Popobawa....!!!

Pomole

JF-Expert Member
Jan 31, 2011
257
7
Popobawa akikutembelea eti lazima umtaarifu mkeo au mumeo au hata watoto kuwa umetembelewa ndio aache mchezo wake na kuhamia kwingine.Je kuna ukweli wowote!!!Kuna mtu mwenye taarifa sahihi au ushuhuda wa mwenza wake au jirani kutembelewa na hicho kiumbe,au zilikuwa fiksi tu za wabongo kutunga mambo......!!!
kuna tofauti kati ya popobawa na jini mahaba?
 
naomba shehe yahaya kama upo humu ndani jibu hili swali!!!
 
Dena,Sijatembelewa!!!!Tatizo ndio hilo,nasikia ukipitiwa lazima utangaze,labda wengine watusaidie inakuwaje
 
Kwa kule nilipokuwa wakati nikiwa mdogo, watu walikuwa wanatangaza kuwa popobawa kapita. Na zilikuwa zinaweza kujuilikana nyumba zote alizopita moja baada ya moja. Ila wakati huo alikuwa anakuja kwa kutesa na siyo kubaka. Lakini sasa mambo yamebadilika, popobawa kabalehe kazi kujigijigi tu. Ila sina uhakika kuwa ni kwa wote anaowatembelea na habari ya kutangaza huwa naisikia sana tu.
 
salini kabla ya kulala hizo ni imani haba hakuna cha popobawa wala nn.
 
Duu... mkuu hizo hekaya za sheikh yahya bado zipo??:lol:

popobawa.jpg

Jaribu kusoma kidogo kuhusu huyu mdudu hapa!!

Popobawa – Unusual Wikipedia Monday « Stuff
 
Dena,Sijatembelewa!!!!Tatizo ndio hilo,nasikia ukipitiwa lazima utangaze,labda wengine watusaidie inakuwaje
Dah!!......................hivi viumbe vingingine bana?Mkuu minafikiri kutangaza ni lazima coz lengo lake yeye ni udharirishaji tu, tehetehetehe!!!!!!!!!!!!
 
Sidhani kama kuna aliyekwishatembelewa na huyo mdudu katika jukwaa hili,na hata kama yupo sidhani kama anaweza kukuthibitishia hapa jukwaani kwa kuwa atakuwa ameshajitangaza huko anakoishi,kwa hiyo basi swali lako naona kama halitapata jibu la uhakika kwani katika wote wanaosimulia visa vya popobawa sijawahi kumuona japo mmoja tu aliyewahi kuelezwa na jirani kuwa ametembelewa achilia mbali mhusika mwenyewe.
 
Paka mweusi,tatizo ni kuwa ucposema kesho anarudi tena,kwa hiyo ili akuache must utangaze!patamu hapo
 
Paka mweusi,tatizo ni kuwa ucposema kesho anarudi tena,kwa hiyo ili akuache must utangaze!patamu hapo

Au ushauri mwingine ukitaka kuhakikisha kama ni kweli au si kweli basi tembelea kisiwani Pemba kisha ukifika katika maskani zao uwaulize na uwe mbishi sana ukisema kuwa hakuna kitu kama hicho,nadhani wiki moja tu utakuwa umepata jibu kama haya mambo ni kweli lazima utangaze au si kweli..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom