Ubadhirifu wa fedha za Mradi wa world bank wa HEET

hiplip

Member
Jun 14, 2013
37
12
Habari zenu wanajamvi,

Mimi nina kero au dukuduku kubwa kuhusu pesa za mradi wa HEET zinazotolewa na world bank. Pesa hizi zilikuja maalum kwa ajili ya kujenga majengo mapya na vifaa vya kisasa ndani ya vyuo vikuu pamoja na kusomesha staffs wake.

Lakini kumekuwa na ubadhirifu mkubwa sana juu ya matumizi ya fedha hizi ambazo ni zaidi ya bilioni 10 naomba nizungumzie chuo kikuu cha University of Dar es Salaam au UDSM kama wengi walivyozoea kama ifuatavyo;

1: Waajiriwa wa kiufundi yaani technical staffs hawasomeshwi na pesa za HEET na wengi walikuwa wameomba ufadhili ili wakaongeze elimu nje au ndani ya nchi kulingana na kitu mtu alichotaka kusomea ila walinyimwa na kujibiwa fedha hakuna na baadhi yao tayari walikuwa wameshapata admission kwenye vyuo tayari.

2: Wamesomesha waajiriwa wachache ambao ni walimu ila technical staffs hawajasomeshwa kabisa hata mmoja kwa fedha hizi

3: Hakuna vifaa vilivyonunuliwa wala majengo mapya yaliyojengwa kupitia fedha hizi.

Serikali tunaomba sana mtume wakaguzi ndani ya huu mradi ili kujua fedha hizi zimetumikaje ubadhirifu ni mkubwa sana sana ndani ya chuo hiki UDSM.
 
Back
Top Bottom