Watanzania tuna tabia ya mazowea na kuona muhali. Na tabia hizo zinakwamisha maendeleo
Nchi inatoa tenda kwa mkandarasi, tunajengewa daraja au barabara iliyo chini ya viwango au yenye dosari ndogo ndogo kadhaa, lakini tunaona muhali kumlazimisha mkandarasi kurekebisha kwanza.
Tabia hiyo imeanzia chini kwa raia mmoja mmoja, kamwe hatujazowea kudai marekebisho au kukataa huduma isiyofikia viwango. Si migahawani, madukani, wala maofisini
Hakuna maendeleo kama hatutaweka nadhari kwenye details. Mambo madogo madogo huzaa makubwa
Zakumi,
Mkuu wangu mbona majibu unayo.. Ikiwa tumepoteza DIRA, hiyo result oriented itatoka wapi?.. au ndio ulitaka kusema hivyo.
Watasema wewe si mpole, sifa kuu ya utanzania.Tabia hiyo imeanzia chini kwa raia mmoja mmoja, kamwe hatujazowea kudai marekebisho au kukataa huduma isiyofikia viwango. Si migahawani, madukani, wala maofisini
Watasema wewe si mpole, sifa kuu ya utanzania.
Ukiuliza haki yako bongo utaitwa mkorofi.
Hata humu ndani same thing, watu wanataka uwe mpole.
Nilipotembelea bongo nilikasirika karibia kila ofisi ya huduma niliyotembelea, na kama humjui mtu pahali ndo mbaya zaidi, labda uwe na pesa ya kuhonga, hayo ni maisha ya kawaida ya mbongo.
AshaDii,Zakumi nionavo mimi ni kuwa kuna tatizo kubwa sana katika jamii ya wananchi wa Tanzania; achilia mbali matatizo ya uongozi. Wananchi tumekua na kasumba ya kuamini kua Maendeleo ya nchi hii yetu changa yataletwa na Uongozi wa Inchi, kwamba raisi akiwa na qualities zote za Uzalendo baaas!
Tunasahau kua Yule kiongozi ana delegate tu, tukisahau kua kila mwananchi ana nafasi yake katika kutaka boresha maisha na maendeleo ya inchini kwake, tukisahau kua ni mwananchi wa kawaida kabisa anae changia kuporomoka na kurudi nyuma kwa maendeleo ya wananchi.
Ma Boss wa taasisi mbali mbali za serkali, Wakubwa wa Mali za Umma, na Viongozi hadi wa chini kwa kiwango kikubwa wanafanya kazi chini ya maadili….
Kila mmoja ni mbinafsi, Kila mmoja hana uzalendo na wala hana Uchungu na mali ile ambayo anasimamia…. Kukomboka kwa inchi.
Na the Irony ni kua hao hao wanachi wanaofanya kazi kinyume cha maadili na kujilimbikizia pesa ambazo sio zao wanazipata kwa Magendo wapo so MAD at leaders such as akina BWM na EL.
Mwalimu katika hotuba yake (Ilikua Mbeya if not mistaken) alim quote Marehemu Rais wa Marekani J. F. Kennedy…. "Usiulize Inchi yako itakufanyia nini, Jiulize wewe Utaifanyia nini Inchi yako". (This quote is applicable to the issue umewakilisha hapa)
Hatuwezi kuondokana na umaskini kama hatujui kujieleza. Kama hatujui kujieleza hatuwezi kupata tunachotaka. Hili linaanzia kwenye mtu mmoja mmoja na hatimae serikalini.
Angalia hapa JamiiForums panapoitwa Home of Great Thinkers kwa mfano, watu hatujui kujieleza na kinachoshangaza zaidi si kuwa mtu hawezi kujieleza tu, lakini hata kuandika Kiswahili hajui na haoni tabu kuwa hajui. Lakini mtu huyo huyo anaona aibu akichapia neno la Kiingereza
Tumeona mifano mingi ya viongozi au wanajamii wakihojiwa kwa Kiswahili na kudumbukiza maneno ya Kiingereza na bila ya aibu kumuomba mtangazaji awa tafsirie kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili lakini hawa hawa hawawezi kamwe kuomba watafsiriwe neno la Kiswahili kwenda kwenye Kiingreza wanapohojiwa kwa Kiingereza.
Maendeleo hayaji bila ya kujikomboa ki-fikra na hajaji bila ya sisi kuweza kuwasiliana vizuri na kuweza kujieleza
Siku zinavozidi kuenda ndio tanavozidi jichanganya na dunia katika mambo mbali mbali…. Na kutumika kwa lugha ngeni is un avoidable Period! For instance…. Kimsingi hapa as a Home of Great thinkers yenye members mbali mbali toka walo verified members, Politicians, Scholars, wanaharakati na the like…. ni mahala ambapo kama Forum kubwa hapa inchini ikiwa na watu wa kila aina na hasa wasomi; things like alternative use of the Language is unavoidable….....
Tunasahau kua Yule kiongozi ana delegate tu, tukisahau kua kila mwananchi ana nafasi yake katika kutaka boresha maisha na maendeleo ya inchini kwake, tukisahau kua ni mwananchi wa kawaida kabisa anae changia kuporomoka na kurudi nyuma kwa maendeleo ya wananchi.
Ndo maana kuna bonuses base on performances etcJMushi,
Wakati serikali imetwaa mashamba ya mkonge kutoka kwa watu binafsi, ilifuata utaratibu wa manamba ambao mtu alikuwa analipwa kutokana na performance yake kazi.
Na badala yake watu wakawa wanalipwa kutokana na masaa ya kazi. Matokeo yake hata wale wafanya kazi mahodari wakawa wavivu.
Na sasa hivi watanzania wengi wamezoea kufanya kazi kwa masaa manane na kurudi nyumbani. Labda tuanze kujenga utamaduni wa kufanya kazi kwa perfomance.
Hapa tunarudi kule kule kwenye sisi Watanzania kukosa umakini kwenye vitu vidogo vidogo na hivyo kushindwa kwenye mambo makubwa yanayoundwa na madogo.
Hakuna tatizo kwa watu kutumia lugha mbadala wakati wa kujieleza, au hata kuchanganya lugha kwa kuazima maneno ya lugha ya kigeni wakati wa kuzungumza Kiswahili. Kinachogomba hapa ni ile watu hususan Great Thinkers au ‘wasomi' kutoweza kuandika Kiswahili cha msingi tu lakini kuweza kuandika lugha ya kigeni, na kuona hilo ni jambo la kawaida.
Suala la wananchi hususan ‘wasomi' kushindwa kuandika Kiswahili si suala dogo, na linaturudisha kwenye mtaala wa elimu yetu na ile tabia Zakumi aloitaja ya kujilemaza kwa kusingizia necha [nature]; ati kwa vile wewe ni Mtanzania basi unajua Kiswahili na hutakiwi kujifunza zaidi. Tupo radhi kujua kuyaandika maneno mazito ya lugha ya kigeni lakini hatujui kuandika maneno yanayotumika kila siku katika lugha ya Kiswahili
Tunatabia ya kuridhika mno na tulivyo, tukipatacho, na tuhudumiwavyo. Na hii si sifa ya wataka maendeleo
In other words una maana kua Viongozi na Watanzania walo wengi wanashindwa kuwajibika ama kua wazalendo sababu ya kuelewa vizuri lugha ya Kiswahili? Gaijin are you serious?
Well nakubaliana na wewe kua ndio wapo wasomi ambao hawawezi kuandika Kiswahili cha msingi na kuweza kuandika lugha ya kigeni; thou bado sijaona kama ndio ipo responsible kwa wao kushindwa fanya kazi zao kwa umakini.
Nitolee mfano mdogo hapa chini ni wazi hata wewe ambae wapenda ujitahidi sana kuandika katika lugha moja kuna wakati wajikuta umechanganya na lugha ngeni. Kama solution nikuliandika hilo neno lisomeke Kiswahili hali ni lugha ngeni swala lipo pale pale.
Nisome vizuri na unielewe, hakuna hata sehemu moja niliyosema kuwa viongozi wanashindwa kuwa wazalendo au kuwajibika kwa sababu hawaelewi lugha ya Kiswahili. Sijui hata umefikiaje hitimisho hilo kutoka kwenye maandiko yangu.
Sijui hili la kudhani Gaijin anasema mtu kutokuelewa Kiswahili sanifu kunamfanya ashindwe kufanya kazi yake kwa umakini linatokea wapi. Mada husika hapa ni namna ya kuondoa umaskini na kuleta maendeleo Tanzania na sio uzalendo au hata viongozi.
Mimi nimeamua kuangalia tatizo kwenye ngazi ya chini. Kuwa Watanzania [sijazungumzia viongozi pekee] tuna tatizo la kutokujua kujieleza na hilo ni moja ya vinavyotukwamisha kupata maendeleo, kwa sababu usipojua kujieleza huwezi kupatiwa huduma stahiki unayoihitaji. Pia usipojua kujieleza huwezi kuwapatia wengine huduma stahiki na badala yake unaweza hata kuwapotosha na kupelekea kuibuka kwa matatizo mengine.
Wataalamu na wasomi wetu wanaposhindwa kujieleza kwa kutumia Kiswahili, inamaanisha kuwa wanashindwa kuwahudumia wananchi wanaowategemea.
Pili tuelewane pia kuwa mimi Gaijin si kipimo cha chochote kwenye jamvi hili, wala si wewe wala mwengine mwenye kujua kuwa Gaijin anajitahidi sana kuandika kwa lugha moja tu. Huwezi kujua kama anajitahidi tu seuze anajitahidi sana. Huwezi kujua chochote kuhusu uwepo au kutokuwepo kwa jitihada wakati Gaijin anapoandika hapa jamvini
Mbali ya hayo, mfano ulioutumia wa kumkosoa Gaijin si sahihi kwa sababu yeye alieleza kuwa ananukuu maneno ya Zakumi .
Tukitaka maendeleo kama taifa lazima tujenge jamii ambayo ipo tayari kukubali makosa na kujirekebisha ili tusonge mbele.
Gaijin what I post I mean, hivo nakua nimekusoama na nimekuelewa.....
Hapo sasa na mimi ndipo niikua nimekushangaa na kushindwa kukuelewa .
Pili tuelewane pia kuwa mimi Gaijin si kipimo cha chochote kwenye jamvi hili, wala si wewe wala mwengine mwenye kujua kuwa Gaijin anajitahidi sana kuandika kwa lugha moja tu. Huwezi kujua kama anajitahidi tu seuze anajitahidi sana. Huwezi kujua chochote kuhusu uwepo au kutokuwepo kwa jitihada wakati Gaijin anapoandika hapa jamvini
Ofcourse Gaijin wewe sio kipimo cha vitu vyote Na hakuna alo kipimo cha vitu vyoote mbona yaweza kua kero ikiwa hivo.
Kuhusu jitihada za Gaijin nje ya jamvi I am not interested....
Hivi unaweza nipa mfano wa Kiongozi ambae anashindwa kufanya kazi yake kwa Ufanisi sababu tu hawezi kujieleza kwa Kiswahili?
Matatizo yale yale ya Mtanzania. Hueleweki! Umenisoma na kunielewa au umeshindwa kunielewa?!.
Ashadii Ama hukunisoma na kuelewa au hujui tofauti baina ya "vitu vyote" na "chochote"
Hakuna anaezungumzia jitihada za Gaijin nje ya jamvi. Kwa ufupi nilichokieleza ni kwamba huwezi kujua kama Gaijin anachukua jitihada sana au kidogo, au haweki jitihada hata chembe anapoandika kwa kutumia lugha moja. Hakuna mwanachama humu Jamiiforums anaeweza kujua jitihada ya mwanachama mwengine wakati wa kuandika hapa jamvini. Tuache kuwatolea hukumu na mahitimisho wanachama tusiowajua.
Sijui kwako wewe kiongozi ni nani, lakini kwangu daktari, mwalimu, bwana/bibi shamba, fundi mchundo wote hao ni sehemu ya viongozi kwenye jamii.
Daktari asipoweza kujieleza kwa lugha ambayo mgonjwa anaweza kumuelewa inaweza kupelekea kupotea kwa maisha.