Prince Bagenda ashambulia vikali M4C ya CHADEMA

huyu mzeee njaa itampeleka pabaya mimi bagenda ni bosi M.E hapa kwetu lakini hana jipya zaidi kutembea vocha mkononi kuomba hela za entertain na makundi kama alivyokuwa nccr
 
we, usicheze na njaa na ukichukulia kwa sasa migomba kule Rubya inaharibiwa na ugonjwa wa 'mnyauko'.
Lakini ninachokumbuka juu ya Price Bagenda alikuwa mtu mwenye akili sana ila inaonekana sasa kaamua 'kufaidika' nazo peke yake badala ya kushare na Watanzania wenzie

Njaa mbaya sana...ila kufulia kisiasa ndio kubaya zaidi
 
Namshauri atumie muda wake kuandika kitabu kuhusu tumaini lililokufa ili walau awezwe kusikilizwa kwani 2005 aliandika kijitabu kuwa JK tumaini lililorejea ...

Sasa anapaswa kuandika kingine kuelekea 2015 kuwa CCM tumaini lililopotea ili walau watu wajue kumbe anaweza akafikiri kwa ufasaha.......
 
Kipindi flani nilisafiri na Bagenda kwenda kwenye moja ya mikutano ya Wanaharakati wa umoja wa Afrika (Mkutano uliotengeneza Azimio la Tripoli-Libya).

Tulizungumza mengi lakini nakumbuka tukiwa kwenye hoteli moja Zurich, Uswiss aliniambia, "Siasa za Tanzania hazihitaji akili nyingi.

Mimi nina watu wangu nikiwalenga wananipa hela maisha yanaenda.Kwanza mimi mwenyewe mgonjwa (Sikuchunguza ni ugonjwa gani alimaanisha) kuna hoja ukiibua hata ukimfuata mtu anakupa hela".

From there nilimu dump Bagenda Prince totally.
Itanichukua miaka ya kuzimu kujadili hoja za huyu (Old man)

Bagenda ni MERCENARY; ukiwa na pesa unamkodisha anaandika yale mambo unayotaka mradi apate bahasha.
 
Hivi huyu alishaacha kazi kule TISS?? Au naye anaendelea kama mzee wa Kiraracha?

Hata hivyo, hana jinsi zaidi ya kutumikia wale wanamuweka mjini!!

Ila ingekuwa bora akajikita kujadili yale mambo anayoyajua vizuri kuliko kudandia treni kwa mbele. Na hata hivyo, inaonesha ana hang over ya kutisha....Anaposema kuwa makundi ndani ya lichama lao la CCM yalinufaisha CHADEMA, ana maana kuwa kwa sasa makundi hakuna??

Ni bora akakaa kimya ili tuzidi kumsahau.....Hivi hawa jamaa wa BKB wana matatizo gani??....au ndo mwendo wa kutafuta mkate kama ndugu zake Salva na Mhingo Rweyemamu???!!
 
Thomas Ngawaiya, Masumbuko Lamwai, Aman Walid Kaborou, Tambwe Hiza, Shaibu Akwilombem. Mkiwajuwa hawa vyema afya zao kisiasa kwa sasa baada kurudi CCM, hapa tunapaswa kuishukuru CCM kwa kuwauwa kisiasa mapema wasaliti wote kabla ya madaraka ya nchi kurudishwa mikononi mwa Umma mwaka 2015. Hongera CCM.
 
Ha ha ha ha ha... huyu jamaa nasikia ni kibarua wa RA pale Sinza Kijiweni a.k.a New Habari Corporation...Msitegemee jipya toka kwake.. anandikka kuwafurahisha mabwana zake.. political theories zake unapplicable nowadays...siku moja nikutana naye Jolly Club mida ya saa 3 asubuhi Jumapili last year anabwia supu. Nikamuuliza vipi siku hizi umerudi kuwa kijani kijani? akanijibu '' mtu hawezi kuwa mpizani for all his life''..Mwacheni agange njaa zake ana watoto jamani.. Mentally fully depreciated ....MWAACHE

Kwa hyo hawezi kua mpinzan cku zote je ccm ikianguka na kua upinzan itakuaje? Huyo ni mfuac wa siasa majitaka
 

Ndo anajitahidi kujionesha kuwa yupo. Hivi kile kitabu chake cha 'JK: Tumaini lililorejea' kiliishia wapi baada ya yeye kutoswa uongozi na JK?
Dah....!! aliandika hadi kitabu cha kumsifia JK?
 
Ha ha ha ha ha... huyu jamaa nasikia ni kibarua wa RA pale Sinza Kijiweni a.k.a New Habari Corporation...Msitegemee jipya toka kwake.. anandikka kuwafurahisha mabwana zake.. political theories zake unapplicable nowadays...siku moja nikutana naye Jolly Club mida ya saa 3 asubuhi Jumapili last year anabwia supu. Nikamuuliza vipi siku hizi umerudi kuwa kijani kijani? akanijibu '' mtu hawezi kuwa mpizani for all his life''..Mwacheni agange njaa zake ana watoto jamani.. Mentally fully depreciated ....MWAACHE
Afadhali amekiri kuwa anafanya siasa za kuganga njaa
 
Kada wa chama cha mapinduzi na mwanasiasa mkongwe nchini Prince Bagenda amekishambulia chama cha Demokrasia na Maendeleo-CDM kwa operesheni yake ya M4C inayotishia uhai wa CCM.
Katika makala yake ndani ya gazeti la RAI Prince Bagenda amedai M4C ni chama kipya cha siasa ndani ya CDM na kusema hali hiyo ni hatari kubwa kwa ukuaji wa chama hicho na amesema utatokea mvutano mkubwa kati ya wafuasi wa CDM na wafuasi wa itikadi ya M4C.
Bagenda pia amesema kampeni ya M4C wanayoongoza nchi nzima inatangaza sera za shari na chuki.Pia amesema CDM walipata kura nyingi uchaguzi mkuu uliopita kutokana na vita ya makundi ndani ya CCM na kamwe si kutokana na chama hicho kuwa na sera nzuri.Amesema CDM hawana Itikadi inayoeleweka hadi sasa ndiyo maana mpaka sasa wajanja kama yeye wako CCM.

Source:RAI Alhamisi

My Take:
Prince Bagenda alishiriki kusambaratisha chama cha NCCR Mageuzi baada ya kuongoza mgogoro mkubwa huku akikimega chama vipande viwili na yeye akiwa Katibu Mkuu kambi ya Mrema.Baada ya kufanikisha kusambaratisha NCCR,Prince Bagenda alihamia CCM ambapo hadi leo yeye ni kada mwaminifu wa CCM.


muulize na ile ya Vuagamba ya CCM kilikua ni chama kingine ndani ya ccm ? ama anacho fanya nape sasa hivi kuzunguka mikoani Nimwanzao wachamakingine ndani ya ccm

Nivigumu sana nyani kuona kundule
 
Huyu naye si aende kule kijijini ajue moja...bado yupo kwenye hizi siasa?[/



kwani kuna aliyemwomba ushauri huyo prince juu ya kuimarisha chama kingine? aimarishe tu chama chake bila kuangalie wengine wanafanya nini.
 
Back
Top Bottom