Prof. Anna , anaweza au wizara imemzidi kimo!

Ndakilawe

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
4,815
2,819
unnamed+(75).jpg


Nimekuwa nikifuatilia ujibuji wa hoja wa Professor juu ya wizara yake, lakini nimekuwa simuelewi kabisa (pamoja na kiswahili chake kibovu), amekuwa akitoka povu sana kwa maslahi ya wachache (CCM) na sio wanyonge (UKAWA)!

Ushauri kwake tafadhali!
 
unnamed+(75).jpg


Nimekuwa nikifuatilia ujibuji wa hoja wa Professor juu ya wizara yake, lakini nimekuwa simuelewi kabisa (pamoja na kiswahili chake kibovu), amekuwa akitoka povu sana kwa maslahi ya wachache (CCM) na sio wanyonge (UKAWA)!


Ushauri kwake tafadhali!

Mkuu hapa nafikiri una issue yako binafsi! Maana swala la performance na kudeliver linaweza kuwaklishwa kwa njia nyingine ambayo ni fair! Lkn swala la kiswahili kibovu linakuja vipi kwenye performance yake kama Waziri wa Ardhi! Hapa nafikiri unatafuta msaada ambao hautaupata kamwe. Hatutaki unafiki hapa, tujaribu kuongea vitu vya uhakika na si kuropoka tu. Nafikiri ujumbe wangu umefika!

 
Tatizo ni mfumo anaofanyia kazi hamruhusu kuonyesha weledi wake, alianza vizuri sana. Tatizo la ardhi haswa kwa Dar hakuna asiye juu jinsi wanaoitwa vigogo walivyojitwalia maeneo yasiyostahili kuwa makazi na kuyageuza matumizi. Kupambana na aina hii ya wavunja sheria ni lazima mfumo unaofanyia kazi uwe nawe bega kwa bega, lakini tunayoyaona tunayaelewa. Ninachoweza mlaumu ni kwanini anaendelea kukaa humo ukiangalia uzoefu alionao na vitu ambavyo angeweza kufanya akiwa nje ya huo mfumo.
Matatizo ya ardhi nchi hii yameletwa na siasa mfu, siasa zisizoangalia long-term benefits za mfumo wa kiikolojia ndo maana ugomvi kati ya jamii za wakulima na wafugaji havitakwisha leo wala kesho. Tukiachana na siasa hizo na kuangalia mustakabali wa nchi na vizazi vijavyo tutaanza kwanza kupanga miji yetu vizuri ili hata miundombinu ya maji au gesi ipite kwa urahisi.
Kwa ufupi mfumo wetu wa uendeshaji wa siasa hapa kwetu haukuruhusu kuonyesha uwezo wa kiutendaji zaidi ya 'wakubwa' zako.
 
Alipoanza uwaziri wake aliingia na gia kubwa kwa kuvunja kuta pale Palm Beach na Agakhan Hospital; wenye nchi wakasema kuwa huyo muacheni kwani ni nguvu ya SODA na kweli toka hapo hajafanya lolote jipya zaidi ya kuingizwa kwenye cc ya magamba na ndio ikawa mwisho wake!!! Viwanja vya wazi vinaendelea kuvamiwa na barabara kufungwa na wenye fedha kama vile nchi haina serikali!!
 
Wizara imemzidi amebaki kuongea kwa jazba na hasira kila akihojiwa kuhusu ubadhilifu anaoufanya.
 
huyu mama wizara imemshinda kabisa wala hana uwezo wa kuwa waziri kabisa, kwanza yeye mwenyewe ni kinara wa kuvamia maeneo ya wazi atawachukulia vipi hatua wezake?
 
Ni kilaza. Ukiangalia alivyopandisha rates za kodi za ardhi ..land rent .. utashangaa sana
 
Toka kapewa hiyo wizara migogoro imeongezeka mara dufu kazi imemshinda
Maeneo ya wazi yanazidi kuuzwa tu
 
huyu mama kwanza angesafisha wizara yake na angefatilia ubadilishaji mbovu wa hati katika ofisi zake hapo ndio angeiweza wizara
 
Muache mama yetu apumzike kazeeka mno ndio muda wa kuanza kupoteza kumbukumbu
Nasikia Muleba agombei tena
 
huyu mama kwanza angesafisha wizara yake na angefatilia ubadilishaji mbovu wa hati katika ofisi zake hapo ndio angeiweza wizara

Rushwa ziko nje nje katika kitengo hicho mkuu. mtu anafuatilia ku renew hati baada ya miaka 30 au33 kuisha anazungushwa miaka 7 na bado hajui atajibiwa lini. Au mtu anaomba hati na kutoa rushwa zaidi ya million moja na bado hata harufu ya hati haipati. pagumu pale!! sitaki kuulizwa kwa nini mtu atoe rushwa kwani hilo ni swali la kinadharia mno.
 
Haya mimi nilisema watu wakabisha. Huyu mama hawezi hawezi hawezi na hawezi. Kazi kubwa aliyoifanya kipindi chake ni kujimilikisha mahekali na mahekali ya ardhi kwenye jimbo lake huku akitumia nafasi yake kuhakikisha anahalalisha umiliki kwa kufyatua hati kwa kila hekali. 2015 kama mbali vile.....
 
Wananchi tusilalamike kwani sisi ndi watoa rushwa na ndio maana shughuli yako hutafanikiwa mpaka utoe chochote. Tukatae kutoa rushwa uone kama kazi hazitafanyika. Na mara nyingine rushwa hutolewa pale mtu anapotaka apewe haki kwa kuvunja sheria! Unataka sehemu ya wazi au pembeni mwa mto unatoa pochi kiwanja kinachongwa.
 
Hakika nami nakubaliana na baadhi ya WanaJF.kuwa mleta mada atakuwa na tatizo binafsi ndo maana tunasikia hadith za kiswahili chake kibovu. Binafsi nashauri mleta maada atupe Comperative analysis kwa kulinganisha watangulizi wa M.Tibaijuka,kwenye Wizara hii halafu tutajua kama ameshindwa au la?
 
Back
Top Bottom