Bahati mbaya sana first born wake ni mwanamke sijui itakuwaje!
Lakini yote tisa Korea Kaskazini haifahamiki kirahisi na sisi watazamaji wa nje!
Wachunguzi wengi walihisi kwamba uongozi wa nchi angepewa Kim Jong-Chul kaka yake na Kim Jong-Un lakini 2009 akatangazwa Kim Jong-Un kama mrithi. (The Country is full of surprises)
Japo kuna mlengo ambao unawaza kama wewe.
Wanasema kwamba Kim Jong-Un akiondoka basi kutakuwa na ombwe kubwa sana la kiuongozi (Power Vacuum) ambayo itasababisha makundi madogo madogo kupigania madaraka na mwishowe nchi yote itasambaratika.
RAND CORPORATION hadi walifanyia utafiti hili jambo na
Dr. Bruce W. Bennet akaliandika chapisho la zaidi ya kurasa 300 hivi.
(Nimeliambatanisha hapa chini)
Ni maoni mazuri lakini ili kuelewa hali ya kisiasa ya Korea Kaskazini ni lazima tuangalie historia yake kwa jicho la tatu kabisa.
Professor Noam Chomsky anasema kwamba Korea Kaskazini iko tofauti kisiasa na Iraq, Libya na Afghanistan; Marekani atakuwa anakosea sana kama anahisi Korea Kaskazini itaanguka baada ya Kim Jong-Un kuondoka. Mfano mzuri kabisa Korea Kaskazini ilikumbwa na Baa la njaa mwaka 1994-1998 na mamilioni ya watu walikufa sana na kibaya zaidi nchi ilikuwa na vikwazo vikali lakini Serikali ya Kim haikuyumba. NATO, Korea Kusini na Japani walitegemea ule ndiyo ungekuwa mwisho lakini hakuna kitu. (Jamaa wanadunda mpaka leo)
KTanzania baada ya vita ya Kagera njaa ilifanya wakiana Zacharia Hanspope wamfurumushe Mzee Nyerere: Kibaya zaidi Nyerere akafa na nchi yote haina mwelekeo mpaka leo.
POLITICAL TEXTURE za nchi ziko tofauti sana kwa hiyo kutaka kutabiri yatakayotokea Korea Kaskazini kwa kulinganisha maanguko ya
Saddam Hussein,
Slobadan Milosevic na
Muhammar Qaddafi ni mawazo ya mwenda wazimu (
FALSE HYPOTHESIS kutengeneza
FALSE INFERENCE)
NB 1: Baada ya Vita ya Kwanza ya dunia viongozi kama
Lloyd George,
Georg Clemenceau na
Vitario Orlando walihisi kwamba wakimuua
Vladmir Illyich Ulyanov Lenin ndiyo utakuwa mwisho wa Urusi ya Kisovyeti (Walisema kwamba bila Lenin wakomunisti hawana kichwa na yeye ndiyo kila kitu pale).
Lenin alipigwa Risasi na hicho ndicho kikawa chanzo cha kuwaunganisha zaidi Wakomunisti nchini humo, bahati mbaya akafa mwaka
1924 kwa Kisukari na Majeraha ya Risasi yasiyopona lakini Urusi ya Kisovyeti na Kikomunisti kama ilivyo Korea Kaskazini ikadumu hadi mwaka 1991.
NB 2:Wakorea Kaskazini wanaweza kumtoa
Kim Jong-Un hata leo lakini ukweli ambao haufichiki ni kwamba hata kiongozi ambaye atakuja baada ya Kim Jong-Un atakuwa na kitu kimoja kinacholingana na familia ya Kim (
Chuki dhidi ya Wamarekani na Mataifa ya Magharibi). Wakorea wanakumbuka vizuri sana ambacho Marekani aliwafanyia mwaka
1953-1953 (
Unnecessary Use of lethal force to target civilian objectives Contrary to the Geneva Conventions of 1949 and Hague Rules of 1907) Hata aingie nani Madarakani Marekani uadui hauwezi kuisha. Professor John Mearsheimer anasema hivi "Katika sehemu zote za dunia, historia huwa haifi kwenye nchi za Mashariki ya Mbali" kifupi huwa hawasahau maadui zao.
CC:
Bukyanagandi ,
Red Giant ,
izzo ,
MSEZA MKULU,
Consigliere,
herikipaji ,
Complex ,
mtembea kwa miguu ,
Gide MK ,
gwijimimi ,
Dotworld ,
py thon ,
Bilionea Asigwa,
Econometrician ,
kilwakivinje ,
Mbimbinho ,
God Heals,
kichakaa man,
Lelommassy