Baada tu ya waziri Mkulo kumaliza kuwasilisha bajeti ya mwaka huu bungeni, mwandishi wa TBC1 akiwa anawahoji wadau nje ya bunge akakutana na Prof. Lipumba (Mchumi).
Mbali na kukosoa mambo kadhaa Lipumba kasema moja ya mapungufu ya bajeti hii ni kuwa tofauti na ile ambayo serilkali iliwasilisha IMF.
Hii mi sijaelewa inakuwaje. Ina maana huwa bajeti za nchi zote duniani huwa zinawasilishwa kwanza IMF kabla hazijasomwa katika mabunge ya nchi husika!!?
UPDATED (9th June 2011):
Mwenyekiti wa CUF bw Lipumba ameichambua bajeti na kubainisha mapungufu kadhaa yakiwemo;
[LIAirport toST=1]
[*]Matumizi ya kawaida ya serikali (trilioni 8) ni makubwa kuliko mapato ya ndani ya serikali (trilioni 6). Kwa maana hiyo serikali itakuwa inakopa fedha kugharamia matumizi ya kawaida
[*]Bajeti haijaainisha mapato yatokanayo na sekta ya madini, ambapo kwa mujibu wa Bw. Lipumba, wakati mauzo ya madini nje ni zaidi ta trillion moja, mapato ya serikali katika sekta hiyo ni bilioni 40 tu
[*]Bajeti imeshindwa kuonyesha utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa miaka mitano uliozinduliwa juzi na raisi. Kwa maana hiyo ama mpango huo ni usanii, au bajeti haitatekelezwa kama ilivyowasilishwa
[/LIST]