Presidential Delivery Unit - Kitengo kipya chini ya Rais - chatengewa Bilioni 29!

Kuna fungu la ajabu sana hapa liinaelekea kupitishwa, hili ni fungu la kutumia 29 Billion kwa ajili ya kuanzisha chombo cha ufwatiliaji wa Miradi ya Kitaifa. Chombo hiki kazi kubwa itakuwa ni kufwatilia utekelezaji wa haraka wa miradi ya kitaifa kazi ambayo sasa hiv inafanywa na Tume ya Mipango. Hivi kweli hii hoja ina mashiko na maswahi kwa wananchi??? Hivi kweli sisi shida yetu ni chombo cha kufwatilia miradi???? Hiyo fedha 29 Bilion ingeweza maliza Miradi mingapi ya maana kabisa kwa wananchi???

Kwanini wasijengewe uwezo hao wanaosimamia sasa hvi na wakizembea kwa nini wasiwajibishwe?????Inasikitisha sana. Wananchi hawana maji, hawana madawa, hatuna madawati,walimu wanadai miaka nenda rudi, serikali imepuuza yote haya na inaamua kutenga 29 Bilion kwa matumiz yasiyo ya lazima kabisa. Hili huitaji kufika chuo kikuu ili kuona ni la kipuuzi.

Haya wabunge wa CCM wameshapitisha matumizi ya 29 bilions na hivyo chombo hicho kitaundwa na kutumia ma bilioni hayokwa ajili ya kufwatilia utekelezaji wa Miradi.

Ndugu zangu watanzania, kama hatutajipanga vizur na kuongeza idadi ya wabunge wa upinzani bungeni na kuwatoa CCM madarakani, maendeleo nchin kwetu ni ndoto za alinacha. Shime watanzania tujipange kuingia Bungeni mana kwa kuwaachia Bunge watu wasio na uzalendo ni kujimaliza wenyewe.

Tatizo lenu huwa hamjiamini kwa hoja zenu toka vichwani mwenu(Independently) mnapenda kumezeshwa hoja, nawashangaa sana, Yaani Mnyika kupinga sio lazima na wewe upinge, waweza kujitegemea kuwaza mambo yenye tija katika nchi acha kuburuzwa kijana, jisimamie,tafuta facts kabla hujapost ushabiki.
Presidential Delivery Unit unajua maana yake? unajua umuhimu wake? kama hujui basi uliza Great Thinkers wakusaidie wewe Great Prepitator ili baadae ujue wapi usimame, unless utaburuzwa hata kwa jambo la hovyo!
 
hii methali imebeba ujumbe mzito sana, yaani wakati naangalia huu upuuzi unaoitwa bunge nusura litoke maana point za CDM na CMM mmmhhhh ni kilio tu yaani CCM wanataka waifilisi nchi kabisa
wasambaa tuna msemo wetu ''mfena gemo aweeea kigha''
CCM wanaangalia maslahi yao kwanza.
 
sijui kama umeuelewa vema huu mpango make waziri kasema miladi itakayolengwa ni miladi ya kitaifa na tukisema kitaifa inamaana ni nchi nzima sasa wewe unachojadili kipi mkuu au hukuelewa hotuba ya waziri vzuri.
Ni kweli waziri kasema hivo, lakini kila mradi wa serikali uwe wa kijiji, wilaya, mkoa au taifa tangu huko nyuma una wasimamizi na wafuatiliaji wa kutosha wakiwa ni pamoja na Technical auditors wa ndani na nje. Hakuna haja ya kuongeza wasimamizi tena kwa pesa nyingi kama hizi hata kama ni miradi ya Nchi nzima wakati Taifa linazihitaji pesa hizi kwa miradi mingine muhimu zaidi. Kama kuna kasoro kwa wasimamizi waliop sasa zilipaswa kubainishwa na wachukuliwe hatua za kisheria. UMENIELEWA MKUU?
 
Kwani Tume ya Mipango haikusanyi taarifa za maendeleo ya mipango yake na kupima(delivery to plan)? Kwani haitoi mwongozo kwenye mipango yake? Kwani haijui changamoto za miradi? Sasa wanajuaje mipango yao imefanikiwa? Labda kiwe chombo mahususi cha kijasusi wa miradi cha kumpa Rais upande wa pili wa shilingi..
 
Tatizo lenu huwa hamjiamini kwa hoja zenu toka vichwani mwenu(Independently) mnapenda kumezeshwa hoja, nawashangaa sana, Yaani Mnyika kupinga sio lazima na wewe upinge, waweza kujitegemea kuwaza mambo yenye tija katika nchi acha kuburuzwa kijana, jisimamie,tafuta facts kabla hujapost ushabiki.
Presidential Delivery Unit unajua maana yake? unajua umuhimu wake? kama hujui basi uliza Great Thinkers wakusaidie wewe Great Prepitator ili baadae ujue wapi usimame, unless utaburuzwa hata kwa jambo la hovyo!

Kwa hiyo na wewe kwa Sababu Waziri kasema na wewe unakubali...hata hujajifirisha kidogo.
Watu kama nyie ni wale tunaita maji mara moja.
Fasta mnagawa tigo
 
Hivi ni kwa nini wote wanaopinga haya matumizi mabaya waonekane wabaya au hawana maana na upande huu wa pili? watu wamepewa muwa lakini wanataka waongezewe na sukari eti ndo muwa utaliwa vizuri zaidi!
 
kwa kweli ukiwaza sana jinsi mambo yanavyoendeshwa katika nchi hii, huku ukilinganisha na utajiri wa kila aina MUNGU aliotupa, na huku ukatazama na hatua kiduchu ya maendeleo tunayopiga , kwa kweli unaweza kuingia msituni ukawa muasi.

Nahoji sana hivi hawa washauri wa raisi wanakazi gani, hawayaoni haya.... leo dhahabu inakwisha lake zone, barrick wanajiandaa kuondoka tumepata nini, ikiwa zone hiyo (lake) hata maji nishida na ziwa victoria lipo

Tumefanya makosa mengi sana, tukaua zaidi ya viwanda 300 nchi nzima, tumeua reli kwa makusudi, etc

Mambo ya epa, richmond, meremeta yamepita hayo zaidi ya trilioni 20 zimepotea zenye uwezo wa kujenga zaidi ya kilomita 2000 za rami

Raisi yupo, hiyo taasisi intakayoundwa ni kula pesa tu, taasisi ngapi zipo kwa kazi maalumu na bado matatizo yapo palepale
mfano, tangu takukururu iundwe rushwa ndio kwanza imeongezeka badala ya kupungua, tena kibaya zaidi kwa mujibu wa ripoti za mwaka 2012, sehemu za kutoa haki na huduma muhimu, kama polisi, na mahakama ndio zinaongoza

kwa sasa katika east africa tz ni ya pilikwa rushwa ikipishana na uganda kwa 1%. SIJUI TUNAKOELEKEA LAKINI NAONA KILA DALILI YA VITA MBELE YA SAFARI, TENA ITAKUWA VITA KALI SANA YA WATU WALIONACHO (AMBAO HAWAFIKI HATA 5% YA WATANZANIA WOTE) NA WATANZANIA MASKINI ZAIDI ZAIDI YA 95 %.

LAKINI NASIKITIKA SANA SIJUI KWANINI VIONGOZI WETU HAWATAKI KUJIFUNZA ATHARI TULIZOKWISHA ZIPATA KWA MIKATABA NA KUFANYA MAMBO KWA 10%, RITES (WAHINDI WA RELI) WAMEKUJA HAPA HATA BILA MTAJI LAKINI WAMEONDOKA NI MABILIONEA. TUMEFANYA MAKOSA KWENYE TANZANITE ONE, LEO IMEKWISHA NINI TUMEPATA???

SASA TUMEAMUA KUUA ELIMU KABISA, HIVI KAMA WATOTO TUNAOSEMA WAMEFAULU HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA, JE HAO WALIOFELI WANAUWEZO GANI>> HUENDA HATA HAWAJUI JINSIA YAO.... INASIKITISHA

TUNAFANYA TENA MAKOSA KAMA HAYOHAYO KWENYE URANIUM, (SELOUS GAME RESERVE-NAMTUMBO) MIKATABA IMESHAINGIWA KINYEMELA, MPAKA WA ENEO LA HIFADHI UMESHASOGEZWA URANIUM ONE TAYARI WAMESHA ANZA KULETA WAFANYAKAZI WAO KWA KILA SEKTA.

SIJUI.... HIYO TAASISI ITAKAYOUNDWA HAITAKUWA NA CHA KUFANYA NI KULA FEDHA ZA KODI YETU, TCRA, AU TACAIDS ZIMESAIDIA NINI???
 
This is too murch.,Kila siku serikali hii rojorojo idara zake zinaposhindwa kufanya kazi zake badala ya kuivunja kwanza au kuifanyia marekebisho mazumbukuku wanaunda idara nyingine juu ya ile ya awali.,Yaani ni kujiongezea ulaji tu kwa wale walio ktk mfumo.
 
Tatizo lenu huwa hamjiamini kwa hoja zenu toka vichwani mwenu(Independently) mnapenda kumezeshwa hoja, nawashangaa sana, Yaani Mnyika kupinga sio lazima na wewe upinge, waweza kujitegemea kuwaza mambo yenye tija katika nchi acha kuburuzwa kijana, jisimamie,tafuta facts kabla hujapost ushabiki.
Presidential Delivery Unit unajua maana yake? unajua umuhimu wake? kama hujui basi uliza Great Thinkers wakusaidie wewe Great Prepitator ili baadae ujue wapi usimame, unless utaburuzwa hata kwa jambo la hovyo!
Wewe ni great thinker au ni great drinker??Kijana mimi nifwatilia sana mijadala inayoendelea, nimesikia pia alichosema Rais wakati ana copy hilo jambo toka Malaysia na nimemsikia vizuri sana wakati Wassira anajiumauma kuelezea ni nini hasa hiyo Bureau itafanya.
Kama ulifwatilia mjadala, kabla Mnyika hajashauri vinginevyo, alitoa wasaa kwa Wassira kuelezea hiyo Bureau itafanya nini.

Naweza nikaielewa tu hoja yako kama wewe ni Mmalaysia, mana Huenda unaufahamu huu mpango from the scratch. Ila kama na wewe ni msoma magazeti hapa nchini na unajifunza toka malaysia huna sifa ya kulitetea hili jambo. Unafahamu sababu zilizowafanya Malaysia kufanikiwa kwa kutumia huo mpango???Kwa taarifa yako tu mafanikio ya Malaysia yametokana na haya mambo: -

  1. Uongozi shupavu na ulio tayari kwa mabadiliko ya kuipeleka nchi mbele.
  2. Kuweka mipango ya kimaendeleo kwa kuzingatia vipaumbele vya kitaifa
  3. Nidhamu katika utendaji na utekelezaji
  4. Uwajibikaji wa serikali na kuwa tayari kukiri madhaifu yake.

Uonavyo wewe sisi hapo tunaweza lipi???? Au unadhan ukishaanza kuiga huo mpango regardless ya haya mauoza yetu tutafanikiwa tu??? Hizo ni ndoto, every model has its assumptions, variables na miiko yake to predict a certain response. Tulitakiwa tujiridhishe kuwa system yetu na ya malaysia zipo sawa ndio tufanye hiyo horizontal shift, wenzetu malaysia walifanya utafiti kuiaccomodate hiyo system kulingana na mazingira ya kwao hawakukurupuka tu tokea kwenye Dinner. Tulichokifanya hapo ni kuchukua ubavu wa Tembo na kuufitisha kwa Swala afy tumekaa pembeni tunasubiria Swala asurvive.

Great Drinker wewe, unachotaka kusema sisi toka tumepata Uhuru miradi yetu ilikuwa haifwatiliwi wala kusimamiwa??? Hicho chombo kitafanya lipi jipya zaid ya usanii??? Kwann basi wasingeanzisha kajikitengo tu ndani ya Tume ya Mipango iliyopo ili kufwatilia hilo kama halifanyiki???? Na tumefikaje hapa kama hayo yalikuwa hayafanyiki??? Tatizo ni kutokutaka kuwajibishana. Wasimamizi wa miradi wanapewa rushwa wanalala mbele.

Msirukierukie mambo na kupinga kila wazo la upinzani, mnatupeleka pabaya. Naimani wewe ni mmoja kati ya magreat drinkers wanaosupport Bilioni moja itengwe kwa ajili ya kuandalia maeneo ya kuzikia viongozi hawa wezi na mafisadi wa kitaifa. Are you really using your brain au mmeshakuwa fifty bricks short of the full load??? Wewe unaweza ukaelezea kunafaida gani ya hilo jina jipya. Kilichokuchanganya wewe ni jina jipya na sio kuwa kuna jipya hapo katika utekelezaji wake. Kama unakumbukumbu nzuri, kwenye sekta ya kilimo tumepitia Abracadabra hizi hizi.

Tulianzaga na kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa, Tukaja kilimo cha kufa na kupona, Tukaja mapinduzi ya Kijani, sasa hiv tupo Kilimo kwanza. Je wewe unaona kunatofauti katika output???Acheni mambo ya ajabu, hiyo ni kauli mbiu tu, nchi hii haisogei kwa vile viongozi wetu tuliowaamini ni wezi, hawana dhamira ya dhati ya kututoa hapa na pia hawataki kuwajibika. Mafanikio hayaletwo na aina ya jina la mpango flani.
 
Presidential delivery unit?
Hapa Chief whip wa gambaz atasema ni tusi, atatafsiri "Kitengo cha kujifungua Rais"
km walivyotafsiri impotent!
 
Wewe ni great thinker au ni great drinker??Kijana mimi nifwatilia sana mijadala inayoendelea, nimesikia pia alichosema Rais wakati ana copy hilo jambo toka Malaysia na nimemsikia vizuri sana wakati Wassira anajiumauma kuelezea ni nini hasa hiyo Bureau itafanya.
Kama ulifwatilia mjadala, kabla Mnyika hajashauri vinginevyo, alitoa wasaa kwa Wassira kuelezea hiyo Bureau itafanya nini.

Naweza nikaielewa tu hoja yako kama wewe ni Mmalaysia, mana Huenda unaufahamu huu mpango from the scratch. Ila kama na wewe ni msoma magazeti hapa nchini na unajifunza toka malaysia huna sifa ya kulitetea hili jambo. Unafahamu sababu zilizowafanya Malaysia kufanikiwa kwa kutumia huo mpango???Kwa taarifa yako tu mafanikio ya Malaysia yametokana na haya mambo: -

  1. Uongozi shupavu na ulio tayari kwa mabadiliko ya kuipeleka nchi mbele.
  2. Kuweka mipango ya kimaendeleo kwa kuzingatia vipaumbele vya kitaifa
  3. Nidhamu katika utendaji na utekelezaji
  4. Uwajibikaji wa serikali na kuwa tayari kukiri madhaifu yake.

Uonavyo wewe sisi hapo tunaweza lipi???? Au unadhan ukishaanza kuiga huo mpango regardless ya haya mauoza yetu tutafanikiwa tu??? Hizo ni ndoto, every model has its assumptions na miiko yake. Tulitakiwa tujiridhisha kuwa system yetu na ya malaysia zipo sawa ndio tufanye hiyo horizontal shift, wenzetu malaysia walifanya utafiti kuiaccomodate hiyo system kulingana na mazingira ya kwao hawakukurupuka tu tokea kwenye Dinner.

Great Drinker wewe, unachotaka kusema sisi toka tumepata Uhuru miradi yetu ilikuwa haifwatiliwi wala kusimamiwa??? Hicho chombo kitafanya lipi jipya zaid ya usanii??? Kwann basi wasingeanzisha kajikitengo tu ndani ya Tume ya Mipango iliyopo ili kufwatilia hilo kama halifanyiki???? Na tumefikaje hapa kama hayo yalikuwa hayafanyiki??? Tatizo ni kutokutaka kuwajibishana. Wasimamizi wa miradi wanapewa rushwa wanalala mbele.

Msirukierukie mambo na kupinga kila wazo la upinzani, mnatupeleka pabaya. Naimani wewe ni mmoja kati ya magreat drinkers wanaosupport Bilioni moja itengwe kwa ajili ya kuandalia maeneo ya kuzikia viongozi hawa wezi na mafisadi wa kitaifa. Are you really using your brain au mmeshakuwa fifty bricks short of the full load??? Wewe unaweza ukaelezea kunafaida gani ya hilo jina jipya. Kilichokuchanganya wewe ni jina jipya na sio kuwa kuna jipya hapo katika utekelezaji wake. Kama unakumbukumbu nzuri, kwenye sekta ya kilimo tumepitia Abracadabra hizi hizi.

Tulianzaga na kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa, Tukaja kilimo cha kufa na kupona, Tukaja mapinduzi ya Kijani, sasa hiv tupo Kilimo kwanza. Je wewe unaona kunatofauti katika output???Acheni mambo ya ajabu, hiyo ni kauli mbiu tu, nchi hii haisogei kwa vile viongozi wetu tuliowaamini ni wezi, hawana dhamira ya dhati ya kututoa hapa na pia hawataki kuwajibika. Mafanikio hayaletwo na aina ya jina la mpango flani.

Kwa kuwa hujui na hujui kama hujui, wewe ni mpumbavu, lakini ungekuwa hujui lakini ukajijua kuwa hujui ukatamani ujulishwe ungekuwa Mjinga ambaye ukieimishwa tu utaelewa.
Ninachokiona kwenye pango la ubongo wako na uboho wa mifupa yako ni kumezeshwa uzinduzi wa kanda maalumu kama sera ya chama chako ibada ya Mtandao wako wa Kigaidi.
Nitajie Majukumu mawili ya Tume ya Mipango na Mipaka yake.
 
Dr F. Ndugulile ----naunga mkono hoja
Anaunga mkono hoja kwa vile yeye ni CCM au kwa vile anaona chombo hicho kinamanufaa kwa wananchi wako wa Kigamboni??? Sisi tunakaa hapa kigamboni tunafukua maji kwa majembe hutadhani hatukatwi kodi. Yeye anakula kipupwe hapo anaitikia tu ndiooooooooooo, hayo ndiyo tuliyomtuma ayatetee??? Kupitisha Bilioni moja kwa ajili ya kutenga eneo la kuzika viongozi wa kitaifa ndio Priority ya Taifa hili???? Shame on you. Hiyo Dr. yake na mambo anayoyafanya inaonekana ni kama Dr. ya Mganga wa jadi, Dr gani cant think independently and stand for the rights of his people.
 
Hoja hujibiwa kwa hoja, hoja haijibiwi kwa matusi, mimi wazazi wangu hawakunifundishwa matusi kama ulivyofundishwa wewe na wazaz wako. Wewe unayejifanya unaujua sana huo mpango as if hiyo model uliidevelop wewe ndo utueleze huo mpango unafaida gani kwa hili taifa.

Wassira ambaye ni Waziri mwenye dhamana alishindwa kuelezea, sasa wewe unayeufahamu zaid uelezee. Mnapoonesha kupanic badala ya kuu spear-head huo mpango wenu ndipo mnapotuthibitishia kuwa kilichowafurahisha ni jina jipya tu, wapo watu wao ni kuchekacheka tu kila Rais anapoongea, wewe ni mmoja wao. Eti Presidential Delivery Unit. Presidential Delivery Unit my foot!
 
Anaunga mkono hoja kwa vile yeye ni CCM au kwa vile anaona chombo hicho kinamanufaa kwa wananchi wako wa Kigamboni??? Sisi tunakaa hapa kigamboni tunafukua maji kwa majembe hutadhani hatukatwi kodi. Yeye anakula kipupwe hapo anaitikia tu ndiooooooooooo, hayo ndiyo tuliyomtuma ayatetee??? Kupitisha Bilioni moja kwa ajili ya kutenga eneo la kuzika viongozi wa kitaifa ndio Priority ya Taifa hili???? Shame on you. Hiyo Dr. yake na mambo anayoyafanya inaonekana ni kama Dr. ya Mganga wa jadi, Dr gani cant think independently and stand for the rights of his people.
Nakushauri tembelea Parliament of Tanzania, kisha tafuta jina langu. Hapo utapata michango yangu Bungeni.
Kwa Hoja yoyote ya maendeleo kwenye Jimbo la Kigamboni nakukaribisha muda wowote kuwasiliana nami. Mmenichagua kuwatumikia na nami nitajitahidi kutimiza wajibu huo.
 
Dr. kwenye zile ndiooooo yako haipo pale??? Kama haipo ule mpango wa kutenga bilioni moja kwa ajili ya wafu wewe unaona ni akili ya kawaida imetumika hapo??? Uliupinga vipi mpango wa kitoto kabisa ule???Kwa faida ya nani mlipitisha zile fedha??? Yaani mnaacha kupitisha fedha ili wananchi walio hai wafaidike, mnatenga fedha kwa ajili ya kuwanufaisha watu hata tusiowajua maana hatujui ni lini nyie viongoz wetu wa kitaifa mtakufa. Hii akili ya ajabu sana.

Unataka kusema Lukuvi akizikwa kwao Isimani hatotulia huko chini??? Mnataka kuongoza taifa hadi mkishakufa???? Yan what was exactly the motive behind that thing, ni kwa faida ya nani hasa???Mnataka kusema sasa kuwa maiti ya kiongozi wa ccm inathamani kubwa sana kuliko wananchi waliohai wanaoishi hilo eneo. Yani waache kuzitumia hekta zote hizo kwa maendeleo yao ili wasubirie Lukuvi afe azikwe hapo.

Sisi watumishi tunaumia sana maana ndio walipa kodi wakubwa nchini. Wafanyabiashara si serikali imeamua wasilipe kodi??? Sasa tutendeeni haki basi mbona hata hicho kidogo kinachopatikana mnakichezea tena????Naumia sana kuona kodi yangu inatumika kwenye kuwatengea eneo la kuwazika. Hivi kaka wewe ukizikwa Kigamboni itakuwaje hasa.

Hivi ni athari gani hasa ingetokea kama hizo 29 bilion zisingeunda hicho chombo mwaka huu, then hizo fedha zote zikasambaza maji Jimboni kwetu???Unataka kusema faida tutayoipata kwa kuanzisha hicho chombo inafar outweigh benefits za sisi wapigakura wenu kupata a basic need kama maji ya kunywa????Hebu vaeni viatu vyetu! Nadhan mnataka kutuambia kuwa hii ni price tunayopaswa kulipa au cost ni cost tunayopaswa kuincur kwa kuchagua kuongozwa badala ya kuongoza. Haina shida!!Ila si busara unapokula na kipofu ukamsika mkono.

Michango yako bungeni itakuwa na maana tu kama ina outputs kwa wananchi wako. Lakin kwa style ile ya kigamboni, kwa kweli ni hata aibu kusema kuwa kiongoz wa eneo lile ni msomi. Nadhan hamtuelezi ukweli ila inaonekana ni ngumu sana kuiongoza hii nchi. Nashauri tufanye one thing at a time ila kwa style hii ya kujifanya vyote twaweza. Itafika miaka 50 mingine tutabak hapa hapa.
 
Dah Mkuu wangu Patriote naomba nitambue kwa upekee michango yako kwenye thread hii....
Ahsante sana, nimekukubali mkuu.
 
Back
Top Bottom