Porokwa apasua jipu la CCJ

Porokwa apasua jipu la CCJ

Kwa haya maelezo nini kipya zaidi ya kusema katumwa na 3 twins.
Huyu bwana anjifunza siasa maana hata kama ni unafiki aliuanza siku nyingi aliposema Lowasa c mamasai na hatumbuliki miongoni mwa wazee wa kimila wa kimasai lakini baadaye alipoahidiwa kuwa atagombea Monduli 2015 bila kikwazo akaona ajirudi kwa Lowasa.
Kwahiyo ukweli anaousema yeye c asili yake ila kukisafisha kundi la 3twins. Namsikitikia kuwa anatumika vibaya.
Hapa tatizo si Mwakyembe au Stta au Mpendazoe.
Tuna tatizo kubwa la mfumo tulionao ikiwa na maana kuwa lazima ugombee kwa jina la chama fulani cha siasa haijalishi ni CDM, CCM, CUF....
Na kama mfumo ni mbaya ni sharti ukane ule mfumo au uwemo mle ndani ili ukaufanyie mageuzi.
 
Dr. Slaa katika kampeni mwakajana nakumbuka alimwambia Sitta kuwa ni MNAFIKI, ingawa Sitta alijitete hata hivyo kuna dalili kwamba Dr alikuwa anajua mambo hayo ila hakutaka kuyaongelea wazi. Hali kadhalika mwakajana baada ya purukushani ya kutaka kumtosa sitta katika kikao cha CCM akiwa bado speaker, Sitta alipita kujinadi kuanzia Mwanza kwenye maafali ya Chuo Kikuu cha Mt. Augustino, Kanisa kuu Songea nk. na wakati huo tetesi ya kutaka kuanzishwa chama kipya toka kwa wanaccm waadilifu zilishavuja ila hatukujua ni nani.
Kwa vyo vyote siri serikalini ilivuja tu kwa njia za kiintelijensia, ndio maana Kikwete alifanya kila awezalo kumtosa Sitta kwenye ubunge na kupitisha hoja ya kumpa nafasi mwanamke ili iwe rahisi vinginevyo hakukuwa na mwenye uwezo wa kushindana na Sita kwenye uspika.
Ni mapokea ya serikali ya CCM wale wanaoonekana kuwa hatari kwa serikali na Chama wakiwa wabunge basi ni kuwaingiza kwenye baraza la mawaziri ili kuwafunga finywa na nyendo zao zifuatiliwe kwa ufanisi zaidi. Ndicho kinachoendelea sasa.
 
Open + Honest = Trust.

How can you entrust your resources, national leadership, develpment programs etc. to such a person using both "yes" and "no" on the same subject. It matters a lot my friend and it is very serious especially when it has involved the national figures. They have got to be truthful.

hivi hili la mwanzilishi, lina faida gani kwa siasa zetu? Waanzilishi wa CDM, CUF, NCCR ni kina nani? Maana ukiachana na uanzilishi, hivi wangapi wametoka upinzani kwenda CCM na vice versa? Inasaidia nini hii katika siasa zetu?
 
usiwe mvivu wa kuelewa

kinachozungumziwa hapa ni dhana ya unafiki na undumilakuwili kwa viongozi wetu ....period
Kubadili uamuzi si lazima kuwa undumilakuwili. Kama wewe ni mchezaji na mnahitaji ushindi, unaambiwa tutaifanya timu yetu kuwa bora kwa kubadili sera na benchi la ufundi, tutanunua wachezaji wapya na hata staff tutawabadilisha, unaweza kuwa na sababu ya kuwaha. Kwao CCM sera mpya ni kujivua gamba, kubadili wachezaji na backroom staff ndio kina Nauye, na mengineyo kina Mwakyembe kupewa nafasi ya uchezaji badala ya kukaa benchi wakarekebishe kasoro ili timu yao ipate ushindi. Kwahiyo kubadili maamuzi si undumila kuwili wala kushindwa. Watu wamebadili maamuzi kwa kuacha kazi zao na baadae kuzirejea au kukancel resignation, wengine walikuwa kwenye process ya kuwataliki wake zao wameamua kuwarejea, kwahiyo hoja ya kubadili maamuzi haina mantiki unless utueleze kivinginevyo!
 
Open + Honest = Trust.

How can you entrust your resources, national leadership, develpment programs etc. to such a person using both "yes" and "no" on the same subject. It matters a lot my friend and it is very serious especially when it has involved the national figures. They have got to be truthful.
Any successful development program has got to be flexible including leadership. If there is an opportunity for changing development policies including the way things are handled, the aggrieved parties at one point may change their position. In every aspects of life, people have and are changing their positions/professionals and ambitions. Why not in politics?
 
Hivi huyu Porokwa bado anadunda CCM? kutokana na haya yote aliyoyamwaha hadharani, CCM inachukua hatua gani? Mimi nina shauku kubwa kwanza kujuwa iwapo CCM itayakubali au itayapinga. Patamu hapa!

CCM unafikiri ichukue hatuwa gani? CCJ kilikuwa chama kama kilivyo CDM na wengine na kwa bahati ni kuwa kutokana na historia waanzilishi wote wa vyama vya upinzani walikuwa CCM. Hata hivyo hata leo kama Mbowe, Slaa, Lipumba, Seif Sharif, Cheyo, Mrema, Mtikila na wengine wakiamuwa kurejea CCM watapokewa kwa Shangwe na hali hiyo iko kwa CDM na wengine watakuwa tayari kupokea wanachama kutoka vyama vyengine> Kwao wao siasa ni ulaji na hivyo kila ukipata mnafiki ndio kuengeza nguvu katika ulaji. Tunaoliwa ni sisi wananchi, wanasiasa wako kazini wakituendesha kwenye Maamndamano ,wakilipana posho na kila wakishinda ubunge ruzuku ndio inazidi ili walipane hizo milioni 7 .
 
Yule kada wa CCM, Daniel ole Porokwa yuko katika mkutano na waandishi wa habari hivi sasa. Nimeambiwa amejipanga kupasua jipu kuhusu uanzishwaji wa CCJ.

Amepanga kueleza kila kitu juu ya chama hicho...

Kwa muda wa takribani wiki mbili sasa, vyombo vya habari vimeripoti maelezo yaliyotolewa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chadema, Mh. Anthony Komu, kwamba Nape Nnauye alikuwa mwasisi wa Chama Cha Jamii (CCJ). Madai haya yakathibitishwa na aliyewahi kuwa mbunge wa Kishapu (CCM), Fred Mpendazoe ambaye alitaja watu kadhaa nikiwamo mimi, kuwa walishiriki au waanzilishi wa chama hicho ambacho hakikuwahi kufanikiwa kupata usajili wa kudumu. Hivyo basi, nimewaita hapa leo hii, ili pamoja na mambo mengine, kueleza ukweli wa hiki ambacho kimeelezwa vizuri na Mheshimiwa Mpendazoe na kimenukuliwa vema na vyombo vya habari, hasa gazeti la kila wiki la MwanaHALISI. Nimeamua kufanya hivyo kwa misingi miwili mikuu.

Kwanza, sisi kama viongozi ni sharti tuwaonyeshe wananchi wetu na wanachama wa chama chetu njia sahihi tunayotakiwa kupita na tuamini katika hiyo njia tunayoelekea. Pili, mmoja wa msingi mkuu wa chama chetu, ni kusema ukweli, na kwamba uwongo na fitina ni mwiko kwa viongozi na wachama wa CCM. Ni kweli niliwahi kuombwa kuwa mmoja wa wanachama waanzishi wa CCJ. Nilikutana mara kadhaa na Mh. Nape Nnauye, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe na Mh. Fred Mpendazoe. Aidha, nilikutana mara moja na Mh. Samwel Sitta baada ya Mh. Nape na Dk. Mwakyembe kunitajia kuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa CCJ, nami kutaka uthibitisho wa hicho walichonieleza.

Naye Mh. Sitta alinieleza kuwa nilichoelezwa na Mh. Nape na Dk. Mwakyembe hakina chembe ya mashaka. Katika mikutano zaidi ya mitano niliyofanya na Mh. Nape na Dk. Mwakyembe wenzangu walinieleza mpango wao wa kuanzisha chama cha siasa kuwa umelenga kuondokana na utawala wa kiimla wa CCM kwa hoja kuwa kilipofikia chama hicho hivi sasa, hakiwezi tena kuaminiwa kukabidhiwa madaraka ya kuongoza dola. Walisema CCM hakiaminiki tena machoni mwa wananchi na kimepoteza mvuto mbele ya umma; yote haya ni kwa kuwa chama hiki kimekuwa kinaacha ile misingi kama ilivyoasisiwa na waasisi wake, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Walinieleza, kihistoria Chama Cha Mapinduzi ni chama cha ukombozi na kilijipa kazi ya kupigania wanyonge, lakini kikafika mahali historia hiyo ikaporomoka kwa kuingia katika mikono ya watu wasiojali, wasiokuwa na maadili ya uongozi na labda wasiowaaminifu. Wakati wote wa mazungumzo yetu, Mh. Nape na Dk. Mwakyembe walikuwa wakisisitiza umuhimu wa mimi kukubali kujiunga haraka na CCJ, ili kurahisisha upatikanaji wa usajili wa kudumu wa chama hiki, lengo likiwa CCJ kiweze kishiriki katika uchaguzi mkuu wa 2010.

Hata hivyo, kila muda ulivyozidi kusogea, ndivyo nilivyopata kujua undani Mh. Mwakyembe na Mh. Nape wa kutaka kuanzisha chama chao cha siasa, kwamba kinachowasukuma katika mpango huo, ni matakwa binafsi ya kisiasa na hivyo nikaanza taratibu kuwa mbali na mkakati wao. Nimeamua kuyasema haya baada ya kuwasikia Mh. Nape na Dk. Mwakyembe wakimkana Mh. Mpendazoe na kimsingi wakikana chama chao – CCJ. Napenda kuwaambia Watanzania, kwamba CCJ ni chama kilichoanzishwa na kuasisiwa na viongozi hao wawili, pamoja na Mh. Sitta kama ambavyo Mpendazoe alivyoeleza. Katika mpango huu, mimi niliahidiwa kusaidiwa kugombea ubunge katika jimbo la Monduli kupitia CCJ, huku Mh. Nape akiahidi kusimama katika jimbo la Ubungo.

Nimeyasema haya ili kuondoa unafiki unaojengeka ndani ya chama chetu na taifa kwa jumla, kwamba kuna kikundi cha watu wanaotaka kupotosha umma juu ya uanzishwaji wa CCJ na ujio wake ili umma uwapime na uamue juu ya watu hao. Mimi kama kada wa CCM niliyefundishwa na kuaminishwa kwamba uongozi ni dhamana na ninayeamini katika misingi ile aliyotuachia Mwalimu Nyerere, nimeamua kuyasema haya ili ukweli ubaki ukweli katika historia ya nchi yetu. Kuyumba kwa chama chetu na hata kufikia hatua ya kuanza kuporomoka kwa kupoteza nafasi mbalimbali kwa vyama vingine kwa wingi tokea kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi katika nchi hii, ni kwa sababu ya kuwa na viongozi wenye malengo na agenda zao binafsi, tofauti na zile za chama chetu.

Hii bila mashaka inanipa sababu ya kuamini kwamba Bunge la Tisa kama mmoja wa mihimili muhimu wa dola, chini ya Mh. Samwel Sitta lilitumika vibaya kufanikisha agenda nyingine ya kuanzisha chama kingine badala ya CCM.

Ni vema Rais Jakaya Kikwete akajua kuwa ndani ya timu yake, kuna wachezaji ambao wako tayari kujifunga na kuinyima timu yao ushindi. Ni vema akaamua kuachana nao kwa maslahi yake na chama chake. Ni maoni yangu kwa dhati kabisa na rai yangu kwa viongozi wa chama, kwamba ni wakati mwafaka watu kama hawa wawajibike au wawajibishwe kwa matendo yao.

Baada ya mimi kushutukia na kutokuwa na imani na minendo ya waasisi wa CCJ na hivyo kujiondoa, nilipata taarifa kuwa baada ya kujiridhisha kuwa chama chao hakitasajiliwa na kuwahi uchaguzi wa 2010, waliamua kufanya mazungumzo na viongozi wa Chadema na kukubaliana kuwa wote kwa pamoja watajiondoa CCM na kujiunga na Chadema ili kugombea nafasi mbalimbali kupitia chama hicho. Kwa ushahidi ninaoutoa, ninawachukua hawa niliowataja kuwa si wasaliti kwangu tu, bali hata kwa chama chenyewe. Nisingeshutuka mapema yangenipata yaliyompata Mpendazoe.

Ninampa pole sana ndugu yangu Fred Mpendazoe. Na hili la Mpendazoe ambaye alikuwa mbunge, akaacha mishahara kadhaa na mafao yake kwa makubaliano ya kazi ya pamoja ambayo nilishirikishwa katika hatua za awali na mwisho wake wakamtosa na sasa wanamkana hadharani, ni moja ya sababu iliyonisukuma sana kutoa ushuhuda huu.

Daniel ole Porokwa,
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

- Hivi ni lini Lowassa ataelewa alama za nyakati kwamba yeye kuwa Rais wa Tanzania, will never happen! Why waste his time na hizi nyepesi nyepesi!

- I mean read our lips sisi wa-Tanzania sio mabwege tena!

Es!
 
Mie nadhani anachofanya sasa ni kuharibu ili wote wakose. Na ameamua kweli na mbaya zaidi ana mtandao mrefu saana serikalini.
 
Mie nadhani anachofanya sasa ni kuharibu ili wote wakose. Na ameamua kweli na mbaya zaidi ana mtandao mrefu saana serikalini.

- Well, lakini soon na yake yatawekwa wazi na ni hayo hayo yaliyosababisha kumuweka nje ya NEC na CC, na mbioni kumuondoa kabisa CCM, sasa kwa nini asiende Upinzani ili awe na strong platform kwa taifa, badala ya kujificha ficha nyuma ya Viongozi wanyonge kama hawa na media? I mean akiwa huko aseme uozo wote wa wenzake na wake uwekwe wazi ili wananchi tuamue pumba na mchelle ulipo!

- Kwenye kikao cha CCM kilichopita si alijionea wazi kwamba CCM inamuhitaji sana Sitta, kuliko yeye na kundi lake sasa anahangaikia nini?

Es!
 
Yawezekana hili la uanzilishi lisiwe na manufaa katika uchumi na umaskini wetu, lakini kinacho-matter hapa ni ETHICS and INTEGRITY. Kiongozi umepewa dhamana ya kuongoza tunategemea kuwa utakuwa MKWELI na si POROJO.

Nimeamua kwa makusudi kuitunza hotuba ya Sitta aliyoitoa Moshi juzi akiwa na Mwakyembe kwenye Secured Hard Drive yangu. Anaonya vijana wasiyumbishwe na wanasiasa kwa ajili ya matumbo yao. He's doing the same thing, anajali tumbo lake kuliko dhamira ya watanzania. Nimefanya makusudi nikiamini kuwa ukikaribia uchaguzi mkuu atakula matapishi yake.
mkuu hapo kwenye red na mimi nazitaka hizi
 
usitumie nguvu kutoa hoja yako. Kama majina yao hayapo kwa msajili, mwakyembe , 6 na nape wakikanusha, kimsingi mimi nitawaamini unless kama unaweza definition nyingine ya '
uanzilishi' mbali na ninayoijua mimi

NASHINDWA KUMWAMINI POROKWA: NI MAMLUKI

Sitasahau siku ambayo Porokwa alitutangazia mhini Arusha azma yake ya kugombea Ubunge wa Monduli kwa kudai kuwa:
1. Lowassa si Mmasai, ni Mmeru ambaye jina lake halisi nI NDOKWARU NDOSSI
2. Ni fisadi ambaye anatumia kofia ya Umasai kujineemesha mwenyewe
3. Yeye Porokwa anaungwa mkono na wazee karibu wote wa Kimasai
4. Atapigana kufa kupona kumyang'anya NDOKWARU kiti cha Ubunge.

Tukamchangia fedha, tukaunda Kamati lakini baadaye tukasikia anajiondoa kugombea Ubunge na kujisalimisha kwa huyo NDOKWARU! Baadaye tukagundua kuwa alipewa pesa, tena kidogo sana, shilingi milioni tatu na kuzawadiwa Ukatibu Msaidizi wa Wilaya na swahiba wa NDOKWARU, bwana Makamba!

Aliyoyaongea yote kuhusu Nape, Mwakyembe na Sitta naamini ni dictation ya NDOKWARU a.k.a Lowassa. Angepata wapi ubavu, mtu mdogo kabisa katika Chama (katibu msaidizi wa Wilaya) kumvuta sharubu bosi wake Nape Nnauye? Naomba mnisaidie, nifanye nini nianze kumwamini tapeli huyu?
 
- Well, lakini soon na yake yatawekwa wazi na ni hayo hayo yaliyosababisha kumuweka nje ya NEC na CC, na mbioni kumuondoa kabisa CCM, sasa kwa nini asiende Upinzani ili awe na strong platform kwa taifa, badala ya kujificha ficha nyuma ya Viongozi wanyonge kama hawa na media? I mean akiwa huko aseme uozo wote wa wenzake na wake uwekwe wazi ili wananchi tuamue pumba na mchelle ulipo!

- Kwenye kikao cha CCM kilichopita si alijionea wazi kwamba CCM inamuhitaji sana Sitta, kuliko yeye na kundi lake sasa anahangaikia nini?

Es!
Huyu hana nguvu tena ya kuongoza chama chochote. Ushauri kwake ilikuwa ni kukubali siasa basi apumzike na afanye mambo mengine. Hao anaowafanyia vurugu ndio wanaomlinda.
 
- Hivi ni lini Lowassa ataelewa alama za nyakati kwamba yeye kuwa Rais wa Tanzania, will never happen! Why waste his time na hizi nyepesi nyepesi!

- I mean read our lips sisi wa-Tanzania sio mabwege tena!

Es!
naomba JK awe na hasira kama hizi
 
NASHINDWA KUMWAMINI POROKWA: NI MAMLUKI

Sitasahau siku ambayo Porokwa alitutangazia mhini Arusha azma yake ya kugombea Ubunge wa Monduli kwa kudai kuwa:
1. Lowassa si Mmasai, ni Mmeru ambaye jina lake halisi nI NDOKWARU NDOSSI
2. Ni fisadi ambaye anatumia kofia ya Umasai kujineemesha mwenyewe
3. Yeye Porokwa anaungwa mkono na wazee karibu wote wa Kimasai
4. Atapigana kufa kupona kumyang'anya NDOKWARU kiti cha Ubunge.

Tukamchangia fedha, tukaunda Kamati lakini baadaye tukasikia anajiondoa kugombea Ubunge na kujisalimisha kwa huyo NDOKWARU! Baadaye tukagundua kuwa alipewa pesa, tena kidogo sana, shilingi milioni tatu na kuzawadiwa Ukatibu Msaidizi wa Wilaya na swahiba wa NDOKWARU, bwana Makamba!

Aliyoyaongea yote kuhusu Nape, Mwakyembe na Sitta naamini ni dictation ya NDOKWARU a.k.a Lowassa. Angepata wapi ubavu, mtu mdogo kabisa katika Chama (katibu msaidizi wa Wilaya) kumvuta sharubu bosi wake Nape Nnauye? Naomba mnisaidie, nifanye nini nianze kumwamini tapeli huyu?

HATA MIMI SIMWAMINI: KATIBU MSAIDIZI WILAYA PRESS CONFERENCE BEN MKAPA BUILDING!

Angefanyia Press Conference yake viwanja vya Mnazi Mmoja au Shule ya Uhuru, ningemwamini kidogo, lakini Ben Mkapa building! Kapata wapi fedha ya kukodisha chumba chenye viyoyozi mlalahoi huyu? Jibu linajulikana - EL!

Angeandaa mwenyewe Press Conference hiyo, ningemwamini kidogo. Lakini katumia agency ya kina Fina Mango, agency ya kulipia! Kapata wapi fedha mlalahoi huyu kama si EL aliyemlamba miguu?

Naambiwa kashuka toka Arusha kwa ndege! Jamani Porokwa, ndege! Mtu ambaye miezi michache iliyopita alikuwa anadandia FUSO za vitunguu kutoka Iringa kwenda Namanga? Hapa, nauona tena mkono wa EL!

Waandishi wengi kama siyo wote tuliokuwepo pale, tumepewa "posho" au MSHIKO! Kapata wapi pesa mlalahoi huyu kama si EL?

Nakubaliana na Mkuu Fataki kuwa si rahisi wala kawaida kwa afisa mdogo wa wilaya kumvaa Mkuu wake wa Idara, Nape, bila mkono wa mafisadi waliompa hizo sh. milioni 3 ajitoe kugombea ubunge Monduli.

Pamoja na Porokwa kuwaambia watu wote kuwa yeye ni mpwa wa Sokoine, bado simwamini x 1,000. Anapenda pesa na rahisi kutumiwa!
 
Was this the case in this regard??

Was this flexibility for the betterment of the Tanzanian community? Has it in any case turned things around?
When in the public service you need to demonstrate your stand openly including your disagreement to what your party, association, or any group is not doing right. Even if it amounts to leaving the party it must be positively defined in an open manner as a subject of conserving the public interest, this will demonstrate your professionalism and maintain trust within and outside your party or team including the public that immoral and unethical leadership is intolerable. After matters have been resolved, your flexibility will then be meaningful. Would you really uplift quiet flexibility in public services?This is what a leader does and not hidding behind doors and then say you have become flexible, why did you not say it before you were flexible? If it wasn't worthy telling us at the time, what make it worthy now? Even in any professionalism you don't just become flexible to matters without consulting your main clients and customers to ensure it adds value and meets the key objective.

Any successful development program has got to be flexible including leadership. If there is an opportunity for changing development policies including the way things are handled, the aggrieved parties at one point may change their position. In every aspects of life, people have and are changing their positions/professionals and ambitions. Why not in politics?
 
Bila shaka haaminiki kwa kila mpenda viongozi makini. Lakini jambo kuu ni kwamba alichosema kina ukweli ndani yake na ndio ametusaidia kwamba tunao viongozi wanafiki ambao hawatakiwi kuaminika pia, hata kidogo. Katika hili ametusaidia na ndilo tatizo la mtu wa kutumiwa mda wowote anakulipua mwenyewe sasa ndo kinachotokea. Mlimtumia na sasa anatumika kwa namna nyingine.

HATA MIMI SIMWAMINI: KATIBU MSAIDIZI WILAYA PRESS CONFERENCE BEN MKAPA BUILDING!

Angefanyia Press Conference yake viwanja vya Mnazi Mmoja au Shule ya Uhuru, ningemwamini kidogo, lakini Ben Mkapa building! Kapata wapi fedha ya kukodisha chumba chenye viyoyozi mlalahoi huyu? Jibu linajulikana - EL!

Angeandaa mwenyewe Press Conference hiyo, ningemwamini kidogo. Lakini katumia agency ya kina Fina Mango, agency ya kulipia! Kapata wapi fedha mlalahoi huyu kama si EL aliyemlamba miguu?

Naambiwa kashuka toka Arusha kwa ndege! Jamani Porokwa, ndege! Mtu ambaye miezi michache iliyopita alikuwa anadandia FUSO za vitunguu kutoka Iringa kwenda Namanga? Hapa, nauona tena mkono wa EL!

Waandishi wengi kama siyo wote tuliokuwepo pale, tumepewa "posho" au MSHIKO! Kapata wapi pesa mlalahoi huyu kama si EL?

Nakubaliana na Mkuu Fataki kuwa si rahisi wala kawaida kwa afisa mdogo wa wilaya kumvaa Mkuu wake wa Idara, Nape, bila mkono wa mafisadi waliompa hizo sh. milioni 3 ajitoe kugombea ubunge Monduli.

Pamoja na Porokwa kuwaambia watu wote kuwa yeye ni mpwa wa Sokoine, bado simwamini x 1,000. Anapenda pesa na rahisi kutumiwa!
 
Bila shaka haaminiki kwa kila mpenda viongozi makini. Lakini jambo kuu ni kwamba alichosema kina ukweli ndani yake na ndio ametusaidia kwamba tunao viongozi wanafiki ambao hawatakiwi kuaminika pia, hata kidogo. Katika hili ametusaidia na ndilo tatizo la mtu wa kutumiwa mda wowote anakulipua mwenyewe sasa ndo kinachotokea. Mlimtumia na sasa anatumika kwa namna nyingine.

- Huuu mchezo wa kutumiwa na kuwalipua wanaokutumia ulimshinda Komandoo kule visiwani, walimtumia wee mpaka kumpitisha Mkapa kuwa rais, lakini time yake ilipofika wakamnyima term ya tatu na wakampiga chini mgomeba wake Biali wakampa Karume, akarudi nyuma na kujifunza upya siasa za taifa, ndio sasa amezielewa ndio wamemrudishia mtu wake Bilal kwenye power, huyu naye Lowassa arudi nyuma na kujifunza tena, kwamba pesa peke yake haziwezi kumpa urais wa bongo!

- Wamemlia wee pesa zake sasa wanamtosa kimaso maso na akifanya mchezo kama anaouchea sasa hivi ataishia lupango!

NANI MWENYE UJASIRI WA KUFANYA HIVI?Nape?
 
Back
Top Bottom