Madia haya kuwa popo haoni yana uhalisia kiasi gani wakuu?
Mimekuwa ara kadhaa nikisikia kuwa nawe huoni kama popo, je ni kweli kuwa popo haoni? Kama anaona anaona mchana na usiku?
Picha Gettyimage
Mimekuwa ara kadhaa nikisikia kuwa nawe huoni kama popo, je ni kweli kuwa popo haoni? Kama anaona anaona mchana na usiku?
Picha Gettyimage
- Tunachokijua
- Popo anatajwa kama mnyama wa kuvutia sana huku akiwa mamalia (mnyama) pekee mwenye uwezo wa kuruka kweli. Hadi kufikia mwaka 2025 ilibainika kuwa kuna takribani spishi 1,500 za popo duniani huku ugunduzi zaidi ukiendelea.
Tovuti ya popo nchini Uingereza inaeleza kuwa Popo wanawakilisha zaidi ya robo ya spishi zote za mamalia nchini Uingereza, na takribani asilimia 20 ya spishi zote za mamalia duniani.
Kwa miaka mingi kumekuwa na imani kuwa popo hana uwezo wa kuona huku wengine wakitumia msamiti huo kurejelea watu kwa kuwaambia "kipofu kama popo" lakini je ni upi ukweli wa madai haya?
Je, ni kweli popo hawaoni?
JamiiCheck kupitia makala kumuhusu mnyama popo zimebaini kuwa madai hayo si ya kweli, kwani popo anao uwezo wa kuona.
Popo wana macho madogo yenye uwezo mkubwa wa kuona, yanayowasaidia kuona katika mazingira yenye giza kubwa ambalo binadamu angeweza kuliona kuwa giza totoro. Ingawa hawaoni kwa ukali na rangi nyingi kama wanavyoona binadamu, uwezo huo unawatosha kwa mahitaji yao.
Kwanini Popo hupendelea kuruka zaidi usiku?
Popo ni aina ya viumbe wanaotumia muda mwingi zaidi usiku kuwa macho (nocturnal), hivyo si rahisi kumuona popo akiruka mchana. Na mara nyingi popo hawaruki mchana pia kwa kuwa wapo kwenye hatari kubwa ya kushambuliwa na wanyama wanaoruka mchana.
Hata hivyo, popo anaweza kuonekana mchana ikiwa ana njaa (kwa mfano jike mwenye mtoto anayehitaji kulishwa), ana kiu (hasa wakati wa joto kali), au amesumbuliwa na shughuli za binadamu, hali inayoweza kumlazimu kuchukua hatari zaidi ili kutafuta chakula.
Popo anawezaje kusafiri gizani?
Licha ya kuwa na uwezo wa kuona, lakini usiku popo hutumia zaidi mwangi kuliko mwanga hii huitwa (echolant) kwa ajili ya kusafiri na kuwinda.
Popo hupata njia yao gizani kwa kusikiliza mwangwi wa sauti. Wanaporuka, hutoa sauti za juu sana (ultrasound) ambazo hugonga vitu vilivyo mbele yao na kurudi kama mwangwi. Mwangwi huo huwasaidia kujua mahali vitu vilipo ili wasigongane navyo wakati wa kuruka. Pia, mwangwi huo huwasaidia popo kuwinda wadudu na wanyama wengine wanapotafuta chakula.