Porokwa apasua jipu la CCJ

Porokwa apasua jipu la CCJ

na tatizo kubwa ni pale watu wanapojitahidi kukataa ukweli wakati ukweli upo dhahiri...bora kukubali ukweli kuliko kupaza sauti kuwa jambo fulani si kweli ilhali wako watu wenye ushahidi...wabongo bana
 
Ni muhimu watu wakaangalia pande zote za shilingi. Ole Porokwa alishawahi kutangaza kumpinga Lowasa, ghafla akabadilika na kwenda kwenye vyombo vya habari kumuomba radhi kwa kutaka kutumia haki yake ya kikatiba na kidemokrasia!!! Porokwa amekuwa ni mtu asiyeeleweka kwa vipimo vyote vya uelewa na kauli zake ni za kuziangalia kwa umakini.

Kama aliitwa ajiunge CCJ hayo angeyasema mapema tena wakati kuna mvurugano ndani ya CCM, lakini angalia ni wakati gani ameamua kuyasema na jiulize ni kwanini.
Siku chache zilizopita mifasadi(hasa pacha 3) walisemekana kutumia mbinu za hali ya juu kujinasua.
Tunakumbuka mapacha walisema tuhuma za kutajwa si ushahidi wa wao kufanya maovu na kuwapa muda wa kujitoa au kuachia nyadhifa ni kuwaonea. Walisema mbona watu wengine wanatajwa katika mambo kadha wa kadha na hawapewei muda iweje wao?

Kitendo cha Nape kutajwa kuwa mwanzilishi wa CCJ kimetumiwa na mapacha ili kujenga hoja ya kuwa kama tuhuma tu zinatosha mtu kuachia ngazi basi Mwakyembe na Sitta nao wapewe muda wa kujitahmini. Ni kwa mantiki hiyo Porokwa amewezeshwa ili awe 'whistle blower' na hapa ndipo mapacha watatu watakapoponea. Utashangaa ishu itavaliwa njuga sana kwasababu mapacha watatu watagawa pesa(wanayo) kununua wasema hovyo ili kujenga hoja ambayo sasa inashika kasi.

Hapa kuna wafa maji (mapacha 3) na wanashika kila kilicho karibu nao hata kama ni ubua. Tuliangalie suala hili kiundani na mtazamo mpana, ushabiki unaweza kuwa ni sehemu ya kuokoa mapacha watatu bila kudhamiria. Kama kuanzisha chama ni usaliti porokwa alitakiwa aseme hili mapema ndani ya vikao vyao au vyombo vya habari, kujitokeza leo ni kununuliwa ili awaokoe mapacha watatu, hasa ikizingatiwa kuwa baada ya 'kutubu' EL alimweka karibu sana.
Sasa mapacha watakuwa na hoja, endapo wao wanatajwa bila ushahidi(kama wanavyodai) basi kila anayetajwa naye afuate mkondo. Kama walivyoanza kuwanunua wenyeviti wa mikoa wa CCM hili watalitumbukiza tu kushadidia hoja yao. Kama hoja ililenga kumweka Nape mahali pagumu, itasaidia kuwaweka wengine mahali rahisi, lakini itakuwa ni jiwe moja kwa ndege wawili kwababu Nape sasa ni mwiba kwao, na akina Sitta na Mwakyembe ni mwiba wa zamani, kama kuna 'kisu' chenye makali pande zote hicho kinafaa mapacha 3.

ni wakati wana CDM popote walipo wajiulize kuna umuhimu wa kulikuza au kulipigia baragumu jambo hili?
Time will tell.

Ni vyema zaidi kwa cdm mapacha watatu wasitoke ccm, thats a greatest wish.
 
hivi hili la mwanzilishi, lina faida gani kwa siasa zetu? Waanzilishi wa CDM, CUF, NCCR ni kina nani? Maana ukiachana na uanzilishi, hivi wangapi wametoka upinzani kwenda CCM na vice versa? Inasaidia nini hii katika siasa zetu?

Yawezekana hili la uanzilishi lisiwe na manufaa katika uchumi na umaskini wetu, lakini kinacho-matter hapa ni ETHICS and INTEGRITY. Kiongozi umepewa dhamana ya kuongoza tunategemea kuwa utakuwa MKWELI na si POROJO.

Nimeamua kwa makusudi kuitunza hotuba ya Sitta aliyoitoa Moshi juzi akiwa na Mwakyembe kwenye Secured Hard Drive yangu. Anaonya vijana wasiyumbishwe na wanasiasa kwa ajili ya matumbo yao. He's doing the same thing, anajali tumbo lake kuliko dhamira ya watanzania. Nimefanya makusudi nikiamini kuwa ukikaribia uchaguzi mkuu atakula matapishi yake.
 
Hayo yote amethibitisha yaliyosemwa na Fred Tungu Mpendazoe, lakini nnyuma yake Porokwa yuko nani? RA na EL?
Safari bado ndefu, viongozi wetu wengi nin wanafiki na bado hawajawa huru. sasa hao wanaokataa maana yake nini? na Huyo Porokwa hayo anayosema alikuwa wapi kuyasema siku zote hadi sasa ndio ajue kuwa wana ccm wanatakiwa kusema ukweli.
 
watanzania tunaoipenda nchi yetu hatutakiwi kumwamini mtu yeyote aliyeko ccm. Ikiwa sitta na mwakyembe wanachukizwa na udhalimu wa ccm unaoua maendeleo ya nchi yetu walipaswa kutokaccm. Kama walitaka kuanzisha ccj kwa ajili ya kujitoa ccm ni vyema lakini sasa bado wako ccm wakifurahia huo uovu wa ccm hawatufai.

Tatizo ccm wanapigana wenyewe na ukionekana kuwapinga hawa wanafiki wanaojifanya wanavua gamba unaonekana unawaunga mkono rachel. sisi tunasema wote hawatufai. Hatuwataki rechel, hatuwataki pia six, mwakyembe, maghufuli na wengine wote wanojifanya wema kwetu lakini wanataka ccm iendelee kuwepo madarakani hata kama wanaangamiza nchi lakini maslahi yao wanayapata kwa gharama ya umaskini wetu.

Wanasiasa wa aina hii ni wabaya kweli make wanadhoofisha nguvu ya walio na uchungu na nchi kuleta mabadiliko. Kinachotokea ni kuwa nguvu ya mabadiliko inagawanywa na hawa wanafiki mwisho wake walewale waovu wanaendela kutawala wao wakiwaunga mkono. Mfano mzuri ni bwana kalonzo msyoka ambaye ni makamu rais wa kenya aliyegawanya nguvu ya odm, kajiunga na kibaki akaendelea kutawala kwa gharama ya kukwamisha mabadiliko ili mradi tu apate maslahi yake.

Hivo iwe kuwa porokwa kaja kwa mkono wa rechel kwetu wazalendo tunafurahia manake wale wanafiki wanaopunguza nguvu ya mabadiliko kwa kujifanya wema kwetu wanadhihirishwa wazi na pia wanaharibu huko wanakopata maslahi yao ya kinafiki.

Hivi mchawi na mwizi wakikutana wakapigana mpaka wakachoka mpaka wakashindwa kwenda kuroga na kuiba nani atafaidi? Siyo yule anayeenda kuibiwa na anayeenda kurogwa? Asubuhi ikifika wakakutwa wamechoka kama watu hawakumjua mwizi watamjua; kama watu hawakumjua mchawi make hawa huwa wanafiki sana atakuwa amejulikana.

umenikuna sana mkuu. Haya lazima tuyangatie to speed up our second revolution
 
hii siyo habari tena, haina tija tena kulijadili labda kama ccm ndio wanataka kuleta hoja mpya ilikusahaulisha watu vitu muhimu tunavyovidai hasa swala la mafisadi na ahadi ya kuvua magamba

yote lazima tuyajadili na kuyashikia bango ili kuharakisha kifo cha ccm kwa manufaa ya watanzania.
 
hivi hili la mwanzilishi, lina faida gani kwa siasa zetu? Waanzilishi wa CDM, CUF, NCCR ni kina nani? Maana ukiachana na uanzilishi, hivi wangapi wametoka upinzani kwenda CCM na vice versa? Inasaidia nini hii katika siasa zetu?

we mwenzitu vipi? Ulion tatizo ? Kama tatizo halipo mbona wanakana chama chao.kama tatizo hulioni basi wewe pia tatizo.
 
CCJ, CCJ, hivi CCJ nayo ni habari kwa sasa? mnajadili mimba ambayo iliharibika ili iweje? mbona kuna watu waliowahi kuhama kabisa vyama vyao na wakajiunga na vyama vingine baadae wakarudi kwenye vyama vyao vya zamani na wakapokewa kama mashujaa na vyeo juu. Kwanza katika siasa za bongo mtu akitaka kujiongezea umaarufu anahama chama chake kisha anarudi tena kama shujaa na kupewa vyeo.

Tujadili mambo ya msingi yanayolihusu taifa letu kwa sasa, sukari bei juu, nyama imekuwa ni anasa, nauli za mabasi juu, mafuta n.k
 
Porokwa asema "ukweli wake" kuhusu kuanzishwa CCJ 22/05/2011
1 Comment


1306074260.jpg
​
Habari imenukuliwa kutoka blogu ya Muhidin Michuzi

Taarifa ya Daniel ole Porokwa, kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa vyombo vya habari.

Kwa muda wa takribani wiki mbili sasa, vyombo vya habari vimeripoti maelezo yaliyotolewa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chadema, Mh. Anthony Komu, kwamba Nape Nnauye alikuwa mwasisi wa Chama Cha Jamii (CCJ).

Madai haya yakathibitishwa na aliyewahi kuwa mbunge wa Kishapu (CCM), Fred Mpendazoe ambaye alitaja watu kadhaa nikiwamo mimi, kuwa walishiriki au waanzilishi wa chama hicho ambacho hakikuwahi kufanikiwa kupata usajili wa kudumu.

Hivyo basi, nimewaita hapa leo hii, ili pamoja na mambo mengine, kueleza ukweli wa hiki ambacho kimeelezwa vizuri na Mheshimiwa Mpendazoe na kimenukuliwa vema na vyombo vya habari, hasa gazeti la kila wiki la MwanaHALISI.

Nimeamua kufanya hivyo kwa misingi miwili mikuu. Kwanza, sisi kama viongozi ni sharti tuwaonyeshe wananchi wetu na wanachama wa chama chetu njia sahihi tunayotakiwa kupita na tuamini katika hiyo njia tunayoelekea.

Pili, mmoja wa msingi mkuu wa chama chetu, ni kusema ukweli, na kwamba uwongo na fitina ni mwiko kwa viongozi na wachama wa CCM.

Ni kweli niliwahi kuombwa kuwa mmoja wa wanachama waanzishi wa CCJ. Nilikutana mara kadhaa na Mh. Nape Nnauye, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe na Mh. Fred Mpendazoe.

Aidha, nilikutana mara moja na Mh. Samwel Sitta baada ya Mh. Nape na Dk. Mwakyembe kunitajia kuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa CCJ, nami kutaka uthibitisho wa hicho walichonieleza.

Naye Mh. Sitta alinieleza kuwa nilichoelezwa na Mh. Nape na Dk. Mwakyembe hakina chembe ya mashaka.

Katika mikutano zaidi ya mitano niliyofanya na Mh. Nape na Dk. Mwakyembe wenzangu walinieleza mpango wao wa kuanzisha chama cha siasa kuwa umelenga kuondokana na utawala wa kiimla wa CCM kwa hoja kuwa kilipofikia chama hicho hivi sasa, hakiwezi tena kuaminiwa kukabidhiwa madaraka ya kuongoza dola.

Walisema CCM hakiaminiki tena machoni mwa wananchi na kimepoteza mvuto mbele ya umma; yote haya ni kwa kuwa chama hiki kimekuwa kinaacha ile misingi kama ilivyoasisiwa na waasisi wake, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Walinieleza, kihistoria Chama Cha Mapinduzi ni chama cha ukombozi na kilijipa kazi ya kupigania wanyonge, lakini kikafika mahali historia hiyo ikaporomoka kwa kuingia katika mikono ya watu wasiojali, wasiokuwa na maadili ya uongozi na labda wasiowaaminifu.

Wakati wote wa mazungumzo yetu, Mh. Nape na Dk. Mwakyembe walikuwa wakisisitiza umuhimu wa mimi kukubali kujiunga haraka na CCJ, ili kurahisisha upatikanaji wa usajili wa kudumu wa chama hiki, lengo likiwa CCJ kiweze kishiriki katika uchaguzi mkuu wa 2010.

Hata hivyo, kila muda ulivyozidi kusogea, ndivyo nilivyopata kujua undani Mh. Mwakyembe na Mh. Nape wa kutaka kuanzisha chama chao cha siasa, kwamba kinachowasukuma katika mpango huo, ni matakwa binafsi ya kisiasa na hivyo nikaanza taratibu kuwa mbali na mkakati wao.

Nimeamua kuyasema haya baada ya kuwasikia Mh. Nape na Dk. Mwakyembe wakimkana Mh. Mpendazoe na kimsingi wakikana chama chao – CCJ.

Napenda kuwaambia Watanzania, kwamba CCJ ni chama kilichoanzishwa na kuasisiwa na viongozi hao wawili, pamoja na Mh. Sitta kama ambavyo Mpendazoe alivyoeleza.

Katika mpango huu, mimi niliahidiwa kusaidiwa kugombea ubunge katika jimbo la Monduli kupitia CCJ, huku Mh. Nape akiahidi kusimama katika jimbo la Ubungo.

Nimeyasema haya ili kuondoa unafiki unaojengeka ndani ya chama chetu na taifa kwa jumla, kwamba kuna kikundi cha watu wanaotaka kupotosha umma juu ya uanzishwaji wa CCJ na ujio wake ili umma uwapime na uamue juu ya watu hao.

Mimi kama kada wa CCM niliyefundishwa na kuaminishwa kwamba uongozi ni dhamana na ninayeamini katika misingi ile aliyotuachia Mwalimu Nyerere, nimeamua kuyasema haya ili ukweli ubaki ukweli katika historia ya nchi yetu.

Kuyumba kwa chama chetu na hata kufikia hatua ya kuanza kuporomoka kwa kupoteza nafasi mbalimbali kwa vyama vingine kwa wingi tokea kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi katika nchi hii, ni kwa sababu ya kuwa na viongozi wenye malengo na agenda zao binafsi, tofauti na zile za chama chetu.

Hii bila mashaka inanipa sababu ya kuamini kwamba Bunge la Tisa kama mmoja wa mihimili muhimu wa dola, chini ya Mh. Samwel Sitta lilitumika vibaya kufanikisha agenda nyingine ya kuanzisha chama kingine badala ya CCM.

Ni vema Rais Jakaya Kikwete akajua kuwa ndani ya timu yake, kuna wachezaji ambao wako tayari kujifunga na kuinyima timu yao ushindi. Ni vema akaamua kuachana nao kwa maslahi yake na chama chake.

Ni maoni yangu kwa dhati kabisa na rai yangu kwa viongozi wa chama, kwamba ni wakati mwafaka watu kama hawa wawajibike au wawajibishwe kwa matendo yao.

Baada ya mimi kushutukia na kutokuwa na imani na minendo ya waasisi wa CCJ na hivyo kujiondoa, nilipata taarifa kuwa baada ya kujiridhisha kuwa chama chao hakitasajiliwa na kuwahi uchaguzi wa 2010, waliamua kufanya mazungumzo na viongozi wa Chadema na kukubaliana kuwa wote kwa pamoja watajiondoa CCM na kujiunga na Chadema ili kugombea nafasi mbalimbali kupitia chama hicho.

Kwa ushahidi ninaoutoa, ninawachukua hawa niliowataja kuwa si wasaliti kwangu tu, bali hata kwa chama chenyewe. Nisingeshutuka mapema yangenipata yaliyompata Mpendazoe. Ninampa pole sana ndugu yangu Fred Mpendazoe.

Na hili la Mpendazoe ambaye alikuwa mbunge, akaacha mishahara kadhaa na mafao yake kwa makubaliano ya kazi ya pamoja ambayo nilishirikishwa katika hatua za awali na mwisho wake wakamtosa na sasa wanamkana hadharani, ni moja ya sababu iliyonisukuma sana kutoa ushuhuda huu.

Daniel ole Porokwa,
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).



source: Wavuti - Habari
 
Haya ndo maelezo ya bwaba Porokwa nimeyatoa kwa Michuzi blog. Watasema yote mwaka huu mpaka kieleweke...

KADA WA CCM AIBUKA NA KUWATAJA WAANZILISHI HALALI WA CHAMA CHA JAMII (CCJ)

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Daniel ole Porokwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo asubuhi juu ya ukweli kuhusu waanzilishi wa Chama Cha Jamii (CCJ).hapo chini ni taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari.Kwa muda wa takribani wiki mbili sasa, vyombo vya habari vimeripoti maelezo yaliyotolewa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chadema, Mh. Anthony Komu, kwamba Nape Nnauye alikuwa mwasisi wa Chama Cha Jamii (CCJ). Madai haya yakathibitishwa na aliyewahi kuwa mbunge wa Kishapu (CCM), Fred Mpendazoe ambaye alitaja watu kadhaa nikiwamo mimi, kuwa walishiriki au waanzilishi wa chama hicho ambacho hakikuwahi kufanikiwa kupata usajili wa kudumu.Hivyo basi, nimewaita hapa leo hii, ili pamoja na mambo mengine, kueleza ukweli wa hiki ambacho kimeelezwa vizuri na Mheshimiwa Mpendazoe na kimenukuliwa vema na vyombo vya habari, hasa gazeti la kila wiki la MwanaHALISI.Nimeamua kufanya hivyo kwa misingi miwili mikuu. Kwanza, sisi kama viongozi ni sharti tuwaonyeshe wananchi wetu na wanachama wa chama chetu njia sahihi tunayotakiwa kupita na tuamini katika hiyo njia tunayoelekea.Pili, mmoja wa msingi mkuu wa chama chetu, ni kusema ukweli, na kwamba uwongo na fitina ni mwiko kwa viongozi na wachama wa CCM.Ni kweli niliwahi kuombwa kuwa mmoja wa wanachama waanzishi wa CCJ. Nilikutana mara kadhaa na Mh. Nape Nnauye, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe na Mh. Fred Mpendazoe.Aidha, nilikutana mara moja na Mh. Samwel Sitta baada ya Mh. Nape na Dk. Mwakyembe kunitajia kuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa CCJ, nami kutaka uthibitisho wa hicho walichonieleza. Naye Mh. Sitta alinieleza kuwa nilichoelezwa na Mh. Nape na Dk. Mwakyembe hakina chembe ya mashaka.Katika mikutano zaidi ya mitano niliyofanya na Mh. Nape na Dk. Mwakyembe wenzangu walinieleza mpango wao wa kuanzisha chama cha siasa kuwa umelenga kuondokana na utawala wa kiimla wa CCM kwa hoja kuwa kilipofikia chama hicho hivi sasa, hakiwezi tena kuaminiwa kukabidhiwa madaraka ya kuongoza dola.Walisema CCM hakiaminiki tena machoni mwa wananchi na kimepoteza mvuto mbele ya umma; yote haya ni kwa kuwa chama hiki kimekuwa kinaacha ile misingi kama ilivyoasisiwa na waasisi wake, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Walinieleza, kihistoria Chama Cha Mapinduzi ni chama cha ukombozi na kilijipa kazi ya kupigania wanyonge, lakini kikafika mahali historia hiyo ikaporomoka kwa kuingia katika mikono ya watu wasiojali, wasiokuwa na maadili ya uongozi na labda wasiowaaminifu.Wakati wote wa mazungumzo yetu, Mh. Nape na Dk. Mwakyembe walikuwa wakisisitiza umuhimu wa mimi kukubali kujiunga haraka na CCJ, ili kurahisisha upatikanaji wa usajili wa kudumu wa chama hiki, lengo likiwa CCJ kiweze kishiriki katika uchaguzi mkuu wa 2010.Hata hivyo, kila muda ulivyozidi kusogea, ndivyo nilivyopata kujua undani Mh. Mwakyembe na Mh. Nape wa kutaka kuanzisha chama chao cha siasa, kwamba kinachowasukuma katika mpango huo, ni matakwa binafsi ya kisiasa na hivyo nikaanza taratibu kuwa mbali na mkakati wao.Nimeamua kuyasema haya baada ya kuwasikia Mh. Nape na Dk. Mwakyembe wakimkana Mh. Mpendazoe na kimsingi wakikana chama chao  CCJ. Napenda kuwaambia Watanzania, kwamba CCJ ni chama kilichoanzishwa na kuasisiwa na viongozi hao wawili, pamoja na Mh. Sitta kama ambavyo Mpendazoe alivyoeleza.Katika mpango huu, mimi niliahidiwa kusaidiwa kugombea ubunge katika jimbo la Monduli kupitia CCJ, huku Mh. Nape akiahidi kusimama katika jimbo la Ubungo.Nimeyasema haya ili kuondoa unafiki unaojengeka ndani ya chama chetu na taifa kwa jumla, kwamba kuna kikundi cha watu wanaotaka kupotosha umma juu ya uanzishwaji wa CCJ na ujio wake ili umma uwapime na uamue juu ya watu hao.Mimi kama kada wa CCM niliyefundishwa na kuaminishwa kwamba uongozi ni dhamana na ninayeamini katika misingi ile aliyotuachia Mwalimu Nyerere, nimeamua kuyasema haya ili ukweli ubaki ukweli katika historia ya nchi yetu.Kuyumba kwa chama chetu na hata kufikia hatua ya kuanza kuporomoka kwa kupoteza nafasi mbalimbali kwa vyama vingine kwa wingi tokea kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi katika nchi hii, ni kwa sababu ya kuwa na viongozi wenye malengo na agenda zao binafsi, tofauti na zile za chama chetu.Hii bila mashaka inanipa sababu ya kuamini kwamba Bunge la Tisa kama mmoja wa mihimili muhimu wa dola, chini ya Mh. Samwel Sitta lilitumika vibaya kufanikisha agenda nyingine ya kuanzisha chama kingine badala ya CCM.Ni vema Rais Jakaya Kikwete akajua kuwa ndani ya timu yake, kuna wachezaji ambao wako tayari kujifunga na kuinyima timu yao ushindi. Ni vema akaamua kuachana nao kwa maslahi yake na chama chake.Ni maoni yangu kwa dhati kabisa na rai yangu kwa viongozi wa chama, kwamba ni wakati mwafaka watu kama hawa wawajibike au wawajibishwe kwa matendo yao. Baada ya mimi kushutukia na kutokuwa na imani na minendo ya waasisi wa CCJ na hivyo kujiondoa, nilipata taarifa kuwa baada ya kujiridhisha kuwa chama chao hakitasajiliwa na kuwahi uchaguzi wa 2010, waliamua kufanya mazungumzo na viongozi wa Chadema na kukubaliana kuwa wote kwa pamoja watajiondoa CCM na kujiunga na Chadema ili kugombea nafasi mbalimbali kupitia chama hicho.Kwa ushahidi ninaoutoa, ninawachukua hawa niliowataja kuwa si wasaliti kwangu tu, bali hata kwa chama chenyewe. Nisingeshutuka mapema yangenipata yaliyompata Mpendazoe. Ninampa pole sana ndugu yangu Fred Mpendazoe.Na hili la Mpendazoe ambaye alikuwa mbunge, akaacha mishahara kadhaa na mafao yake kwa makubaliano ya kazi ya pamoja ambayo nilishirikishwa katika hatua za awali na mwisho wake wakamtosa na sasa wanamkana hadharani, ni moja ya sababu iliyonisukuma sana kutoa ushuhuda huu. Daniel ole Porokwa,Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Duuh! Nape hapa huchomoki na ukiendelea kubisha unazidi kujimaliza mana tutajiwa mpaka hotel mlizokuwa mnakutana kufanya vikao vyenu na mpaka wahudumu waliomihudumia! Umekuja kwa pupa sasa tulia upewe dozi!
 
Ni vyema zaidi kwa cdm mapacha watatu wasitoke ccm, thats a greatest wish.

Kwa 'short term political strategy' ni nzuri, kwa taifa na long term strategy nina wasi wasi.
Mimi huwa natanguliza utaifa kwanza ndio maana uwepo wa mapacha naona ni balaa na mzigo kwa nchi yenye mizigo mizito zaidi.
Mapacha wakitoweka katika mizani ya kisiasa,yakuhodhi serikali na kupunguza nguvu zao haramu za 'kiuchumi' itatusaidia sana wananchi.

Kisiasa, inaweza kuonekana ni mtaji kwa CDM lakini jiulize uwezo wa mapacha ilivyotumbukiza sumu inayoiathiri CDM kwa kiwango fulani.
Ni mapacha waliotumia media zao kuchomeka udini wakati wa uchaguzi kwa hofu kuwa CDM walikuwa wanaelekea kushika dola na kwao si jambo zuri. Sumu hiyo imesahahulika aliyeiweka na sasa imeathiri sana CDM kimtazamo. CDM inatumia nguvu kujibu hoja zitokanazo na sumu ya RA na kuchukua muda mwingi ambao ungetumika kueleza sera.

Kwa muundo wa serikali yetu na mamlaka ya kikatiba, kisiasa na maamuzi, uwepo wa mpacha ambao wapo tayari kutumia kila mbinu au silaha kwa manufaa yao kutakuwa na ushawishi mkubwa sana katika mabadiliko tunayotarajia. Ni hawa wameweza kushawishi uteuzi wa viongozi serikalini na ngazi za kisiasa, ni kwa mtaji huo matarajio ya tume huru au katiba yanaweza kukwazwa sana. Tusisahau lengo la mapacha ni kuwania uongozi wa juu wa taifa,uwepo wao una impact kubwa sana katika ku-shape future ya nchi yetu.

CDM watumie ushawishi wa hoja na sera na si kusubiri makosa ya CCM, nikimaanisha siasa ni mkakati na si kamari.

Ni maoni tu.
 
khaaa hiki chama jamani hivi kwa nini wasifunge mlango wapigane ?
 
ni muhimu watu wakaangalia pande zote za shilingi. Ole porokwa alishawahi kutangaza kumpinga lowasa, ghafla akabadilika na kwenda kwenye vyombo vya habari kumuomba radhi kwa kutaka kutumia haki yake ya kikatiba na kidemokrasia!!! Porokwa amekuwa ni mtu asiyeeleweka kwa vipimo vyote vya uelewa na kauli zake ni za kuziangalia kwa umakini.

Kama aliitwa ajiunge ccj hayo angeyasema mapema tena wakati kuna mvurugano ndani ya ccm, lakini angalia ni wakati gani ameamua kuyasema na jiulize ni kwanini.
Siku chache zilizopita mifasadi(hasa pacha 3) walisemekana kutumia mbinu za hali ya juu kujinasua.
Tunakumbuka mapacha walisema tuhuma za kutajwa si ushahidi wa wao kufanya maovu na kuwapa muda wa kujitoa au kuachia nyadhifa ni kuwaonea. Walisema mbona watu wengine wanatajwa katika mambo kadha wa kadha na hawapewei muda iweje wao?

Kitendo cha nape kutajwa kuwa mwanzilishi wa ccj kimetumiwa na mapacha ili kujenga hoja ya kuwa kama tuhuma tu zinatosha mtu kuachia ngazi basi mwakyembe na sitta nao wapewe muda wa kujitahmini. Ni kwa mantiki hiyo porokwa amewezeshwa ili awe 'whistle blower' na hapa ndipo mapacha watatu watakapoponea. Utashangaa ishu itavaliwa njuga sana kwasababu mapacha watatu watagawa pesa(wanayo) kununua wasema hovyo ili kujenga hoja ambayo sasa inashika kasi.

Hapa kuna wafa maji (mapacha 3) na wanashika kila kilicho karibu nao hata kama ni ubua. Tuliangalie suala hili kiundani na mtazamo mpana, ushabiki unaweza kuwa ni sehemu ya kuokoa mapacha watatu bila kudhamiria. Kama kuanzisha chama ni usaliti porokwa alitakiwa aseme hili mapema ndani ya vikao vyao au vyombo vya habari, kujitokeza leo ni kununuliwa ili awaokoe mapacha watatu, hasa ikizingatiwa kuwa baada ya 'kutubu' el alimweka karibu sana.
Sasa mapacha watakuwa na hoja, endapo wao wanatajwa bila ushahidi(kama wanavyodai) basi kila anayetajwa naye afuate mkondo. Kama walivyoanza kuwanunua wenyeviti wa mikoa wa ccm hili watalitumbukiza tu kushadidia hoja yao. Kama hoja ililenga kumweka nape mahali pagumu, itasaidia kuwaweka wengine mahali rahisi, lakini itakuwa ni jiwe moja kwa ndege wawili kwababu nape sasa ni mwiba kwao, na akina sitta na mwakyembe ni mwiba wa zamani, kama kuna 'kisu' chenye makali pande zote hicho kinafaa mapacha 3.

Ni wakati wana cdm popote walipo wajiulize kuna umuhimu wa kulikuza au kulipigia baragumu jambo hili?
Time will tell.

mi naona yote tayashikie bango ili ccm ife haraka kwa maslahi ya taifa.
 
hivi hili la mwanzilishi, lina faida gani kwa siasa zetu? Waanzilishi wa CDM, CUF, NCCR ni kina nani? Maana ukiachana na uanzilishi, hivi wangapi wametoka upinzani kwenda CCM na vice versa? Inasaidia nini hii katika siasa zetu?

wewe kama huoni tatizo wewe pia ni tatizo tena kubwa.
 
Tuna angalia Uadilifu kwa maslahi ya Taifa! Habari ya vyama ni utashi wa mtu! Ila kama kuna ufisadi wamefanya Sitta,Mwakyembe na Nape hapo tupambane nao lakini kwa hili la kuanzisha chama kingine liko ki-CCM zaidi nashangaa hata watu wa Chadema kulichukulia kama agenda! Leo Mpendazoe katoka CCM yuko CDM kapitia CCJ sasa unaweza sema tusimwamini Mpendazoe kisa kahama au kabadilisha chama? Ina muondolea uaminifu mwana siasa kuhama au kubadili chama? Mwalimu Nyerere aliwahi kusema "CCM sio baba wala Mama yangu kama kuna Chama kitaonekana kina mlengo mzuri naweza kuwapa kadi yenu CCM" hivyo tunapoteza muda kujadili hoja mfu!
Hapa tunajadili unafiki wa Sita, Mwakyembe na Nape. Shujaa hapa ni Mpendazoe. Ni dhahiri kuwa watanzania tumechoshwa na siasa na uongozi dhalimu wa CCM. Kwa muda mrefu nimejiuzliza na kuita nchi yangu Tanzania ni ya watu waoga wasiothubutu. Wasiojitokeza na kujitolea kama Mandela, wasiowajasiri kama Raila Odinga, Morgan Tshangerai au Besigye nchini Uganda. Yaani haiwezekani nchi ina wanasiasa wanaofanana tu akili zao katika karne hii ya demokrasi na vyama vingi kama hao si unafiki wa mtumikie kafiri upate mradi wako.
Sita, Mwakyembe na Nape ambao ndio wanaojipambanua CCM kama watu wasafi na ambao wanaweza kuwa mtaji adimu uliobaki CCM kama walitaka kuanzisha chama kingine ili kutoka CCM sisi hatuna tatizo na hilo. Tatizo letu ni kwanini kama walitaka kutoka CCM, na kuwa waliona uchafu wa CCM kama tunavouona sisi wazalendo, WANAFANYA NINI HUKO BADO? Nhh kama sio kulinda maslahi yao kwa gharama ya uongozi mbovu na umaskini kwa watanzania? Tunataka wanasiasa walio tayari kuacha utamu wa ufalme wa Misri kuungana na sisi watumwa wa Israel. Sitta, Mwakyembe na Nape wameshindwa kuacha nyama na asali za Misri tutawaamini vipi wakati tutakapokuwa tunapigana kurudisha heshima yetu. Kama kwa hali ya kawaida tu wametusaliti itakapofika watu kufungwa na kupigwa mijeledi si ndo watatusaliti zaidi mchana mchana.
Kama hujanielewa mwana magamba Mrengo wa kati kanywe kikombe kwa Babu utapona na kunielewa.
 
CCJ, CCJ, hivi CCJ nayo ni habari kwa sasa? mnajadili mimba ambayo iliharibika ili iweje? mbona kuna watu waliowahi kuhama kabisa vyama vyao na wakajiunga na vyama vingine baadae wakarudi kwenye vyama vyao vya zamani na wakapokewa kama mashujaa na vyeo juu. Kwanza katika siasa za bongo mtu akitaka kujiongezea umaarufu anahama chama chake kisha anarudi tena kama shujaa na kupewa vyeo.

Tujadili mambo ya msingi yanayolihusu taifa letu kwa sasa, sukari bei juu, nyama imekuwa ni anasa, nauli za mabasi juu, mafuta n.k

NI VIZURI KUENDELEA KILIJADILI HILI SAULA ILI KUJUA NANI NI MNAFIKI NA NANI SII MNAFIKI ILI BAADAYE TUSIJE TUKAMCHUGUA MNAFIKI KUONGOZA HILI TAIFA NA BAADA AKAJA KUTUMALIZA KABISA.(mtu mnafiki na rahisi kawasariti watu wake kwa maslahi yake binafsi)
 
hivi hili la mwanzilishi, lina faida gani kwa siasa zetu? Waanzilishi wa CDM, CUF, NCCR ni kina nani? Maana ukiachana na uanzilishi, hivi wangapi wametoka upinzani kwenda CCM na vice versa? Inasaidia nini hii katika siasa zetu?

Suala hapa si uanzilishi bali ni hujuma na uasi ndani ya chama. Kumbuka wakati CCJ inaanzishwa waanzilishi wake ukiachia mweyekiti na katibu walioshirikishwa tu walikuwa hawafahamiki. Sasa hiyo ni hujuma na uasi ndani ya chama. Kama Sitta, Dr Mwakyembe na Nape walitaka tusiamini kuwa ulikuwa usalitina hujuma basi walipaswa kuwa wazi kwamba wanaondoka Chama Cha Magamba na Kuanzisha CCJ. Kwahiyo Nape na waanzilishi wenzake ni wasaliti kwahiyo chama cha mavuvuzela (CCM) kiwe nao makini.
 
Back
Top Bottom