Popo Bawa . . . . . | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Popo Bawa . . . . .

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bikra, Jun 2, 2009.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  Jun 2, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  KATIKA miaka ya nyuma, hapa jijini Dares Salaam kulitokea uvumi kuwa kulikuwapo na shetani aliyekuwa akiitwa Pop Bawa. Kwa kukaririwa mara kwa mara, uvumi huo ukasambaa kwa kasi kama moto katika nyika. Mradi kikaingia kishindo kikubwa sana, mpaka wakaazi wengi wa mkoa huu wakaingiwa na woga wa kubakwa na Popo Bawa!


  Safari moja ikaja habari kuwa Pop Bawa ametiwa nguvuni, na ameshikiliwa katika kituo cha Polisi cha Buguruni. Watu wa kila rika wakamimimika katika kituo hicho kumwangalia kiumbe huyo wa ajabu.


  Kilichochangia zaidi kukubalika kwamba kweli alikuwapo Popo Bawa ni kuwa kila aliyerudi kutoka Buguruni alihakikisha kweli ameshuhudia tokeo la kukamatwa Popo Bawa! Ilikuwa ukipita mitaani utakuta makundi ya watu yakizungumzia juu ya kukamatwa kwa dude hilo.


  Mimi mwenyewe siku hiyo nilipokuwa nikipita karibu na soko kuu la Kariakoo, nilimwona kijana mmoja wa Kibaniani ambaye alikuwa ni jirani yangu na ni dereva wa teksi, amezungukwa na KUNDI KUBWA LA WATU, WAKIMSIKILIZA AKIWAELEZEA JUU YA TUKIO HILO LA BUGURUNI. Aliwahadithia kuwa yeye mwenyewe alikuwa akitokea huko Buguruni, na ameshuhudia jambo hilo.


  Baadhi ya wale waliokuwa wakimsikiliza wakasema, "wako wapi wale waliokuwa wakipinga habari za Popo Bawa, waje wamsikilize huyu dereva wa teksi. Yeye mwenyewe ametokea Buguruni na amemwona Popo Bawa!"


  Hata na mimi nilikuwa karibu nimsadiki. Lakini ikanipitikia akilini kwa nini kwanza simwulizi maswali ili kupata uhakika? Basi nikamwuliza, "wewe unatokea Buguruni hivi sasa?" Akanijibu, "Diyo!" Nikaendelea kumwuliza, "Wewe umemwona kwa macho yako huyo Popo Bawa?" Akasema, "Mimi hapana ona kwa macho. Lakini mimi ona watu mingi Polisi Buguruni. Yote wasema Popo Bawa kwisa kamata. Iko dani polisi!"


  Pale pale nikakumbuka maneno ya Gobbels, aliyekuwa Waziri wa Propaganda wa utawala wa Hitler, katika vita vikuu vya dunia. Gobbels alisema kuwa jambo lo lote, japokuwa la uongo, ukitaka litangae na likubalike upesi basi litangaze, kasha ulikariri mara kwa mara.


  Naam, japokuwa habari, za Popo Bawa zilikuwa ni uzushi, lakini kwa vile zilikuwa zikikaririwa mara kwa mara watu wakazisadiki. Baadhi ya watu, tena wengi tu, wakaingiwa na hofu, kwa jambo lisilokuwapo kabisa!
   
Loading...