Prof. Kapuya atishia kuishitaki JamiiForums...

Tamko la Kapuya linachekesha.

Kila baada ya mistari miwili "Heshima yangu niliyojijengea kwa muda mrefu"

Bila shaka heshima anayozungumzia ni hii hapa:

attachment.php
Mkuu umefanya nimecheka sana.
 
Upepo tu huu utapita, mambo mangapi yalikuja yakapita na tumeyasahau..!
 
hahahaha kapuya na wakili wake wote wajinga kabisa.

heti aje mahakamani aeleze jinsi alivyo ambukizwa virus hahahah kumbe ni kweli aliambukizwa.

heti niligawa line na simu toka zamani hahaha yani ni kweli kapuya uligawa line na simu yake?haha heti hilo ni tamko la profesa hahaha.
 
Huyu mjamaa anazidi kujipaka matope, soma tamko lake alilozambaza kwenda kwa vyombo vya habari leo.
Angalia kwenye highlight in red: Hichio chombo cha kutengeneza massage kinamilikiwa na chama kimoja cha upinzani (bila shaka CDM) na chama chake pia.
Lakini ukweli ni kwamba chombo hicho kililalamikiwa na CDM kwamba CCM ndiyo walikileta nchini na si CDM. Kama itakumbukwa, miezi kadha iliyopita kulitokea kutumiani meseji za kashfa kwa wabunge wa CDM ambao walilamika kuwa CCM ndiyo waliingiza kifaa hicho.
_____________________

TAMKO LANGU KWA UMMA JUU YA UZUSHI UNAOENEZWA DHIDI YANGU.
Ndugu wanahabari,
Baada ya kumshukuru na kumtukuza mwenyezi Mungu mwingi wa rehema. Natanguliza salamu zangu za pole kwa familia ya marehemu mwanazuoni na mwanaharakati mwenzangu Dkt Sengondo Mvungi aliyetangulia mbele ya Haki siku chache zilizopita huko Afrika ya kusini.
Ndugu zangu wanahabari,
Wengi mnanifahamu na kuifahamu vema historia yangu katika utendaji kazi na utumishi wa umma wa Watanzania. Nimekuwa nikiitumikia nchi yangu kwa kipindi kirefu katika Nyanja na sekta mbali mbali kuanzia Darasani mpaka kwenye siasa.
Kwa msingi huo, mimi Profesa Juma Kapuya, siku zote ninajikuta mwenye wajibu endelevu wa kuendelea kulitumikia Taifa langu kila siku mpaka kufikia mwisho wa Nguvu zangu.
Ndugu wanahabari,
Hivi karibuni nikiwa huku jimboni kuendelea na shuhuli za utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kumezuka Tuhuma kadhaa zilizoelekezwa dhidi yamgu zikiasisiwa na wanasiasa wenzangu wa ndani na nje ya chama changu ili kudhoofisha juhudi na utendaji wangu wa kila siku.
Tuhuma hizo zisizokuwa na kichwa wala miguu na pia kutokuwa na ukweli wowote, wamekuwa wakizitoa kwa kumtumia msichana anayedai amefanyiwa vitendo visivyofaa na mimi. Mimi simfahamu na sijui hizi shutuma zinatokea wapi.
Ndugu wanahabari,

Kwa tamko hili ninapenda kuwaambia kuwa nimefedheheshwa sana na uwezo mdogo wa kisiasa unaofanywa na hawa watu kwa kuwa dhamira yao haitatimia. Napenda niwakumbushe ndugu zangu kwamba tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na wapinzani wangu wameanza kunichafua ili nionekane sifai.
Ninapenda kuwaambia watanzania na wananchi wa jimbo langu kuwa wanatakiwa wazipuuze taarifa hizi kwa kuwa hazina ukweli wowote na kwamba ni za kutungwa zenye lengo la kunidharirisha na kuniondolea heshima yangu niliyojijengea kwenye jamii kwa kipindi kirefu sasa. Waswahili wanasema dawa ya mjinga ni kumpuuza
Na hili linajidhihirisha zaidi kwa habari hii kuandikwa na chombo kimoja tu cha habari kinachotumiwa na chama kimoja cha siasa na baadhi ya wanasiasa wa chama changu wasiokitakia heri chama chetu, naomba kuwashukuru na kuwapongeza vyombo vingine vya habari kwa umakini wenu wa kuwa na nauelewa wa kutoandika kitu bila kukifanyia uchunguzi na kubaini ukweli ulivyo.

Chombo hiki cha habari kiliwahi kuripoti mwaka jana kuwa kuna mitambo imeingizwa nchini inayoweza kuandika ujumbe na kisha kuufanya uonekane umetoka kwenye namba Fulani, kwa kipindi kile sikuwaelewa, lakini sasa ninawaelewa na nimewaona kuwa wako sahihi na wao ndio waliouingiza mtambo huu na sasa wameamua kuutumia dhidi yangu kwa kutengeneza meseji na kuzihusianisha na mimi. Ninaamini ukweli utawaumbua muda si mrefu.
Ndugu wanahabari,
Nimeijenga heshima yangu na familia yangu kwa jamii yangu kwa kipindi kirefu mno, kwa hivyo siwezi kuruhusu heshima niliyoijenga kwa miongo kadhaa karibiwa na kupotezwa na watu wachache tena kwa muda mfupi namna hii.
Hivyop basi nimechukua hatua za kisheria kuhakikisha heshima yangu inaendelea kulindwa na utu wangu unaheshimiwa.
Nimemwagiza mwanasheria wangu afungue kesi na tayari amewashitaki watu wote wanaohusika kwenye mpango huu na tayari wameshapokea taarifa ya kuitwa mahakamani.
Nitaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote watakaoendelea kutaka kujipatia umaarufu ama wa kisiasa au wowote ule kwa kutumia jina langu.
Hayo yote ni kwa kuzingatia ukweli kwamba nchi yetu inaendeshwa kwa misingi ya kisheria na kufuata na kuheshimu haki na wajibu wakila mmoja wetu.
Kwenye hilo ninawaambia ‘’janja yao nimeigundua, na hawatafanikiwa’’
Ninatoa Rai kwa yeyote mwenye kuona hilo jambo lina ukweli alipeleke kwenye vyombo husika ili lishuhulikiwe kwa mujibu wa sheria na sio kutumia vyombo vya habari kuchafuana.
Mwisho ninasisitiza kuwa nitaendelea kuilinda na kuitetea heshima yangu niliyojijengea kwa jamii kwa muda mrefu sasa na sitaruhusukuiona ikiharibiwa na wajanja wachache kwa maslahi yao binafsi.
Tuendelee kuijenga nchi yetu,
Mungu Ibariki Tanzania

Imetolewa leo tarehe 15.11.2013 nami
Prof. Juma A.Kapuya
Mbunge – urambo magharibi
S.L.P 45 Kaliua Tabora
Simu 0784993930

hahaha maelezo ya wakili wake na maelezo yake kwenye waraka huu yatamfunga.Kwenye maelezo ya wakili wake amekataa kwamba namba 0784993930 haitumii tena,lakini kwenye maelezo yake binafsi kwa vyombo vya habari kaiandika namba hiyo hiyo kama namba yake hapo sehemu ya mwisho alipoandika adress na contacts zake.
 
SIKU chache baada ya Waziri wa zamani na Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM) kutuhumiwa kumbaka na kutishia kumuua binti mdogo wa miaka 16, kiongozi huyo ameibuka na kutoa utetezi wa kujikanganya.

Akizungumza kupitia kwa wakili wake, Yasin Memba, mbunge huyo alitishia kuliburuza gazeti hili mahakamani endapo halitamwomba msamaha ndani ya siku saba.

Pamoja na kukataa kwake kumfahamu binti huyo, Kapuya amekiri kumiliki simu namba 0784993930 ambayo imekuwa ikitumiwa kuwasiliana naye ikiwemo kumtumia ujumbe mfupi wa maneno (sms) wa vitisho.

Hata hivyo, katika namna ya kushangaza, Kapuya alidai kwamba simu hiyo aliishaigawa miezi sita iliyopita, na hivyo hausiki kwa namna moja ama nyingine na tuhuma alizopewa.

Lakini wakati Kapuya akikwepa mtego huo, Novemba 9, mwaka huu, gazeti hili liliwasiliana naye kupitia namba hiyo hiyo anayodai kwamba alishaigawa miezi sita iliyopita.

Tarehe hiyo, gazeti hili liliwasiliana na mbunge huyo ili kuthibitisha tuhuma zilizokuwa zikimkabili wilayani Kaliua za kumpiga makofi kiongozi mmoja wa CCM.

Kapuya kupitia namba hiyo, alitoa utetezi wake ambapo gazeti hili lina sauti yake.

Utetezi wake pia unaongeza utata kwani hakufafanua ilikuwaje akagawa namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina lake kwa mtu mwingine, huku ikiendelea kutuma fedha na vitisho kwa binti huyo.Katika utetezi wake jana, Kapuya alikana kutomjua binti huyo wala dada yake, na kwamba yeye si mwathirika wa ugonjwa wa ukimwi.

Alilishutumu gazeti hili kuwa lilijifanya hakimu kwa kuchapisha tuhuma zake bila kumpa nafasi ya kujitetea kama ilivyo kawaida kwenye tasnia ya habari.

Hata hiyo, ukweli ni kwamba nafasi hiyo aliipata, lakini hakuitumia kwani alipopigiwa, simu yake ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni dereva wake na kutaka aelezwe sababu za kutafutwa bosi wake.

Hata alipoelezwa kuwa anayehitajika ni bosi wake, alisita kisha alitoa namba nyingine ya simu akitaka atafutwe kupitia namba hiyo.

Lakini muda wote namba hiyo haikupokelewa na hata alipopigwa tena namba ya awali, nayo iliita bila kupokelewa.

Wakili Memba alidai kuwa mteja wake, alimweleza kuwa habari ile imemletea madhara na usumbufu mkubwa katika familia yake, jamii na kumvunjia heshima yake.

"Kwa sababu hiyo, amenielekeza niwapatie siku saba gazeti la Tanzania Daima, mitandao ya kijamii ukiwemo wa Jamii Forum, Justina John na Vituko Mtaani ambao walichapisha habari hiyo, waombe radhi kwa uzito ule ule la sivyo atavishitaki mahakamani.

"Kama hawataomba radhi, basi atafungua kesi mbili, moja ni kwa ajili ya gazeti la Tanzania Daima na hiyo mitandao ya kijamii, na kesi ya pili ni ya kuhusu huyo mtoto anayedaiwa kubakwa na kuambukizwa ukimwi," alisema.

Aliongeza kuwa wanataka mtoto huyo aje mahakamani athibitishe aliambukizwaje ukimwi na alete ushahidi unaoonyesha Kapuya ana ukimwi.

Memba aliuomba umma kuelewa kuwa habari hiyo iliyochapishwa na Tanzania Daima haiusiani na chama chake wala serikali.

Kwa siku mbili mfululizo gazeti hili lilifichua tuhuma za Kapuya kudaiwa kumbaka mtoto huyo, na hata baada ya kubaini siri hiyo imevuja, alimpigia simu mtoto huyo, na baadaye kutuma meseji kadhaa za vitisho.

Tanzania Daima ilishuhudia baadhi ya meseji za simu zilizotumwa na Prof. Kapuya kwenda kwa mtoto huyo.Juzi alfajiri saa 11:21 kupitia simu yake alituma ujumbe kwa mtoto huyo: "Chagueni kunisubiri tuje tuongee au mnataka kufa?"

Baadaye saa 1:07 asubuhi, alituma ujumbe mwingine kutoka simu hiyo hiyo kwenda kwa mtoto huyo, ukisema: "Mkiuawa, itakuwa nzuri, itawapunguzia gharama za kuishi. Usitake kugombana na serikali, mtoto mdogo kama wewe. Sisi ndo wenye nchi yetu."

Baadhi ya mashirika yanayotetea makundi kadhaa yakiwamo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) yalijitokeza kuwasaidia watoto hao, ambao ni yatima.

Mtoto huyo na dada yake, wakizungumza na gazeti hili kwa hofu mafichoni, walisema kwa sasa hawana imani tena kama kuna serikali nchini Tanzania kwa kuwa wamedhalilishwa, wametembezwa hadi bungeni na wabunge bila hatua kuchukuliwa, licha ya kutoa taarifa katika Kituo Cha polisi Oysterbay tangu mwaka jana.

Hata hivyo, kabla ya tukio la watoto hao kuripotiwa ofisi za gazeti hili, juzi usiku kulikuwa na watu waliokuja wakiwatafuta watoto hao, huku wakiwatisha kwa simu na kuwatolea maneno ya kejeli, wakidai watawamwagia tindikali.

Juzi gazeti hili lilichapisha habari kuhusu mwanafunzi huyo aliyesema kuwa waziri huyo alimbaka kwenye hoteli moja ya kitalii iliyoko jijini Dar es Salaam mwaka 2011, na kurudia tena kitendo hicho katika Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala Juni 3, 2012 alipoitwa kwenda kuchukua ada kwa mara ya pili.

CHANZO: TANZANIA DAIMA

Unajua ukweli unauma,waandishi wengi ni wahuni sana,hivi mpaka wanaandika habari hiyo just kwa habari ya kumsikiliza Huyu binti,hivi niwaulize wangapi mnarhibitisha kuwa kapuya ni muathirika wa ukimwi?hivi kapuya akipimwa ikathibitishwa hajaathirika mwandishi utakua na la kujibu,au mtaendekea kulazimisha siasa zenu za kihuni mnazochafua watu?kwa nini tunajenga taifa la watu wanaotunga kusingizia na kuchafua watu?kwa nini hayuhangaiki kuyakabili mabonde mazuri na misitu kulima na kuzalisha badala yake siasa za kihuni ndo kazi zetu za kutwa?tunashabikia utumbo vijana kwa wazee,tunawezajekushindana katika ulimwengu huu kwa kuwa na kundi kubwa la vijana wanaofikiria siasa chafu na kuzishabikia?

Kama kijana Makini nawashauri vijana wakitanzania tuibane setikali tuzalishe katika kilimo,ufugaji na usindikaji,tuyakabili masoko ya ndani na nje,tuijenge nchi,tuache kushabikia mambo ambayo yanadumaza akili na utashi wetu,Tanzania ni nchi pekee katika Ukanda wa Afrika ya mashariki ambapo kila kijana Amekua politician,

Vijana wengi hatuna makazi bora,tuishinikize serilali tuzalishe na kukopeshwa nyumba,tuna viongozi makini kama skins Mchechu wa NHC tuwstumie kuliko kujipendtkeza kutwa kwa wanasiasa tukidhani tunalikomboa taifa.

Hakuna mijadala ya maana,kutwa kushabikia umbea na uzandiki,Kuna mambo ya Elimu,Ajira,Kilimo na sayansi,lakini vijana wote humu ni upuuzi tuu,wachache watanielewa.
 
Kapuya si naye ana bendi? Mbona hatukushangaa akina papi kocha walipotuhumiwa na kuhukumiwa
kifungo cha maisha?
Mi naona kusudio lake la kushtaki ni jema,awashtaki tanzania daima,ili waweke mezani ushahidi
ili kapaya afungwe maisha kwa raha zake.
 
Nami naongeza swali kutokana na jibu lako:
Hivi ataamini vp kama anamaambukizi bila kwenda kupima? Hivi tutaamini tu kauli ya huyo mhudumu aliyemwambia kuwa jamaa anamaambukizi,labda huyo mama anaugomvi binafsi na Kapuya!
inaonekana yeye(mtoto)amepima,maana kuna tetesi kuwa alishaanza kutumia mashudu(arv's). Tatizo ninaloliona mimi,anaweza kuwa ameambukizwa na wahuni na wengine lkn akaamua kuangushia mzigo kwa kapuya. Hv ikithibitika kapuya hana ngoma itakuwaje?
 
The county is torn apart and sawn assunder by youngmen who always thinks of progress is at playing politics,Poor Tanzanian Youth
 
MEMBER OF PARLIAMENT CV

[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TH="colspan: 3, align: left"]GENERAL[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD]Salutation[/TD]
[TD]Honourable[/TD]
[TD="width: 42%, align: center"]Member picture
1011.jpg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]First Name:[/TD]
[TD]Prof. Juma[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Middle Name:[/TD]
[TD]Athumani[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Last Name:[/TD]
[TD]Kapuya[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 20%"]Member Type:[/TD]
[TD="width: 38%"]Constituency Member[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Constituent:[/TD]
[TD]Urambo Magharibi[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Political Party:[/TD]
[TD]CCM[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Office Location:[/TD]
[TD]P.O. Box 11365, Dar es Salaam[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Office Phone:[/TD]
[TD]+255 784 993930/+255 776 784185[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Ext.:[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Office Fax:[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Office E-mail:[/TD]
[TD]jkapuya@parliament.go.tz[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Member Status:[/TD]
[TD]Current Member[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Date of Birth[/TD]
[TD]22 June 1945[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TH="colspan: 5, align: left"]EDUCATION[/TH]
[/TR]
[TR]
[TH="width: 35%"]School Name/Location[/TH]
[TH="width: 27%"]Course/Degree/Award[/TH]
[TH="width: 15%, align: center"]Start Date[/TH]
[TH="width: 13%, align: center"]End Date[/TH]
[TH="width: 10%, align: center"]Level[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD]University College of Wales Aberystwyth[/TD]
[TD="align: center"]PhD (Botany)[/TD]
[TD="align: center"]1972[/TD]
[TD="align: center"]1975[/TD]
[TD="align: center"]PHD[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]University of Dar es Salaam[/TD]
[TD="align: center"]MSc. (Botany)[/TD]
[TD="align: center"]1971[/TD]
[TD="align: center"]1972[/TD]
[TD="align: center"]MASTERS DEGREE[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]University of Dar es Salaam[/TD]
[TD="align: center"]BSc. (Education) Hons[/TD]
[TD="align: center"]1968[/TD]
[TD="align: center"]1971[/TD]
[TD="align: center"]GRADUATE[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Katholicke University, Nijmegen[/TD]
[TD="align: center"]Certificate[/TD]
[TD="align: center"]1982[/TD]
[TD="align: center"]1983[/TD]
[TD="align: center"]CERTIFICATE[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]International Atomic Energy Agency[/TD]
[TD="align: center"]Certificate[/TD]
[TD="align: center"]1986[/TD]
[TD="align: center"]1986[/TD]
[TD="align: center"]CERTIFICATE[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Tabora Boys Secondary School[/TD]
[TD="align: center"]A-Level Education[/TD]
[TD="align: center"]1966[/TD]
[TD="align: center"]1967[/TD]
[TD="align: center"]HIGH SCHOOL[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Tabora Boys Secondary School[/TD]
[TD="align: center"]O-Level Education[/TD]
[TD="align: center"]1962[/TD]
[TD="align: center"]1965[/TD]
[TD="align: center"]SECONDARY[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kaliua Primary School[/TD]
[TD="align: center"]Primary Education[/TD]
[TD="align: center"]1954[/TD]
[TD="align: center"]1957[/TD]
[TD="align: center"]PRIMARY[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Sikonge Middle School[/TD]
[TD="align: center"]Primary Education[/TD]
[TD="align: center"]1958[/TD]
[TD="align: center"]1961[/TD]
[TD="align: center"]PRIMARY[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TH="colspan: 4, align: left"]EMPLOYMENT HISTORY[/TH]
[/TR]
[TR]
[TH]Company Name[/TH]
[TH="align: center"]Position[/TH]
[TH="align: center"]From[/TH]
[TH="align: center"]To[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD]Ministry of Defence & National Serv.[/TD]
[TD]Minister[/TD]
[TD="align: center"]2006[/TD]
[TD="align: center"]2/8/2008[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Ministry of Labour, Employment and Youth Development[/TD]
[TD]Minister[/TD]
[TD="align: center"]2/13/2008[/TD]
[TD="align: center"]2010[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]The Parliament of Tanzania[/TD]
[TD]Member - Urambo West Constituency[/TD]
[TD="align: center"]1995[/TD]
[TD="align: center"]2015[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]University of Dar es Salaam[/TD]
[TD]Professor of Botany[/TD]
[TD="align: center"]1987[/TD]
[TD="align: center"]1995[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]University of Dar es Salaam[/TD]
[TD]Associate Professor(Botany)[/TD]
[TD="align: center"]1983[/TD]
[TD="align: center"]1987[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]University of Dar es Salaam[/TD]
[TD]Senior Lecturer(Botany)[/TD]
[TD="align: center"]1978[/TD]
[TD="align: center"]1983[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]University of Dar es Salaam[/TD]
[TD]Lecturer(Botany)[/TD]
[TD="align: center"]1976[/TD]
[TD="align: center"]1978[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]University of Dar es Salaam[/TD]
[TD]Assistant Lecturer(Botany)[/TD]
[TD="align: center"]1974[/TD]
[TD="align: center"]1976[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]University of Dar es Salaam[/TD]
[TD]Tutorial Assistant(Botany)[/TD]
[TD="align: center"]1971[/TD]
[TD="align: center"]1974[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TH="colspan: 4, align: left"]POLITICAL EXPERIENCE[/TH]
[/TR]
[TR]
[TH="class: text_menu, width: 47%"]Ministry/Political Party/Location[/TH]
[TH="class: text_menu, width: 31%, align: center"]Position[/TH]
[TH="class: text_menu, width: 12%, align: center"]From[/TH]
[TH="class: text_menu, width: 10%, align: center"]To[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD]Chama Cha Mapinduzi - CCM[/TD]
[TD]Member of National Executive Council (NEC)[/TD]
[TD="align: center"]1997[/TD]
[TD="align: center"]Todate[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Chama Cha Mapinduzi - CCM[/TD]
[TD]Ten Cells Leader(Darajani) - UDSM[/TD]
[TD="align: center"]1983[/TD]
[TD="align: center"]1995[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Chama Cha Mapinduzi - CCM[/TD]
[TD]Ambassodor[/TD]
[TD="align: center"]1977[/TD]
[TD="align: center"]1997[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]TANU-Tanganyika Youth League(University of DSM)[/TD]
[TD]Advisor/Member[/TD]
[TD="align: center"]1972[/TD]
[TD="align: center"]1977[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Hiyo namba ya simu aliigawa lini? Kwa nani? Ameshindwa kutoa taarifa hata bungeni ili waitoe kwenye orodha ya namba zake za simu? Unaweza vipi kumshawishi mtu kwamba hiyo sio namba yake huku kwenye taarifa zake rasmiza bunge ndio inayoonekana?
 
Nitafurahi sana kama hakimu wa kesi hii akiwa yule yule aliyewakaanga familia ya Nguza,tena naamini hii ina ushahidi ulio wazi wala haitamchukua muda kuisoma hukumu......mzee ana laana huyu,kawachoka wacheza show wake sasa anahamia kwa vident,nyambaf.
 
KILIO KILIO KILIO WIZARA YA ELIMU.
Kapuya kaharibu wake za watu wizara ya Elimuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kuna vilio vimekolea wizarani hadi sasa idadi ya wanawake wizara ya Elimu makao makuu ni 6 (six) (Sita).

Wawili wamekiri kuogopa kusoma gazeti (eti hawataki kufa na presha)) na mmoja anadai aaaaaahhh tumekwishaaaa, jamani huyu baba ni muuaji!!!!!
 
Nami naongeza swali kutokana na jibu lako:
Hivi ataamini vp kama anamaambukizi bila kwenda kupima? Hivi tutaamini tu kauli ya huyo mhudumu aliyemwambia kuwa jamaa anamaambukizi,labda huyo mama anaugomvi binafsi na Kapuya!

hii ni kazi ya taasisi nyingine kufanyia kazi hizi tetesi
 
SIKU chache baada ya Waziri wa zamani na Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM) kutuhumiwa kumbaka na kutishia kumuua binti mdogo wa miaka 16, kiongozi huyo ameibuka na kutoa utetezi wa kujikanganya.

Akizungumza kupitia kwa wakili wake, Yasin Memba, mbunge huyo alitishia kuliburuza gazeti hili mahakamani endapo halitamwomba msamaha ndani ya siku saba.

Pamoja na kukataa kwake kumfahamu binti huyo, Kapuya amekiri kumiliki simu namba 0784993930 ambayo imekuwa ikitumiwa kuwasiliana naye ikiwemo kumtumia ujumbe mfupi wa maneno (sms) wa vitisho.

Hata hivyo, katika namna ya kushangaza, Kapuya alidai kwamba simu hiyo aliishaigawa miezi sita iliyopita, na hivyo hausiki kwa namna moja ama nyingine na tuhuma alizopewa.

Lakini wakati Kapuya akikwepa mtego huo, Novemba 9, mwaka huu, gazeti hili liliwasiliana naye kupitia namba hiyo hiyo anayodai kwamba alishaigawa miezi sita iliyopita.

Tarehe hiyo, gazeti hili liliwasiliana na mbunge huyo ili kuthibitisha tuhuma zilizokuwa zikimkabili wilayani Kaliua za kumpiga makofi kiongozi mmoja wa CCM.

Kapuya kupitia namba hiyo, alitoa utetezi wake ambapo gazeti hili lina sauti yake.

Utetezi wake pia unaongeza utata kwani hakufafanua ilikuwaje akagawa namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina lake kwa mtu mwingine, huku ikiendelea kutuma fedha na vitisho kwa binti huyo.Katika utetezi wake jana, Kapuya alikana kutomjua binti huyo wala dada yake, na kwamba yeye si mwathirika wa ugonjwa wa ukimwi.

Alilishutumu gazeti hili kuwa lilijifanya hakimu kwa kuchapisha tuhuma zake bila kumpa nafasi ya kujitetea kama ilivyo kawaida kwenye tasnia ya habari.

Hata hiyo, ukweli ni kwamba nafasi hiyo aliipata, lakini hakuitumia kwani alipopigiwa, simu yake ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni dereva wake na kutaka aelezwe sababu za kutafutwa bosi wake.

Hata alipoelezwa kuwa anayehitajika ni bosi wake, alisita kisha alitoa namba nyingine ya simu akitaka atafutwe kupitia namba hiyo.

Lakini muda wote namba hiyo haikupokelewa na hata alipopigwa tena namba ya awali, nayo iliita bila kupokelewa.

Wakili Memba alidai kuwa mteja wake, alimweleza kuwa habari ile imemletea madhara na usumbufu mkubwa katika familia yake, jamii na kumvunjia heshima yake.

"Kwa sababu hiyo, amenielekeza niwapatie siku saba gazeti la Tanzania Daima, mitandao ya kijamii ukiwemo wa Jamii Forum, Justina John na Vituko Mtaani ambao walichapisha habari hiyo, waombe radhi kwa uzito ule ule la sivyo atavishitaki mahakamani.

"Kama hawataomba radhi, basi atafungua kesi mbili, moja ni kwa ajili ya gazeti la Tanzania Daima na hiyo mitandao ya kijamii, na kesi ya pili ni ya kuhusu huyo mtoto anayedaiwa kubakwa na kuambukizwa ukimwi," alisema.

Aliongeza kuwa wanataka mtoto huyo aje mahakamani athibitishe aliambukizwaje ukimwi na alete ushahidi unaoonyesha Kapuya ana ukimwi.

Memba aliuomba umma kuelewa kuwa habari hiyo iliyochapishwa na Tanzania Daima haiusiani na chama chake wala serikali.

Kwa siku mbili mfululizo gazeti hili lilifichua tuhuma za Kapuya kudaiwa kumbaka mtoto huyo, na hata baada ya kubaini siri hiyo imevuja, alimpigia simu mtoto huyo, na baadaye kutuma meseji kadhaa za vitisho.

Tanzania Daima ilishuhudia baadhi ya meseji za simu zilizotumwa na Prof. Kapuya kwenda kwa mtoto huyo.Juzi alfajiri saa 11:21 kupitia simu yake alituma ujumbe kwa mtoto huyo: "Chagueni kunisubiri tuje tuongee au mnataka kufa?"

Baadaye saa 1:07 asubuhi, alituma ujumbe mwingine kutoka simu hiyo hiyo kwenda kwa mtoto huyo, ukisema: "Mkiuawa, itakuwa nzuri, itawapunguzia gharama za kuishi. Usitake kugombana na serikali, mtoto mdogo kama wewe. Sisi ndo wenye nchi yetu."

Baadhi ya mashirika yanayotetea makundi kadhaa yakiwamo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) yalijitokeza kuwasaidia watoto hao, ambao ni yatima.

Mtoto huyo na dada yake, wakizungumza na gazeti hili kwa hofu mafichoni, walisema kwa sasa hawana imani tena kama kuna serikali nchini Tanzania kwa kuwa wamedhalilishwa, wametembezwa hadi bungeni na wabunge bila hatua kuchukuliwa, licha ya kutoa taarifa katika Kituo Cha polisi Oysterbay tangu mwaka jana.

Hata hivyo, kabla ya tukio la watoto hao kuripotiwa ofisi za gazeti hili, juzi usiku kulikuwa na watu waliokuja wakiwatafuta watoto hao, huku wakiwatisha kwa simu na kuwatolea maneno ya kejeli, wakidai watawamwagia tindikali.

Juzi gazeti hili lilichapisha habari kuhusu mwanafunzi huyo aliyesema kuwa waziri huyo alimbaka kwenye hoteli moja ya kitalii iliyoko jijini Dar es Salaam mwaka 2011, na kurudia tena kitendo hicho katika Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala Juni 3, 2012 alipoitwa kwenda kuchukua ada kwa mara ya pili.

CHANZO: TANZANIA DAIMA

Huyu mjamaa anazidi kujipaka matope, soma tamko lake alilozambaza kwenda kwa vyombo vya habari leo.
Angalia kwenye highlight in red: Hichio chombo cha kutengeneza massage kinamilikiwa na chama kimoja cha upinzani (bila shaka CDM) na chama chake pia.
Lakini ukweli ni kwamba chombo hicho kililalamikiwa na CDM kwamba CCM ndiyo walikileta nchini na si CDM. Kama itakumbukwa, miezi kadha iliyopita kulitokea kutumiani meseji za kashfa kwa wabunge wa CDM ambao walilamika kuwa CCM ndiyo waliingiza kifaa

Yellow journalism, or the yellow press, is a type of journalism that presents little or no legitimate well-researched news and instead uses eye-catching headlines to sell more newspapers.Techniques may include exaggerations of news events, scandal-mongering, or sensationalism. By extension, the term yellow journalism is used today as a pejorative to decry any journalism that treats news in an unprofessional or unethical fashion.

Campbell (2001) defines yellow press newspapers as having daily multi-column front-page headlines covering a variety of topics, such as sports and scandal, using bold layouts (with large illustrations and perhaps color), heavy reliance on unnamed sources, and unabashed self-promotion. The term was extensively used to describe certain major New York City newspapers about 1900 as they battled for circulation.
Frank Luther Mott (1941) defines yellow journalism in terms of five characteristics:

scare headlines in huge print, often of minor news
lavish use of pictures, or imaginary drawings
use of faked interviews, misleading headlines, pseudoscience, and a parade of false learning from so-called experts
emphasis on full-color Sunday supplements, usually with comic strips
Dramatic sympathy with the "underdog" against the system
 
Sasa Le Professori unagawaje bunduki na risasi? Yaani hueleweki, uligawa sim au line au vyote?Kwa vyovyote vile hii kesi kama itaenda mahakamani itakua moja ya kesi rahisi kuliko nyingi za aina hii. Prof. Kwanza ana makosa mengi, kisheria huruhusiwi kutumia SIMCARD ambayo haijasajiliwa kwa jina lako na hivyo hivyo huruhusiwi kuigawa,kuitoa zawadi n.k. Pili huruhusiwi kutoa vitisho vya aina yoyote kwa mtu yeyote kwa kua eti tu wewe ni powerful, achilia mbali hayo ya kubaka na kumuambukiza mtu maradhi kwa makusudi.Inatakiwa Prof.ajipange si kidogo.
SIKU chache baada ya Waziri wa zamani na Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM) kutuhumiwa kumbaka na kutishia kumuua binti mdogo wa miaka 16, kiongozi huyo ameibuka na kutoa utetezi wa kujikanganya.

Akizungumza kupitia kwa wakili wake, Yasin Memba, mbunge huyo alitishia kuliburuza gazeti hili mahakamani endapo halitamwomba msamaha ndani ya siku saba.

Pamoja na kukataa kwake kumfahamu binti huyo, Kapuya amekiri kumiliki simu namba 0784993930 ambayo imekuwa ikitumiwa kuwasiliana naye ikiwemo kumtumia ujumbe mfupi wa maneno (sms) wa vitisho.

Hata hivyo, katika namna ya kushangaza, Kapuya alidai kwamba simu hiyo aliishaigawa miezi sita iliyopita, na hivyo hausiki kwa namna moja ama nyingine na tuhuma alizopewa.

Lakini wakati Kapuya akikwepa mtego huo, Novemba 9, mwaka huu, gazeti hili liliwasiliana naye kupitia namba hiyo hiyo anayodai kwamba alishaigawa miezi sita iliyopita.

Tarehe hiyo, gazeti hili liliwasiliana na mbunge huyo ili kuthibitisha tuhuma zilizokuwa zikimkabili wilayani Kaliua za kumpiga makofi kiongozi mmoja wa CCM.

Kapuya kupitia namba hiyo, alitoa utetezi wake ambapo gazeti hili lina sauti yake.

Utetezi wake pia unaongeza utata kwani hakufafanua ilikuwaje akagawa namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina lake kwa mtu mwingine, huku ikiendelea kutuma fedha na vitisho kwa binti huyo.Katika utetezi wake jana, Kapuya alikana kutomjua binti huyo wala dada yake, na kwamba yeye si mwathirika wa ugonjwa wa ukimwi.

Alilishutumu gazeti hili kuwa lilijifanya hakimu kwa kuchapisha tuhuma zake bila kumpa nafasi ya kujitetea kama ilivyo kawaida kwenye tasnia ya habari.

Hata hiyo, ukweli ni kwamba nafasi hiyo aliipata, lakini hakuitumia kwani alipopigiwa, simu yake ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni dereva wake na kutaka aelezwe sababu za kutafutwa bosi wake.

Hata alipoelezwa kuwa anayehitajika ni bosi wake, alisita kisha alitoa namba nyingine ya simu akitaka atafutwe kupitia namba hiyo.

Lakini muda wote namba hiyo haikupokelewa na hata alipopigwa tena namba ya awali, nayo iliita bila kupokelewa.

Wakili Memba alidai kuwa mteja wake, alimweleza kuwa habari ile imemletea madhara na usumbufu mkubwa katika familia yake, jamii na kumvunjia heshima yake.

"Kwa sababu hiyo, amenielekeza niwapatie siku saba gazeti la Tanzania Daima, mitandao ya kijamii ukiwemo wa Jamii Forum, Justina John na Vituko Mtaani ambao walichapisha habari hiyo, waombe radhi kwa uzito ule ule la sivyo atavishitaki mahakamani.

"Kama hawataomba radhi, basi atafungua kesi mbili, moja ni kwa ajili ya gazeti la Tanzania Daima na hiyo mitandao ya kijamii, na kesi ya pili ni ya kuhusu huyo mtoto anayedaiwa kubakwa na kuambukizwa ukimwi," alisema.

Aliongeza kuwa wanataka mtoto huyo aje mahakamani athibitishe aliambukizwaje ukimwi na alete ushahidi unaoonyesha Kapuya ana ukimwi.

Memba aliuomba umma kuelewa kuwa habari hiyo iliyochapishwa na Tanzania Daima haiusiani na chama chake wala serikali.

Kwa siku mbili mfululizo gazeti hili lilifichua tuhuma za Kapuya kudaiwa kumbaka mtoto huyo, na hata baada ya kubaini siri hiyo imevuja, alimpigia simu mtoto huyo, na baadaye kutuma meseji kadhaa za vitisho.

Tanzania Daima ilishuhudia baadhi ya meseji za simu zilizotumwa na Prof. Kapuya kwenda kwa mtoto huyo.Juzi alfajiri saa 11:21 kupitia simu yake alituma ujumbe kwa mtoto huyo: "Chagueni kunisubiri tuje tuongee au mnataka kufa?"

Baadaye saa 1:07 asubuhi, alituma ujumbe mwingine kutoka simu hiyo hiyo kwenda kwa mtoto huyo, ukisema: "Mkiuawa, itakuwa nzuri, itawapunguzia gharama za kuishi. Usitake kugombana na serikali, mtoto mdogo kama wewe. Sisi ndo wenye nchi yetu."

Baadhi ya mashirika yanayotetea makundi kadhaa yakiwamo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) yalijitokeza kuwasaidia watoto hao, ambao ni yatima.

Mtoto huyo na dada yake, wakizungumza na gazeti hili kwa hofu mafichoni, walisema kwa sasa hawana imani tena kama kuna serikali nchini Tanzania kwa kuwa wamedhalilishwa, wametembezwa hadi bungeni na wabunge bila hatua kuchukuliwa, licha ya kutoa taarifa katika Kituo Cha polisi Oysterbay tangu mwaka jana.

Hata hivyo, kabla ya tukio la watoto hao kuripotiwa ofisi za gazeti hili, juzi usiku kulikuwa na watu waliokuja wakiwatafuta watoto hao, huku wakiwatisha kwa simu na kuwatolea maneno ya kejeli, wakidai watawamwagia tindikali.

Juzi gazeti hili lilichapisha habari kuhusu mwanafunzi huyo aliyesema kuwa waziri huyo alimbaka kwenye hoteli moja ya kitalii iliyoko jijini Dar es Salaam mwaka 2011, na kurudia tena kitendo hicho katika Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala Juni 3, 2012 alipoitwa kwenda kuchukua ada kwa mara ya pili.

CHANZO: TANZANIA DAIMA
 
Unajua razor wire zina tatizo moja, ikikunasa ukaanza kufurukuta inazidi kuzama kwenye mwili!..sasa huyu mzee kanaswa kwenye razor wire, na anazidi kufurukuta na kuharibu mambo kabisaa, mwanasheria wake sijui hajamshauri au anataka kumpiga pesa tuu!
:shocked:
 
Hivi ikiwa kapuya atathibitika ni negative wewe mwandishi utajibu mini?
 
naona wajinga wenzie wanaanza kuweka isue ya kuambukizwa ukimwi ndio issue kubwa pekee. hapa swala kubwa la kwanza ni kubaka, awe amemwambukiza ukimwi au hajamwambukiza ni kwamba kabaka katoto!
 
akaishitaki tu, mbona zeutamu ilifungwa lakini siku hizi blog zimejaa... domain itabadilishwa tu, kwanza hatofika mbali since kuna probability kubwa kukutwa na hatia
 
Back
Top Bottom