Prof. Kabudi kuanza na Katiba Mpya

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,745
4,277
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kuwa mchakato wa Katiba mpya uko pale pale.

Prof. Kabudi amesema hayo wakati alipokutana na Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge, amesema kuwa hajakutana na viongozi wake kuzungumzia suala la Katiba Mpya, ingawa anajua mambo mengine kuhusu mchakato huo ambao wakati wa maandalizi yake alikuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Amesema kuwa mchakato wa Katiba mpya uko pale pale hivyo pindi mchakato huo utakapo kamilika kwenye ofisi yake atauwasilisha kwenye kamati hiyo.

Aidha, Prof. Kabudi ameongeza kuwa ana muda mfupi katika wizara hiyo na kwamba, hajapata muda wa kukutana na mabosi wake akiwamo Waziri Mkuu, ili wazungumzie suala la Katiba Mpya.

Hata hivyo, amesema kuwa mchakato huo unahitaji umakini mkubwa hivyo atafanya kazi kulingana na utaratibu wa kisheria ili liwe na mwanzo na mwisho mzuri.

Chanzo: Dar24
 
Thubutu.
Anajaribu kutikisa kiberiti cha Magufuli.
Kama hataonywa basi atatumbuliwa haraka sana. Hizo hoja za katiba mpya Magufuli alishasema hazitaki kabisa kuzisikia kwa sababu sio wakati wake na hazina maana kwake.
 
Sitoshangaa tuliyonayo hataki kuisikia
 
Hawa ndio aina ya wasomi wanaojua nini wafanye sio wanashria uchwara waliokimbilia kuvunja TLS.
 
Hawa ndio aina ya wasomi wanaojua nini wafanye sio wanashria uchwara waliokimbilia kuvunja TLS.
Kwani amefanya nini? Kipimo chake ni hili yeye alikuwa kwenye tume ya mabadiliko ya katiba waliokuja na rasimu ya warioba ilikuwa imejaa mapendekezo ya serikali tatu na maoni mengi sana ya watanzania yaliyokuja kuondolewa kibabe na CCM kwenye BMK, je atafufua ile rasimu ya warioba au ataendelea na hii najisi??
 
Dikteta hata hii iliyopo haitaki na anaikiuka kila mara ndio akubali ya warioba mh thubutu huyu kabudi anataka kutimuliwa mapema tuu
 
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kuwa mchakato wa Katiba mpya uko pale pale.

Prof. Kabudi amesema hayo wakati alipokutana na Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge, amesema kuwa hajakutana na viongozi wake kuzungumzia suala la Katiba Mpya, ingawa anajua mambo mengine kuhusu mchakato huo ambao wakati wa maandalizi yake alikuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Amesema kuwa mchakato wa Katiba mpya uko pale pale hivyo pindi mchakato huo utakapo kamilika kwenye ofisi yake atauwasilisha kwenye kamati hiyo.

Aidha, Prof. Kabudi ameongeza kuwa ana muda mfupi katika wizara hiyo na kwamba, hajapata muda wa kukutana na mabosi wake akiwamo Waziri Mkuu, ili wazungumzie suala la Katiba Mpya.

Hata hivyo, amesema kuwa mchakato huo unahitaji umakini mkubwa hivyo atafanya kazi kulingana na utaratibu wa kisheria ili liwe na mwanzo na mwisho mzuri.

Chanzo: Dar24
Katiba mpya itakuwa na tija baada ya kunyosha nchi na kuweka system nzuri za kiutendaji. Hivyo mchakato wa katiba mpya utafuata mpango kazi wa kunyosha na kuweka system iliyobora
 
Watanzania, kama kwlei huu ndio mtazamo wa Professor Paramagamba, anahitaji kuungwa mkono.

Mara nyingine inakuwa vigumu kwa raisi kufanya kila ktu yeye binafsi hata visivyokuwa kweny e taaluma yake.
Paramagamba ni mtu ambaye hajawahi kuonyesha unafiki kama yule wa kufuta TLS.

Ikiw araisi amempa mandate hiyo, na kwa kuwa mtu msomi hawezi kukurupuka kutunga kazi nje ya JD yake, bila shaka raisi amemuamini na kumwona ni mtu sahihi amayeweza kufanikisha mchakato wa ktiba mpya wakati yeye raisi akinyoosha nchi.

Na kama ndivyo, naomba tuione nia sahihi ya raisi katika hili. Pengine aliyoyoasema mwenzo yalikuwa yanajikita zaidi kwenye lengo la kushughulikia vipaumbele dharura ambazo sasa wakati wake umekwisha.

Tukubali kuelewa kwamba watu hukosea lakini pia wana uwezo wa kubadilika. Ikiwa kulikuwa na makosa hapo awali tukayasema, basi pia tunatakiwa kusema pale tunapoona mabadilko. Tusilazimishemtu adumu katika makosa na tukalazimisha milki ya makosa hata pale mtu anapoonyesha kukubali kubadilika na kuweza kurekebisha makosa.

Kunyoosha nchi ni pamoja na ku enhance sustainability ya ubunifu na misingi anayoisimamia ambayo haiwezi kuwa endelevu pasipo katiba mathubuti. Bila shaka raisi anafahamu kwamba juhudi zake zote na nguvu anazotumia zitakuwa ni kujilisha na upepoe na zitayeyuka mara atakapoachia ngazi kama vile leo mambo yanavyoenda sehemu ambazo hajaziitupia macho. Anaelewa kwamba alifanya juhudi nyingi katiak wizara za ardhi, ujenzi lakini hakuan weizara aliyorithisha culture yake ya kazi hata moja. HIvyo ni dhahiri kwamb bila nguvu ya katiba, hakuna mabadiliko endelevu yatatokea kwa kuw akila kiongozi aakayekuja atafanya kichwa chake vile kinamtuma. Hii ni hatari.

Lakini pia raisi hawezi kumtumbua Paramagamba kwa kushughulikia katiba ya wananchi kwa kuwa anaelewa pasipokuwa na katiba sahihi, hata yeye na uzao wake wako kwenye utarajiwa wa udharirishwaji. Bila shaka amajifunza kwa yaliyomkuta Nape na kuona yanaweza kumkuta hata yeye ama watu wake wa karibu mara wakiwa nje ya madaraka ikiwa tu mambo mazito yataendelea kuwekezwa kwenye aklii na utashi wamtu mmoja.

Lengo letu kuu liwe ni kujenga nchi na si kujenga watu. Tushirikiane kwa nia ya dhati kabisa katika kujenga Tanzania imara na idumuyo kwa kukemea maovu na kuunga mkono ama kushirki katika jitihada za mafanikio.

Kwa mantiki hiii, ninaomba tumshukuru sana Raisi kwa kuliona hili na kumpa mamlaka Prof. Kulisimamia ili lifike mwisho salama.

Ninadhani kama ishara ya nia thatibi ya mabadiliko, mchakato wa katiba mpya utaanzia pale alipoishia jaji na tume yake. Muundo wa bunge la katiba hautakuwa wa kihuni wenye lengo la kuhujumu tena. Bunge la jamhuri halitakuwa bunge la katiba tena na kwamba tutapata katiba isiyolinda kundi la watu bali lkatiba inayoona na kujali haki na wajibu wa kila Mtanzania.

Natanguliza shukrani.
 
Hana huo ubavu..... you may take it to the bank... and never will it happen soon or later in this Adm....
 
Katiba mpya itakuwa na tija baada ya kunyosha nchi na kuweka system nzuri za kiutendaji. Hivyo mchakato wa katiba mpya utafuata mpango kazi wa kunyosha na kuweka system iliyobora
... Hoja ya kilofa sana.
 
Bosi wake alishasema kwenye uchaguzi haku ahidi katiba mpya yy ni nani hata airejeshe?

Naona anajisemesha tu
Prof ni msomi mueledi, mjuzi wa ujenzi wa hoja za Msingi.
Penye hoja nzuri, murua na zenye Maslahi mapana ya Nchi, Jeuri/kiburi huyeyukaaa!!!
 
Back
Top Bottom