Prof. Janabi unataka uwapangie watu ratiba za kula?

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,702
36,141
Hivi ndivyo vichekesho ambavyo vinapatikana Bongo.

Prof. wa kwenye media, professor Janabi siku moja nilimsikia anasema kuwa kama unavaa nguo yenye kiuno size 37 wewe ni mgonjwa. Inamaana huyu Prof. hajui kuwa kuna watu naturally wana maumbo makubwa?

Kama mwili wako una umbo dogo ukinenepa na kuvaa suruali size 32 yawezekana uko over weight. Kuna mtu mwingine akivaa suruali size 34 kulingana na mwili wake hapo tunasema anaumwa na amekonda.
Huyu Janabi hata BMI ya form 2 ina maana kaisahau?

Zaidi ya yote ni kwamba kila mtu aishi apendavyo. Hata gymnast na athletes wengi wanakufa chini ya miaka 55, hivyo maisha hayana kanuni.
 
Prof uchwara sawa na Mwenzakw Kabudi tu. Sasa prof hana tofauti na Lokole huyo. Jana anasema tusile vitu vitamu. Eti hata kula chungwa au ndizi ni hatari kwa afya. Jamaa anatengeneza tension bila sababu yoyote na anatafuta trending kama Mwijaku sasa.
Haya ndio yale ya yule Dr. wa kisabato aliyewaharibu Watanzania kwa kushindia Dona.
Dona ina sumu na inaharibu uwezo wa kufikiri wazungu wameprove.
Sasa hivi Watanzania wanapiga Dona mno
 
Hivi Janabi ni cardiologist ama Nutritionist?

Maana anavyoongelea chakula ni kama vile yeye ni specialized Nutritionist.

Ama ukiwa daktari unaweza kuzungumzia jambo lolote la chakula?
Huu mswali inabidi akandamizwe na Mwanahabari aliechafukwa sio hawa wanaopangiwa cha kuuliza wakifika kwenye Press kila mmoja anapewa karatasi yenye maswali waliulize na wasiulize maswali tofauti na yaliyopo kwenye hio karatasi yaan Prof anakua amekuja na majibu ya kila swali litakalo uliza sio swali la ghafla.
 
Siyo kazi yake kugundua dawa yeye si pharmacist
Ndugu huko Ulaya madaktari hugundua dawa, na pharmacist nao hugundua dawa.

Haya nitajie dawa iliyogundulika na pharmacist wa chuo kikuu cha Tanzania na hiyo dawa imevuka mpaka wa nchi? Usinitajie ile dawa yenye mchanganyiko wa limau, vitunguu swaumu na ndimu ambayo NIMRI walikopi uswahilini kipindi cha COVID.

Kama daktari hatakiwi kuzijui dawa na effects zake kwanini wanawaandikia dawa wagonjwa?
 
Janabi msanii anaenjoy kiki ya kutrend mitandaoni.

Mwenyewe ukimuangalia tu unaona kafubaa kama ana utapia mlo.

Janabi ni ile design ya watu wa fanya ninachosema sio ninachofanya. Ukute jioni ananyuti kwenye vijiwe vya alkasus mixer njugu na mihogo mibichi ila tu akapate kimoko nyumbani, halafu anatuhubiria mambo ya kujishindisha njaa.
 
Uliyeanzisha Uzi, wewe umegundua Nini? Janabi anaongea kutokana na kile anaona kwa wagonjwa wake, ni haki yake ya msingi kuzungumza na kutoa tahadhari. Kama hutaki acha, haina haja ya kudharau professional yake kwasababu zako zisizo na mashiko.

Nakushauri tu, jitahidi uwe na utaalamu uliobobea halafu uongeze tukusikie nyau wewe
 
Ndugu huko Ulaya madaktari hugundua dawa, na pharmacist nao hugundua dawa.
Haya nitajie dawa iliyogundulika na pharmacist wa chuo kikuu cha Tanzania na hiyo dawa imevuka mpaka wa nchi?.
Kama daktari hatakiwi kuzijui dawa na effects zake kwanini wanawaandikia dawa wagonjwa?
Sisi hatuna kituo cha ugunduzi wa madawa au kipo ??
 
Back
Top Bottom