Kwamba maudhui ya kile kitabu chake cha mwaka 2006 ''Tumaini Lilillorejea'' yaliegemea katika itikadi gani?Yafaa pia atueleze sasa tuzingatie nini hasa kama udhihirisho ama hakikisho la Tumaini hilo ambalo wengine hatulioni hadi leo.Halafu NCCR-Mageuzi aliyopata kuiongoza ilipata kuwa na itikadi?Wananchi walikiunga mkono chama hicho ,mwaka 1995, kwa sababu kilikuwa na itikadi iliyokuwa wazi na yenye kueleweka?Hapana.Wananchi walikuwa wanataka mageuzi na mabadiliko.Walichoshwa na hali iliyokuwepo,basi!Je,kuondoka kwake NCCR kulichangiwa na kubadilika kwa itikadi yake ama kuna kingine?Kama hakuondoka kwa sababu za kiitikadi pekee,kwa nini, sasa ,uchambuzi wake uegemee katika itikadi pekee?
Atambue kuwa,hata sasa, wananchi wanaosaka mabadiliko hawataki kujua sana misamiati ya ''itakadi'' , ''falsafa'', ''mwelekeo'' ama ''Imani''!!Wao wanataka mabadiliko..Kama hajaiona ''itikadi'' ,tumwache aendelee kuitafuta anaweza kuiona ADC ama DP ama CHAUSTA! ikiwa baadhi ya wahafidhina wanadhani hatuna itikadi hilo litatatuliwa mbele ya safari...
Mwisho,baadhi yetu tunamtazama Bagenda kama msaliti na kama mtu aliyekosa msimamo.
Baadhi yetu tulikuwa wasomaji wa makala zake wakati huo RAI ikiiunguruma kweli kweli..Alitujengea roho za upinzani tungali wadogo kabisa -tukisoma gazeti la ''RAI'' lililokuwa likiletwa nyumbani na wazazi wetu- .Tukajenga,hatimaye, mashaka dhidi ya watawala.Sasa tumeota sugu kweli kweli ..Baadhi yetu tumweka nadhiri kuwa kamwe hatuwezi kukana dhamira zetu. Hakuna kurudi nyuma.Yeye aendelee kulingoja ''Tumaini Lililokuwa lireje''!!