Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Ubungo, wilayani Ubungo mkoani Dar es Salaam wamehoji kwa sauti moja hatua za Mbunge wa jimbo hilo anayemaliza muda wake, Profesa Kitila Mkumbo, kuhusu utekelezaji wa ahadi zake mbalimbali ikiwamo ujenzi wa ukingo wa Mto Gide ambao huleta mafuriko makubwa katika makazi ya wananchi hasa kipindi cha mvua.
Wakiwa katika mkutano wa kampeni za ndani uliofanyika kwenye Kata ya Kimara siku ya Alhamisi, baadhi ya wajumbe walihoji ni kwa nini ukingo wa mto huo haukujengwa licha ya kuwa ni miongoni mwa ahadi kuu za Prof. Kitila katika kipindi chake cha ubunge.
Soma: Makazi ya Wananchi 500 Ubungo - Kisiwani (Dar) yapo hatarini, tunaomba Serikali itujengee mifereji ya kusafirisha maji ya mvua kutoka Barabara Kuu
Akijibu hoja hiyo, Prof. Kitila ameeleza kuwa tayari alichukua hatua kwa kutumia Shilingi milioni tano kutoka kwenye mfuko wake wa Mbunge kwa kila kata inayopakana na mto huo, ikiwemo Kimara. Amesema fedha hizo zilielekezwa katika juhudi za muda mfupi za kupunguza athari za mto huo wakati serikali ikiendelea na taratibu za utekelezaji wa mradi mkubwa wa kudhibiti mafuriko. Amesisitiza kuwa akipewa ridhaa tena, atalifuatilia kwa ukaribu zaidi hadi lifikie mwisho
Mkutano huo ni sehemu ya mwendelezo wa mikutano ya wagombea ubunge na udiwani wa CCM kuomba ridhaa ya kuteuliwa tena kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao wa Oktoba 2025.