Pongezi za dhati kwa Mh.Edward Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pongezi za dhati kwa Mh.Edward Lowassa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Oct 19, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Oct 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ndugu wana JF,nimefurahishwa sana na kauli ya Mh.E.Lowasa juu ya vyombo vyetu vya habari hapa Tanzania kuhusu kutumia mda mwingi ktk kuzungumzia mambo yasiyo na msingi na kuacha mambo ya msingi yakiambaa na njia,

  kwa kweli nampongeza kwa kuwaambia ukweli mtupu kwani ukilinganisha na nchi za wenzetu vyombo vyetu vya habari vimebakia kupiga propaganda ili mradi mkono uende kinywani,

  MH.E.Lowasa anasema

  "Ndugu wanahabari nazungumza nanyi baada ya kurejea nikitokea katika nchi za Nigeria, Malaysia, Singapore, India, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani ambako nilipata fursa ya kujifunza mambo mengi lakini moja muhimu likiwa ni

  vyombo vya habari (kwa maana ya waandishi wa habari) na wanasiasa wanavyotumia muda wao mwingi kujadili masuala yanayogusa maisha na maendeleo ya watu wao.

  Tofauti na kile wanachofanya wenzetu hapa nyumbani, ninyi wanahabari na sisi wanasiasa tumekuwa tukitumia muda wetu mwingi kujadili watu na propaganda za kisiasa zisizo na tija wakati tukitambua kwamba, taifa linakabiliwa na changamoto nyingi kama zile za kuhamasisha uwezekazji wa ndani na nje ya nchi, kuimarisha mifumo ya utawala bora, kuporomka kwa thamani ya shilingi kila kukicha, mdororo wa uchumi, tatizo kubwa la ajira kwa vijana, kushuka kwa kiwango cha elimu na ugumu wa maisha kwa ujumla. TUNAPASWA KUJISAHIHISHA."

  source: Wavuti - Habari"
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Umeshawahi kujiuliza ni nani alikuwa ana finance hizo propaganda katika vyombo vya habari? Nani amekuwa anahonga waandishi habari ili aandikwe mazuri yake tu? Tokeni hapa.
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Unashangaza mno kwa kumshangilia kwa sababu tu ya yeye kukukwapulia kodi yako na kugoma zunguzia chochote zaidi ya kukuita wewe na mimi twende tukamsikilize anavyomuomba rafiki yake msamaha kwa kufanyia chama chake vimbwanga kule Arusha?

  Nadhani alihitaji tu kwenda moja kwa moja kumwambia hayo huko huko Magogoni bila kutupigia mikelele.

  Kwetu sisi tulitarajia kusikia akisema kwamba baada ya kumrudia Mungu sasa basi ameamua kutubu, kututaka radhi na kurudisha kiasi chote alichokichota kwenye kodi yetu.

  Wengi tultegemea kusikia maoni yake kukiri kwamba hakukuwa kuumbwa kampuni inayoitwa Richmond dunia zaidi ya kubakia kitu cha kufikirika tu mawazoni hivyo hata warithi wake Dowans na Simbyon na zinakosa uhalali wowote kuanza kutumbua macho eti wanasubiri malipo kutoka kwetu.

  Hata hivyo, ruksa endelea kumpamba Shujaa wako wa Ufisadi kwa Wa-Tanzania.
   
 4. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #4
  Oct 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni kwamba ndugu yangu tayari ulikuwa na matarajio kichwani,sasa matarajio yanapokwenda kinyume na ulivyotaka basi lazima iwe tofauti,lakini mimi nachosimamia ni kile juu ya vyombo vya habari na habari za udaku na kuacha mambo ya msingi,
  hayo mengine niwewe na matakwa yako juu ya yale uliyotaka kuyasikia kutoka kwa Mh
   
 5. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,726
  Likes Received: 3,144
  Trophy Points: 280
  Pongezi za dhati for what? Kuendelea kuwafanya watanzania bado ni wajinga kutokana na utetezi wake na vitisho vyake kwa waandishi wa habari au kuvunja kimya cha muda mrefu which is which here?!!!
   
 6. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mbona yeye hajazungumzia mabonyeti yanawahusu watanzania hasa mgao wa umeme na ushiriki wake katika kufanya mambo yawe mabaya zaidi?
   
 7. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nitoke vipi!!!!!!!??????
   
 8. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  muhuni tu hana lolote ati hajaona mapungufu ya Rais kajikosha tu
   
 9. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Sawa ndugu; Yeye Lowassa amezungumzia mambo gani ambayo sio "propaganda za kisiasa zisizo na tija"?

  Katika maongezi yake ametoa wazo gani au tatuzi la swala lipi la kitaifa?
   
 10. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Mashart za mganga wake hayo.
   
 11. N

  Naipendatz JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 914
  Likes Received: 326
  Trophy Points: 80
  Me nimeacha kusoma,kusikiliza or kuangalia vyombo vya habari vya kibongo! Ni upuuzi mtupu! EL 4 2015
   
 12. Shenkalwa

  Shenkalwa JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hawa magamba naona sasa wamechanganyikiwa hata wanalolifanya halieleweki. Mtu kama EL kwenda kuwaita waandishi wa habari na kuongea alichoongea ni upuuzi mtupu. Hii ni kupoteza muda wa watu. Anaweweseka hata anachokiongea hakina kichwa wala miguuu. Yeye anaongelea anachafuliwa anachafuliwa badala ya kujibu hoja na tuhuma zinazoelekezwa kwake. Utaziitaje tuhuma nzito zinazoelekezwa kwako "kuchafuliwa" badala ya kuzijibu???
  Hao anaosema wanamchafua na inatosha wana hoja nzito ambazo alitakiwa azikiri au azikanushe badala yake anasema inatosha. Hiyo inatosha inatusaidia nini. Alijiuzulu uwaziri mkuu baada ya kuona uzito wa tuhuma zinazomkabili, sasa kujiuzulu tu hakutoshi anapaswa kuwajibika zaidi kwa yeye na wenzake kurudisha fedha walizowaibia watanganyika kupitia mikataba hewa ya richmond/dowans na sasa simbyon. Watanganyika bado tunasubiri majibu kutoka kwake kwa ajili ya tuhuma hizo nzito na alipoita waandishi wa habari tulitarajia ataongelea hayo siyo kulalamikalalamika anachafuliwa badala ya hoja. Na kama hajajibu tuhuma hizo ataendelea kutakiwa ajibu na hapo atakuwa hachafuliwi kwa namna yeyote kama anavyodai yeye. Aidha tulitegemea angewajibika kwa kuachia nyadhifa nyingine alizo nazo kuanzia kwenye chama chake cha magamba mpaka bungeni baada ya yeye mwenyewe kujihoji na kujitafakari na hasa baada ya kushindwa kukana tuhuma zinazomhusu. Na wewe uliyefurahishwa na kauli zake bila shaka una walakini.
   
 13. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  tatizo kubwa linaloonekana hapa ni kuwa watz wengi tumekuwa wakosoaji kwa wasiopenda kukosolewa na hata mkosoaji yeye mwenyewe hapendi kukosolewa.Lowasa anaona kuandikwa na vyombo kwa mabaya yanayoaminiwa sio vizuri lakini wakati huo yeye hapendi kuwaeleza waandishi wa habari ili waandike ukweli
  Je,vyombo vya habari vingekuwa vinaandika mazuri ya lowasa angelalamika?bila shaka SIYO,sasa kuna shida gani kuwaeleza waandishi ukweli ila kuwatoa kwenye hayo matope?unawakosoa vyombo vya habari ilihali wewe mwenyewe hutaki kukosolewa kwenye mambo ya msingi.
  Kwa upande mwingine vyombo vya habari vinaona kuwa kukosolewa na lowasa ni kama WAMETISHWA badala ya kuchukua kama changamoto ktk kazi yao.Kama muanziisha thread alivyosema vyombo vingi vya habari vimewekeza zaidi kuwajadili binafsi na mambo ya siasa yasiyo na tija kwa taifa kwa wakati huu;mfano lowasa for 2015-hii inatusaidia nini sisi watu tuliochoka na maisha magumu?matokeo yake tunajikuta tunabakia kusoma habari hazitukomboi kifikra,kiuchumi,kijamii,kisasa,nk.
  Ukiangalia magazeti yetu mengi kwa kila siku yamepambwa na siasa tupu;mara yule ufisadi umefanyika hapa,mara pale.Hayo mimi sikatai kuwa siasa ina nguvu sana ktk mustakabali wa taifa lakini "je,ni kila siku?"

  Lazima watz tufike sehemu tuache ubishi;"tukubali kukosolewa kama ambavyo tuko tayari kuwakosoa wengine"
   
Loading...