Prof. Lipumba na Bajeti ya 2011/2012 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Lipumba na Bajeti ya 2011/2012

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kilimasera, Apr 27, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, inayotarajiwa kusomwa katika Mkutano ujao wa Bunge, itakuwa ngumu.

  Aliyasema hayo jana alipozungumza katika mahojiano maalum na NIPASHE, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam juzi.

  Alisema ugumu wa bajeti hiyo, unatokana na viashiria kuonyesha uwezekano mkubwa wa nchi wafadhili na taasisi wahisani duniani wanaosaidia bajeti ya serikali kupunguza misaada yao katika bajeti ya mwaka huu.

  "Bajeti ya mwaka huu itakuwa ngumu, ngumu, ngumu sana," alisema Profesa Lipumba alipotakiwa na NIPASHE kutoa maoni yake kwamba, nini kifanyike ili hali iwe nzuri katika bajeti ya mwaka huu.

  Profesa Lipumba alisema nchi wafadhili na taasisi wahisani zinazosaidia bajeti ya serikali, zitapunguza misaada yao kutokana na baadhi yao kukabiliwa na matatizo ya kiuchumi na nyingine kuchukizwa na mambo kadhaa yanayofanywa na serikali ya Tanzania. Baadhi ya mambo hayo, ni pamoja na usimamizi mbaya wa fedha, ambazo serikali hupata.

  "Nchi za Ulaya zinapunguza misaada. Kwa mfano kama Ireland wana matatizo. Sasa kama walikuwa wakikusaidia dola milioni 6, hawawezi kukusaidia tena kiasi walichokuwa wakikusaidia," alisema Profesa Lipumba. Alisema Uholanzi ni miongoni mwa nchi wafadhili, ambazo hazifurahishwi na serikali inavyosimamia fedha inazopata.

  Alisema kielelezo kimojawapo kinachothibitisha usimamizi mbaya wa fedha za umma, ni upotevu wa mabilioni ya shilingi kwa mwezi unaosababishwa na vitendo vya uchakachuaji ubora wa mafuta vilivyokithiri nchini. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Charles Mwijage, kumekuwa na takwimu tofauti za kiasi cha fedha, ambazo serikali hupoteza kwa mwezi kutokana na vitendo vya uchakachuaji ubora wa mafuta nchini.

  Mwijage, ambaye pia ni Mbunge wa Muleba Kaskazini (CCM), alisema tofauti hiyo inaonekana katika taarifa ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambayo inaeleza kuwa fedha, ambazo serikali hupoteza kwa mwezi kutokana na uchakachuaji ubora wa mafuta ni Sh. bilioni 25.
   
 2. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Huyu mjinga hajanyamaza tu? yale aliyomshauri rais mwinyi ikulu ndio bado anatuletea? yeye na mwinyi walifanya lipi zuri kuondoa umaskini?
   
 3. E. J. Magarinza

  E. J. Magarinza Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Baada tu ya waziri Mkulo kumaliza kuwasilisha bajeti ya mwaka huu bungeni, mwandishi wa TBC1 akiwa anawahoji wadau nje ya bunge akakutana na Prof. Lipumba (Mchumi).

  Mbali na kukosoa mambo kadhaa Lipumba kasema moja ya mapungufu ya bajeti hii ni kuwa tofauti na ile ambayo serilkali iliwasilisha IMF.

  Hii mi sijaelewa inakuwaje. Ina maana huwa bajeti za nchi zote duniani huwa zinawasilishwa kwanza IMF kabla hazijasomwa katika mabunge ya nchi husika!!?

  UPDATED (9th June 2011):

  Mwenyekiti wa CUF bw Lipumba ameichambua bajeti na kubainisha mapungufu kadhaa yakiwemo;

  1. Matumizi ya kawaida ya serikali (trilioni 8) ni makubwa kuliko mapato ya ndani ya serikali (trilioni 6). Kwa maana hiyo serikali itakuwa inakopa fedha kugharamia matumizi ya kawaida
  2. Bajeti haijaainisha mapato yatokanayo na sekta ya madini, ambapo kwa mujibu wa Bw. Lipumba, wakati mauzo ya madini nje ni zaidi ta trillion moja, mapato ya serikali katika sekta hiyo ni bilioni 40 tu
  3. Bajeti imeshindwa kuonyesha utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa miaka mitano uliozinduliwa juzi na raisi. Kwa maana hiyo ama mpango huo ni usanii, au bajeti haitatekelezwa kama ilivyowasilishwa
   
 4. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Unauliza jibu!!
   
 5. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ndio maana ya kuwa nchi tegemezi duniani wakati una rasilimali za kukufanya uwe mtegemewa!
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  On the red: Yes. Serikali wanapeleka kwa wafadhili wote kabla ya kusomwa bungeni. Kumbuka December mwaka jana kulikuwa na malumbano kati wa serikali na wafadhili wanaochangia kwenye bajeti ya serikali (GBS) na chanzo ilikuwa ni huu usanii wa kuwa na different versions za budget. Maandalizi ya bajeti iliyosomwa leo yalianza mwaka jana wafadhili waligundua 'holes' kwenye numbers. Nadhani wakina Mkullo walijisahau kuwa wenzetu sio wavivu wa kusoma, wao wanaangalia kila nukta na koma. Nahisi hata hii version ya bajeti aliyosoma Mkullo itawaletea serikali matatizo kwa sababu iko kisiasa zaidi wakati ukweli vianzo vya mapato vya ndani ni 'matatizo'.
   
 7. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,448
  Likes Received: 781
  Trophy Points: 280
  Bajeti hii inategemea IMF, Word Bank na Lundo la wafadhili.Wasipofanya hivyo hizo pesa nyingine watazipata wapi?Hawatakuwa na kiburi bila IMF.Kwani hawajafanya home work yao kama watawala.
   
 8. oba

  oba JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Obvious, bajeti iliyosomwa leo ukiwakabidhi wachumi waliobobea IMF watakuona zoba maana huku wananchi wako wakiwa na njaa katikati ya utajiri( kuwa na maisha duni wakati tuna raslimali nyingi na za kutosha) wewe unangangania kipato kitokane na kodi za pombe!
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ukiomba mkopo ktk financial institution yeyote wanaweza kudai upeleke financial statement yako na business plan hivyo sii jambo la ajabu kwani hata ukiomba visa tu wanaweza omba kuona account na mengineyo.. Ukisha kuwa taifa tegemezi bajeti sio siri tena na wala haijawa siri.
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Bajeti kimeo wee toka enzi za nyerere kila mwaka ushuru wa bia na sigara juua,yaani hakuna altenative sources za revenue!imagine recurrent exp ni 8tril wakati uwezo wetu wa mapato ni 7tril manake ata kulipana mishahara twangoja wahisani none sense kabsaaa!ni vyema ukatembeza kapu kwa ajili ya development expenditures not otherwise
   
 11. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Ndugu yangu hili kama linafanyika itakuwa kwa nchi zetu masikini hasa za kiafrica ambazo bado hatujapata uhuru.
   
 12. fikirini

  fikirini Senior Member

  #12
  Jun 8, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tumezidi kuwanyenyekea akina IMF,WB kwa uvivu na ubinafsi wa viongozi wetu.
   
 13. k

  kany Member

  #13
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 20, 2010
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaonaje mkuu? Tukiungana kama Egypt hatuwezi kumpata kiongozi atakayeweza kupigania maslahi yetu kama watanzania na kuondokana na huu ubinafsi uliopo? Na pia tukiwaelimisha askari wetu kuwa tunapodai maslahi ya nchi ni pamoja na wao si watatuelewa waache kupiga watu watakapoandamana???? Mimi naamini inawezekana mkuu. Ni hayo tu
   
 14. M

  MPG JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bajeti ya kipumbavu wakati tunamadini tumebaki kutegemea pombe kama mbadala
   
 15. N

  Nonda JF-Expert Member

  #15
  Jun 9, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Gaddafi put an end to these futile pleas and offered US$ 300 million. The African Development Bank with US$50 million and the West African Development Bank with US$27 million contributed to the project which was brought to fruition in December 2007. Africa’s gain was Europe’s loss. No wonder Gaddafi has become a villain for France, Britain and other imperialists though he is a hero for Africa.

  Gaddafi had also pledged to fund three ambitious African projects — the creation of an African investment bank, an African monetary fund and an African central bank. Africa felt that these Africa-centred institutions were necessary to end its dependence on the IMF and the World Bank — institutions that prescribe unrealistic and unpopular measures to qualify for loans. These conditions which include measures to privatize natural resources and allowing unlimited access to foreign companies are designed to keep Africa eternally poor or dependant on the West. Libya had pledged funds for these projects from its investments in the United States. The US$ 30 billion which the Barack Obama administration froze (or robbed) at the first signs of the orchestrated troubles in the Libyan town of Benghazi was meant to finance these three African projects which would have given Africa some economic freedom.

  Soma hapa Gaddafi's refusal of the World Bank, IMF, Western multinationals & AFRICOM: the real casus belli obscured by 'humanitarian' deceits | empirestrikesblack
   
 16. N

  Nonda JF-Expert Member

  #16
  Jun 9, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Attack on World Bank
  Some of the revolutionary leaders who are here as my guests were obliged to create parties, and you may ask why have Mandela or Mugabe, or any of these other leaders, created a party? They were forced to and told: Either you do that or you will not get any loans from the World Bank. They did it because they felt obliged to and not because they believed in it...

  Let us talk about the World Bank, the IMF and the World Trade Organization. These must be ours or we will reject them. If it is a world bank it must then belong to all of us and it should not impose anything on us. But what it does is that it imposes its will on the people. Libya makes a huge contributions to the World Bank and the IMF. Therefore it is our bank. Why should anyone in America, or any other place, or on behalf of Zionism and imperialism, impose their terms on the peoples since the bank is not their bank but is the bank of each one of us?

  That is enough. Let us create the Mathaba's bank, the International Bank of the World Mathaba. Let us create a bank. We can create a bank and we will grant loans to one another [applause]. Let all our states withdraw their contributions from the World Bank and put them in this bank. Since the World Bank has become a nightmare and a sword hanging over our heads; and since it imposes humiliating and destructive terms on us; and since it controls the price of our children's bread and controls our food and drink, and also the price of fuel, clothes, food, drink and water, we do not want it, and let America and Zionism stay in it. They are welcome to stay in their bank.
  We should withdraw our contributions and create a bank for the Third World and for the forces part of this Mathaba [applause]. We have the support of all the organizations. As I have said the masses of Seattle are with us and are against all these nightmares. All the jobless in Europe, in their millions, are also with us...

  THE WORLD MATHABA
   
 17. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #17
  Jun 9, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Binafsi nimependa sana comments za Prof. Lipumba juu ya Bajeti, km mtaalamu wa mambo ya uchumi amesema bajeti hii INAMAPUNGUFU MENGI NA MAKUBWA SANA, kwani ktk bajeti hii utekelezaji wa ule mpango wa maendeleo, uliosomwa juzi na JK hauonyeshwi, then bajeti imeshindwa kuweka bayana mchango wa sekta ya madini ktk maendeleo, kubwa zaidi HII BAJETI KWA ASILIMIA KUBWA INATEGEMEA KUCHANGIWA TOKA KWA WAHISANI, SIO BUSARA KUJIVUNIA BUDGET TEGEMEZI! Ngoja akaipitie vyema then a ataiweka bayana!
   
 18. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #18
  Jun 9, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Mwenyekiti wa CUF bw Lipumba ameichambua bajeti na kubainisha mapungufu kadhaa yakiwemo;

  1. Matumizi ya kawaida ya serikali (trilioni 8) ni makubwa kuliko mapato ya ndani ya serikali (trilioni 6). Kwa maana hiyo serikali itakuwa inakopa fedha kugharamia matumizi ya kawaida
  2. Bajeti haijaainisha mapato yatokanayo na sekta ya madini, ambapo kwa mujibu wa Bw. Lipumba, wakati mauzo ya madini nje ni zaidi ta trillion moja, mapato ya serikali katika sekta hiyo ni bilioni 40 tu
  3. Bajeti imeshindwa kuonyesha utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa miaka mitano uliozinduliwa juzi na raisi. Kwa maana hiyo ama mpango huo ni usanii, au bajeti haitatekelezwa kama ilivyowasilishwa
  Source; TBC1
   
 19. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #19
  Jun 9, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Lipumba ni prof not bwana.....
  Kuhusu mada ni kwamba Lipumba amefafanua vizuri sana,na kila mwaka huwa anachambua kuhusu mambo hayo,ila sasa watengenezaji wa bajeti mbona hawaeleweki?????
   
 20. F

  FJM JF-Expert Member

  #20
  Jun 9, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hazina kuna upungufu mkubwa sana wa wataalam wa uchumi. Kwa muda wafadhili wamekuwa wanashauri Wizara ya Fedha wakope wataalam toka Bank kuu ambapo walau kuna watu wanaolewa mambo lakini hakuna kilichofanyika. Nahisi hata magogoni kuna udhaifu kwenye kitengo cha ushauri wa mambo ya ki-uchumi. Inawezekana waliopo wana vyeti vizuri na hata kinadharia wanaelewa uchumi lakini hawana concrete/creative ideas za kukabili changamoto za uchumi wa 'Nchi zinazoendelea'!

  Nilimuona rais juzi anasema Tanzania ni mojawapo ya nchi 20 duniani zilizo na uchumi uanokuwa kwa kasi kubwa! Statistically anaweza kuwa sawa, lakini inabidi akumbuke how big is the Tanzania's economy? Yaani ni hivi unaweza kuwa na mwanafunzi mmoja darasani leo, then kesho yake akaongezeka mwingine mmoja - statistically hapo utasema number ya wanafunzi ime-double!!! Viongozi wetu wajifunze kuona vitu in 'relative' terms! Si vyote ving'aavyo ni dhahabu!
   
Loading...