Basi kama uko Duniani nadhan sio Tz. Hivi NSSF ni nini bila watendaji, watendaji ambao ndo wenye dhamana ya kuzisimamia hizo uziitazo sheria zako pendwa? Hamna kutenganisha hivyo vitu kaka. Kwa taarifa yako hii mifuko ingekuwa ni hiari kujiunga mgeishia kujiunga nyie wafanyakazi wa huo mfuko tu!
Niko Tanzania huku nanjilinji naandaa miche ya korosho....napanga kupanda hekari mia mwaka huu .
Katika hii mifuko yote kuna mchango wa lazima ukiwa mwajiriwa na kuna mchango wa hiyari kama akiba yako ya baadae hapa unaweza kuwa mwajiriwa au mkulima kama Mimi ambapo kiwango cha mchango najiamulia kulingana na kipato cha wakati husika.
Sasa unapolaumu mfuko wa jamii mheshimiwa poyoyo mkubwa, umewahi jiuliza how helpful your government is to you by making sure that kuna sheria ya lazima inayomtaka mwajiri wako akuchangie kuanzia asilimia kumi ya mshahara ghafi wako na wewe ukajichagia inayobakia kisha wakakutunzia kwa kipindi chote cha ajira yako uje upewe wakati umepungukiwa nguvu kama Mimi Bibi yako huku nanjilinji?
Unaachiwa asilimia 90 ya kipato chako cha mwezi, kiwango ambacho kiukweli umeshindwa kujitunzia kisha unakuja kuilalamikia hiyo serikali yako.
Hivi ukiambiwa ujitunzie mwenyewe hiyo asilimia kumi utaweza kweli?
Baada ya miaka mitano hadi thelathini ya kukaa kwenye ajira pesa pekee unayoitegemea ni hii unayoilalamikia hapa kwanini unakatwa kwa lazima....tafakari sana.
Ukipewa Uhuru huwezi itunza hiyo asilimia kumi hakika, wacha iendelee kuwa lazima kukatwa itakufaa nyakati kama hizi nilizonazo Mimi Bibi yako nimezeeka nakula hivi vijisenti sasa
Na hii sheria Sisi wazee tulipendekeza kuwa inatufaa maana zile hela ninyi vijana wetu mnatusaidia kutumia tunaishiwa muda mfupi kisha malipo ya mwezi madogo sasa Bora tupewe kiasi Tu maana tukiwa kazini hatukulipwa mihela mingi na tuliweza ishi vizuri Sana au kwa tabu Sana ila tuliishi, sasa Bora kibaki kikubwa tulipwe parefu kwa mwezi tusione gap na tusijeujutia uzee wetu.
Tunajuwa ninyi vijana wetu mna majukumu mengi hamtoweza kutusapoti mahitaji yetu yote uzeeni tutawashosha.
Sisi wazee tuliipendekeza sheria ibadilishwe na tumefurahi sana.
Na nyie muwe mnahudhuria vikao vya hii mifuko mtoe mapendekezo yenu.