BRICKS NA MALENGO YA KILA NCHI.
CHINA - apate nishati(mafuta, makaa,madini kinywa) na eneo la biashara.
URUSI - apate Washirika wa Kijeshi kukabiliana na NATO, kutengeneza multipolar world (dunia isio moja) ili kuondoa kwa haraka ukubwa wa Magharibi duniani kiuchumi.
IRAN - apate ahueni ya vikwazo vya uchumi kutoka magharibi kwa kuondoa ukubwa wa nchi za mgharibi na Kuondoa nguvu ya ushawishi wa Saudi Arabia mashariki ya Kati.
SOUTH AFRICA- apate ahueni ya mikopo isio na riba, biashara na misaada kutoka China, Urusi na India kujikwamua na uchumi usio kua kwa miaka mingi.
BRAZIL- apate uwekezaji wa mitaji katika sekta zake za viwanda na biashara asa kutoka China na apate mahali pa kuuza bidhaa zake za magari, ndege na nyingine ambazo zimekosa wateja pale South America kutokana washindani wake US, Mexico, Canada na EU ambao ndio wanatawala Soko la Latin America na Caribbean.
SAUD ARABIA - apate biashara zake za mafuta kwa kuegemea pande zote za globle West, globle East na globle South. Pia ana hofu uchumi wa magari ya umeme na uondoaji wa nishati chafu unaopigiwa upatu na G7 pamoja na EU utakata biashara yake ya mafuta kwahiyo anawai uku BRICKS kwa kuwa BRICKS hawana sera hiyo ili auze pale West watakapokacha wese lake.
ETHIOPIA - apate msaada wa haraka wa nishati, chakula na fursa za biashara ili kusaidia idadi yake ya watu walio masikini na vita. Yupo pale koumba tu.
AGENTINA - apate msaada wa kuondoa madeni aliyo nayo na uchumi mgumu taifa inalopiatia kwa miaka. Anatafuta pa kupumulia shida zake.
European Union ili ujiunge lazima upewe mashariti ya Kufanya kama 1. Kurekebisha mifumo yako ya kitaasisi kuendana na matakwa ya EU na nchi wanachama. Uchumi, Sheria, mazingira, rushwa, Siasa na demokrasia, kilimo, fedha na benki na e.t.c lakini BRICKS unajiunga ata kama nchi yako inavita kama Ethiopia, ina uchumi mbovu kama Agentina, South Africa, au ata kama ina sera mbovu za kisiasa.
2. G7 zote zina uchumi mkubwa na viwanda na zinachangia katika pato la Bank ya dunia kwa pamoja na kuingia G7 ni uchumi wako kuwa namba 1 hadi 7 kiuchumi, kiviwanda na kimapato lakini BRICKS inaokota ata kama nchi haina data za kiuchumi.
3. BRICKS kila mtu ana malengo yake, wakati EU ni economic forum, na G7 ni economic forum na NATO ni Military forum.
4. Je unawezaje kumlinganisha South Africa au Ethiopia na China katika mizani ya biashara?, Ilitakiwa Ethiopia upewe miaka 5 ijirekebishe kisera na kiuchumi alafu ujiunge na BRICKS sasa imeingizwa chap kwa haraka wakati ina vita za ndani na amhara, Oromia na Tigrai, sasa uwo si umoja wa mambo mengi sana.
MI NAONA ILE POINT YA HISTORY FORM TWO YA, FAILURE OF REGIONAL BLOCK/ORGANISATION IS, 1. Different idiologes between member states ina apply hapa. Uyu uchumi, uyu amani ,uyu ukubwa, uyu biashara, uyu nishati, uyu tukomoane.
Naomba nichangie hoja Yako hii kwa kutofautiana nana wewe bila chuki.
Umeandika mambo meeeengi lakini naona hata wewe hujaelewa malengo ya Brics.
Hujaelewa kwa sababu umekalili mambo.
Hivi kwani ni lazima Kila umoja ukiundwa lazima ufanane na WA EU na G7?
Nini sababu ya kuunda umoja mbdala?
Kwani EU na G7 ndio kipimo Cha ustaarabu duniani?
Nani aliewapa EU na G7 mamalaka ya kua kipimo Cha kuunda umoja,au mamalaka hayo.
Kwani watu wakiunda umoja mpya wenye malengo tofauti kabisa na umoja miingine iliyotangulia hapa duniani watapoteza uhalali?
Mfano mdogo TU west wanajinasibu wao kua ndio baba wa demokrasia na nyinyi mnawaunga mkono kwa hilo,na demokrasia ni uhuru wa kutofautiana mawazo na kua na mawazo tofauti au mbadala.ndio maana utakuta huko ulaya na USA Kuna vyama tofautitofauti vya kisiasa,mfano USA kua republican na democratic hivi havifanani kwa sera,Sasa kwa Nini kusiwe na chama kimoja TU?
Sasa kwa Nini msiione Brics kama imekuja na malengo ofauti na mapya kimuundo?ambayo ni tofauti kabisa na umoja zingine, na hivyo kuonekana kua ndio mfano Bora kabisa wa demokrasia?
Kwa mfano Kuna ccm, kwa Nini Sasa iwepo chadema au nccr?
Kwani chadema lazima ije na sera zote za ccm? Je Kuna haja Gani ya kua na chedam? kwa Nini tusiwe na ccm peke yake?
UK Kuna labour na conservative hivi vina sera tofauti, kwa Nini kusiwe na chama kimoja TU?
Hivi ndivyo ilivyovkwq G7,EU na hata G20 halikadharika OPEC,sadec na ECOWAS Kila kimoja kina sera zake ma malengo yake.
Sasa kwa Nini mnataka Brics icopy na kupest kwa EU na G7?
Inakua wapi Sasa maana ya vyama vingi?
Tufanye mfano Brics ni chama katika levo ya kidunia.
Nchi yoyote itaamua kujiunga upande inaotaka.
Brics kuchukua wanachama masikini kama Ethiopia Ina malengo yake tofauti na EU nao Wana malengo Yao,EU sio kipimo Cha kuanzisha umoja.brics Ina sababu zake na EU Wana sababu zao kuhusu wanachama.
Kama Brics itafeli sio ajabu maana maisha ni kujaribu TU.
Je walitakiwa wasianzishe Brics kwa hofu ya kuja kufeli?
Hizo ni akili,ni uwoga.
Mimi nafikiri tuipe Brics muda,kwani muda utajibu.