TBC muda huu Kuna mahojiano,
Mh Ndugai Kaulizwa swali kuhusu kupunguziwa posho zao kashindwa kutoa jibu na msimamo wake
Na Mh. Hamad Rashid wa CUF yeye kasema posho analipwa 150,000 analala hotel shiling 80,000 Anamlipa dereva wake sh 30,000/= na kula elf 40,000/= na kumaliza kwa kusema kuwa haoni kama kuna hela inabaki hapo,
Swali langu ni, Hivi dereva wa mmbunge analipwa na Mbunge??,
Hivi wabunge wanalipwa shilingi ngapi kama posho??, coz hiyo figa nanikumbuka na ni ya kitambo, nikosoeni kama nimekosea, nielimisheni inapowezekana!
Hela yake ya chakula ni kubwa kuliko hela ya matumizi yote ya binadamu mwenzie hii inaonyesha tumbo lake ni muhimu kuliko maisha bora kwa mtu aliyeshikilia uhai wake!Kweli kabisa,anakula elf40 anaona ni poa kabisa,wanafunzi wanasema elf5 haitoshi wabunge
wana washangaa,....wapuuzi kabisa!===Tunaitaga ujinga wa nyani kuona nini... ya mwenzie!!!
Devera analipwa elf30 kwa siku kweli?=== Ndo hivo jamaa kasema sasa
so dereva anakula nini?=====hakufafanua!
ana lala wapi kwa hiyo hiyo elf30 kwa siku? -------Labda atalala kwenye Gari
Kweli,PATA HELA TUJUE TABIA YAKO!!!!!
Na Mh. Hamad Rashid wa CUF yeye kasema posho analipwa 150,000 analala hotel shiling 80,000 Anamlipa dereva wake sh 30,000/= na kula elf 40,000/= na kumaliza kwa kusema kuwa haoni kama kuna hela inabaki hapo,
Jameni, mbona Mh. Hamad hakutoa mchanganuo wa dereva wake? Posho anayomlipa ni ndogo kulinganisha na pesa anayotumia kwa chakula tu. Yeye anatumia ngapi kwenye kulala, kula na kuitumia familia yake huko kwao? Nadhani viongoz wetu wanadhan wao ndo wana haki ya kupata hivyo wanavyopata.
Hata hivyo, upinzani umetoa mawazo yao tu. Kama wangekuwa wao wanaandaa bajeti kwa ajili ya watanzania wangewafanyia nini. Sasa kuanza kuona mjadala ya kupinga mawazo yao na mapendekezo mimi nashangaa kabisa. Kwa kweli mimi sioni hata maana ya wabunge kulipwa mishahara, kwangu mimi ubunge sio fani ya mtu kujivunia hadi kustahili kupata mshahara. Ndo mana rushwa kwenye uchaguzi zinazidi kuongezeka kwani watu hufuata maslahi badala ya kuwaletea maendeleo wananchi.
Its good because we now begin to know true colours of our leaders. Hawako tayari kupunguziwa maslahi yao kwa ajili ya kuwaletea wananchi ustawi ambao walijinadi kuwa wataupigania. Kiama chao kinakuja kwani 2015 sio mbali kama wanavyodhani.
2015 tutashuhudia vihoja na Mahoka ya wanasiasa wetu, mungu niweke hai nisikose vimbwanga!
siku tukipata wabunge wa CCM ambao wapo kwa ajili ya wananchi hoja kama hizi hawatozipuuza, lakini wale wapo kwa ajili ya mitumbo yao ndio maana utayaona hayo. Katika Hili mimi ningeomba media zote zitangaze hoja moja tu ya Posho kuondolewa na hoja ya chiligati abakie nayo mwenyewe na ndugai wake, naamini ikitangazwa kama vile alivotangazwa Babu wa loliondo mpaka wagonjwa wakakimbia mahospitali na kwenda kufia kule loliondo basi tutafanikiwa. Kwa vile jamaa wamejifanya vichwa ngumu ktk hili basi wabunge wa upinzani wote msirudi nyuma litekelezeni hili kwa vitendo halafu media zote ziitangaze sana tena sana kwa wananchi juu ya kinachofanywa na wabunge wa ccm ambao watang'ang'ania kuchukua posho hiyo na wawe wanatajwa majina uone kama hawaachii wenyewe, nakwambia wataanza kusutana kwahili na watakuwa wamejitengenezea picha mbovu sana kwa wapiga kura wao.
Media zimenunuliwa ndugu, na ukitangaza sana utapigwa kitu cha BAN
Hatuzungumzia posho ya kuwa nje ya kituo cha kazi (perdiem), tunazungumzia posho ya vikao, hapo kuna double payment, amelipwa kwenda dodoma kuhudhuria kikao cha bunge na amelipwa kwa kukaa mjengoni, wapinzani wanachotaka iondolewa ya kukaa mjengoni maana tayari washalipwa hela ya kuhudhuria vikao vya bunge.Ila katika hali ya kawaida, inawezekana kweli kwa mbunge au mfanyakazi yeyote wa serikali au wa makampuni binafsi kutoka nje ya kituo chake cha kazi for official duties bila ya kulipwa posho??? Kuwa muwazi weka siasa kando
ANAKULA 40,000/= KWA SIKU DU??HUYU MUISLAM NI SOO,HII SI NI BEI YA MBUZI MKUBWA BEBERU NA KRET MBILI ZA KILIMANJARO,NA MAJI KATON MOJA KWELI JAMAA YUKO JUU
ANAMPA DEREVA WAKE 30,000/= PER DAY MAANA YAKE JAMAA ANATENGENEZA
30,000 X 30=900,000/=
SASA BUNGE HILI N LA MIEZI MITATU
900,000 X 3=2,700,000/=
MSHAHARA WA DEREVA SH 900,000/= KWA MWEZI HAIWEZEKANI
SI KWELI HUYU MPEMBA ANADANGANYA UMMA
mnafki tuu hana lolote
Hatuzungumzia posho ya kuwa nje ya kituo cha kazi (perdiem), tunazungumzia posho ya vikao, hapo kuna double payment, amelipwa kwenda dodoma kuhudhuria kikao cha bunge na amelipwa kwa kukaa mjengoni, wapinzani wanachotaka iondolewa ya kukaa mjengoni maana tayari washalipwa hela ya kuhudhuria vikao vya bunge.
Fedha za Serikali hutawaliwa kwa mujibu wa Kanuni za fedha za Serikali.Kanuni hizo huelekeza stahili ya kila mtumishi anapokuwa nje ya kituo chake cha kazi. Stahili ya watumishi wenye hadhi ya mbunge hivi sasa ni Shs 80,000/= tu kwa usiku mmoja anapokuwa nje ya kituo chake cha kazi.
Katika kanuni za fedha za Serikali hakuna kitu kama posho ya vikao kwa watu ambao waliomba wenyewe kazi ambazo hufanyika maofisini ambapo niia mojawapo ya kutimiza wajibu wao ni kuhudhuria na kushiriki katika vikao k.m vikao vya bunge. Ikumbukwe kuwa wasomi huomba kazi za kutumia akili ambazo nyingi hufanyika maofisini kupitia vikao, mikutano, semina, warsha, kongamano n.k ndio maana husalimika na shuruba za kilimo, kazi ngumu kama vibarua n.k. Iweje wasomi hao leo wageuke na kudai kulipw posho kwa kazi ambazo wanalipwa mishahara na ambazo kwa vigezo vyote ni nyepesi na hufanyika katika amzingira mazuri kuliko kazi wafanyazo wananchi wa kawaida?
Kanuni za Ajira na Fedha za Serikali hutaja aina ya watumishi ambao wanastahili kupata wasaidizi kama vile makatibu wahutasi (Secretaries) madereva n.k. Kwa mujibu wa majibu ya kifisadi ya Mhe Hamda Rashid inaonyesha kuwa Kanuni za Ajira na Fedha za Serikali haziwatambui wabunge kuwa hadhi ya kupatiwa madereva, kama zingekuwa zinatambua hilo madereva wa wabunge wangeajiriwa na Serikali (ofisi ya bunge), na kulipwa mishahara na posho na Serikali kama madereva wa wengine wa Serikali. Toka lini ukasikia Waziri au Katibu Mkuu au Mkurugenzi wa Wizara anagawana Posho yake safari na dereva wake?.
Kinachojitokeza hapa ni kuwa wabunge wetu wanajikweza sana pasipo kutazama umasikini wa wapiga kura wao ndio maana wanakuwa na mahitaji makubwa ya kuhitaji dereva n.k. Ofisi ya bunge inamiliki idadi kubwa ya mabasi kwa ajili ya kuwasafirisha wabunge kwenda na kutoka katika vikao vya bunge kutokea ofisi za bunge; ambapoi kutokea hapo wabunge wanatakiwa kutumia usafiri wa umma kama vile treni, mabasi n.k ili kujua hali halisi ya usafiri wanaotumia wananchi.
Ni kwanini kila mbunge apige gari moto kuelekea Dodoma? kama sio ufujaji wa fedha za walipa kodi. Ndio maana wabunge wanajiingiza katika ufisadi wa posho mbili mbili ili kumudu maisha haya ya anasa.
Ndio maana wabunge waroho kama Mhe Hamad Rashid na wenzake wote wanaotetea utaratibu huu wa kifisadi wanalazimika kutetea wizi wa fedha za serikali kwa njia ya posho za vikao ili kufidia masiha ya anasa ya wabunge wetu.
Hapo kwenye red hakikisheni mnapeleka wakristo kwa wingi unguja na pemba ili 2015 wasirudi hawa maana ni hatari sana.
Sasa kama wameshapewa per diem zao ni busara kwa wapiga kelele kwenye majukwaa wakaandika barua ya kusudio la kuondolewa hizo posho bila ya hivyo itakuwa ni unafiki tu.
Pale walimdunga swali, infact nilichoona hakulipenda swali na kusema tunasubiri walete hoja bungeni!Mbona Ndugai kakurupuka, ameongea kama mbunge au kama naibu spiker. Maana kama naibu spiker hawezi kuanza kuponda hoja ya mbunge kwa kuwa ni haki ya mbunge kupeleka hoja binafsi,na yeye kama naibu spiker hatakiwi kuelemea upande wowote.
Mkuu Shossi huyo jamaa aliyeingiza udini msamehe bure tu, sie tuzungumzie je ni haki hawa watu kupata posho mbili kwa kazi moja?Hapo kwenye red hakikisheni mnapeleka wakristo kwa wingi unguja na pemba ili 2015 wasirudi hawa maana ni hatari sana.
una analyse kwa kutumia makalioWakuu natanguliza samahani kwa nitakayemkwaza lakini ukweli katika hili siwaelewi viongozi wa vyama vya upinzani including CHADEMA kama wako serious! Hivi wanashindwa nini kususia posho hizo za wabunge??? Je kisingizio ni kwa sababu wakiacha CCM wanachukua?? If yes, Je inaleta mantiki yoyote?? Kama CCM wanaziiba, (na of course ndivyo ilivyo) je wao wanaona wakiziacha watakuwa wamewasusia CCM na hivyo bora na wao waziibe??? Jamani, hili linanikoseha raha na kunipa wasiwasi kama kweli dhamira yetu ya kuikomboa nchi hii inadhihirshwa hasa na tunachokisema na kukikariri kila siku.
Najua CCM hawataruhusu kuziondoa hizo posho ambazo sisi tunaamini kuwa ni kuwaibia wananchi wanyonge wa nchi hii!! Sasa je, kwa sababu CCM watakataa basi na wabunge wa CHADEMA wazichukue!!! Gosh!! Why? Hoping that two blacks will eventually make white??? TUACHE UZEMBE!!! NA TUMAANISHE KWA DHATI TUNAPOSEMA TUNA DHAMIRA YA KUMKOMBOA MWANANCHI ALIYEKATA TAMAA KUTOKANA NA UONEVU WA SERIKALI YA KIKWETE!!!! Viongozi wetu tunaomba mtutoe mashaka na kulifanunua hili!
Naanguliza shukurani kwa viongozi watakaochukua hatua kulifafanua kwa makini suala hili!
Post ya huyo jamaa haijatulia na wala sijaipenda kuingiza udini ila sometimes unaweza kuignore tu itakusaidia, sasa pia ulichoandika sio sahihi mkuu, na machonkwangu havinipendezi, Especially udini
Mimi nadhan tungekuwa wa kweli tu, ofisi kubwa ya mwanasiasa makini ni jukwaani, sidhan kama kuna dhambi kuyasemea mambo hayo jukwaani, kama hoja ni kuandika barua tu basi hakuna haja ya kukaa bungeni waandikiane barua tu mambo yote yajadiliwe kwa barua.Sasa kama wameshapewa per diem zao ni busara kwa wapiga kelele kwenye majukwaa wakaandika barua ya kusudio la kuondolewa hizo posho bila ya hivyo itakuwa ni unafiki tu.
Nafikiri wewe ni mmoja wa watu ambao hudandia mada bila ya kuzisoma kisawasawa. Alichosema Mhe Zitto ktk bajeti ya kambi ya upinzani ni kuwa wabunge hulipwa posho za aina mbili kwa siku, ya kwanza inayitwa Sitting Allowance ya SHS 80,000/= kwa ajili ya kukaa katika vikao vya bunge; na ya pili ni posho ya kujikimu kwa lugha ya kigeni huitwa "Subsistence Allowance" ya Shs 70,000/= kwa ajili ya chakula, malazi n.k kwa kuwa viako vya bunge hufanyika nje ya vituo vyao vya kazi kwa maana ya maimbo yao ya uchaguzi. Ndipo akahoji uhalali wa mbunge kulipwa posho ya kukaa katika vaikao vya bunge ilihali kazi aliyoomba ni kuwawakilisha wananchi katika bunge na tayari analipwa mshahara kwa kazi hiyo hiyo.
Hivyo bajeti ya upinzani inapendekeza posho ya kujikumu iendelee na posho ya kukaa katika vikao vya bunge iondolewe. Vivyo hivyo kwa kwa watumishi wa serikalini hususan wakubwa wakikaa katika vikao mwisho hupitishwa bahasha zenye posho ilihali waliomba wenyewe kazi za kutumia akili katika vikao ndio maana hawafanyi kazi za shuruba kama vile kilimo, vibarua n.k. Kiutendo cha watumishi wa serikali tena wa kada ya juu tu, kulipwa posho ya kutimiza wajibu wao ambao tayari wanalipwa mishahara kuutimiza ni ufujaji mkubwa wa fedha za walipa kodi. Ndio maana vikao serikalini haviishi. Kinachotokea wanapanga vikao kufanyika katika mikoa nje ya vituo vya kazi na kupata posho mbili kama wabunge yaani posho ya vikao na posho ya kujikimu.
Je hiyo ndio siasa kwako?
Wapiga kelele ni akina nani mkuu!??