Prof. Maghembe amekalia kuti kavu

Katika siku zote leo ndio nimekuona kichwa! hongera sana mkuu

hata mimi nimeshangaa ile taarifa ya kuachiwa kwa mifugo bila masharti yoyote
Ulitaka hiyo mifugo iachiwe kwa masharti gani..?
 
Hizo chuki za kikabila peleka kwenu. Ng'ombe zilikuwa detained kwa kosa gani..?
 
Sijui nisemeje ila sijawahi kumkubali Prof Maghembe. Magumashi matupu
 
Rafik issue ya kagera huyo jamaa aliyetumbuliwa alikiuka agizo la serikali la kutoshika ngombe ambazo ziko kwenye hifadhi hadi pale watapata maeneo ya kulisha hiyo mifugo na hilo lilisemwa bungeni in June
 
Maghembe hachomoki....ni vyema viongozi wetu wakajua sasa hivi kila linalofanyika popote linanaswa na vyombo vya usalama na ikibidi linatua mezani kwa Rais haraka. Acheni kufanya kazi kwa mazoea ....JPM hatanii na ana full support ya vyombo vyote vya ulinzi na usalama. Dawa ni moja tu ....fata sheria hata uwe nani ....this is very serious ......wanaofikiri ni nguvu ya soda wataumia bure ....
 
--SIONI TATIZO LAKE/
TUACHE CHUKI BINAFSI...
Hebu chukulia Waziri kaagiza ng'ombe wasikamatwe had wafugaji watakapotengewa maeneo mbadala, halafu Mhifadhi akakaidi unadhan kuna kuheshimiana hapo..? Watu wanapenda kula nyama kila siku lakn hawatak kujua hao ng'ombe wanatoka wapi na wanakula nin. Shiiida..!
 
Wewe huyo huyo ndiye uliunga mkono pale ambapo katibu mkuu wa chama chako walipoitwa mawaziri mizigo maghembe akiwa mmoja wa hao mawaziri mizigo!...Alipoteuliwa na mkulu,Ukaonyesha wasiwasi kwa prof!.....Baada ya suku 100 prof.akiwa ofisini kama waziri,Ukasema kuwa prof ana kasi ya utendaji unayoendana nasi ya mkulu!....Leo umeibuka na kusema prof amekalia kuti kavu na hana uwezo wa kuongoza wizara!...Angalia mkuu usije kuwa vuguvugu kwani watakutapika!.....uck mwema
 
 
Ila hii habari ni mpasuko kwa kweli. Yaani Waziri anamsimamisha muhifadhi kwa kusimamia sheria!!!

Kuna thread ilikuja humu ya Msukuma kushinikiza jamaa asimamishwe. Ramo Makani naye kaingia mtegoni. Huku unasimamisha muhifadhi wa wanyama wetu, Rais anafanya ziara shtukizi anakutana na vitu Wizarani kwako.

Kama ni mie ningeandika resignation letter mapema sana. Aibu hii ataificha wapi? Na sauti lake lile sasa...
 
Kuna jangili mmoja anaitwa Lazaro Nyalandu sijui wanamuacha vipi. Huu tunaohangaika nao ndio mtandao wake aliomkabidhi Maghembe.
 
rais alikuwa halali anawapima hawa wateule wake afu wewe unasema aliteua wenye uwezo mdogo! huu kama sio uchochezi ni nini?!
 
Haina haja na sidhani kama atamtumbua... wakati anamteua alijua kabisa uwezo wake... na sio Maghembe tu... wapo wengi walioteuliwa kwa kigezo cha ukada...

Na usishangae akitolewa huyo akawekwa Lipumba..
 
Ili mambo yawe mazuri inabidi yaharibike kwanza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…