Pride Comes Before the Fall: CHADEMA inabidi wajipange upya

daaaah kwani watu mnatumia kiungo gani kufikiri chadema na ccm nani mwenye pride(ego)?
 
Umemuita mjinga bila sababu; na hiyo ndio CDM ya sasa. Uwezo wa kujenga hoja umepungua sana. Miaka ya zamani vijana wa CDM walitisha hapa jukwaani kwa michango yao constructive..

Ukiona kijana anaongea Utanganyika jua kuna tatizo hapo; na for the benefit ya Nchi ni nadra kushinda uchaguzi wowote. Hata kama nchi ilikosea lakini sisi wabara ni watanzania zaidi kuliko watanganyika. Hiyo ni tunu yetu, hata mataifa ya ulaya yamekosea mambo mengi lakini yanajitahidi kumantain hayo waliyoyakosea hadi leo. Ni tunu zao. Imagine UK hadi leo wana utawala wa kifalme na hawana mpango wa kuuacha, sisi miaka sitini tu tunaongea utanganyika. Mbaya sana hii. Kwa mtu aliyezaliwa 1980 anaijua hata hiyo Tanganyika?

Ukirudi kwenye mada; mtoa hoja yuko sahihi, ni rahisi zaidi kudeal na CDM ya leo kuliko ya zamani. Imagine baada ya TAL kuwekwa ndani, kiongozi gani mwingine kwa sasa anaweza akaitisha mkutano nje ya jimbo lake na akaatract mass kubwa ukimtoa Makamu kwa Cheo chake? (Angalia hata mwitikio wa mkutano wa Heche jana mbarali na kyela) Yaani pambalu aende Arusha alafu apate watu? Sosopi aende Maswa apate watu?? lakini CDM ya sasa inawaona wastaafu ni wasaliti... wakati CCM ina hazina kubwa. Huwezi kushinda uchaguzi kama hauna akili za kisiasa....
Sijakuelewa una maana gani kwamba hamna kiongozi aliyejitokeza kumtetea TAL, viongozi wote wanaogopa kukamatwa, hawatadhubutu kuja hadharani kuonesha support kwa TAL.

Ila hamna kesi ya kumtia hatiani. Wanasheria wengi tu na Civil Society na Mataifa mengi yapo Nyuma yake. Vivyo hivyo kwa Mikutano ya Mkoani hali ni hiyo hiyo, watu wanaogopa kupigwa Mabomu ya Machozi na Maudhi menginne. Sio kwamba CDM imepoteza umaarufu.

Tofauti na Mawazo yako. Vitisho vya vikipungua watu watafurika Mikutano sio ya CDM tu bali na Vyama vinginne vya upinzani.
 
Mbowe alipotoka rumande alikaa na Samia wakakubaliana mazungumzo yatakayo wapeleka kwenye maridhiano. Mazungumzo hayo yalifanikisha yafuatayo:
1. Viongozi waliokuwa wakimbizi waliweza kurudi nchini na kuendelea na shughuli za siasa. Baadhi yao ndio sasa wanaongoza CDM. Inawezekana bila mazungumzo ya maridhiano wangekuwa bado wakimbizi hivyo ingekuwa vigumu kushiriki katika uchaguzi.
2. Zuio la mikutano ya hadhara na mingine ya kisiasa likaondolewa. Lingekuwa bado lipo, hii mikutano ya NRNE isingefanikiwa.
3. Wanachama wa Chadema waliokuwa ndani waliachiwa na kesi zao kufutwa. Hali hii imeongeza imani kwa CDM kuwa inapigania wanachama wake.
Kitu kingine ni kuwa CDM iliweza kukubali kupokea ruzuku yao ambayo iliwawezesha kununua jengo lao la Makao Makuu na kukipunguzia mzigo wa gharama za uendeshaji.
Naam, waliendelea kufanyiwa dhulma lakini walikuwa katika nafasi nzuri ya kukabiliana nazo kwa sababu kwa kiasi kikubwa CDM ilikuwa imeungana.
Uongozi mpya umesema wazi kuwa strategy ya Mbowe haina tija na kinachohitajika ni approach ambayo ni more confrontational. Approach ambayo ni ya ninja ninja. Na hakuna kubembelezans. Ams uko nasi au wewe ni adui yetu. Mafanikio ya approach hiyo mpaka sasa ni:
1. Kumekuwa na muitiko mkubwa kutoka kwa wananchi kuhusiana na wito wao wa NRNE.
2. Wanachama na watu wengine wa kawaida wameonyesha moyo wa kuchangia mfuko wa chama.
3. Dunia nzima imetambua uwepo wa CDM.

Lakini pamoja na hayo mafanikio, yafuatayo yametokea:
1. CDM imeondolewa katika orodha ya vyama vitakavyo shiriki uchaguzi mwaka huu. Kuna uwezekano mdogo sana wa hali hii kubadilika.
2. Mfuasi mkubwa ambae sasa ni mwanachama alishikwa na kuwekwa ndani. Alifutiwa kesi bila presha yeyote kutoka kwa wananchi.
3. Mwenyekiti wa CHADEMA yuko rumande. Ukiondoa juhudi zinazofanywa nje ya nchi na taasisi chache nchini, hamna presha kubwa kutoka kwa wananchi ya kutaka aachiwe.
4. Mwanachama maarufu wa CDM amepotea katika mazingira ya ajabu. Nako pia tunasikia vitisho tu jukwaani na mitandaoni lakini hatuoni presha kubwa ikifanyika on the ground za kuhakikisha yeye na wengine waliopotea kabla wanapatikana. Presha hizo ni maandamano, sit ins, hunger strikes,
5. Chadema imegawanyika, na baadhi ya waliokuwa viongozi na wanachama waandamizi wamejitoa kwenye chama. Matokeo ya hatua hii ajenda kubwa ya chama sasa inaonekana ni kukabiliana na wale wanaodai kuwa ni wasaliti. Matusi, uongo, ghiliba n.k. vimetumika kuwachafua watu ambao wamekitumikia chama chao kwa miaka mingi sana.
6. Uteuzi wa watendaji wakuu wa chama na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu umebatilishwa na Mamlaka husika.

Kutokana na yote haya, nawashauri CDM isiendelee kukaza shingo. Ni wakati wa kuwasikiliza viongozi wao wa zamani ili wakinusuru chama chao. Wanahitaji busara za mtu kama Mbowe.

Najua kuwa itawauma sana lakini uongozi makini unahitaji flexibility ya kuweza kugeuza position of weakness kuwa strength. Lakini nahisi kwa kiasi kikubwa pride yao itawazuia kufanya hivyo.

Amandla...
 
Kabla ya uchaguzi wa CDM, baadhi yetu tulisema CCM ilitaka Lissu ashinde kwa sababu ni rahisi zaidi kum handle kuliko Mbowe. Mojawapo ya sababu ya kusema hivi ni campaign za wazi ambazo wafuasi maarufu wa CCM walikuwa wanamfanyia Mbowe. Lengo lao lilikuwa watu wahisi kuwa Mbowe ni kibaraka na hivyo wampigie kura Lissu. Walijua kuwa Lissu ni passionate, ana confidence kubwa juu ya uwezo wake, hawezi kukaa na washauri kwa sababu hapendi kukosolewa na ni mtu mwenye visasi.

Mbowe ni tofauti. Ni pragmatic (anaisoma hali halisi na kucheza nayo vizuri hata kama ni kula matapishi yake), ni ruthless katika kufikia lengo la chama chake, ana ego lakini yuko tayari kuwa nyuma ya pazia, ana base nzuri ya washauri na wafadhili kwa sababu anawasikiliza. Pragmatism ya Mbowe inamuwezesha kufanya kazi na hata wale waliomkosea ili mradi chama chake kielekee kwenye kutimiza lengo lake.

Team Lissu ilipozua mambo ya pesa za Abduli ilikuwa wimbo mzuri kwa CCM. Lissu na Heche waliposhinda ndoto yao ikatimia.

Amandla...
Pumba tupu
 
Acha maduka yaondoke chama kibaki safi.
Kuhusu uchaguzi sio kipaumbele chetu kwa wakati huu ambao kura haziheshimiwi.
Wasimamizi wa uchaguzi kugeuka wapiga kura ili kuisaidia ccm.
Bila mageuzi ya kweli katika mfumo wa uchaguzi, kupiga kura ni ujinga na uwendawazimu
 
Kabla ya uchaguzi wa CDM, baadhi yetu tulisema CCM ilitaka Lissu ashinde kwa sababu ni rahisi zaidi kum handle kuliko Mbowe. Mojawapo ya sababu ya kusema hivi ni campaign za wazi ambazo wafuasi maarufu wa CCM walikuwa wanamfanyia Mbowe. Lengo lao lilikuwa watu wahisi kuwa Mbowe ni kibaraka na hivyo wampigie kura Lissu. Walijua kuwa Lissu ni passionate, ana confidence kubwa juu ya uwezo wake, hawezi kukaa na washauri kwa sababu hapendi kukosolewa na ni mtu mwenye visasi.

Mbowe ni tofauti. Ni pragmatic (anaisoma hali halisi na kucheza nayo vizuri hata kama ni kula matapishi yake), ni ruthless katika kufikia lengo la chama chake, ana ego lakini yuko tayari kuwa nyuma ya pazia, ana base nzuri ya washauri na wafadhili kwa sababu anawasikiliza. Pragmatism ya Mbowe inamuwezesha kufanya kazi na hata wale waliomkosea ili mradi chama chake kielekee kwenye kutimiza lengo lake.

Team Lissu ilipozua mambo ya pesa za Abduli ilikuwa wimbo mzuri kwa CCM. Lissu na Heche waliposhinda ndoto yao ikatimia.

Amandla...
Kama ndivyo Lisu alivyo kwa nini chama kilimpatia nafasi ya kugombea urais?
 
Umeandika pumba na siwezi kupoteza muda kuzijibu
Lakini ukazijibu kwa kuandika pumba. Mimi niko tofauti na wewe. Nikiona michango yako haina tija kwangu nakuweka kwenye 'ignore list'. Kwa kufanya hivyo silikoni tena. Ukiona sikujibu ujue kuwa uko kwenye hiyo list.

Amandla...
 
Kama ndivyo Lisu alivyo kwa nini chama kilimpatia nafasi ya kugombea urais?
Hilo swali linapaswa kujibiwa na CDM wenyewe. Labda kwa sababu Lissu ni charismatic sana ana mvuto mkubwa na anaweza kujenga hoja ikaeleweka kirahisi. Aidha, ana ujasiri wa kusema yale ambayo watu wengi wanaogopa kusema.

Wengi tuliamini kuwa hiyo ndio haiba yake hata nje ya majukwaa. Mimi naamini kuwa pamoja na mapungufu yake, kama patakuwa na uchaguzi wa haki na uwazi anaweza kushinda. Lakini akishinda atakuwa autocratic na atalipa kisasi kwa wote ambao anaamini walimkosea.

Amandla...
 
Back
Top Bottom