prof maji marefu

MARASA YOKOHAMA

New Member
Mar 29, 2011
3
0
Kwa jinsi huyu mbunge alivyochangia hoja bungeni, nashindwa kuamini kura alipataje! Au wanaume nao wana viti maalum????
 
Ha ha ha ha kasema eti alichukuwa amepanga kuzungumza eti tayari wasemaji wa mwanzo wamekisema so hana cha kusema "wamemfilisi" kweli huyu mganga ni wa kiti maalum
 
Tuweni wazi na wakweli,viongozi wengi wa CCM hawana uwezo wa kujenga hoja....Maji Marefu ni baadhi wa wabunge wengi ambao ni wadhaifu kwenye kujenga hoja na kuzungumza kama kiongozi.....Angalia vijana kama Godbless Lema,Sugu mwenyewe anajenga hoja kwa umakini,John Mnyika nk....hawa ni baadhi ya watu makini toka CDM ambao unapowasikiliza utagundua jambo kwenye kujenga hoja.....
 
Ndivyo tulivyoamua kulingana na katiba yetu tuliyotungiwa. Tusishangae. Wakati leo hii hata mhudumu wa ofisi anatakiwa kuwa na elimu ya kidato cha nne, viongozi wa kuchaguliwa wanatakiwa kujua kusoma na kuandika tu. Tusimshangae. Huo ndio umakini watu.
 
Majimarefu hata hajui kuwa kile kiwanda cha mkumbala [TEMBO CHIPBOARDS] kilitaifishwa zamani na sasa ni mali ya watu binafsi!! Bado anazungumzia habari ya mamlaka ya mkonge hana habari kuwa wakina Shamte wamekwishagawana mashamba!! Wabunge wa kijani ni vilaza kweli kweli!!
 
Marehemu Remy Ongala alishaimba zamani,ila binadamu hatusikilizagi na kuelewa.UBAYA TUMEUKARIBISHA WENYEWE,wewe unajua huyu ni fundi viatu eti unamchagua kuwa mwenyekiti wa CCM,katiba ya chama anajua, hajui........... matokeo yake?Profesa Maji Marefu...
 
Wajenga hoja wapo cdm na wapiga porojo (makamba, hiza, msabaha, shigela, kikwete, ridhiwan, salma, ...) wapo chama cha majambozi!
 
teh teh teh teh! Et ki2 la saba B! Ahahahahahaaaaa... B unampa umaarufu mkuu! Ki2 cha saba D hicho af shule ya kata...
 
Kwa jinsi huyu mbunge alivyochangia hoja bungeni, nashindwa kuamini kura alipataje! Au wanaume nao wana viti maalum????

Jaman kipind cha kampen nilibahatika kuwepo kwenye jimbo la bwana maji marefu kama mdau wa mambo ya uchaguzi, nilihusika vipi ni siri yangu. Unajua watu wa mkoa/jimbo lake huwa huamini sana ushirikina sasa yeye ahadi aliyotoa ni kuwasaidia kuwatambua wachawi wanaowaloga watoto wao na wanaofanya majirani zao wasifanikiwe kwenye mashamba yao.

Sasa mambo ya chini ya kapeti katika siasa ndani ya chama ilikuwa ni namna gani mheshimiwa huyu maji marefu atakavyofanya kwani elimu yake ni darasa la saba na miswada mingi bungeni ni ya kiingereza. Yeye mwenyewe akawa na matumaini kuwa Bendera angemsaidia sana kwani CCM walishapanga kwenye kura ya maoni kumpitisha kwa nguvu, lakini tofauti na matarajio yao vijana wa Korogwe mjini wakafanya juu chini kumpinga Bendera na hivo Mheshimiwa Maji marefu akachinjiwa baharini na ndo maana mayaona hayo madudu huko bungeni.

Na bado atayafanya madudu mengi kwani elimu yake yenyewe mgogoro. Watanzania walimuacha mtu mwenye elimu na kumpatia kura huyu ambae hata upeo hana japo wanasema aliwajengea shule na watoto wao wanasoma. Alikurupuka tu kutoka Nairobi alikokuwa akiagua na kuja kipindi cha uchaguzi kugombea.

Hiyo ndo historia fupi ya Bwana Maji Marefu uingia bungeni kama muwakilishi wa wananchi wa jimbo la Korogwe vijijini.
 
Hivi yule mke wa mtu ambaye inasabikika alishirikiana naye kupora mali ya mume wa mama huyo na watoto wakaja juu ile kesi imeishia wapi kule kenya...

Jamaa alishirikiana na mke wa mtu kupora mali za familia..
 
kama we humkubali wananchi wake wamemkubali na wamemtuma lol!!!!
 
Ngoja Maji Marefu awatumie MAJINI mnaochana kuhusu elimu na uwezo wake wa kujenga hoja ndio mtatia akili kama hamjamfata mchana kweupe na Paka Mweusi na Mbuzi wa kijani kama masharti ya dawa.
 
Back
Top Bottom