CUF Habari
JF-Expert Member
- Dec 12, 2019
- 239
- 234
NCHI HII INAHITAJI RAIS MCHUMI NA MWENYE HURUMA NA WATANZANIA MKINICHAGUA KUWA RAIS NTAFUTA UMASIKINI KATIKA NYANJA ZOTE"PROF.LIPUMBA"
IRINGA MJINI
Ukuaji wa uchumi wa Tanzania haujaambatana na kasi kubwa ya kupungua kwa watu masikini. Idadi ya watu masikini kwa kutumia kipimo cha taifa cha umasikini (mtu mzima kutumia shilingi 50,000/ au zaidi kwa mwezi) imeongezeka toka watu milioni 12.3 mwaka 2011 na kufikia watu milioni 14 mwaka 2018. Kwa kutumia kipimo cha kimataifa cha umaskini, Watanzania zaidi ya milioni 27 ni masikini.
Utafiti uliofanywa na serikali mwaka 2016 kuhusu umaskini wa watoto (Child Poverty in Tanzania) ulibaini kuwa asilimia 74 ya watoto wa Tanzania wanaishi katika mazingira ya umaskini kwa tafsiri pana inayojumuisha lishe, afya, hifadhi iliyo salama, elimu, mazingira, maji na makazi.