Precision Air wanatia huruma

Precision Air wanatia huruma

and 998 others

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Posts
28,512
Reaction score
40,350
Aisee kama wewe ni msafiri kati ya JNIA (Dar) na ama Kilimanjaro (KIA) au Mwanza (Kwa Mbeya PW ameshachemsha na haendi tena).

Utakuwa ume-note jinsi hawa Precision (PW) wanavyopelekwa mputa mputa na Fastjet yaani kuna wakati inabidi safari ya saa 1 asubuhi abiria wahamishiwa ndege ya jioni.

Kiukweli mimi kama si safari ya kulipiwa na ofisi (serikalini) chaguo langu ni Fastjet kwanza wako on-time (Kuondoka na kufika) kwa wakati tofauti na PW.

Fastjet pelekeni ndege Nairobi & Entebe muwamalize PW & KQ wanatulangua sana.
 
TUPA KULE PRECISION na nauli za US Dollar (USD) Huku serikali inakataza kufanya payment kwa dola wenyewe (kwenye website) eti ukibook ni kwa dola yet unatakiwa kulipia tiketi kwa Voda M-PESA. Crazy?????

Halafu hii ya USD wameiweka mwezi wa tano mwishoni au wa sita mwanzoni. Maana mwezi wa tano katikati nilinunua tiketi online ya kwenda Zanzibar ilikuwa kwa shilingi wenzangu wakataka kusafiri baadaye kuingia online tunakutana na bei za USD kwa local flights niliishiwa nguvu.
 
Yaani Precision wanaeleka shimoni pamoja na kuwa bailed out na KQ bado wana shughuli pevu mbele ya FASTJET labda Precision waanzishe route kwenye mikoa ambayo wana viwanja vidogo vya ndege (SUMBAWANGA, TABORA, KIGOMA, BUKOBA, LINDI etc.) ambapo AIRBUS za FASTJET haziwezi kutua. Vinginevyo PW waanzishe kampuni ya Mabasi DAR-MORO.
 
Yaani PW ni kama mtoto yatima sasa wanaonekana kama vile wamefiwa na wazazi wao. Nilikuwa nakwenda mbeya duuh! nikaambiwa eti PW & ATC hawaendi tena. kuchek fastjet wanaenda asubuhi na jioni.

Tena unaweza ku-book online na kulipa kwa m-pesa au tigo pesa ile unamalizia kulipia tayari washakutumia tiketi (in PDF) kwenye e-mail yako. yaani hata huitaji kupambana na foleni kwenda kulipia tiketi ofisini kwao kama ilivyo kwa ATC. Asante sana Fastjet mmerahisisha maisha sana kwa wafanyakazi/wafanyabiashara ambao muda ni mali.
 
nimeuza hisa zangu za precision tangu mwaka juzi mpaka leo ninaambiwa no customer na hisa zipo nyingi sokon
 
Hahahaaaa siwapendi kama nini. Kuna siku nilitoka Zanzibar to Dar nikalipa nauli 83,000/= Baada ya kufika uwanjani pale nikapigwa 11, 000/= ya mapato. Nilikasirika sana dada wa mapato akaniambia siku nyingine usipande tena Precision maana ndo tabia zao.
 
Kwanza wahudumu wana maringo sana huko PW ni bora kusafiri na ngorika kuliko kupanda PW ndege kama basi
 
Boing ndo basi tena mtabakia na hivyo vi ATR vyenu nyambafu zenu. Siwapendi hawa na kwa taarifa tuu wadada muwe wakali na mabwana zenu maana hao crew wanagawa namba kama pipi kiufupi wanajitongozesha.
 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1407190459.062933.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1407190459.062933.jpg
    96.5 KB · Views: 910
Yaani Precision wanaeleka shimoni pamoja na kuwa bailed out na KQ bado wana shughuli pevu mbele ya FASTJET labda Precision waanzishe route kwenye mikoa ambayo wana viwanja vidogo vya ndege (SUMBAWANGA, TABORA, KIGOMA, BUKOBA, LINDI etc.) ambapo AIRBUS za FASTJET haziwezi kutua. Vinginevyo PW waanzishe kampuni ya Mabasi DAR-MORO.

Mpaka wataanzisha safari za wilayani! Wapeleke Ndege MASWA, MEATU, Kasulu, Kibondo n.k kwingine majamaa hayachelewi kuwafuata!! Au vinginevyo washushe bei!!!
 
"Msiache mbachao kwa mswala upitao"

Hata hivyo ni vyema kuwe na ushindani wa kibiashara kwa namna hii ili kuboresa huduma kwa watumiaji...

Ilipaswa yawepo tena mshirika mengine kama mawili zaidi ili kuwe na uchaguzi mbalimbali kwa wasafiri...
 
Back
Top Bottom