Press conference: Lowassa apelekewa ujumbe mzito

Duh!! Mbona kama jamaa kavuta shuka asubuhi, Kwani kuna vyeo vilivyobaki? Nape, Makonda and the like walicheza karata zao wakati zilikuwa zinahitajika. Sasa huyu jamaa anaibuka wakati kumeshakucha
huyu mleta uzi ndio watanzania tunaowahitaji katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu,watu wanaothubutu kujitoa mhanga kusema ukweli bila kuogopa mungu akujalie wasije team lowasa wakakutimua nyumbani kama walivyomtimua mzee kasori
 
Bila Edward Lowassa CCM Mtaangukia Pua; Mpuuzeni Huyu Kijana anasumbuliwa na Njaa ya Kufa Mtu. Hakuna la Maana aliloliandika tofauti na Kupigia Debe Kundi lake huko CCM>
woote ccm mna laana ya njaa,afadhali huyu kaikataa kuiendekeza njaa na kujitoa hadharani
 
sijui amekula maharage ya wapi huyu hoza!nilikuwa namuheshimu san lakini sasa simuheshimu teeeenaaaa amelewa lewa tu hovyo kuja hapa na kuandika upuuzi wake kwa lowasa watanzania hatukubali wenye akili kama hoza ni kama mtoto mdogo aliyevishwa pampasi hoza nenda zakoooo tuachie lowasa wetuuuu hatupo kichama sasa tunaangalia mtu anayetufaa watanzania sasa ccm mtuache na lowasa sasa aaaahhhh!!! huu ni wakati wa lowasaaaaaaaa na mabadilikooooooo ya kweliiiiiiiiiiiiiiiiiiiii...
wewe na wenzako kundi la njaa nani kawaroga,kwani mna uhaki,ka gani kwamba lowasa akipitishwa na ccm ndio ameukwaa urais,hiki ni kipindi tofauti na ccm inapitia njia kilichopitia chama cha KANU kule kenya kwa hiyo jianadeni kujutia madhambi yenu.:lol::lol::lol::lol::lol:
 
Nasema hivi,iwe jua au mvua lowassa ndio rais mtarajiwa,mnamfahamu vizuri utendaji wake,hana mchezo wala undugu kwenye kazi,mnaanza mchecheto mapema hivi,kazi mnayo,jamani kama unajijua ni mvivu huko serikarini tafuta njia ya kuchomoka mapema.ccm oyeeeee!!
 
Mhmhmhmh wewe Francis Hoza wewe.Umeshindwa na Asenga ujumbe wa Baraza Kuu la Taifa na sasa unataka kupambana na Lowassa!

Pole sana!
 
Tukiendekeza majungu sidhani kama tutafika
Nafikiri kila kitu tuachieni sisi wananchi tuhamue kiongozi yupi tunamhitaji.
Sifa za uongozi zipo wazi kwa kila mwenye hekima na busara anajua yupi bora na yupi pumba sasa hofu ya nini hadi kuchafuana?
Kama ni kweli Edward alikuwa na hayo basi CCM sio makini
 
Aroo we kijana una msongo wa Mawazo...?
Nenda kachimbe viazi Gairo weee...umekosa point....

Hivi Hata hao waandishi wa habari hawakuchoka kukusikiliza ukirudia point moja Mara 3....


For yo information sasa, tunamwapisha hata akifia kwenye gwaride uwanja wa taifa pouwa tuuu
 
Summarize!!!!!story ndeefuuuuu.
Lowasa na Slaaa ndo watu ambao tukichanganya mawazo yao tutapa kitu kimoja kizuri bila kuangalia ushabiki.mi sina chama nina mgombea .kati ya lowasa na slaaa mi nachagua lowasa.but slaaa na mtu tofauti na lowasa bora slaaa jembe letu
Mkuu katika hao wote wa hovyo kabisa hawafai hata kwa mboga tu.
 
Uchafu mtupu.
Kama ni ufisadi, yes Lowassa ni fisadi, na hajaanza leo wala jana. Kwa CCM ufisadi sio issue kabisa, hakuna kada mwandamizi wa CCM ambaye hana chembe chembe za Ufisadi. Okay Lowassa ni Fisadi, kwanini hamshinikizi afukuzwe kwenye chama?

Nilitamani mambo hayo yote yasemwe na viongozi wa CCM toka siku ile Lowassa anateuliwa na Kikwete kuwa waziri mkuu, lakini sio leo hii wakati Lowassa anataka kugombea urais.
Siku si nyingi Vijana hawa hawa wa UVCCM watakuwa wanakesha mtandaoni humu humu kumpigia kampeni Lowasa ili awe rais mara baada ya kuteuliwa na CCM.
 
Huyu Hoza mwaka jana tarehe 1 alikuwa Monduli na alinyimwa fedha million 10 na Lowassa, naona amepandisha hasira sasa
 
Anza kabisa kutafuta makazi ya kudumu nchi za jirani maana baada ya octoba utaliwa nyama nakuhakikishia bwana hoza na hao waliokutanguliza.
 
Inaeleweka wazi wazi kuwa Hoza ametumwa na Mwigulu Nchemba azungumze hayo. Hizi njaa zitawamaliza vijana ambao wanashindwa kufikiri mara mbili mbili kwa kuchanganya na za kwao
 
Atakuwa kapata majibu had sasa kwamba lowasa hajitafutii umaarufu km yeye anavyowaza, bali watu ndo wanamtafuta awe raisi.
mtu mzima afu mwanaume unakaa chini kutunga pamphlet ya majungu....
kule kwetu ungeonjeshwa kisu cha moto,
taarifa za mipasho km hizi atoe mwanke sio ww mwanamme
simjui lowasa namuona tu kwenye tv, ila umenikwaza kuliko siku yoyote leo juu ya mambo ya utawala wa nchi
 
LOWASSA HAFAI, hilo ni kweli. Lakini pia CCM haifai kabisa.

Nikubaliane na mtoa mada kwa msingi huu ya kuwa kwa kadiri Lowassa alivyofisadi na kuhujumu Taifa hili, kadhalika chama cha mtoa hoja kimeifisadi na kulihujumu Taifa mara 100 zaidi; hivyo LOWASSA NA CCM wote hawatufai kabisaaaaa!!!!
 
Back
Top Bottom