Precision hawana specific rates kama fly540 na coastal aviation? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Precision hawana specific rates kama fly540 na coastal aviation?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MPadmire, Jan 26, 2010.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Wana JF,

  Ukijaribu kuangalia katika mashirika ya ndege, ambayo ni active ni Precision Air, Coastal aviation na fly540. Mashirika yote hayo yana website, kuna flight schedule na booking online.Lakini website ya precision haina bei. Sijui ni kwa nini wanakwepa kuweka bei?

  Coastal Aviation na fly540 wameweka bei. Sasa precision kwa nini wanakwepa kuweka bei?
   
 2. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ingawa sio msemaji wa Precision Air (PW) lakini ninavyofikiri ni hivi;

  Kimsingi PW wanauza safari zao kupitia SITA Reservation System katika ofisi zao na Galileo by TravelPort na Amedeus systems katika ofisi za wakala wao au Travel Agents. Ili uweze kuuza kupitia website yake PW inabidi ifanye "intergration" kati ya website yake na SITA Reservation System ili kuweza kudhibiti booking na mauzo na hiyo inahitaji resources za kutosha. Tofauti na Coastal na Fly540 ambao wao reservation system zao ni web based hivyo hakuna utata na complications sana. Ni swala la muda nao PW wakipata resources watakuwa kama KLM na Emirates kwa kuunganisha website yao na systems zingine walizonazo.
   
 3. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hawana bei maalum kwa sababu, katika flight hiyo hiyo moja labda ya kwenda Arusha, na hakuna Business class, wote class moja, lakini bei tofauti.. Inafuatana ni nani kati yenu alianza kununua tiketi au kufanya booking. kila unavyozidi kuchelewa kufanya booking au kununua tiketi kufikia siku ya flight yako, na nauli inaongezeka.. Kama nimekosea naomba mnisaidie..
   
Loading...