“Kwa mujibu wa Ibara ya 33(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana taswira tatu muhimu. Rais wetu ni Mkuu wa Nchi; Rais wetu ni Kiongozi wa Serikali; na Rais wetu ni Amiri Jeshi Mkuu. Kwa utambulisho huu wa kikatiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nembo muhimu ya umoja wa kitaifa. Kwa sababu hii, tuzingatie sana wosia wa Baba wa Taifa. Katika kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (uk.59-60), Mwalimu ametuasa: “…huwezi kumtikisa Rais wa Nchi bila kuitikisa nchi yenyewe. Ni vizuri jambo hili likatamkwa waziwazi”. Ndugu wanachama wenzangu na watanzania wote kwa ujumla tunao wajibu kama chama, kama nchi na kama watanzania kulinda taswira ya Rais wetu wakati wote na popopte pale ndani na nje ya nchi”- Prof. Mkumbo.
Prof. Kitila Alexander Mkumbo, Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kuandaa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 akizungumza wakati akiwasilisha Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM, Ijumaa tarehe 30 Mei 2025, Dodoma.