TUNDU LISSU mwanaharakati mzuri lakini siyo presidential material.

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Baada ya kumtafakari sana Mheshimiwa Tundu Lissu imebidi nikiri kutoka sakafu ya moyo wangu huyu atatusaidia sana kwenye kuainisha matatizo yaliko lakini hana majibu yake na haya ni mapungufu makubwa ambayo hatuwezi kuyafumbia macho.

Moja, alijivunia umaarufu kwa kukosoa serikali zote mbili za JK na JPM lakini hakupendekeza nini kifanyike kutibu matatizo aliyoyaona.

Mbili, JK alishangaa watu wanamwamini pamoja ana wapotosha kwenye uhaja wa katiba mpya na hili Lissu alilithibitisha alipounga mkono rasimu ya Warioba ambayo haikuwa na upya wowote zaidi ya kuzigeuza sheria za kawaida kuwa kanuni za kutunga sheria kinyume na matakwa ya kuandika katiba.

Tatu, alihoji Mwendazake kuvunja mikataba lakini hajawahi kutoa mbadala hata mmoja,

Nne, baada ya kovid- 19 kukimbia na ubunge wa viti maalumu Tundu Lissu alikuwa mstari wa mbele kushinikiza wafukuzwe uanachama bila ya kujua alikuwa anakidhoofisha chama chake.

Tano, swala la bandari kajikita katika uonevu wa kihistoria lakini hatujuzi ufumbuzi wake uko wapi. Ni kweli sisiemu imecheza faulo lakini sasa tufanye nini na mikataba wamekwisha kusaini na hawana mpango wa kujitoa.

Sita, angependa tupate katiba mpya lakini hadi leo yeye na wenzie hawajawahi kuandika rasimu yao ili tuweze kuimulika kwenye darubini. Sana sana kavalia njuga mapungufu tu ya katiba iliyopo bila kutupa mbadala na tukielewa hakuna katiba kamilifu. Yaani hata watakapopendekeza kama ipo itakuwa na dosari nyingi tu.

Mwisho, baada ya kumtafakari kwa undani tumefikia kumwona siyo kiongozi wa kutegemewa kuongoza nchi bali ni mhamasishaji mzuri na pia mwanaharakati lakini siyo presidential material atakuja kuwa kama Raila Amolo Odinga tu.
 
Huyu jamaa ata ujumbe wa halmashauri ya kijiji hafai.
 
Mwanaharakati yeyote mzuri na liberal ni kiongozi bora na ni presidential material.
 
Back
Top Bottom