeye kwanza ni Mtanzania, kisha ni Mzanzibari, wakati kiukweli kabisa, kwa Wanzanzibari walio wengi, wao kwanza ni Wazanzibari kwanza, kisha ndio Watanzania.

Hebu msikilize Prof. Mbarawa.

Tuwachagize Presidential Materials Wagombee?.
Kuna Watanzania wengi wenye sifa za kutuletaa rais bora kabisa, lakini wengine hawana vyama, wengine wala hawauwazi urais, hivyo wanapotokea watu wenye sifa kama Prof. Mbarawa, unaweza kukuta ndio wale type ya watu hawauwazii hata huo urais, lazima wachagizwe, hata katika hao wagombea Zaidi ya 40 wa CCM ile 2015, sio wote waliutaka urais, kuna baadhi walifuatwa na kuchagizwa kwenda kuchukua fomu na kugombea, hivyo mnaonaje wale wote wenye presidential personalities, or presidential materials, tuwachagize waanze kufikiria kugombe.

Hitimisho, Tusisubiri Marais Wajitokee Tuu, Tuanze Kutengeneza Marais.
Kuna kauli isemayo, leaders are born and not made, Mimi ni muumini wa good leaders are made, besides kuwa born, hivyo lets start making our leaders by grooming them to be good leaders. Kwa upande wangu kwa 2020, nimeishamspoti mmoja kutoka upinzani,
Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? ...Ameonyesha ...

Na kwa 2025, niliishamspoti mmoja.
Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa ... - jamiiforums.com
huyu Prof. Mbarawa ni wapili, tuendelee kuwaibua presidential materials ili kufikia 2025, tupate viongozi bora, japo mimi binafsi niko kwenye lile kundi tunaotaka 2025 katiba ibadilishwe Magufuli aendelee kama nilivyouliza hapa.
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa ...

Namalizia kwa lile lile swali la msingi, Jee Tanzania, Tuanze Utamaduni wa Kuwaspoti Watanzania Presidential Materials, na KuwaGroom ili Tupate Rais Bora, Au Tuendelee Kuwaacha Tuu Yoyote Anayeutaka Urais, Awe Hata Kama Sio Presidential Material?.
Jumamosi Njema,

Paskali
Ukitizama kiongozi bora kwa eneo analotoka au analoliwakilisha nidhamu na uwezo wake aitoshi mfano Kiongozi bora Zanzibar ni sawa na kiongozi mmoja aliemudu kuongoza tarafa vizuri sana Tanzania wapo wengi sana .ukimchukua Raisi Rwanda au Burundi ni sawa na mkuu wa mkoa moja TZ Ukimchukua Raisi wa Kenya au Uganda mmoja wapo ni sawa na kiongozi mmoja mzuri tuu. Wa moja ya kanda kati ya kanda nne Tanzania .kwa maana hii yako Pascal ni kosa ataa kuiga aina ya uongozi kutoka Tarafa,wilaya,mkoa,kanda,kwa maana ya Rwanda.Burundi,Zanzibar,Kenya,Uganda,Sudani north or South ukaja kuutumia Tanzania .vinginevyo mara moja utaanza kuonekana unapendelea kanda au mkoa unao toka .na siaajabu ndio kinacho anzaa kuonekana kwasasa .Tz ni big Brother Africa Mashariki na kaati .Tunatakiwa Tunaiga Amerika,China,Brazil,Hispaania,india,na kadhalika uongozi na kiongozi awe mwenye mtazamo wa kitaifa na kimataifa na maana alievuka kila kitu ndio mzee .siasa za kuganga njaa
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali,
Naanza kwa swali la msingi, Jee Tanzania, Tuanze Utamaduni wa Kuwaspoti Watanzania Presidential Materials, na KuwaGroom ili Tupate Rais Bora, Au Tuendelee Kuwaacha Tuu Yoyote Anayeutaka Urais, Awe Hata Kama Sio Presidential Material?.

Sifa za Urais wa Tanzania.
Nafasi ya urais wa JMT, inashikwa na raia yoyote wa JMT mwenye sifa na vigezo. Tangu JMT imezaliwa mwaka 1964, hadi leo Zaidi ya miaka 53, ni Mtanzania mmoja tuu kutoka Zanzibar, aliyekidhi sifa na vigezo hadi kuweza kuwa rais wa JMT, Wazanzibari wengine wote wenye sifa waliojaribu, hawakuweza kupata kutokana na kuzidiwa sifa na vigezo na wagombea kutoka bara, matokeo yake hadi leo sisi bara ni 4 kwa 1 Zanzibar. Hali hii ilipelekea nikashauri
Je, kunahitajika affirmative action ili Mzanzibari aweze tena kuwa Rais wa JMT?

Lakini leo, baada ya kumsikiliza Mtanzania huyu ambaye ni Mzanzibari, kiukweli kabisa, nimemkubali sana kuwa ana kidhi sifa na vigezo hadi sifa za ziada za nationalism ya Utanzania kwanza, na ni mzalendo wa kweli, kwa sababu kwa kauli na matendo, amethibitisha pasi shaka kuwa yeye kwanza ni Mtanzania, kisha ni Mzanzibari, wakati kiukweli kabisa, kwa Wanzanzibari walio wengi, wao kwanza ni Wazanzibari kwanza, kisha ndio Watanzania.

Hebu msikilize Prof. Mbarawa.

Tuwachagize Presidential Materials Wagombee?.
Kuna Watanzania wengi wenye sifa za kutuletaa rais bora kabisa, lakini wengine hawana vyama, wengine wala hawauwazi urais, hivyo wanapotokea watu wenye sifa kama Prof. Mbarawa, unaweza kukuta ndio wale type ya watu hawauwazii hata huo urais, lazima wachagizwe, hata katika hao wagombea Zaidi ya 40 wa CCM ile 2015, sio wote waliutaka urais, kuna baadhi walifuatwa na kuchagizwa kwenda kuchukua fomu na kugombea, hivyo mnaonaje wale wote wenye presidential personalities, or presidential materials, tuwachagize waanze kufikiria kugombe.

Hitimisho, Tusisubiri Marais Wajitokee Tuu, Tuanze Kutengeneza Marais.
Kuna kauli isemayo, leaders are born and not made, Mimi ni muumini wa good leaders are made, besides kuwa born, hivyo lets start making our leaders by grooming them to be good leaders. Kwa upande wangu kwa 2020, nimeishamspoti mmoja kutoka upinzani,
Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? ...Ameonyesha ...

Na kwa 2025, niliishamspoti mmoja.
Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa ... - jamiiforums.com
huyu Prof. Mbarawa ni wapili, tuendelee kuwaibua presidential materials ili kufikia 2025, tupate viongozi bora, japo mimi binafsi niko kwenye lile kundi tunaotaka 2025 katiba ibadilishwe Magufuli aendelee kama nilivyouliza hapa.
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa ...

Namalizia kwa lile lile swali la msingi, Jee Tanzania, Tuanze Utamaduni wa Kuwaspoti Watanzania Presidential Materials, na KuwaGroom ili Tupate Rais Bora, Au Tuendelee Kuwaacha Tuu Yoyote Anayeutaka Urais, Awe Hata Kama Sio Presidential Material?.
Jumamosi Njema,

Paskali

Pascal,

Ni kweli Makame Mbarawa has very well-developed self awareness. He speaks softly and never shouts. Lakini kama unawafahamu Wapemba vizuri, wengi wako hivyo. They are not naturally predisposed to shouting. Hii ni tabia ya kiungwana ambayo ni sehemu ya desturi zao.

Lakini “u-sure” na tabia ya uungwana katika kuongea pekee havimfanyi mtu kuwa presidential material. Ni lazima sisi kama taifa tujitambue: tufahamu matatizo yetu ni yapi, tuko wapi na tunaelekea wapi na hapo ndipo tutakapokuwa katika nafasi ya kutambua tunataka kiongozi (rais) wa aina gani.

Tanzania ni nchi maskini. Miaka 56 ya uhuru bado nchi inaogelea katika dimbwi la umaskini na hadi sasa hakuna dalili yoyote ya kujinasua. Kwa upande mwingine, mtu ambaye ni presidential material ni lazima afahamu njia na namna ya kuiondoa nchi hapa ilipo na kuipeleka mbele kwa kasi kubwa kuelekea maendeleo ya kweli na endelevu.

Kati ya matatizo makubwa yanayoikabili Tanzania kwa sasa ni athari za kuwa na katiba mbovu isiyoweka misingi thabiti ya kidemokrasia, utawala wa sheria, mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili ya dola na checks and balances. Hiki pekee ni kikwazo kikubwa cha maendeleo kwa sababu mifumo ya kiutawala iliyopo haitoi fursa kwa sauti za wananchi kusikilka.

(Tafiti kadhaa zimethibitisha kuwepo kwa uhusiano wa moja kwa moja kati ya utawala wa kidemokrasia na maendeleo ya kiuchumi. Soma hii mada: Political Institutions, Economic Growth, and Democracy: The Substitute Effect).

Kwa upande mwingine, kazi kubwa ya rais ni kutekeleza maono yake kwa nchi yake na kusimamia tunu za taifa (katiba, sheria, nk). Sasa swali la kujiuliza ni je, Mbarawa ana maono gani kwa hii nchi? Ili kuweza kutathmini maono yake ni lazima kufahamu itikadi yake (imani yake ya kisiasa na kijamii) ni ipi.

Uzoefu unathibitisha kuwa Mbarawa hana hata chembe ya u- presidential material. Hafai! Mbarawa hana rekodi yoyote inayoonyesha kuwa yeye ni muumuni wa kweli wa demokrasia, utawala wa sheria na haki za raia. Akiwa waziri, wizara yake imetekeleza ubomoaji wa kikatili wa maelfu ya makazi ya raia ilhali kukiwa na zuio la mahakama. Kiuhalisia Mbarawa, kama msimamizi mkuu wa sera katika wizara yake, ni mtuhumiwa nambari wani wa uhalifu wa kudharau amri ya mahakama na ukiukaji wa haki za binadamu. Na hapa hawezi kujinasua kamwe!

Kutokana na maelezo haya, ni maoni yangu kuwa badala ya kujadili ni nani ambaye ni presidential material, ni vema tukajikita katika kupigania nchi iwe na taasisi imara za kisiasa na za kiutawala ambazo zitatoa fursa, in the first place, kwa mtu ambaye kweli ni presidential material kuwa rais. Hivyo, katiba mpya ni hitaji la lazima kwa Tanzania.
 
Anayetembelea magongo hawezi kuongoza! Kabla ya kutaja majina ya watu 'presidential material' tujikite kwanza kuainisha aina ya nchi tunayohitaji pamoja na vigezo vya kiongozi wake mkuu ajaye. Kwanza kabisa nadhani tunahitaji nchi xa jamii iliyostaarabika inayothamini uhai wa binadamu na inayochukia ulaghai wa aina yoyote katika kutafuta uongozi wa kisiasa. Pili, more than anything else, nchi hii sasa inahitaji kiongozi mkereketwa wa haki za binadamu; uncompromising kwenye suala la haki za binadamu na raia. Tunataka kiongozi jasiri ambaye atatambua kuwa jukumu lake la kwanza ni kuthamini na kulinda kwa nguvu zote uhai wa kila raia na hivyo kutumia akili yake yote na mamlaka yake yote kuung'oa huu ushetani unaonyemelea nchi yetu wa kudhani usalama wake unahitaji baadhi ya raia kunyang'anywa uhai.

Sandinistas, naunga mkono hoja yako kwa aslimia mia moja. Mawazo yako yanashabihiana na mtazamo wangu katika post yangu hapo juu.

Cheers!
 
kitu kimoja ni chama cha mapinduzi kina watu wengi wazuri wanaofikiriwa kugombea urais ni wakati wa vyama vya upinzani kutengeneza watu wao badala ya kusubiri wagombea walioshindwa kwenye mchujo wa ccm
Ni vigumu Mbalawa kupata nafasi kwani wazanzibar wana laana pale walipomkataa Salim kwa vigezo vya kibaguzi kumbuka wao ndio waliongoza kumchafua kama salim angekuwa rais uwezo ambao angeonyesha sidhani kama tungekuwa tunawahofu kuja kututawala ila ulimbukeni wao ukiongozwa na aliyekuwa rais wao Amani abeid Karumewasubiri sana kutoa rais wa muungano

Ubaguzi si kitu kizuri.
 
Hatuhitaji 'presidential material or non presidential material' - people change pictures dont! Tunahitaji msingi bora na imara ambao hautabadilika bila theluthi mbili ya wananchi wa jamhuri hii yaani katiba iliyo bora ili kwamba hata tukiweka jiwe litazingatia matakwa na mahitaji ya watu wetu niliwahi kusema tuliwapa CCM nchi cheki tunavyoisoma namba naogopa pia kuwapa CHADEMA wasije wakabadili gia angani .Tumepotea kama taifa kwa hiyo inabidi tuanze upya vinginevyo tiutazidi kutokomea mwisho tutaingia kwenye shimo ambalo tutashindwa kutoka!
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali,
Naanza kwa swali la msingi, Jee Tanzania, Tuanze Utamaduni wa Kuwaspoti Watanzania Wenye Uwezo wa Uraisi, Yaani Presidential Materials, na KuwaGroom ili Tupate Rais Bora, Au Tuendelee Kuwaacha Tuu Mtanzania Yoyote
Mwenye Sifa na Vigezo, Anayeutaka Urais, Awe Tuu Rais Wetu Hata Kama Sio Presidential Material, Hivyo Kuwa na Hatari ya Uwezekano wa Kumpata Bora Rais Badala ya Raisi Bora?.

Sifa za Urais wa Tanzania.
Nafasi ya urais wa JMT, inashikwa na raia yoyote wa JMT mwenye sifa na vigezo. Tangu JMT imezaliwa mwaka 1964, hadi leo Zaidi ya miaka 53, ni Mtanzania mmoja tuu kutoka Zanzibar, aliyekidhi sifa na vigezo hadi kuweza kuwa rais wa JMT, Wazanzibari wengine wote wenye sifa waliojaribu, hawakuweza kupata kutokana na kuzidiwa sifa na vigezo na wagombea kutoka bara, matokeo yake hadi leo sisi bara ni 4 kwa 1 Zanzibar. Hali hii ilipelekea nikashauri
Je, kunahitajika affirmative action ili Mzanzibari aweze tena kuwa Rais wa JMT?

Lakini leo, baada ya kumsikiliza Mtanzania huyu ambaye ni Mzanzibari, Prof. Makame Mbarawa, kiukweli kabisa, nimemkubali sana kuwa ana kidhi sifa na vigezo hadi sifa za ziada za nationalism ya Utanzania kwanza, na ni mzalendo wa kweli, kwa sababu kwa kauli na matendo, amethibitisha pasi shaka kuwa yeye kwanza ni Mtanzania, kisha ni Mzanzibari, wakati kiukweli kabisa, kwa Wanzanzibari walio wengi, wao kwanza ni Wazanzibari kwanza, kisha ndio Watanzania.

Hebu msikilize Prof. Mbarawa.

Tuwachagize Presidential Materials Wagombee?.
Kuna Watanzania wengi wenye sifa za kutuletaa rais bora kabisa, lakini wengine hawana vyama, wengine wala hawauwazi urais, hivyo wanapotokea watu wenye sifa kama Prof. Mbarawa, unaweza kukuta ndio wale type ya watu hawauwazii hata huo urais, lazima wachagizwe, hata katika hao wagombea Zaidi ya 40 wa CCM ile 2015, sio wote waliutaka urais, kuna baadhi walifuatwa na kuchagizwa kwenda kuchukua fomu na kugombea, hivyo mnaonaje wale wote wenye presidential personalities, or presidential materials, tuwachagize waanze kufikiria kugombea.

Hitimisho, Tusisubiri Marais Wajitokee Tuu, Tuanze Kutengeneza Marais.
Kuna kauli isemayo, leaders are born and not made, Mimi ni muumini wa good leaders are made, besides kuwa born, hivyo lets start making our leaders by grooming them to be good leaders. Kwa upande wangu kwa 2020, nimeishamspoti mmoja kutoka upinzani,
Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? ...Ameonyesha ...

Na kwa 2025, niliishamspoti mmoja.
Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa ... - jamiiforums.com
huyu Prof. Mbarawa ni wapili, tuendelee kuwaibua presidential materials ili kufikia 2025, tupate viongozi bora, japo mimi binafsi niko kwenye lile kundi tunaotaka 2025 katiba ibadilishwe Magufuli aendelee kama nilivyouliza hapa.
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa ...

Namalizia kwa lile lile swali la msingi, Jee Tanzania, Tuanze Utamaduni wa Kuwaspoti Watanzania Wenye Uwezo wa Uraisi, Yaani Presidential Materials, na KuwaGroom ili Tupate Rais Bora, Au Tuendelee Kuwaacha Tuu Mtanzania Yoyote
Mwenye Sifa na Vigezo, Anayeutaka Urais, Awe Tuu Rais Wetu Hata Kama Sio Presidential Material, Hivyo Kuwa na Hatari ya Uwezekano wa Kumpata Bora Rais Badala ya Raisi Bora?.
Mfano mzuri ni huyu Prof. Mbarawa, achagizwe akampokee Dr. Shein pale Zanzibar, 2020, ili 2025, aje kumpokea Magufuli huku bara.
Jumamosi Njema,

Paskali

Paskali tatizo la Professor Mbarawa hachaguliki kwao,kajaribu mara mbili hakuwavutia wazanzibari kwa lolote.

Presidential materials kama akina JF Kennedy, Julius Nyerere, Ronald Reagan,Baraka Obama wana sifa mbili kuu mvuto na speech eloquence.
Huku kwetu mara nyingi tunalazimisha impossibles ,wachache wanaamlia wengi.

Huwo mvuto haupatikani shuleni ni natural.
 
Back
Top Bottom