Porokwa apasua jipu la CCJ

Porokwa apasua jipu la CCJ

Watanzania bwana.. hivi alitoa ushahidi gani wa kuonesha kuwa kweli alikutana na hao jamaa zaidi ya mara tano na walichozungumzia hakikuwa kitu kingine isipokuwa CCJ?
 
You are wrong there!!!!!!! Si lazima majina yote ya waanzilishi yawepo katika daftari la msajili! Narudia, siyo lazima! Watajwa walihusika 100 pwercent ila hawakutaka kwanza majina yao yajulikane hadi chama kingepata permanent registration ili wajitokeze, na baadhi yao -- kama vile Sitta -- kugombea urais.

Kwa nini hutaki kuona along these lines?
Mkuu Marksman...unachosemaa ni kweli, kwa msajili kuna majina mawili tu ambayo ni ya Kiyabo na Muabhi....Na kama unavyojua, jamaa hawa walijificha kwanza ili chama kipate usajili kisha ndo waje, na alichosema Porokwa ni kweli, tulianza mazungumzo na CDM ili kushirikiana nao hata kama tungepata usajili wa kudumu. Hivyo mazungumzo yetu na CDM hayakuanza baada ya CCJ kukosa kusajiliwa.

Na kama watanzania watakumbukuka, kwenye press conference moja au mbili kama sikosei, niliwahi kusema CCJ inamgombea urais anayekubalika kuliko Kikwete wa CCM so hapa nilikuwa namaanisha Mh. Sitta.
 
Watanzania bwana.. hivi alitoa ushahidi gani wa kuonesha kuwa kweli alikutana na hao jamaa zaidi ya mara tano na walichozungumzia hakikuwa kitu kingine isipokuwa CCJ?

Mzee Mwanakijiji....

Kwa hili ni ngumu sana kutoa ushahidi wazi kwamba Porokwa alikutana na hawa jamaa...Mfano mimi niliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCJ, niliwahi kukutana na Mwakyembe na akanipa llift toka Kawe tulikofanyia kikao na kunirudisha nyumbani...Baadaye akaenda kuwa-join Makonda na Porokwa ambao tulikuwa nao wote kwa kikao... Hatukupiga picha na kwa kuwa mikutano hii ilikuwa ya siri sana ndo maana ni ngumu kukupa evidensi...

Sasa, mimi sina hakika kama Porokwa amezungumza haya kwa kuamua kusema ukweli au amesukumwa na mtu fulani, hata hivyo ukweli utabaki pale pale... Sitta, Mwakyembe, Nape, Mpendazoe, na Mwambalasa ndiyo waanzailishi wa CCJ. Hata hivyo kuna idadi ndefu ya wanaCCM waliokuwa wakiisapoti CCJ na kama nilivyosema ni ngumu kutoa ushahidi coz kumbuka walifanya hivi kwa usiri mkubwa. Hata hivyo mtu halazimishwi kuukubali au kuukataa ukweli huu...
 
hivi hili la mwanzilishi, lina faida gani kwa siasa zetu? Waanzilishi wa CDM, CUF, NCCR ni kina nani? Maana ukiachana na uanzilishi, hivi wangapi wametoka upinzani kwenda CCM na vice versa? Inasaidia nini hii katika siasa zetu?

Credibility, openness, stand by your actions and decisions and admit mistakes/failures and learn from them and go forward. The problem here is not about being a founder member is about denying the truth. It means that you are trustworthy to lead the people before tomorrow you will betry them for your own gains. They should accept it that they had that motive but after seeing CCM has changed the way of getting the people who will run for elections in different constituencies they changed their mind and remained with CCM.
 
Hongera Parokwa kwa kutujuza, "...Nilikutana mara kadhaa na Mh. Nape Nnauye, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe na Mh. Fred Mpendazoe."

Excellent, is better tumejua ukweli, but don't see on the single side of a coin, on other side hawa Six, Dr. Mwakyembe & Nnauye wote MAADUI wa EL, RA so huyu mmaasai Porokwa no doughts, no questions, very clear, anatumika as a political stabbing tool kuwamaliza hawa wana CCM of which ndio wenye maadili kuliko hao mafisadi, kwanza CCJ hata kusajiliwa ilishindikana, so what is all this saga? Ni mafisadi wanawatumia any
means kuwachafua hawa, halafu USHAIDI uko wapi walikuwa wanakutana mara tano tano, kama kuna signed papers, picha za vikao alete basi, Watz open ur eyes people mafisadi long arms are in actions
 
Nadhani ni muhimu to set the record straight, kwa kuanglia timeline ya matukio. Sitta, Mwakyembe na Nape walijitoa CCJ kabla ya uchaguzi chama kilipokosa usajili.

Kuhsu kuahidiwa vyeo, hawakahidiwa wote kwa wakati mmoja. Nape aliahidiwa na kupewa kabla ya uchaguzi. Sitta haku-negotiate mpk alipotoswa uspika na akaanza mazungumzo na CDM. Mwakyembe haijajukana when exactly.

Ishu ya kujivua magamba haikuwa idea ya wala siyo initiators. Na mpaka sasa ktk semina elekezi Sitta na Mwakyembe wamekaa na kukubali kugombezwa kama watoto na JK.

They are just there for money n power, hawana uzalendo! Tusitake kuwapa sifa wasizostahili, they took a gamble and lost, then crawled back to get whatever they could bargain.
 
JK asipoangalia CCM hii ataiacha mahututi. CCM angalieni kwa undani chanzo cha mgawanyiko/mpasuko ndani mwenu ili muweze kujinasua.
Binafsi nadhani uteuzi wa Nape kuwa katibu muenezi CCM waliteleza, anaongea sana bila kupima maneno yake.

Labda ameteuliwa kwa sababu kuna wakati alikuwa na mgogoro na EL kuhusu jengo la UVCCM upanga, wakaona kuwa ataendelea kumchafua EL ndiyo maana akawekwa hapo. Labda lengo kuu ilikuwa EL na sasa kwa jinsi asivyopima prons and cons za kauli zake anaweza akaiharibia CCM.

CCM kama CCM ina sera nzuri tena sana tatizo ni kutafsiri hizo sera kuweka katika vitendo kwa ajili ya Watanzania wote. Na hapo ndipo inapotakiwa CCM iwe makini na makada wake wengi ambao ni matajiri sana na mioyo yao ni ya kibepari and hujuma.

CCM imekuwa ikiwalazimisha watu wenye fedha wawe wanachama wake kwa kuwawekea vikwazo wafanyabiashara wengi ambao wameonekana kuwa tofauti nao. Watu kama hawa hawana mapenzi na Chama bali wameingia huko kujilinda na kulinda mali zao.
 
Porokwa ni Kilaza wa kutupwa namjua in and out. Naomba aeleze umma wa Watanzania nini kilimtoa katka "Uchungaji"??
 
Watanzania bwana.. hivi alitoa ushahidi gani wa kuonesha kuwa kweli alikutana na hao jamaa zaidi ya mara tano na walichozungumzia hakikuwa kitu kingine isipokuwa CCJ?
Mzee Mwanakijiji,
Wewe unajua nini kuhusu CCJ? Kwa weledi na uelewa wako mambo ya Tanzania na Watanzania lazima kuna kitu unajua kuhusu uanzishwaji wa chama hiki kabla kukiunga mkono kama ulivyofanya wakati fulani humu. Kwa kuwa sasa hakipo na hakitakuwepo tena bora jambo hili la kihistoria lililoleta hamasa ya aina yake hapa nchini likawekwa sawa. Usiachie watu kuipindisha historia ya nchi yetu.
 
Hawa kina Mhe. Sitta na Mwakyembe, ni wasaliti tu, walitaka kuiua CCM, kwa kuunda CCJ. Fitina zao ndizo zilizoifanya Serikali ya CCM isitekeleze kwa umakini mkubwa Ilani yake ya 2005, kwa kuwa Serikali ikawa sasa inaligopa Bunge, baada ya sakata la Richmond.

Ni vema tu Lowassa aliwahi kutekeleza ujenzi wa Shule za Kata, kabla hajajiuzulu kwa fitina za Richmond! Vinginevyo, kulikuwa hakuna cha kuonyesha. Ndiyo maana JK akapata kura 61% tu, mwaka 2010, kutoka 80%+ mwaka 2005! Ndiyo maana Sitta akang'olewa Uspika kwa msimamo kuwa "sasa tunataka Spika mwanamke"! Wana-CCM amkeni! Waswahili husema: "Kikulacho ki Nguoni Mwako"!


Bwassa
 
Mzee Mwanakijiji....

Kwa hili ni ngumu sana kutoa ushahidi wazi kwamba Porokwa alikutana na hawa jamaa...Mfano mimi niliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCJ, niliwahi kukutana na Mwakyembe na akanipa llift toka Kawe tulikofanyia kikao na kunirudisha nyumbani...Baadaye akaenda kuwa-join Makonda na Porokwa ambao tulikuwa nao wote kwa kikao... Hatukupiga picha na kwa kuwa mikutano hii ilikuwa ya siri sana ndo maana ni ngumu kukupa evidensi...

Sasa, mimi sina hakika kama Porokwa amezungumza haya kwa kuamua kusema ukweli au amesukumwa na mtu fulani, hata hivyo ukweli utabaki pale pale... Sitta, Mwakyembe, Nape, Mpendazoe, na Mwambalasa ndiyo waanzailishi wa CCJ. Hata hivyo kuna idadi ndefu ya wanaCCM waliokuwa wakiisapoti CCJ na kama nilivyosema ni ngumu kutoa ushahidi coz kumbuka walifanya hivi kwa usiri mkubwa. Hata hivyo mtu halazimishwi kuukubali au kuukataa ukweli huu...

Kaka
Hata Mwanakijiji na alikuwepo akirusha makombora kutokea kule..... Hukujua hilo? Labda jina lake halisi, bottom line yetu ni kupiga kotekote kama ni advantage kwa Lowassa sawa ila siku itakuwa kwa Sitta.
 
TUjiulize, Huyu Ole porokwa anatokea mkoa gani na huo mkoa wanachama wa CCM wamejeruhiwa Kiasi gani na kauli za mwakyembe na nape na Sitta wakati wa Bunge lililopita. Porokwa aseme ukweli kuwa anamsemea nani.

AAche kutupiga changa la macho.
 
hivi hili la mwanzilishi, lina faida gani kwa siasa zetu? Waanzilishi wa CDM, CUF, NCCR ni kina nani? Maana ukiachana na uanzilishi, hivi wangapi wametoka upinzani kwenda CCM na vice versa? Inasaidia nini hii katika siasa zetu?
Kayaandke haya Jambo Leo... Ok?
 
Huu mjadala wa ccj ni njama za kufanya ufisadi na magamba yasahauliwe kujadiliwa.
 
Kama kweli Nape ni mmoja kati ya waanzilishi wa CCJ, mimi binafsi namkubali mpaka hapo alipo. Kwa muonekano wa kawaida tu CCJ, ndio imekamata usukani baada ya CCM magamba kuangukia pua, baada ya vikao vya Dodoma.CCJ imeonyesha kuwa ni Chama ambacho hakikuwa lelemama kama wengi tunavyodhani, kilijiwekea chanel nyingi za kukamata siasa za Tanzania. Chanel ya Ofisi ya Tendwa ilishindikana kwa kuzibwa na Rechels lakini bado CCJ haikukata tamaa na sasa, imetua kwenye kiini cha CCM kama kirusi kikiwamega wale walikuwa wanakibania. CCJ sasa iko na ina nafasi ndani ya CCM. Ndio maana wale waliopinga usajili wake sasa wanapata shida kubwa, shame on them and shame on Tendwa. CCJ sasa imepata usajili ndani ya CCM kwa kutumia njia za panya, sasa inawamega akina Rechel lazima waipate joto ya jiwe. Na kwa msingi huo hata Tendwa huu ndio msimu wako wa mwisho, kwani si CDM wala CCJ iliyondani ya CCM watakaobaki na wewe baada ya uchaguzi wa 2015 kama mmoja wapo atashinda, kwani Mafisadi wenzako uliokuwa unawapendelea mpaka sasa upepo unawavumia vibaya mno katika siasa za Tanzania. Mpaka sasa wanaona aibu kujitokeza hadharani badala yake wanatuma messanger wao kama Daniel Ole Porokwa kutueleza waanzilishi wa CCJ. Wanzilishi wa CCJ sisi kwetu si habari mpya kwani siasa za Tanzania baada ya kashfa ya Richmond kusomwa kule Dodoma zilionekana wazi kuambata na vitendo vya wazi vya watuhumiwa wa Richmond kulipa kisasi na zililenga zaidi kuwaengua walihusika kuwatema ndani CCM.Katika vita ile wapambanaji wengi wamepotezwa kwenye siasa, kama akina Chegeni, Sererii nk. Wengine bado walipita Mlango wa nyuma kama ndugu yetu Shibuda. Na wengine walijaribu kupita mlango wa nyuma, bado wakazuiwa (Mpendazole). Lakini wengine waliendelea kupigana ndani na sasa wameshika usukani. Tunajua walivyokuwa ndani ya misukosuko ya kutemwa CCM walipenda kukisajili CCJ ili kiwe shock absorver kama watadondoshwa. Na wangedondwa pia CCM kubwa ingeyumba, wazee wa CCM waliliona hilo walimweleza mkulu kuwa ukiwatema hao kamwe hatutakuwa salama. Hatimaye walibakizwa CCM na ndio mwisho wa harakati za Usajili wa CCJ. Kwa misingi mingine CCJ iliunganishwa ndani ya CCM. Si kuunganiswa tu, sasa inatoa amri na kuwasaga wazi akina Rechel.
CCJ pambana nao huko ndani ya CCM mpaka waone kuchungu watoke wenyewe. Na hii inanipa mwanga kuwa mwaka 2015 uchaguzi utakuwa kati ya CDM vs CCJ.
Mkuu hawa wana nguvu la hela. Wana mtandao, na CCM yote huko mashinani wameshikilia wao. Unadhani CCJ itawaweza?
 
Hivi kunamtu anakumbuka kama Sitta alicomment chochote juu ya kujiondoa katika chama Mpendazoe? Tulitegemea Sitta kama Spika angemtaka Mpendazoe athibitishe kwa barua, ili jimbo lake lijulikane liko wazi. Lakini Sitta alika kimya, kwa sababu alijua huyu alikuwa mwenzake...
 
Yote yanayosemwa ni kweli kabisa. Lakini la msingi lingine hapa wana JF kujua ni kuwa hapana shaka mkulu alipata habari hizi na alishauriwa na kuchukua uamuzi wa kuhakikisha kuwa watu hawa hawa ambao CCM waliona walielekea kuwapa shida wanabaki ndani ya serikali ili kuwafunga midomo na kuwapa uwaziri. Msisahu Nape pia akapewa ukuu wa wilaya na leo hii msemaji mkuu wa CCM. Haya yote si kwa bahati mbaya.

Inaonekana wazi 'wapinga ufisadi' ndani ya CCM wameshinda kwani leo hii CCM wamelete ajenda ya kujivua gamba. Kwa hapa hakuna geni, mkulu na wenake wamewagwaya akina Sitta na wenziwe, huu utabaki kuwa ukweli pasipo shaka. Na yote hii inaonesha serikali ya Kikwete ilivyo dhaifu isivyo na misingi yoyote zaidi ya kuwa kama bendera kufuata upepo. Hatari sana.
 
Back
Top Bottom