Prof. Janabi anakera sana walafi na watu wasio na akili. Janabi atangazwe kuwa shujaa wa taifa

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,892
155,910
Let us talk reality! Mimi sio mdau kabisa wa huyu professor. Pengine kuna mambo yake baadhi siyapendi kabisa ila hichi anachokiongea kuhusu ulaji anaongea ukweli asilimia mia na zaidi mbaya zaidi wa tz huwa ni wabishi kwa kila kitu, naomba nikuangazie vitu kadha wa kadha 😭😭

Leo hii ng'ombe wa kienyeji wanapigwa vita pengine wanatokomea kabisa, ng'ombe tulio nao ni wale mnaowaita wa kisasa ambao bila sindano hawaendi lazima madawa na ma chemicals jiulize maswali je maziwa unayokunywa ni salama? Ndio yele walokunywa babu zetu?

Mahindi ya kilimo cha zamani yamepotea sasahivi tunaambiwa kuna mbegu za kisasa na za muda mfupi, tena bila madawa hayakui so jiulize ugali unaokula tena bila kukoboa ni salama?

Mchele wa zamani umepotea leo kuna mbegu ya kisasa ya madawa 😭😭😭

Hali kadhalika matunda yote ni ya kisasa.

Maji tunayokunywa sio yale ya chemichemi ni yale ya viwandani yenye chemical.

Kwahiyo binadamu wa sasa ndie anaemuangamiza binadamu mwenzake.

Jiulize kuanzia asbh mpaka jua linachoea unakula chemical tu mwilini utapona kweli? Ndio maana leo umri mdogo ndio wanaoondoka kwa haraka, please mweleweni Janabi.
 
Watu wamemmaindi vibaya, wanamkandia, wanaona anawakera na kuwatisha katika mitindo yao ya kula na kunywa hovyo wakati wanaambiwa ukweli.
Waswahili wa Tanzania hawapendi kuambiwa ukweli, ukiwaambia uwongo ndio wanasadiki, ndio maana nyerere aliwadanganya kuwa mwenge unaleta amani. Mungu hadhihakiwi, miaka kadhaa mbele Nduli idd amin akaishambulia Tanzania, nyerere akaumbuka.

Badala ya kuupeleka mwenge uwanja wa vita, wakapeleka askari wetu ambao wakafa mamia kwa mamia.
 
Watanzania wanaambiwa Ukweli awataki. Wewe uliona wapi Ata Wanawake wana vitambi😁Watu wanafakamia miwali saa 2 Usiku utafikiri wanakwenda Vitani kumbe wanaenda Kitandani kulala. Asbh Chai sukari vijiko 3 , Chapati 3, na Supu juu
Hatari sana. Tunalundika mawanga a mimafuta kwenye milo yetu. Tumeamua mdomo upitishe mauti zetu, ndio maana magonjwa yasiyoambukizika yanashika kasi.

Tutumie midomo yetu vyema. Mdomo ni lango la afya
 
Huwa najiuliza hivi kweli ng'ombe anayetoa lita 30 za maziwa kweli yale maziwa yana nutrients za kufaa kwa binadamu?

Tumefuga ng'ombe kijijini inatakiwa maximum atoe lita 1

Mti wa mmpapai una urefu wa futi 3, hata mtoto wangu wa miaka 4 anaangua papai akiwa amesimama

Sent using Jamii Forums mobile app
Mpapai una miezi miwili unaanza kuzaa matunda
 
Janabi anazingua sana, ulaji wa mtu unategemea sana aina ya kazi anazofanya. Tuache kula carbohydrates wakati kazi zetu zinahitaji matumizi ya nguvu, anataka tufe?

Hizi teachings zake mara nyingi zinalenga wale wanafanya kazi maofisini, mda mwingi wamekaa, wanamiliki usafiri binafsi nk. Mtu ni mkulima, anaamka saa11 kwemda shambani, ale milo miwili? ale matunda jioni akalale? Huyu jamaa amewahi kuwa mkulima kweli?
 
1708591217250.jpg
 
Back
Top Bottom