Precision Air wanatia huruma

Precision Air wanatia huruma

Labda wamrudishe Kioko.........huyu mama aliyepo PW imemshinda kabisa. Hata bia aliziondoa inflight kwa sababu ya imani yake!
Alphonse Kioko na Moses aliekua CFO ndio walioua hili shirika, hata suffering ya hili shirika sasa ni matokeo ya mengi waliofanya kipindi Chao. Kwa sasa Moses ni mmoja ya matajiri wakubwa tu Kenya kwa hela walizomuibia Mzee Ngaleku Michael Shirima. Mikataba mingi waliingia ya kifisadi ukiwemo wa ukopeshaji wa hizi ATR Turboprop.

Kimsingi hili shirika lilishindwa kuendana na rapid growth yao likafikia hapa chini ya management yao. Pengine labda aliekua CEO msaidizi Bw. Allan Shara angeweza kua mtu muafaka ila ndio hivyo tena wakenya walitakiwa washike zile top na crucial managerial posts!
 
Acha wewe sasa Precision Air kuchelewa na Fastjet kuondoka kwa wakati kuna uhusiano gani?Hayo ni makampuni mawili tofauti yana changamoto tofauti kabisa.
Halafu nakushangaa unakaa kushadadia Fastjet kama vile ni ya baba ako,Penda vya kwenu ndo maana hatuendelei kazi kushadadia vitu vya watu wakati vya kwetu vinaharibika.We unapanda ndege unalipa nauli sawa na basi unajiona mjanja utalipiwa dogo, ama la iko siku watakwambia ndege imeisha mafuta mkiwa angani nione kama utakuwa na mbawa za kutua mwenyewe.

Precision ni shirika la kizalendo ambalo limekuwa likisapoti uchumi wetu kwa miaka mingi sasa vinakuja vindege vya ajabu ajabu mnakaa kushadadia tuu...

Penda vya kwenu bwana ,cancelation,delays n.k ni vitu vya kawaida kwenye usafiri wa anga kama hujui uliza.

Nawashangaa sana mnaoshangilia fastjet subiri PW waache kuto huduma muone mtafanywa nini.SALI SANA PW ISIFE

Angalau umewapa ukweli. Serikali ilibidi iisaidie kampuni hiyo ya kizalendo ambayo ilibeba bendera ya TZ wakati Atc ikiwa hoi na kabla fastjet haijaja na bei zake za kuizika precision. Subiri imalize kazi ya kuizika precision uone nauli zake zitakavyo paa.
 
hawa PRECISION kiukweli wanatia huruma majuzi nilisafiri nao toka KIA-DAR kupitia ZNZ daah kwanza mkiingia ndege imezimwa (AC hazifanyi kaz) FULL JOTO mpaka saa ya kuondoka ndo PILOT akawasha AC tukapaa siku ya kurudi hivyo hivyo mkiingia ndegeni jotooo mkitua znz kusubiria/kushuka ndege inazimwa. sasa kwenye PROMOTION zao ndo kituko cha mwaka wanadai nauli ni 5,000/= kumbe nauli inafika 150,000 (ONE WAY) wenzao FASTJET 6,600 (Promotion ONE WAY LOCAL FLIGHTS) ukiweka na KODI ni 19200
 
Hahhahahhahahahahah hizi bussiness ngoja tuisubiri community airline maana kama mapacha vile na fastjet
 
KQ wanatuumiza kupita maelezo yaani kwenda tu Nairobi na kurudi kama huna 433 USD (Return) kapande SPIDER BUS urushwe rushwe siku nzima & mubebe bange pale ofisini kwao Mianzini Arusha ( kitu cha Arusha) ndo uione Nairobi na wakati wa kurudi mtasimama vituo vyote kushusha na kubeba miraa (mirungi)

Hiyo nauli inakaribia nauli ya kutoka Dar to Istanbul kwenda na kurudi kwa Turkish airline
 
Presisheni sidhani kama wanajielewa kwa kweli sasa wanadai ya promosheni 195,000/= ONE WAY (Domestic Flights) wakati mpinzani ao fastjet 79,000 (one way) route hizo hizo za babu CHIRIMA
 
Waswahili mkipata chungu kipya cha zamani kinabezwa...hata kama kilifanya mchango wake vya kutosha.

FIESTA VS WASAFI.
Hivi hatuwez kum-"poach" CEO wa Qatar au Emirates akaja kutufanyia kazi hapa nchin kulirudisha ShirikA kwenye anga za kimataifa.
 
Viongozi wa serikari ndio wateja wazuri wa airplane wote ni air tz lazima wachoke
 
Back
Top Bottom