Prof Kabudi atueleze kutoka Trilioni 360 hadi bilioni 700

mapessa

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
612
1,045
Kosa moja siku zote linaloendelea kutugharimu basi ni kusikiliza bila kuelewa hatupo tayari kusikiliza tumejianda kujibu kila wakati.

Inawezekana hii ni tabia yetu ya kutotafuta Ukweli, binafsi suala la Makinikia nimekuwa nikilifahamu hata kabla ya Mhe. Magufuli kuliweka kwenye meza ya hadhara kupitia ripoti mbili ya Prof Ossoro na Prof Mruma.

Huenda Barrick waliona ugumu wa hali iliyopo mbele yao. Mzozo ulianza pale Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakati ule simkumbuki jina vizuri alipozuiwa kuingia kwenye mgodi wa Buzwagi Kahama.

Hii ilikuwa red alert kuna mambo ambayo Barrick hawakuwa wameafikiana na Serikali kuhusu Mkuu wa Mkoa kutaka kukagua chumba maalum cha kuhifadhi dhahabu bila idhini ya wenye mali.
Hali hii ilikuwa ni kawaida kwenye serikali ile maofisa wa Serikali hawakuruhusiwa kuingia kwenye miradi ya SGR, Bwawa la Nyerere hata kuulizia juu ya uagizaji wa ndege za Air Tanzania.

Tarehe 2-March-2017
Rais Magufuli alitoa tamko la kuzuia mchanga wenye madini maarufu kama Makinikia kutokusafirishwa kwenda nje ya nchi.
Tamko alilolitoa akiweka Jiwe la msingi ktk kiwanda cha kutengeneza marumaru cha Godwill ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani.

Rais Magufuli aliunda tume mbili za uchunguzi pamoja na watu wa TRA, Ripoti ilionesha kuwa ACCACIA wamekwepa kulipa kodi ya shilingi trilion 68 kwa miaka 17.

Ilipofika June 15, 2018 Mgodi wa Buzwagi ukatangazwa kufungwa ndipo hapa sisi na Wataalam wengine tulipopata nafasi ya kutengeneza program maalum ya Buzwagi katika ushirikishwaji wa Wafanyakazi wake kuelekea kufungwa kwa mgodi katika kipindi cha miaka miwili yaani mgodi ulikuwa ufungwe 2020.

Mgodi wa Buzwagi ni sehemu ya makampuni ya ACACIA ndiyo sehemu kubwa iliathiriwa na kuzuiwa kwa mchanga uliofahamika kuwa una madini (Makinikia).

Tulikuja na Programu maalum iliyofahamika kama “NO HARM 2020” kuwaanda Wafanyakazi wa mgodi na maisha baada ya kufungwa kwa mgodi mpango huu ulikuwa maalum kusimamia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mgodi kufungwa kuhakikisha hatua za mwisho wa Buzwagi zinaendeshwa kwa njia ambayo itawaandaa Wafanyakazi na Jamii kwa fursa mpya.

Unaweza kuhoji uzalendo wangu uko wapi kwenye haya kwanini tuyaseme leo, ukweli ni kwamba haya tuliyasema kabla hata na baada tena kwa uwazi bila uficho Ilikuwa Ili tushinde ishu ya Makinikia lazima tujitoe MIGA Convetion ambao sisi Tanzania ni wanachama kwa kirefu ni Multilateral Investment Guarantee Agency ya Benki ya Dunia.

Hii inakataza kwa mwanachama haruhusiwi kumnyang’ang’anya mali mwekezaji kama serikali ya awamu ya tano ilivyofanya kwenye Makinikia, kule tulikuwa tunakwenda kupata hasara zaidi ya hasara. Tungeweza kusimama na msimamo wetu wa ripoti ya Osoro na Mruma kwa kijitoa MIGA ni kama ambavyo Marekani haitambui Mahakama ya uhalifu wa kivita ICC pamoja na ubabe wao wanaoufanya hapa Dunia Marekani hashitakiwi ICC.

Serikali haikuplay smart ilitumua nguvu zaidi na propaganda nadhani ni Sawa waliamua kumpiga mtu waliyemfunga mikono kwakuwa hata washauri walikuwa wanashuriwa na wanaye mshauri.

Ripoti ya Prof Osoro ilionyesha Serikali ilikuwa inapoteza trilioni 68.59 ambazo zilikuwa ni Sawa na Bajeti ya miaka miwili ya serikali kwa makadirio ya bajeti ya Mwaka 2017/18
Kihoja ni Pale Serikali hiyohiyo kupitia kamati ya mashauriano chini ya Prof Kabudi ilikubali kulipwa bilion 700 Sawa na dola milioni 300 na katika makubaliano hayo haikuwekwa wazi ni Lini hizi hela zitatolewa kwa serikali walitanguliza kishika uchumba cha shilingi milioni 100.

Hata sisi Wazelendo uchwara tuliona tutapigwa kwasababu tulisema wamekwepa kulipa trilioni 68 halafu kirahisi tukalipwa bilioni 700 means walitushinda mezani.

Mambo anayotakiwa Luaga Mpina kumuuliza Prof Aidan palamagamba kabudi ni kwanini.

Serikali ilikubali kupoteza shilingi trilion 360 kama adhabu ya ucheleweshaji wa kulipa kodi kwa kampuni ya ACACIA na kupokea bilioni 700???

Swali la Pili

Kitu gani kiliwasibu kamati ya mashauriano kuamua majadiliano ya malipo yakafanyike nje ya nchi….??

Tufunike kombe mwanaharamu apite kuwa kamati ya Prof Osoro, Prof Mruma na wataalam wa kodi TRA ilikuwa Rubbish…..??

Tusio Wazalendo tunamkumbusha Luhaga Mpina makubaliano ya serikali ya Magufuli na Accacia yalisimamiwa na Prof Kabudi Oktoba 2017, pande hizo mbili ziliafikiana kuwa kampuni hiyo kuilipa Serikali ya Tanzania hisa ya asilimia 16 na mgawo wa asilimia hamsini ya mapato ya mauzo ya dhahabu kutoka migodi 3 inayoimiliki..

Barrick pia walikubali kutoa Dola za Kimarekani milioni 300 (hizi bilioni 700) kama malipo ya kuonesha nia njema ya kufidia fedha zilizotokana na upotevu wa mapato kutokana na biashara ya kampuni hiyo.

Mwisho wa kununukuu ilipofika 24-January 2020 Rais Magufuli alitoa ruhusa makontena yenye makinikia yaliyokamatwa bandarini Dar es Salaam yauzwe.

Aliagiza makontena yakabidhiwe kampuni ya Twiga Minerals Corporation, yatafutiwe mteja yauzwe kampuni ya Twiga na Kampuni ya Barrick wanufaike.

Asanteni.
 
Kabudi alikuwa anamuingiza chaka Magufuli. Hakuwa na weledi wa sheria zaidi ya makaratasi ya darasani
 
Kwanini walilipa 700 billion? Tuanzie hapo kwanza halafu tujadili 360 trillions.
 
FB_IMG_1663951325426.jpg
 
Back
Top Bottom