Pope Benedict xvi Apingwa ujerumani!

Pope Benedict xvi Apingwa ujerumani!

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
5,139
Reaction score
1,149
[h=3]WABUNGE WA UJERUMANI WATOKA NJE KUMPINGA POPE BENEDICT XVI.[/h]

Pope Benedict XVI akilihutubia Bunge la Ujerumani.

Wabunge wa Bunge la Ujerumani septemba 22,2011 walitoka Bungeni kupinga Papa kulihutubia Bunge hilo. Kitendo hicho walifanya kutokana na kutokukubaliana naye katika mambo matatu. La kwanza wanapinga kwa Kanisa Katoliki kuto ruhusu matumizi ya KONDOMU, la pili kwa vitendo viovu vinavyofanywa na Makasisi ya Kanisa hilo vya kuwadhalilisha watu kijimsia nadhani mtakuwa mnanielewa na mwisho wanapinga kwa Papa kulihutubia Bunge hilo kwa sababu ya kutotaka kuunganisha Siasa na Dini.
Papa huyo ni mjerumani ambaye amezaliwa Bayern Kusini mwa Ujerumani.
 
Naunga mkono kitenda cha kutokuunganisha dini na siasa
 
Papa ndiyo walewale magamba tu,kuruhusu watu wazini ndyo lengo la kuruhusu kondom,kunajisi watoto
 
WABUNGE WA UJERUMANI WATOKA NJE KUMPINGA POPE BENEDICT XVI.

Pope Benedict XVI akilihutubia Bunge la Ujerumani.

Wabunge wa Bunge la Ujerumani septemba 22,2011 walitoka Bungeni kupinga Papa kulihutubia Bunge hilo. Kitendo hicho walifanya kutokana na kutokukubaliana naye katika mambo matatu. La kwanza wanapinga kwa Kanisa Katoliki kuto ruhusu matumizi ya KONDOMU, la pili kwa vitendo viovu vinavyofanywa na Makasisi ya Kanisa hilo vya kuwadhalilisha watu kijimsia nadhani mtakuwa mnanielewa na mwisho wanapinga kwa Papa kulihutubia Bunge hilo kwa sababu ya kutotaka kuunganisha Siasa na Dini.
Papa huyo ni mjerumani ambaye amezaliwa Bayern Kusini mwa Ujerumani.

Habari hii si ngeni ilishatoka kwenye baadhi ya vyombo vya habari hapa Tanzania mwezi uliopita.

Haina maana kwamba papa hakubaliki nchini Ujerumani, bali hayo ni mambo ya kisiasa. Na kujua jambo hilo inabidi uielewe historia ya dini katoliki nchini ujerumani na chimbuko la madhehebu ya kilutheri kutoka ukatoliki nchini ujerumani. Mabadiliko na msuguano wa madhehebu ya dini ulianza nchini ujerumani miaka mingi ambapo Martin Luther alipohasi dini Katoliki na kuanzisha kanisa la kilutheli.

Mwendelezo huo na ukitilia maani kwamba kuna baadhi ya wabunge katika bunge ni Waluteli ni dhahiri kilichotokea kimefikwa vazi la kisiasa wakati nyuma ya pazia kuna mantiki nyingine yenye mwelekeo wa mikinzano ya kihistori. Historia ya kuzuka kwa Kanisa la Kiluteri nchini Ujerumani ilianzia kwenye ujenzi wa kanisa kuu la Peters, Vatican-Roma miaka hiyo. Sipendi kueleza historia yote hapa kwa sababu huu si uwanja wa dini.
 
Duh ila si vyema kuchanganya dini
na siasa jambo hili linaathari vby
hapa tz linakamata kasi
 
Back
Top Bottom