Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Nimeshangazwa sana na uamuzi wa Edward Lowasa kubadili gia angani ghafla na sasa anaonekana kuwa na mahaba na Rais Magufuli. Najua mahaba haya ni ya kinafiki na yanalenga kumsahaulisha Rais asipambane kisawasawa na wale wote waliohusika na uuzwaji wa Rasilimali zetu akiwemo Edward Lowasa.
Hoja ya kusema anamuunga mkono Rais eti kwa sababu anatekeleza Ilani ya UKAWA, huu ni unafiki uliopitiliza. Magufuli anatekeleza Ilani ya CCM na hiki anachosimamia sasa alikifikiria hata kabla hajaamua kugombea Urais. Naamini kila Mtanzania anayo ile Video Clip ikionesha jinsi anavyokerwa na usafirishaji mchanga wa Dhahabu long years ago.
Nitoe wito kwa Rais Magufuli. Usirudi nyuma. Pambana na kila aliyehusika na baada ya hapo tutakuwa salama. Upo ushahidi wa wazi wa Lowasa kuhusika kwenye maskandali mengi hapa nchini. Suala la IPTL na uuzwaji wa mgodi wa Buzwagi. Ushahidi upo na hakuna mahala Lowasa ataponea. Hizi mbeleko za Lowasa kwa Rais Magufuli kwa sasa ni too late.